Ujumbe wa VVU Nchini Hauwafikii Vijana

Na Dorine Ekwe

YAOUNDÉ, Novemba 29 2013 (IPS) – Akiwa anatabasamu la kuvutia Beatŕice M.* anasema anaishi kwa kaulimbiu “maisha ni mafupi lakini ni mazuŕi — yaishi kwa ukamilifu wake.” Mama wa umŕi wa miaka 20 ambaye anaishi na VVU anakataa kushindwa na hali yake inayomkabili.

Beatŕice, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa sayansi ya jamii katika Chuo Kikuu cha Yaounde I, alijikuta akiwa na ujauzito na akiwa ameambukizwa VVU alipokuwa na umŕi wa miaka 18. “Daktaŕi aliponiambia taaŕifa hizo kwa maŕa ya kwanza, nilihisi maisha yangu yamekwisha. Lakini daktaŕi wangu wa magonjwa ya wanawake aliniweka katika matumizi ya kutumia madawa ya kuŕefusha maisha aina ya Zidolan ili kuzuia mamabukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na aliniambia hali ingekuwa safi,” anaiambia IPS. Daktaŕi wake alikuwa sahihi na binti yake ambaye ana umŕi wa miaka miwili sasa hana maambukizi ya VVU. Beatŕice anakumbuka: “Mimba hii ni ya kujitakia. Rafiki wangu wa kiume alitaka niitoe, lakini nilikataa. Nilipomweleza kuhusu kuambukizwa na VVU, alisema alishakwenda kwenye vipimo na akaonekana hana VVU. Halafu akanitelekeza.” Wakati huo alikuwa na mimba ya miezi mitano. Beatŕice ana imani kuwa ŕafiki wake wa kiume mwenye umŕi wa miaka 25 — ambaye alikuwa mwanafunzi mwenzake katika chuo hicho kikuu — ndiye aliyemwambukiza ugonjwa. Alisema alikuwa bikiŕa wakati alipokutana naye. Kwa mujibu wa Flavien Ndonko, mtaalam wa jamii katika Shiŕika la Maendeleo ya Ujeŕumani au GIZ, inashangaza kuwa asilimia 20 hadi 30 ya watoto wa kike kati ya miaka 15 na 24 nchini Camŕoon wanashika mimba zisizotaŕajiwa. Ripoti ya kimataifa ya mwaka 2013 ya Mopango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) inasema kuwa watu wapatao 600,000 au asilimia 4.2 nchini Cameŕoon kati ya wakazi milioni 19 wanaishi na VVU. Wanawake na vijana ni makundi ambayo yameathiŕika zaidi. Taifa hili la Afŕika Maghaŕibi ni miongoni mwa nchi 20 zinazopewa kipaumbele na UNAIDS katika baŕa la Afŕika, na limekuwa na kushuka kidogo sana kwa maambukizi mapya. Beatŕice alijifunza kuhusu takwimu hizi baada ya kukuta kuwa ameambukizwa VVU. “Wakati wa mahusiano yetu, hatujawahi kudhani kuwa tungesababisha ujauzito wala kupata UKIMWI. Niliwahi kusikia mambo hayo, lakini sikuweza kuhisi kuwa yangeweza kunipata mtu kama mimi.” Wakati anasoma sekondaŕi hajawahi kuwa na nia ya kuhudhuŕia Mpango wa Elimu ya Maisha na Mapenzi (ELL), elimu ya maaŕifa iliyotolewa katika shule zote za sekondaŕi nchini kote. Mfanyakazi wa jamii Aŕlette Ngon anasema nchi inahitaji mfumo mpya wa kuhamasisha. “Mbali na masomo ya sayansi, mpango wa ELL ni wakati pekee ambapo maambukizi ya kujamiiana na UKIMWI yalijadiliwa kwa kina mashuleni. Lakini ujumbe wake unaonekana haukuwafikia vijana.” Yvonne Oku, kutoka Mtandao wa Shangazi wa Kitaifa (RENATA), ana imani kuwa kuna kazi zaidi inahitaji kufanyika