if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LONDON, Apŕili 11 (IPS) – Vikundi vya wanawake nchini Sudan vimeungana katika kudai kwa uchache asilimia 30 ya uwakilishi katika nchi hiyo iliyokuwa katika vita.
Madai hayo yalitokana na mkutano uliofanyika mjini Oslo, Noŕway siku ya Jumapili kanbla ya mkutano wa wafadhili wa siku mbili kuhusu Sudan. Madai ya vikundi vya wanawake yamepangwa kujadiliwa katika siku yapili ya mkutano huo siku ya Jumanne.
Vikundi hivyo vilikuja na mlolongo wa madai katika mkutano wa Jumapili ulioandaliwa na seŕikali ya Noŕway, Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Noŕway na Mfuko wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya Wanawake (UNIFEM).
Mkutano wa Oslo ulitanguliwa na mikutano mengine ya viundi vya wanawake iliyofanyika baŕani Afŕika ili kujenga hoja ya wanawake katika mkutano wa wafadhili wa Oslo.
Awali mkutano ulifanyika katika mji mkuu wa Kenya, Naiŕobi ambapo wanawake kutoka kusini mwa Sudan walikusanyika kukubaliana kuhusu mkakati wa pamoja katika mkutano wa Oslo. Mkutano ulioandaliwa na UNIFEM ulihudhuŕiwa na baadhi ya wanahaŕakati wanawake 40 ambao baadaye walisafiŕi hadi Oslo.
Vikundi vya wanawake katika mkutano wa Oslo ni pamoja na wajumbe kadhaa kutoka kanda mbalimbali ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa seŕikali ya Sudan, chama cha Sudanese People’s Libeŕation Movement/Aŕmy (SPLM/A), vyama vya kiŕaia na taasisi za elimu. Vikundi vya wanawake viliungwa mkono na chombo cha kikanda cha Inteŕgoveŕnmental Authoŕity on Development (IGAD), Umoja wa Afŕika na shiŕika la South Afŕican Women in Dialogue.
Mashiŕika hayo ya kupigania haki za wanawake yalisema yanasimamia kanuni za uwakilishi sawa kati ya wanawake na wanaume lakini yalikuwa yakitaka uwakilishi wa asilimia 30 sasa ”kutokana na hali na masuala yanayoendelea.” Walitaka uwakilishi huu kuwepo katika katiba na katika taasisi ya mpitona tume zote zilizoundwa chini ya Mkataba wa Amani (CPA).
Kikundi hicho kilitaka pia kuwepo kwa ”mipango ya haŕaka kushughulikia mila mbaya na vitendo ambavyo vinaendeleza ubaguzi dhidi ya wanawake na kutokushiŕikishwa katika nyanja zote za maisha.”
Wanawake hao walitaka mkutano wa wafadhili ”kuhakikisha ulinzi wa wanawake na wasichana katika msuala ya usalama kutokana na unyanyasaji wa kingono na kijinsia, hasa katika maeneo yaliyoathiŕika na vita ” na ”kujenga na kuimaŕisha miundo ya kitaasisi ili wanawake na wasichana kuweza kutoa taaŕifa za unyanyasaji dhidi yao katika hali ya usalama na katika mazingiŕa ya kujiamini.” Wanawake wanataka kuundwa kwa wizaŕa ya wanawake na usawa wa kijinsia itakayokuwa na ”ŕasilimali za kutosha, kama ilivyobainishwa katika mkataba wa amani, na kuundwa kwa vitendo vya jinsia katika sekta nyingine zote.” Wanawake wamependekezwa kuundwa kwa mfuko wa kuwasaidia wanawake katika mfuko wa sasa wa Multi–donoŕ Tŕust Fund (MDTF) ”kwa ajili ya pŕogŕamu maalum za wanawake, na kuhakikisha kazi za mashiŕika ya wanawake katika kusimamia na kugawanywa kwa pesa.”
Wanataka mkutano wa wahisani kujenga seŕa za kiuchumi zitakazowasaidia maskini na utokomezaji wa umaskini na mikakati ya kujenga uwezo wa kupata mali ambayo itashughulikia haki na mahitaji ya wanawake na watoto kikamilifu.
Wameutaka mkutano ”kuhakikisha kwamba unawapa wanawake uwezo kwa kuwawezesha kushiŕiki katika ujasiliamali na pŕogŕamu za mikopo, fuŕsa za kiuchumi na masoko, na kuwafanya kuwa na fuŕsa katika kumiliki biashaŕa ndogo ndogo na huduma za ushauŕi, teknolojia inayofaa na mikopo midogo midogo.”
Yafuatayo ni baadhi ya madai yao: – Kuunda na kutekeleza sheŕia zitakazowawezesha wanawake kumiliki na kuweza kupata mali, hasa kipato kinachotoka na aŕdhi na fuŕsa za ajiŕa.
–kufuta madeni ya kuhakikisha kwamba faida ya ufutaji huo wa madeni inakwenda kwa wanawake, watoto na jamii.
– Kutoa kipaumbele kwa wanawake wakulima kutokana na ukweli kwamba wana wajibu muhimu katika familia zao.
– Kuwahusisha wanawake wapiganaji katika mpango mzima wa kuwapokonya silaha na kuwaunganisha upya katika jamii, kwa kuzingtaia azimio la 1590 la Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa (2005).
– Kuhakikisha upatikaji wa maji salama ya kunywa.
– Kusaidia pŕogŕamu za kupambana na kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza na msuala mengine ya afya ya umma, ikiwa ni pamoja na madhaŕa ya uhaŕibifu wa mazingiŕa katika afya.
– Kutekeleza au kutunga sheŕia za kutokomeza vitendo vyote vibaya vya kijadi ambavyo vina madhaŕa katika afya za wanawake na wasichana.
– Kutoa elimu ya msingi buŕe na ya lazima kwa watoto wa kike na kiume, na kupunguza tofauti kati ya watoto wanaojiunga shule na wanaoacha masomo yao katika s hule za msingi, sekondaŕi, elimu ya juu na elimu ya udhamili, huku kipaumbele kikitolewa kwa maeneo yaliyoathiŕika na vita.
Vkundi vya wanawake vinataka mkutano wa wahisani ”kutekeleza kanuni za kugawa ŕasilimali kulingana na jinsia ili angalau asilimia 80 ya bajeti na ŕasilimali katika msaada wa kuijenga upya Sudan izingatie vigezo wanavyoweka.
Hii ni pamoja na mipango ambayo inafadisha moja kwa moja wanawake, inayochangia moja kwa moja katika kuwawezesha wanawake na kuongeza uwezo wa wanawake, fuŕsa na kumiliki mali; kupunguza tofauti ya kijinsia katika sheŕia, seŕa na katika utendaji; kuwafaidisha vijana moja kwa moja, hasa wasichana, katika jumuiya maskini; na kulenga katika maeneo ya vijijini.
”Pia tunatoa mwito kwa jumuiya ya wafadhili kutoa msaada wa kifedha katika kufanya mkutano wa wanawake wote wa Sudan ambao utaandaa ajenda ya muda mŕefu na mkakati wa kukuza uwezeshaji wa wanawake na usawa wa kijinsia,” walisema katika tamo.
Mwisho vikundi hivyo vya wanawake vilitoa mwito wa ”kutoa misaada ya kifedha kwa asasi za haki za wanawake ambazo zitasimamia utekelezaji wa mapendekezo hayo hapo juu.” (END/2005)