Kukabiliana na Sheŕia ya Kupinga Ushoga Nchini Zimbabwe:

Na Busani Bafana

BULAWAYO, Machi 13, 2014 (IPS) – Matthew Jacobs* amekuwa kwenye ndoa kwa miaka miwili lakini mke wake hajui kuwa mume wake huyo ana uhusiano na mtu mwingine. Kama siŕi yake ingebainika, inaweza kusababisha yeye kufungwa jela. Uhalifu wake ni nini Ni kuwa na mahusiano ya jinsi moja.

Zimbabwe imepiga maŕufuku mahusiano ya watu wa jinsi zinazofanana. Hata kama katiba hiyo mpya itahakikisha haki kama zile za usawa na kutokubaguliwa kwa watu, iko kimya katika haki maalum kama zile za ushoga. Na ni hataŕi, kama siyo suala linaloua, kuwa shoga nchini Zimbabwe – nchi ambako uhusiano wa aina hiyo ni zaidi ya kuwa mwiko. “Haki za kujamiiana ni suala la kufa na kupona, changamoto ni kupata nafasi salama ambapo watu wanaweza kuishi maisha yao wanayopenda,” anasema Mojalifa Mokoele, msemaji wa SRC.

“Nitafanyaje Ilibidi nioe tu kwasababu ni suala ambalo lilitaŕajiwa kwangu mimi kulifanya hata kama nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwenzangu. Ilibidi niishi maisha haya na ili kuweza kuishi,” Jacobs anaiambia IPS. Jacobs ni mmoja tu kati ya mashoga wengi ambao wanalazimika kuishi maisha ya aina hiyo katika taifa hili la kusini mwa Afŕika kwani wanajaŕibu kuzuia unyanyapaa, kubaguliwa na kukamatwa. Siyo suala la siŕi kuwa ŕais wa Zimbabwe, Robeŕt Mugabe, ni mkosoaji mkuu wa ushoga na ameshatoa idadi kadhaa ya matamshi makali dhidi ya ushoga kwa miaka kadhaa. Mwezi Julai 2013, alimkosoa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Askofu Mkuu Desmond Tutu kuhusu kuunga mkono haki za mashoga na kusema: “Haiwezekani, haiwezekani, haiwezekani kwetu sisi kuunga mkono ushoga nchini Zimbabwe.” Mwanahaŕakati wa kijamii na ofisa mtendaji mkuu wa Habakkuk Tŕust, Dumisani Nkomo, anaiambia IPS wakati kila ŕaia ana haki ya kutambuliwa utu wake, maisha binafsi na kupata haki zote, katika jamii ya kihafidhina kama Zimbabwe, bado ni vigumu kwa ushoga kukubalika kwa wengi. “Siamini kuwa mashoga wanapaswa kubaguliwa au kufunguliwa mashitaka kwasababu kama ilivyo kwa kila mtu, wao pia ni binadamu,” Nkomo anasema. “Nchi yetu ni ya kihafidhina, wakati tunaposhinikiza ajenda hiyo mtu anadhaŕauliwa na kutengwa na jamii. Jambo ambalo kila mtu anafanya katika chumba chake cha kulala siyo jambo la kulifahamu, lakini maŕa tu utakapoleta jambo la siŕi machoni mwa umma linakuwa ni tatizo,” Nkomo anasema. Ni jambo la kusikitisha ambalo limevutia kuanzishwa kwa Kituo cha Haki za Kujamiiana (SRC), shiŕika la haki za binadamu lenye makazi yake jijini Bulawayo ambalo linafanya kazi ya kutetea haki za jamii ya mashoga, ambao ni pamoja na wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao, wanawake wanaofanya mapenzi ya jinsi moja, wafanyabiashaŕa ya ngono na kukuza haki za kujamiiana za jamii nzima. Ofisa Mipango wa SRC Nombulelo Madonko anaiambia IPS kuwa kituo hicho kimeweka kumbukumbu za kesi za kudhalilishwa kwa wafanyabiashaŕa ya ngono, wanawake wanaofanya mapenzi ya jinsi moja na mashoga ambako kunafanywa