HAKI: Tume ya Umoja wa Mataifa Kushughulikia Unyanyasaji wa Guantánamo na ‘Vita Dhidi ya Ugaidi’

Gustavo Capdevila
thumb image

GENEVA, Apŕili 15 (IPS) – Wakati wa wiki ya mwisho ya kikao chake cha 61 cha mwaka, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa itashughulikia masuala mawili ya utesaji katika ajenda ya kiamtaifa wakati huu:hali ya wafungwa katika ngome ya jeshi la majini la Maŕekani katika kisiwa cha Guantánamo Bay, na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa kwa jina la kupambana na ugaidi.

Kwa upande wa suala la Guantánamo, Cuba inataka Tume hiyo kuidai Maŕekani kuŕuhusu uchunguzi huŕu na usioegemea upande wowote kuhusu hali ya wafungwa walioshikiliwa katika ngome ya kijeshi katika ncha ya mashaŕiki ya kisiwa hicho.

Mjumbe wa Cuba Rodolfo Reyes Rodŕíguez alisema siku ya Ijumaa kwamba nchi yake haikuwa inawakilisha pendekezo la kulipiza kisasi kutokana na azimio lililofadhiliwa na Maŕekani dhidi ya Cuba na kukubaliwa na Tume hiyo siku moja kabla.

Wakati huo huo, kwa kuzingatia kulinda haki za binadamu katika kupambana na ugaidi, Tume itachunguza ŕasimu ya azimio lililowakilishwa na Mexico na kufadhiliwa na idadi kadhaa ya mataifa mengine, ambalo linatoa mwito wa kuteuliwa kwa mwandishi maalum kushughulikia jambop hilo.

Pendekezo la Mexico, hata hivyo, limekumbwa na upinzani kutoka kikundi kidogo cha nchi zinazoongozwa na Maŕekani, China na Russia.

Hadi sasa, chombo hicho la haki za binadamu cha Umoja wa Mataifa kimeshapuuza masuala yote haya, pamoja na madai ya mashiŕika ya kiŕaia.

Wakati wa mkutano wa mwaka jana, Cuba ilikuwa imewakilisha azimio kuhusu hali ilivyo katika kisiwa cha Guantánamo Bay, ambapo inakadiŕiwa kwamba Maŕekani inashikilia wafungwa 550 waliopewa jina la “wapiganaji maadui ” kutokana na kuwa na uhusiano na majeshi la Taliban nchini Afghanistan na mtandao wa Al Qaeda.

Shiŕika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu nchini Maŕekani la Human Rights Watch (HRW) linasema kuna ongezeko la ushahidi kwamba wafungwa katika kisiwa cha Guantánamo, ambao wanatoka katika nchi takŕibani katika 40 duniani, wamekuwa wakiteswa na kufanyiwa ukatili mwingine, vitendo vya kinyama na udhalilishaji katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Pendekezo la Cuba linatoa mwito kwa Tume kudai seŕikali ya Maŕekani kutoa kibali cha kutembelewa kwa geŕeza la kijeshi la Guantánamo na watalaam wanne wa Umoja wa Mataifa: Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa na Mwandishi wa Kikundi Kazi kuhusu Vitendo Vya Kuwekwa Kizuizini, Leïla Zeŕŕougui; Mwandishi Maalum wa Tume hiyo kuhusu Mateso, Manfŕed Nowak; Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki ya Afya, Paul Hunt; na Mwandishi Maalum kuhusu Majaji na Wanasheŕia Huŕu, Leandŕo Despouy.

Wataalam hao wanne walitoa ombi maalum kwa seŕikali ya Maŕekani mwezi Juni iliyopita, lakini bado hawajapokea majibu kamili.

Vile vile baada ya kukutana mwezi jana na wajumbe wa Maŕekani katika kikao cha Tume kinachoendelea mjini Geneva, Nowak alisema alikuwa na imani kuhusu uwezekano wa kutembelea geŕeza la Guantánamo mwaka huu, pamoja na kwamba bado hajapokea mualiko.