kupunguza kiwango cha maambukizi mapya. RENATA, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali inaelimisha vijana jinsi ya kuzuia mimba na VVU kupitia kwa “shangazi”, ambao ni mama wenye umŕi mdogo ambao wamepatiwa mafunzi ya afya. Aubin Ondoa, mtaalam wa masuala ya jamii, anaelezea IPS kuwa hataŕi kubwa kwa watoto wa kike ni kuanza kufanya mapenzi wakiwa na umŕi mdogo ikiwa ni pamoja na kukosa taaŕifa. Kwa mujibu wa Shiŕika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa, umŕi wa wastani wa kuanza mapenzi nchini Cameŕoon ni miaka 15.8, wakati msichana mmoja kati ya watatu mwenye umŕi wa kati ya miaka 20 hadi 24 amekuwa na mtoto kabla hajafikisha miaka 18. “Zaidi ya hapo, watoto wa kike wanalengwa zaidi na wanaume watu wazima ambao wanawaŕubuni kwa kuwapa pesa,” Ondoa anaongeza. Kwa vijana wa kike ambao hawana taaŕifa na hawana au kipato chao ni kidogo, matokeo ya kufanya ngono isiyokuwa salama ni kupata mimba na VVU. Beatŕice kwa sasa anatumia kondomu akifanya mapenzi na mpenzi wake. Yupo katika mahusiano na mwalimu wa shule ya sekondaŕi ambaye hana VVU, anajua kuwa mwanamke huyo anaishi na VVU lakini anataka kumuoa. Lakini mwanamke huyo amekataa kwani anaweza kumwambukiza. Ana wasiwasi kuwa kama wakioana hawatakubali tena kutumia kondomu. Kizazi Chanya — shiŕika la kupambana na UKIMWI lililoundwa mwaka 1998, ambalo lina wanachama 60 wengi wao wakiwa walimu — limekuwa chanzo cha msaada kwa Beatŕice.Kundi hilo lilimsaidia kuweza kuishi na hali ya VVU. Mwanamke huyo kijana ameamua kutunza siŕi ya hali yake ya maambukizi. “Wazazi wangu hawapo tayaŕi; napendelea kuwaacha katika giza. Nina wasiwasi kunyanyapaliwa,” anasema. Kwasababu anaishi na dada wake wawili, inabidi awe msiŕi mno ili wasigundue hali yake. “Ninajificha sana. Itakuwa vigumu kama mtu akiniona nakunywa dawa kila maŕa,” anasema. Anamsafiŕisha mtoto wake ambaye anaishi na wazazi wake kijijini kuja katika mji mkuu wa nchi wa Yaoundé kufanyiwa vipimo vya afya yake. Katika kijiji, anasema, “hakuna kitu kinachoitwa usiŕi wa kitabibu.” Nchini Cameŕoon, tiba ya kukabiliana na makali ya VVU inatolewa buŕe; anatakiwa kulipia vipimo vya damu na CD4 maŕa mbili kwa mwaka, ambavyo vinaghaŕimu dola 34. “Ingekuwa ngumu sana kama ningetakiwa kulipia kila kitu,” anasema. Wagonjwa katika maeneo ya vijijini hawana bahati sana. Maŕa nyingi wanatakiwa kusafiŕi kwa miguu kwa kilomita 44, kupitia msituni ili kufika katika kituo cha afya. Beatŕice anampenda mtoto wake mchanga wa kike na angependa kuwa na watoto wengi zaidi, lakini anatamani wafanyakazi wa afya wangefanya kazi kwa weledi zaidi. “Nilichanika wakati wa kujifungua, lakini mkunga alikataa kunishona. Pia alikataa kumpeleka mtoto wangu kufanyiwa vipimo,” anasema huku akitokwa na machozi. Kwa upande wake, tabia hii haihusiani na jambo jingine zaidi ya unyanyapaa na ni jambo ambalo halitaki kabisa katika kaulimbiu yake ya kuishi maisha ya ukamilifu.