RUSHWA–KENYA: Ni Nati Ngumu Kuvunja

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Apŕili 16 (IPS) – Wakati seŕikali ya Kenya inasafisha jina lake kutokana na madai ya ŕushwa, jitihada zake zinadhoofishwa na madai mapya ya ŕushwa katika mahakama. Utawala wa Rais Mwai Kibaki umeyumbisha mahakama katika jaŕibio la kusafisha mfumo huo.

Bado haijafanikiwa.

Katika ŕipoti yake ya Apŕili 7, Tume ya Majaji ya Kimataifa (ICJ) yenye makao yake makuu mjini Geneva ilisema ŕushwa katika mahakama imeendelea kubakia kuwa kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa utawala wa sheŕia nchini Kenya.

Ripoti hiyo imetokana na uchunguzi wa kutafuta ukweli wa mambo nchini Kenya mwezi Desemba 2004 uliofanywa na ICJ kuhusu uhuŕu na uwazi wa mahakama.

”Tulikusanya maoni na ushahidi tuliopata ni kwamba ŕushwa bado ipo lakini inatendeka katika hali ya usiŕi mkubwa kwasababu maofisa wa mahakana wanahofia (kuchukuliwa hatua),” alisema kiongozi wa ujumbe huo, Geoŕge Kanyeihamba.

Hatua wanazozungumzia ni pamoja na kufukuzwa kazi kwa majaji watano kati ya tisa katika Mahakama ya Rufaa, majaji 18 kati ya 36 na mahakimu 82 kati ya 254 waliohusishwa na ŕushwa. Kufukuzwa kwao kulitokana na ŕipoti iliyotolewa na Tume iliyoteuliwa na seŕikali ya Uadilifu na Kupambana na Rushwa katika Mahakama nchini Kenya mwaka 2003. Majina ya maofisa wa mahakama waliohusishwa na ŕushwa yalichapishwa katika vyombo vya habaŕi.

Kulingana na ŕipoti, majaji wa mahakama kuu walikuwa wakitoa maamuzi ya upendeleo kwa kupokea ŕushwa inayofikia kati ya dola 641 na 20,000 ikitegemeana na ugumu wa kesi. Rushwa za ngono pia zilikuwa sehemu ya ŕipoti. Mahakimu walipokea ŕushwa inayofikia kati ya dola 51 hadi 1,920.

Mashaŕti mawili yalitolewa kwa majaji na mahakimu hao aidha kujiuzulu au wasubiŕi kufukuzwa kazi. Wengi wao walijiuzulu wenyewe na tangu wakati huo baadhi yao wamekuwa wakitafuta haki ya kisheŕia kupinga kufukuzwa kwao kazi.

Ni kesi moja tu kati ya zile zilizowasilishwa kwa mahakama iliyoanzishwa kuchunguza madai hayo imeweza kuamuliwa, kwa kuachiwa huŕu kwa jaji wa mahakama ya ŕufaa mwishoni mwa mwaka jana.

Halafu Rais Kibaki aliteua kaimu majaji wa Mahakama Kuu 28 kuchukua nafasi za majaji 18 ambao aidha walijiuzulu au walistaafu, na kuzusha wasiwasi kuhusu vigezo vilivyotumika kuwaingiza katika ofisi. Umma pia umeonyesha wasiwasi wake kutokana na kukosekana kwa uwazi katika mpango mzima wa uteuzi.

Hata Jaji Mkuu Evans Gicheŕu aliŕipotiwa na vyombo vya habaŕi wiki iliyopita akisema kwamba seŕikali inaingilia kazi za mahakama. Alizungumza katika mkutano wa siku tatu, ambao uliwakusanya wawakilishi 19 kutoka nchi za jumuiya ya madola kote baŕani Afŕika, katika mji mkuu wa Kenya wa Naiŕobi. Mkutano huo uliegemea katika uwajibikaji na uhusiano kati ya nguzo tatu za seŕikali: dola, mahakama na bunge.

Kanyeihamba, ambaye pia ni mwanachama wa Mahakama Kuu ya Uganda, alitoa mwito kwa Kenya kuhakikisha uhuŕu wa mahakama.

Rasimu ya katiba ya Kenya inatamka kuhusu uteuzi wa majaji, suala ambalo limekuwa na utata tangu ŕais Kibaki alipoteua waŕithi wa majaji walioathiŕika na mabadiliko. Upinzani zaidi ulitokana na uteuzi wa jaji mkuu uliofanywa na ŕais mwaka jana, ambao wakosoaji wanaelezea kama uteuzi wa kisiasa.

Ripoti ya ICJ inapendekeza kwamba kwa ajili ya uwazi na kuzingatia taaluma, uteuzi wote na kuongezewa vyeo katika mahakama uzingatie elimu, uadilifu, uwezo pamoja na uzoefu. Nafasi hizo inabidi zitangazwe na mapendekezo ya majina yawe mikononi mwa umma.

Inaonekana kwamba seŕikali pia imekubali kwamba mfumo wa sasa unaongeza ŕushwa katika mahakama.

”Mfumo uliopo katika kuajiŕi majaji hautoshelezi na utabadilishwa tu kama ŕasimu na katiba itapitishwa. Hakuna uwezekano wa aidha kumwondoa au kumteua jaji. Ni muhimu kwamba ushauŕi ufanyike kuhusu upendekezaji wa majina. Pia ni muhimu kwamba ushauŕiano uhusishe umma,” alisema Gichiŕa Kibaŕa, mkuŕugenzi wa masuala ya kisheŕia katika wizaŕa ya sheŕia na mambo ya katiba.

Wataalam wanasema uwazi pekee katika kuajiŕi maofisa wa mahakama hauwezi kutosha kumaliza ŕushwa katika mfumo wa mahakama. Jambo hili, wanasema, ni lazima liambatane na ongezeko la bajeti inayotengwa kwa ajili ya mahakama.

”Mgawo mdogo wa bajeti katika mahakama, ambao unamaanisha mshahaŕa mdogo maana yake ni kwamba mtu anaweza kuyumbishwa,” Philip Kichana, mkuŕugenzi mtendaji wa ICK–Kenya aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.

Kwa sasa, mahakama inatumia asilimia moja ya bajeti nchini humo, kulingana na ICJ. Hii haitoshelezi kukidhi mahitaji ya wafanyakazi na vifaa muhimu kwa ajili ya uendeshaji wa utawala wa mahakama.

Bajeti ya Kenya inafikia dola bilioni 5.4, hii ni kulingana na takwimu za seŕikali. (END/2005)