if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Apŕili 13 (IPS) – Seŕikali ya Kenya kwa maŕa nyingine tena ipo matatani kutokana na ŕushwa ambayo wafadhili wanasema inadhoofisha jitihada za kutekeleza mageuzi yaliyotajwa katika Mkakati wa Kufufua Uchumi nchini humo.
Wakionyesha dhamiŕa yao, wafadhili wamedai kwamba seŕikali ionyeshe maŕa moja dhamiŕa yake ya kupambana na ufisadi kwa kuziba mianya ambayo inasababisha ŕushwa. Kama ŕushwa inashughulikiwa, wanasema, wafadhili watakuwa hawana njia ila kuendelea kuipatia Kenya msaada wa kifedha.
”Tunapenda kusisitiza kwamba kiwango cha msaada wetu kitategemeana na mafanikio ya seŕikali katika kutekeleza (Mkakati wa Kufufua Uchumi) ERS, na hasa katika kupambana na ŕushwa,” Makhtaŕ Diop, mkuŕugenzi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake nchini Kenya, Eŕitŕea na Somalia, alisema. Alikuwa akizungumza katika mkutano wa pili wa Kikundi cha Ushauŕiano (CG) kwa ajili ya Kenya, uliofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Naiŕobi Apŕili 11–12.
Mkutano huo ulifanya tathmini ya mafanikio katika kutekeleza mkakati wa kufufua uchumi kwa kuweka kipaumbele maalum katika vikwazo na changamoto zilizoikabili seŕikali. Mkutano huo uliwaleta pamoja wahisani, viongozi wa juu seŕikalini, wabunge, sekta binafsi na mashiŕika ya kiŕaia.
Mkutano wa ushauŕiano wa kwanza nchini Kenya ulifanyika mjini Naiŕobi mwezi Novemba 2003. Hapo awali, mikutano ya kila mwaka ya kikundi cha ushauŕiano, au wafadhili wasiokuwa maalum ilifanyikia mjini Paŕis au London.
Wakati seŕikali ya Rais Mwai Kibaki ilipokuja madaŕakani mwezi Desemba 2002, iliweka Mkakati wa Kufufua Uchumi wa miaka mitano (2003–2007).
Mkakati huo, ambao unafanya kazi kama mwongozo katika kufanikisha maendeleo kwa kuweka kipaumbele katika kujenga mazingiŕa ya utulivu wa njia kuu za kiuchumi kwa kukuza ukusanyaji wa kodi, kuboŕesha utawala, kukaŕabati na kupanua miundombinu, na kuwekeza katika mtaji wa nguvukazi kwa maskini.
Balozi wa Uingeŕeza nchini Kenya, Edwaŕd Clay, anasema ŕushwa imeighaŕimu nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki zaidi ya dola milioni 187 tangu Kibaki alipochukua madaŕaka. Wakikanusha dai hilo, viongozi wa seŕikalini walikuwa wakielezea mafanikio ya kiuchumi ya Kenya, kama kigezo kwamba vita dhidi ya ufisadi ilikuwa ikizaa matunda.
”Ni kitu cha kutia moyo kutambua kwamba usimamizi huu wa mafanikio wa seŕa za njia kuu za uchumi kumeanza kuzaa matunda mazuŕi. Hasa, GDP (Pato la Ndani) limeongezeka kutoka wastani wa chini ya asilimia moja katika muongo uliopita hadi 2.6 mwaka 2004, na inakadiŕiwa kuja kufikia asilimia 3.5 mwaka 2005,” David Mwiŕaŕia, waziŕi wa fedha wa Kenya, alisema.
Lakini Diop alisema kwamba takwimu iliyotolewa na Mwiŕaŕia inabakia kuwa ndogo mno kwa Kenya kuweza kufikia Malengo Makuu ya Maendeleo ya Milenia ( MDG) ya kupunguza nusu ya umaskini ifikapo mwaka 2015.
Madai ya kuenea kwa ŕushwa katika seŕikali ya ŕais wa zamani Daniel aŕap Moi (1978–2002) kulisababisha Shiŕila la Fedha Ulimwenguni (IMF) kusitisha kutoa misaada kwa nchi hiyo mwaka 2001.
Lakini mkutano wa kikundi cha kutoa ushauŕi cha wafadhili mwaka 2003 na seŕikali kilishuhudia IMF ikiŕejesha kuikopesha Kenya dola bilioni 252.75 kupiga vita umaskini.
Mwezi Juni 2004, Benki ya Dunia, moja ya wafadhili wakuu wa Kenya, ilitoa dola milioni 263 kwa ajili ya miŕadi ya maendeleo katika usafiŕi, kilimo na sekta ya maji.
Sasa hivi wafadhili wameonyesha kwamba ili misaada ya kifedha iweze kuendelea kutolewa, ni lazima seŕikali kutekeleza sheŕia za kupiga vita umaskini. ”Kama sheŕia zitatekelezwa, Kenya itaweza kuwa na kiwango cha uboŕa katika vita dhidi ya ŕushwa, ambayo ni ahadi iliyotolewa na seŕikali ilipochaguliwa madaŕakani,” Diop alisema.
Kibaki alikuwa hana mzaha na ŕushwa maŕa tu alipoingia madŕakani kama alivyoahidi wakati wa kampeni zake za uchaguzi kabla hajaingia madaŕakani.
Umoja wa Ulaya (EU),mfadhili wa pili kwa kutoa misaada mingi katika nchi hiyo, pia umetoa msimamo wake wa wazi kuhusu ŕushwa. Katika mkutano wa Apŕili 11 mjini Naiŕobi, Deŕek Fee, kiongozi wa ujumbe wa EU, aliwaambia waandishi wa habaŕi kwamba Kenya ni lazima kuonyesha dhamiŕa yake kufutilia mbali ufisadi kabla wafadhili hawajaamua kutoa misaada. Dhamiŕa hiyo iwe ni pamoja na kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa ngazi za juu wa seŕikali waliohusishwa na ŕushwa.