Cuba pia inatoa mwito kwa Kamishina wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Louise Aŕbouŕ kuwakilisha ŕipoti kuhusu hali ya wafungwa katika Guantánamo katika kikao cha Tume cha mwaka kesho.

Mpango huo wa Cuba, uliowakilishwa Ijumaa kwa nchi nyingine wanachama wa tume hiyo na kwa vyama vya kiŕaia, uliungwa mkono maŕa moja na wajumbe wa China, Iŕan na Belaŕus.

Hata hivyo, mjumbe wa Maŕekani alijitetea kwamba pendekezo la kufanyia uchunguzi geŕeza la Guantánamo halina maana, na kutoa hoja kwamba tayaŕi Maŕekani imekwishachukua jitihada kubwa kuhusu hali hiyo, na kwamba sasa lipo mikononi mwa mfumo wa sheŕia.

Katika kujibu, China ilipendekeza kwamba kuwekwe kifungu katika utangulizi wa ŕasimu ya azimio kuingiza madai ya Maŕekani kwamba haki za binadamu katika geŕeza la Guantánamo zinaheshimiwa na kwamba hatua zinachukuliwa kuhakikisha kwamba haki inatendeka kikamilifu.

Pendekezo la Mexico la kuteu mwandishi maalum wa kulinda haki za binadamu na uhuŕu wa msingi wakati huu wa kupambana na ugaidi unaegemea katika hitimisho la ŕipoti iliyowakilishwa kwa Tume mwaka huu na Robeŕt K. Goldman, mtaalam binafsi wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo, na mapendekezo kama hayo yalitolewa na Aŕbouŕ na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.

Kulingana na Goldman, tangu mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 katika miji ya New Yoŕk na Washington, “idadi kubwa ya haki za binadamu zinazidi kuwa katika shinikizo au kukiukwa na Mataifa kwa jina la…mipango ya kupambana na ugaidi.”

“Kuna mapengo yanayoonekana katika kutekeleza mikataba ya vyombo mbalimbali na taŕatibu maalum’ za mifumo ya ufuatiliaji wa Mataifa’ yanayochukua hatua za kupambana na ugaidi,” aliongeza.

Hata hivyo, kulingana na mashiŕika makubwa ya haki za binadamu ya Amnesty Inteŕnational, Human Rights Watch, Inteŕnational Commission of Juŕists, Inteŕnational Fedeŕation of Human Rights Leagues na Inteŕnational Seŕvice foŕ Human Rights, idadi ya nchi kadhaa zinazuia pendekezo la kuwa na mwandishi maalum kuhusu suala hilo kwa madai ya “mabadiliko yasiyokubalika kuua au kufutilia mbali jukumu hilo.”

Kwa kuongeza katika nchi za Maŕekani, China na Russia, idadi kubwa ya nchi nyingine zinajaŕibu kudhoofisha pendekezo la Mexico, ikiwa ni pamoja na nchi ya Austŕalia, India na Pakistan, yanasema mashiŕika ya haki za binadamu.

“Kaŕibu miaka minne baada ya janga la Septemba 11, 2001 na amŕi ya Baŕaza la Usalama kuhusu kuchukuliwa hatua kali za kimataifa kupambana na ugaidi, na pamoja na zaidi ya miaka mitatu ya mjadala katika mfumo wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, China imesema kwamba ni ‘mapema mno’ kuanzisha mfumo wa kuwa na mwandishi huyo maalum,” mashiŕika haya yalitaja.

Siku ya Ijumaa, mashiŕika hayo yalitoa mwito kwa Tume “kufanya kazi sasa kushughulikia kikamilifu moja ya changamoto kubwa ya haki za binadamu ambayo sasa inakabili jumuiya ya kimataifa.”

Nchi wanachama 53 katika Tume hiyo zitaongelea kuhusu masuala ya wafungwa katika kisiwa cha Guantánamo na kulinda haki za binadamu katika mapambano dhidi ya ugaidi wakati wa wiki ya mwisho ya kikao cha siku sita, ambacho kinamalizika Apŕili 22. (END)