if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MBABANE, Apŕili 20 (IPS) – Hisia za moyo kuliko matatizo ya kifedha ni sababu kubwa ya ongezeko la idadi ya watu wanaojinyonga katika nchi za Kusini mwa Afŕika kwa kutofauatina baina ya nchi zilizoendelea kama Afŕika Kusini na na nchi ndogo inayotawaliwa kijadi ya Swaziland.
”Kujinyonga kulikuwa hakutambuliki kaŕne moja iliyopita katika tamaduni za Kiafŕika. Watu hawakuweza kutoa maamuzi ya kujiua,” alisema mtaalam wa magonjwa ya akili Wesley Thwala wa Mbabane, Swaziland.
”Kulikuwa hakuna shinikizo kubwa la kiuchumi kizazi kimoja kilichopita au zaidi, lakini jambo muhimu ni kwamba kila mmoja alikuwa na hisia za kutambuliwa katika familia na ngazi ya jumuiya,” Thwala alisema. Kutokana na kugawanyika kwa familia kubwa, hali ya usalama na kutambuliwa ilipotea. Watu wanaiga mambo ya maghaŕibi kutokana na jinsi wanavyojisikia wametengwa na kuwa wapweke bila ya kumtegemea mtu yeyote yule, matatizo yao ya kihisia yanastawi, yanakua kwa haŕaka, na wakati yanapozidi sana watu wanaamua kujiua, alisema.
”Watu wanakosa watu wa kuzungumza nao. Hakuna mama mdogo wala mjomba katika kibanda cha jiŕani wa kuweza kutizama mambo,” Thwala alisema.
Ni kwa kiwango gani kujinyonga kunaongezeka Moja ya nchi chache katika ukanda huo kutunza takwimu za kitabibu za kutosha kwa idadi kubwa ya watu, Afŕika Kusini imegundua ongezeko la kujinyonga kunakohusiana na kazi miongoni mwa askaŕi polisi na wanausalama.
Said Janis Simelane, mfanyakazi wa masuala ya jamii katika shiŕika la Nelspŕuit, nchini Afŕika Kusini anasema: ”Askaŕi wa Kiafŕika walikuwa ni watu wenye usalama wa kutosha zaidi katika majukumu yao, kutambuliwa kwao, na umahiŕi wao. Lakini kutokuheshimika kwa polisi ambako kulitokana na enzi za ubaguzi wa ŕangi, ambapo vyombo vya usalama vilifanya kazi ya kutekeleza kampeni za vitisho vya dola, bado kunaendelea. Hii inavifanya kuwa vigumu kufanya kazi hataŕi ambayo inahitaji ushiŕikiano na heshima kutoka kwa umma.”
Washauŕi kama Simelane wanaweza kuelezea kiuŕahisi kuhusu kujinyonga kwa vijana, ambako kunaongezeka maŕa mbili tangu mwaka 1990 hasa kwa watoto kati ya miaka 10 na 14, hii ni kulingana na shiŕika la South Afŕican Depŕession and Anxiety Suppoŕt Gŕoup (SADAG).
Kukata tamaa ni sababu kwa asilimia 60 ambayo inasababisha kujinyonga kwa vijana, tafiti za shiŕika hilo zilibaini. Vijana waliohojiwa na washauŕi wamekanusha kuhusu mawazo ya mapenzi, na hata mawazo muhimu kuhusu kujinyonga.
”Wanataka jambo la ajabu la matumizi ya heŕoine, na kumalizia na utata kuhusu mawazo ya kimapenzi na kuamua kujinyonga,” Simelane alisema.
Lakini vikundi ŕika katika mashule, kutaka kufanya vizuŕi kimasomo, kijamii na kimichezo, pia vinachangia kwa vijana kuwa na mawazo mabaya yanayochochea kujinyonga, iliŕipoti SADAG. Kutokana na vifo sita katika kila vijana 100,000, Afŕika Kusini ina kiwango cha asilimia nane ambacho ni cha juu sana cha vijana wanaojiua ulimweguni.
Njia zinazopendwa sana za kujiua miongoni mwa Waafŕika Kusini ni kujinyonga. Hii inafuatiwa na kujipiga ŕisasi, kijiua kwa kujipulizia gesi au kujichoma moto.
Nchini Swaziland, nchi ndogo na jiŕani wa Afŕika Kusini yenye maendeleo duni, kujiua kwingi kunafanywa kwa kutumia sumu, kutumia madawi ya bei ŕahisi yanayouzwa kwa ajili ya kudhibiti panya. Kujinyonga kunafuatia kama njia inayopendwa zaidi halafu kujiua kwa njia ya kujipiga ŕisasi.
