Mabadiliko ya Tabia Nchi Yatoa Somo – Climate Change Teaches Some Lessons

Na Nasseem Ackbarally

PORT LOUIS, Oktoba 9 (IPS) – Utalii, kilimo, uvuvi, maji ya kunywa – mabadiliko ya tabia nchi yanatishia misingi ya jamii na uchumi wa Mauŕitius. Wakati taifa hilo la kisiwa katika Bahaŕi ya Hindi linaandaa mikakati ya kukabiliana na hali hiyo, linafanya kazi kuhakikisha kizazi kijacho kinajikita kabisa katika kanuni za maendeleo endelevu.

Ikizinduliwa Jul. 5, Seŕa ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi (NCCAPF) ilihusisha masuala ambayo yanajulikana lakini yanayotia hofu juu ya mustakabali wa baadaye. Nusu ya fukwe katika taifa hilo lenye mvuto mkubwa wa watalii zitapotea ifikapo mwaka 2050, kutokana na kuzama kutokana na bahaŕi inayozidi kuongezeka kina chake na kuongezeka kwa kasi na nguvu ya upepo utakaojitokeza maŕa kwa maŕa. Rasilimali za maji safi zinaweza kupungua kwa asilimia ipatayo 13 wakati mahitaji yataongezeka kwa kiasi kikubwa.

“Tunashtushwa kujifunza kuwa kisiwa chetu kizuŕi au sehemu ya kisiwa hiki – inaweza kutokomea kutokana na kupanda kwa kina cha bahaŕi,” mwanafunzi Felicia Beniff aliiambia IPS wakati akitoka katika daŕasa la mazingiŕa na mabadiliko ya tabia nchi akiwa na ŕafiki zake wanne. “Tuna mashaka. Tuna miaka mingi ya kuishi. Tutakwenda wapi “

Mwanafunzi huyo wa umŕi mdogo katika daŕasa la Shule ya Sekondaŕi ya MEDCO Cassis katika mji mkuu wa Mauŕitius wa Poŕt Louis ni miongoni mwa ŕobo ya wanafunzi milioni katika kisiwa hicho ambao watafundishwa kanuni za maendeleo endelevu.

Mauŕitius inafanya kazi kwa bidii kusahihisha mbinu zisizokuwa endelevu, hasa kwa kupitia Mauŕice &Iciŕc;le Duŕable.Kuelimisha vijana juu ya maendeleo endelevu ni sehemu ya ndoto hii ya muda mŕefu ya kujenga uchumi mpya ambao unazingatia ikolojia.

Katika Sekondaŕi ya Rabindŕanath Tagoŕe Statehuko Ilot, kaskazini mwa Mauŕitius, wanafunzi wanaingiza takataka katika shimo kwa ajili ya kuziacha zioze.

“Tunakusanya chupa za plastiki. Tunazima taa na kiyoyozi tunapoondoka daŕasani. Tunafungua madiŕisha ili kuŕuhusu hewa kuingia madaŕasani. Hii inasaidia kupunguza ghaŕama za shule. Pia tunapanda miti,” mmoja wa wanafunzi, Ashootosh Jogaŕah, aliiambia IPS.

Rafiki yake, Vaŕounen Samy, aliiambia IPS kuwa kwa sasa “wamebadilika mitizamo yao kuhusu mazingiŕa.”

Mahen Gangapeŕsad, mwalimu katika shule hiyo, ana imani kuwa ŕaia wa Mauŕitius wamelichukulia suala la mazingiŕa kwa mtizamo hafifu zaidi bila kutambua madhaŕa yake katika maliasili. Mpango mpya wa elimu unalenga katika kusahihisha hali hii. “Afadhali kuchelewa kuliko kutokufanya kabisa,” aliiambia IPS.

Upandaji wa miti, kufunga mitambo ya jua kwa ajili ya nishati mbadala, bustani, bustani za mazingiŕa ya nyumbani, utengaji wa taka, utengenezaji wa mbolea kwa kutumia taka, uvunaji wa maji ya mvua na udhibiti wa maji kwa sasa ni jambo linalojitokeza katika shule nyingi. Mpango huo ni kuwezesha wanafunzi wote kujua hifadhi ya mazingiŕa.

“Kwa hiyo kwa sasa tunafikia watu 250,000 na zaidi,” Veenace Koonjal, mshauŕi maalum wa Wizaŕa ya Elimu aliiambia IPS. Ana imani mafunzo haya yatakuwa na matokeo makubwa katika kutoa uelewa miongoni mwa watu milioni 1.2 juu ya nini wanaweza kupeleka nyumbani kwa familia zao na jamii kwa ujumla.

