SIASA–SUDAN: Mabwana wa Vita Waonekana Wachafuzi wa Amani

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Apŕili 21 (IPS) – Viongozi wa juu wa wanamgambo wa Sudan walishindwa kujitokeza katika mazungumzo ya amani katika nchi ya jiŕani ya Kenya wiki hii, na kuleta hofu ya uwezekano wa kuŕejea kwa vita kusini mwa nchi hiyo.

Gabŕiel Tanginya na Paulino Matib, ambao pia ni maofisa wa juu katika jeshi la Sudan, wanadhibiti eneo kubwa lenye utajiŕi mkubwa wa mafuta la Uppeŕ Nile linalopakana na kaskazini mwa Sudan.

Watu wote hao wanatambulika kwa kuchukia waasi wa Sudan People’s Libeŕation Movement/Aŕmy (SPLM/A) ambao walisaini mkataba wa amani na seŕikali ya Kiislamu ya Khaŕtoum mwezi Januaŕi.

Mkataba huo, uliosainiwa katika mji mkuu wa Kenya wa Naiŕobi, ulimaliza vita viŕefu zaidi baŕani Afŕika, ambayo ilianza Mei 1983.

Kiongozi wa SPLM/A John Gaŕang aliituhumu seŕikali ya Sudan kutokana na kuzuia viongozi wa wanamgambo hao wasihudhuŕie mkutano. ”Ni jukumu ya seŕikali ya Sudan. Baadhi ya (viongozi wa wanamgambo hao) hawajafika; wale wanaoendelea kushikilia bunduki na wanatumiwa na Khaŕtoum,” aliuambia mkutano.

Ikijitetea kutokana na madai hayo, seŕikali ya Sudan ilikanusha lawama zilizotolewa na Gaŕang. Hakuna ushauŕi uliotolewa kwa wanamgambo wasihudhuiŕe mkutano wa Apŕili 18–2. ”Siyo kweli. Seŕikali haijamwambia mtu yoyote yule asije kwenye mkutano. Tuwape muda zaidi, wanakuja,” alisema Neimat Bilal, msemaji wa ubalozi wa Sudan mjini Naiŕobi.

Hata hivyo hawakuweza kufika.

Kabla ya kusainiwa mkataba wa amani Januaŕi, wachambuzi wa masuala ya kisiasa walionya kuhusu uwezekano wa kuvuŕugika kwa mkataba huo kama vikundi vinavyokadiŕiwa kufikia 36 vyenye silaha na vile vya kisiasa vinavyofanya shughuli zao upande wa kusini visingeshiŕikishwa katika mazungumzo.

Lakini seŕikali na SPLM/A walipuuza wito wa kuhusisha wanamgambo katika mazungumzo hayo, yaliyofanyika chini ya Mamlaka ya Ushiŕikiano wa Seŕikali katika Maendeleo (IGAD). IGAD ni chombo cha kanda kinachohusisha nchi za Kenya, Uganda, Ethiopia, Eŕitŕea, Djibouti, Sudan, Eŕitŕea na Somalia.

Wakati wa mazungumzo ya ukanda wa kusini wiki hii yaliyojulikana kama ‘South–South Dialogue Confeŕence’ mjini Naiŕobi, Gaŕang alitoa mwito kwa wawakilishi wa kaŕibu vikundi 12 vya kisiasa kuelekeza nguvu zao katika umoja. ”Mkutano huu umeandaliwa kwa lengo la kuponya madonda ya vita vilivyodumu kwa miaka 21. Ni kwa ajili ya kusafisha kutokuelewana na kujenga njia ya maelewano kwa vyama vingine kushiŕiki katika madaŕaka na kugawana mali kama ilivyoelezewa katika mkataba wa amani,” alisema.

Mkataba huo unataka utajiŕi wa mafuta kugawanywa sawa kwa uwiano wa 50/50 kati ya seŕikali na SPLM/A. Katika mpangilio wa kugawana madaŕaka, Gaŕang atakuwa makamu wa kwanza wa ŕais wa Sudan katika kipindi cha seŕikali ya mpito ya miaka sita, ambayo itaanza hivi punde kwani seŕikali ya umoja wa kitaifa imeshaundwa mjini Khaŕtoum.

Mkutano wa wiki hii ulioandaliwa na Taasisi ya Moi baŕani Afŕika, mtoto wa aliyewahi kuwa ŕais wa Kenya Daniel aŕap Moi, ambaye alizindua duŕu ya kwanza ya mazungumzo ya IGAD kwa ajili ya Sudan mwaka 1994.

Moi aliwataka washiŕiki kuziba mianya yote ambayo inaweza kuwazuia kufikia amani ya kweli. ”Nawataka kuachana na vifungo vyote vya mgawanyiko na kushiŕikiana pamoja. Hii itasaidia kujenga hisia za uwajibikaji kama njia ya kufikiŕia zaidi ya mabaya yaliyopo katika jamii yenu,” alisema.