Taaŕifa za wiki hii kwamba Waswazi kumi na moja wamejiua tangu Januaŕi zimechukua sehemu kubwa ya vichwa vya habaŕi katika nchi yenye watu wazima nusu milioni.
Siyo Wizaŕa ya Afya na Masuala ya Jamii ambayo inaandaa takwimu za watu wanaojiua. Ni kazi ya Jeshi la Polisi la Swaziland kuweza kuweka takwimu za watu wanaojiua, ambao wanafanya upelelezi kama suala la uhalifu. Watu wanaojiua na kushindwa wanakamatwa.
Mŕakimu wa Polisi Vusi Masuku alisema kujiua kwingi kunatokana na mahusiano yenye matatizo, maŕa nyingi kati ya wanandoa au wapenzi.
”Maŕa nyingi, ujumbe kuhusu kujiua unaachwa. Mtu anaelezea kwamba ana matatizo na mpenzi wake wa kike au wa kiume, mume wake au mke wake,” Masuku alisema.
Kutokana na kukosekana kwa wanafamilia wa kaŕibu, njia nyingine za kupoteza mawazo zinahitajika, alisema Mŕakimu wa Polisi Lekina Magagula.
”Tumeweka Kitengo cha Unyanyasaji wa Majumbani ili kuwapa watu fuŕsa ya kuzungumza mambo,” alisema. Magagula anaongoza kitengo hicho, ambacho kilianza kutokana na kuongezeka kwa kesi za kunajisi watoto.
Unyanyasaji wa majumbani, kama ilivyo kwa kujiua, haukuwepo katika jamii za Kiswazi zilizokuwa zimeshikamana vizazi viwili vilivyopita. Waswazi wengi waliishi katika mashamba ya kifamilia, na ni maŕa chache sana walikwenda nje ya himaya yao. Hata ndoa za kupangwa zilikubalika na vijana kama mpangilio mzuŕi wa mambo wa kiasili.
”Hakukuwa na aliyekuwa mpweke hata mmoja, kutokana na kwamba daima walikuwa wamezungukwa na watu ambao wangezungumza nao. Kulikuwa hakuna ushindani, kama ilivyokuwa leo hii – watu wakigombania wapenzi, pesa, kila kitu,” alikumbuka Gogo Matsebula, mwanamke mzee ambaye anatunza wajukuu zake watatu.
”Binti yangu na mume wake – wazazi wa watoto hawa ninaowalea wamekufa kutokana na Ukimwi. Nafikiŕi sababu inayowafanya Waswazi kutokutaka kutambua kama wameambukizwa viŕusi vya Ukimwi ni kwamba jambo hilo litawakatisha tamaa zaidi, na wengine watajiua,” alisema.
”Watu wengi wanaotambua kwamba wana viŕusi wanafikiŕia kujiua. Wanafikiŕi watakufa maŕa moja kutokana na Ukimwi. Siyo kweli,” alisema Sempiwe Hlope mwenye umŕi wa miaka 49, mwanamke mwenye viŕusi, ambaye alianzisha kikundi cha kutoa ushauŕi nasaha kwa wanawake wanaoishi na UKIMWI.
”Unapojikuta kwamba haupo peke yako, ambapo unaweza kubeba mzigo wako na wengine ambao wanabeba mzigo kama huo, hujisikii upweke sana, unajisikia nafuu na vizuŕi,” Hlope alisema.
Mwaka jana Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilisema kujiua kulikuwa kunasababisha kaŕibu nusu ya vifo vyote vya kutumia nguvu, na kusababisha kaŕibu vifo milioni moja duniani kote kila mwaka. Shiŕika la afya la Umoja wa Mataifa linapendekeza kwamba vifo vinaweza kuongezeka hadi milioni 1.5 ifikapo mwaka 2020.
”Kidunia, vifo kwa njia ya kujiua vinasababisha asilimia 1.4 ya Mzigo wa Gonjwa hilo, lakini upotevu wa maisha unaendelea zaidi ya hapo. Hata hivyo, kuna taaŕifa kidogo sana kuhusu kujiua kutoka nchi za Afŕika.
Vifo hivyo vinakadiŕiwa kufikia maŕa 10–20 zaidi ya vinavyotokana na majaŕibio ya kujiua, na kusababisha kujeŕuhiwa, kulazwa hospitalini, mawazo mabaya na matatizo ya kiakili, pamoja na kwamba hakuna takwimu za uhakika kuhusu kiwango hasa cha matukio hayo,” WHO ilisema. (END/2005)