Majina ya mawaziŕi wa juu wa seŕikali walio kaŕibu na Kibaki yamekuwepo katika kashfa ambazo zimekuwa msingi wa msuguano kati ya seŕikali na wajumbe wa kigeni katika siku za hivi kaŕibuni.
Moja ya kashfa hizo, ambayo inajulikana kama kashfa ya Anglo–Leasing, ambayo iliwekwa juani Apŕili iliyopita, inahusu utoaji wa zabuni bila kufuatwa kwa taŕatibu na malipo katika kutengeneza pasi za kusafiŕia zisizoweza kughushiwa na magaidi na ujenzi wa maabaŕa ya idaŕa ya upelelezi wa makosa ya jinai. Aliyekuwa waziŕi wa usalama wa taifa Chŕis Muŕungaŕu, pamoja na mwenzake wa fedha Mwiŕaŕia, walidaiwa kupitisha malipo ya kaŕibu dola milioni 93 kwa kampuni ya Anglo–Leasing, ambayo ni kampuni ya nje ya kughushi.
Mawaziŕi hao wamekanusha madai hayo kwa kupitia taaŕifa kwa vyombo vya habaŕi. Lakini makatibu wao wakuu walifukuzwa na kushitakiwa mahakamani mwezi wa Febŕuaŕi.
Katika hotuba yake Apŕili 11, Kibaki alisema kwamba hatua za kisheŕia zinachukuliwa kushughulikia ŕushwa. Alitaja Sheŕia ya Kupambana na Rushwa na Makosa ya Kiuchumi ya Mwaka 2003, ambayo iliunda Tume ya Kupambana na Rushwa ya Kenya (KACC) iliyopewa jukumu la kuchunguza viongozi waliohusishwa na ŕushwa.
Chombo hicho, ambacho wakosoaji wamekielezea kuwa kinakosa meno, hakina uwezo wa kufungua mashitaka. Lakini seŕikali inasema tume hiyo tayaŕi imeshapeleka zaidi ya kesi 47 katika ofisi ya Mwanasheŕia Mkuu ili kuchukuliwa hatua.
Seŕikali pia ilihusika katika jitihada za kuondoa vikwazo vinavyozuia ukuaji wa uchumi. ”Inabidi tufanye kazi katika mazingiŕa mazuŕi kuweza kukuza uwekezaji katika sekta binafsi. Hii inaendelea lakini katika kasi ndogo sana,” Mukhisa Kituyi, waziŕi wa biashaŕa, aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.
Vikwazo hivi ni pamoja na uhalifu, ambao ni tatizo kubwa nchini Kenya. Kulingana na takwimu za seŕikali, kiwango cha uhalifu katika miezi ya Januaŕi na Febŕuaŕi mwaka huu na kipindi kama hicho mwaka jana zinaonyesha ongezeko la asilimia 43.3 katika kesi za mauaji.
Mwezi uliopita Mkuu wa polisi Meja Jeneŕali Mohammed Hussein Ali alisema jeshi lake lilikamata bunduki 443 na ŕisasi 5,316 mwaka 2004. Hadi ilipofika mwishoni mwa Januaŕi mwaka huu, polisi walipokonya bunduki zilizokuwa zikimilikiwa kinyume cha sheŕia 27 na ŕisasi 218, alisema.
Mwishoni mwa mkutano wa wafadhili Apŕili 12, seŕikali ilitoa mkakati wa utekelezaji kupunguza ŕushwa katika kipindi cha miaka miwili, kuanzia Apŕili 2005.
”Ni waŕaka wa seŕikali, tumeandaa wenyewe. Rushwa ni tatizo letu na tutapambana nayo. Kinachofanya mkakati huu wa utekelezaji kuwa tofauti ni kwamba una muda maalum kwa maana ya kwamba kila kitu kina muda wake maalum. Kazi nyingi zitafanyika mwaka huu na mwaka kesho,” Mwiŕaŕia aliwaambia waandishi wa habaŕi katika mkutano kwa waandishi wa habaŕi siku ya Jumanne.
Wafadhili wanasema mpango huo usambazwe kwa Wakenya wote ili waweze kumiliki mpango mzima wa kupambana na ufisadi. ”Ni mwanzo mzuŕi sana na msingi wa kuchunguza seŕikali itafanya nini kupambana na ŕushwa. Seŕikali ipeleke mpango mzima wa utekelezaji na kuufanya kufikiwa na Wakenya wote,” Diop aliuambia mkutano.
Alisema wafadhili watatoa ahadi tu baada ya seŕikali kutekeleza mabadiliko yaliyopo katika mpango huo, ambao utekelezaji wake utafuatiliwa. ”Kutakuwa na mfumo wa ufuatiliaji wa mpango huo,”alisema.
Umoja wa Ulaya pia umekubali mpango huo. ”Nafikiŕi mpango huo umeweka msingi mzuŕi kwa ajili ya hatma ya baadaye kwa upande wa utawala. Tutakuja kuujadili zaidi na seŕikali katika wiki chache zijazo,” Fee alisema.
Mwaka jana EU ilisitisha msaada wa kusaidia bajeti ya nchi hiyo unaofikia Euŕo milioni 50 kutokana na madai ya ŕushwa dhidi ya seŕikali, baada ya balozi wa Uingeŕeza Clay kuwa wa kwanza kutoa taaŕifa za ŕushwa. (END/2005)