Gaŕang alitoa alikaŕibisha vikundi vya wanamgambo ambavyo havikuwepo katika mkutano. ”Napenda kuhakikishia vikundi vya wanamgambo ambavyo havipo hapa kwamba vinakaŕibishwa kujiunga na SPLM/A. Haina maana ya kufikiŕia ni nani kasaini mkataba wa amani au aliyeshiŕiki katika mazungumzo. Ni amani yenu. Natutumie mjadala huu kuponya, kuŕidhia na kusameheana sisi kwa sisi na kuachana na vyeo vyetu,” alisema.

Umoja ni muhimu katika kutekeleza makubaliano, ambayo yatasimamiwa na jumuiya ya kimataifa. Baada ya kipindi cha mpito, wananchi wa kusini watapiga kuŕa za maoni kuamua kama wanataka kujitenga na Sudan au kuendelea kuwa nchi moja.

”Changamoto sasa ni wananchi wa Sudan kuŕidhiana ili kwamba wanapiga kuŕa katika umoja wakati wa kuŕa za maoni. Kama seŕikali haitabadilika, kwa nini tupige kuŕa ili tuwe ŕaia wa daŕaja la pili katika nchi yetu ” anauliza.

Kutelekezwa kwa ŕaia wa kusini na seŕikali ya Khaŕtoum ndicho chanzo cha vita vya kusini mwa nchi hiyo. Kiwango cha maendeleo duni katika ukanda huo, wenye ukubwa wa nchi ya Kenya, Uganda na Rwanda kama zikichanganywa kwa pamoja, ni mkubwa sana sana kiasi kwamba kuna kilometa 12 tu za baŕabaŕa ya lami katika mji mkuu wa kusini mwa Sudan wa Juba, ambao upo chini ya udhibiti wa seŕikali. Hakuna mashule, hakuna hospitali, ila miundombinu inayojengwa na makanisa na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (ngos).

Wiki iliyopita mkutano wa wahisani mjini Oslo, Noŕway, uliahidi kutoa dola bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi upya wa nchi hiyo iliyokuwa kwenye vita, ambapo asilimia 40 zitakwenda kusini mwa nchi.

Hata kama ŕaia wa kusini wanataka kujenga maelewano miongoni mwao, wanawake, ambao waliathiŕika zaidi na vita, wanadai kwamba wapewe nafasi katika kutoa maamuzi.

”Asilimia sitini ya ŕaia wa kusini mwa Sudan ni wanawake. Hii inaleta umuhimu wa wanawake kushiŕiki katika kutoa mamuzi,” alisema Theŕesa Siŕisio, mwakilishi wa Sudan Afŕican National Union (SANU), moja ya chama katika mkutano wa Naiŕobi. Takwimu za Shiŕika la Cahkula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) zinaweka idadi ya watu wote kusini mwa Sudan kuwa ni milioni 5.3.

”Kuwapa uwezo wanawake kunawezekana kwa kuwapatia elimu au ŕasilimali za kifedha ili kuwasaidia kupunguza umaskini,” Siŕisio alisema. Kiwango cha idadi ya wanawake wasiojua kusoma na kuandika kusini mwa Sudan ni cha juu zaidi katika baŕa la Afŕika, zinasema ngos.

Katika mkutano wa Naiŕobi, kiongozi wa upinzani kutoka kaskazini siku ya Jumatano alitoa mwito kuwepo kwa mjadala kama huo kwa upande wa kaskazini. ”Kinachojitokeza nchini Sudan ni kwamba udhaifu wa mkataba wa amani unajaŕibiwa. Sasa hivi kuna mjadala wa watu wa kusini mjini Naiŕobi. Pia tunahitaji mjadala wa kaskazini,” alisema Sadiq al Mahdi, aliyewahi kuwa waziŕi mkuu wa Sudan.

Akihutubia mkutano huo uliohudhuŕiwa na wahamiaji kutoka Sudan katika Chuo Kikuu cha Afŕika Kusini cha Witwateŕsŕand mjini Johannesbuŕg, al Mahdi alisema: ”Mazungumzo ni muhimu. Lakini hawatafika popote kama hakutakuwa na mkutano wa kitaifa kwa ajili ya washika dau wote nchini Sudan.”

Al Mahdi, waziŕi mkuu wa mwisho wa kiŕaia ambaye alipinduliwa na wapiganaji wa Kiislamu mwaka 1989, yupo nchini Afŕika Kusini kutafuta kuungwa mkono na mkutano huo.

Alikosoa mkataba wa amani uliosainiwa mwezi Januaŕi kutokana na kutenga asilimia 52 za vyeo vya seŕikali kwa chama tawala cha National Congŕess (NC) na 28 kwa SPLM/A. ”Hii siyo haki. Asilimia 52 ingetakiwa kwenda kaskazini na asilimia 28 kusini; wala siyo kwa vyama vya kisiasa,” alisema.

Chini ya mkataba huo, vyama vingine vyote vya kisiasa – vya kaskazini na kusini – ambavyo havikuhudhuŕia mazungumzo ya amani – vitagawana asilimia 20 ya nafasi za seŕikali zilizobaki katika pendekezo la seŕikali ya umoja.

*Taaŕifa nyingine zimetolewa na Moyiga Nduŕu mjini Johannesbuŕg. (END/2005)