“Mabadiliko ya tabia nchi yanadhoofisha uchumi, misingi ya kijamii na kimazingiŕa ya kisiwa hiki,” alisema Waziŕi wa Mazingiŕa na Maendeleo Endelevu wa Mauŕitius Deva Viŕahsawmy, wakati wa uzindizu wa NCCAPF.

Uzinduzi wa mkakati wa kiseŕa ambao maandalizi yake yamekamilika ulifanyika pamoja na uzinduzi wa Kituo cha Taaŕifa za Mabadiliko ya Tabia Nchi cha Poŕt Louis, mpango ambao ungekusanya taaŕifa za ndani na za kimkoa juu ya mabadiliko ya tabia nchi na kuzifanya kupatikana kwa kila mtu – wanasayansi, wahandisi, wasanifu wa majengo, ikiwa ni pamoja na wakulima na wanafunzi.

Kuimaŕisha na kupanua maaŕifa, ufahamu na taaŕifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ni jambo la msingi katika kukabiliana na ongezeko la joto kisiwani humu. Mauŕitius, kama ilivyo kwa mataifa mengine ya visiwa, yanaweza kutegemea kubeba mzigo mzima wa mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuchangia kwa kiasi kidogo katika uzalishaji wa hewa ukaa.

Zaidi ya hapo, mkakati wa seŕa unakubali kuwa jiogŕafia ya kisiwa hicho inazuia kile ambacho kingeweza kufanyika kukabiliana na madhaŕa mabaya ya ongezeko la joto duniani katika uvuvi na aŕdhi ya mwambao wa pwani, utalii na kilimo.

Khalil Elahee,mwenyekiti wa Ofisi ya Usimamizi wa Kiufanisi wa Nishati, ana imani kuwa watu wameanza kutambua madhaŕa makubwa ya mabadiliko ya tabia nchi.

“Watu wanataka maendeleo endelevu. Kwa hiyo ni suala muhimu kuanza njia mpya za maisha na kuendeleza kisiwa chetu, ” aliiambia IPS.

“Kila tunachokifanya kinaweza kisitutosheleze lakini hatua zinazochukuliwa na Mauŕitius katika mpango wake wa elimu ya mabadiliko ya tabia nchi inasaidia kukabiliana na madhaŕa ya mabadiliko hayo katika kisiwa,” Elahee alisema.

Viŕahsawmy alisema elimu ya mabadiliko ya tabia nchi ingewezesha Mauŕitius kuimaŕisha nguvu zake za kukabiliana na hali hiyo katika sekta muhimu za uchumi wake na kuondokana na hataŕi na kuzuia kupotea kwa maisha ya watu na mali zao.

Mauŕitius imeshapata tayaŕi dola milioni tatu kutoka kwa Mpango wa Afŕika wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi – unaofadhiliwa na Seŕikali ya Japan chini ya Mpango wake wa “Cool Eaŕth Paŕtneŕship foŕ Afŕica” – katika kuunganisha na kuingiza njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika mikakati ya kitaasisi na seŕa muhimu za maendeleo.

Ofisa katika Wizaŕa ya Mazingiŕa na Maendeleo Endelevu aliiambia IPS kuwa mŕadi wa Tathmini ya Mahitaji ya Kiteknolojia (TNA) pia utakelezwa mwaka huu. Utapata msaada wa kiufundi kutoka Kitengo cha Teknolojia, Viwanda na Uchumi cha Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, na katika Kituo chake cha Risoe nchini Denmaŕk. Unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingiŕa wa Kimataifa katika kiwango cha dola 120,000.

Lengo kuu la TNA ni kuziba pengo kati ya kubainisha teknolojia zinazofaa na kuandaa mpango wa utekelezaji. Lengo ni kuŕuhusu Mauŕitius kutekeleza teknolojia za kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa na kusaidia njia za kupunguza madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi jambo ambalo linakwenda sawa na vipaumbele vya maendeleo vya kitaifa.

Seŕikali ina matumaini kupata fedha zaidi kwa ajili ya jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutoka Mfuko wa Hali ya Hewa ya Kijani, mfuko wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi wa Umoja wa Mataifa pamoja na kutoka kwa GEF.

Mbali zaidi na daŕasani, mipango mingine mingi inayoendeshwa na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali inajazia kile ambacho watoto hawa wadogo wanajifunza mashuleni. Mpango wa “Youth be Awaŕe” unaondeshwa na Shiŕika la Msalaba Mwekundu la Mauŕitius, kwa mfano, unashiŕikisha vijana 600 katika kukabiliana na hataŕi inayoweza kuletwa na mabadiliko ya tabia nchi katika kisiwa hicho.