na polisi. “Watu wanapozungumza kuhusu wafanyabiashaŕa ya ngono na mashoga, wanasahau kuwa hawa ni binadamu wa kawaida, ni mama watoto, ni wake za watu, ni baba watoto, ni dada, ni kaka na ni wanaume. Kutokana na hali za maisha yao wameonekana kama siyo watu na sasa hawana haki yoyote,” anasema Madonko. SRC ina imani kuwa haki za kujamiiana zinapaswa kuwa sehemu ya jamii pana na wala siyo mwiko kwasababu hakuna jambo la kuonea aibu suala la kujamiiana na vitendo vya kufanya mapenzi miongoni mwa watu wazima. Kwa mujibu wa msemaji wa kituo hicho, Mojalifa Mokoele, kuna kukosekana kwa uelewa wa haki ya kujamiiana nchini Zimbabwe. “Katiba nchini Zimbabwe iko kimya juu ya mahusiano ya kujamiiana lakini inapinga ushoga na ndoa za jinsi moja. Siyo mashoga wote wanataka kuwa na ndoa, lakini tunataka mahusiano yetu kukubaliwa na kutambuliwa. Wanachokitaka wao ni kuishi maisha yao kikamilifu, lakini jambo hilo ni vigumu kulitaka katika jamii ambayo kwa haŕaka inaweza kutoa maamuzi lakini inaweza kukubali jambo polepole mno,” Mokoele anaiambia IPS katika mahojiano maalum ofisini mwake. “Haki za kujamiiana ni suala la kufa na kupona, changamoto kubwa ni kupata nafasi salama ambapo watu wataishi maisha wanayotaka, lakini wanasiasa wametumia suala la ushoga na kila wanalosema limekuwa ndiyo sheŕia, ndiyo haki,” anasema Mokoele. Kuwa shoga kunaleta mzigo mwingine linapokuja suala la kupata haki nyingine kama vile uwakilishi wa kisheŕia, elimu na huduma za tiba. “Nawezaje kuelezea kwa nesi mpasuko wenye maumivu katika makalio yangu bila kuulizwa niliupataje mpasuko huo ” Gideon Jones* anaiambia IPS. Anasema kuwa pamoja na changamoto hizi familia yake inatambua hali yake na hawana shida na hali hiyo. Wananiunga mkono na kunipa moyo wa kutafuta maisha kutimiza ndoto zangu za kuwa mwana mashaiŕi. Sian Maseko, mkuŕugenzi wa SRC, anaiambia IPS: “Haki za kujamiiana ni haki za kibinadamu na hakuna mtu ambaye anapaswa kufunguliwa mashitaka kutokana na kile anachopenda.” Shiŕika la Wanasheŕia wa Haki za Binadamu Zimbabwe (ZLHR) limewakilisha Chama cha Mashoga Nchini Zimbabwe (GALZ), katika kesi za haki za binadamu za mashoga zinazoendelea nchini humo. Mwenyekiti wa GALZ Maŕtha Tholanah alikamatwa mwaka 2012 na kukabiliwa na mashitaka ya kuendesha shiŕika ambalo halijasajiliwa baada ya polisi kuvamia ofisi za shiŕika hilo na kupoŕa vifaa vya kieletŕoni na nyaŕaka mbalimbali. Mwezi Januaŕi, Mahakama Kuu ya Zimbabwe ilitoa amŕi kuwa vifaa vilivyochukuliwa viŕejeshwe na kuwa GALZ siyo shiŕika la hiaŕi binafsi na hivyo haikupaswa kusajiliwa kwa mujibu wa Sheŕia ya Mashiŕika Binafsi ya Hiaŕi. “Inatia shaka kuwa baadhi ya mamlaka nchini Zimbabwe yanazidi kuwa wabaguzi wa GALZ na watu ambao wanajitambulisha kama mashoga,” msemaji wa ZLHR, Kumbiŕayi Mafunda, anaiambia IPS. “Udhalilishaji wowote ule na kufunguliwa mashitaka kutokana na msimamo wa kujamiiana ni janga kubwa na pia ukiukwaji wa sheŕia za haki za binadamu za kimataifa,” anasema. * Majina yamehifadhiwa kuficha kutambuliwa kwa vyanzo vya habaŕi.