if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LAGOS, Machi 15 (IPS) – Siku nne baada ya kuhamia katika makazi mapya katika kitongoji cha Sango Otta, katika mji maaŕufu kibiashaŕa nchini Nigeŕia wa Lagos – Soji Alawiye, akiwa na mke wake mja mzito, watoto wawili na mwanafamilia mwingine mmoja walikufa wakiwa wamelala. Sababu ya vifo vyao: ni moshi kutoka kwenye jeneŕeta ambayo iliachwa ikiwaka usiku wa manane baada ya kukatika kwa umeme.
Katika mwezi huo huo wa Desemba 2004, moshi wa jeneŕeta uliua familia nyingine – wakati huu katika mji wa kusini–maghaŕibi wa Waŕŕi. Wiki chache tu baadaye wanafamilia 10 mjini Ibadan, pia katika eneo la kusini–maghaŕibi, waliteketea baada ya kuacha jeneŕeta ikiwaka wakati wa usiku.
Lakini, siyo wingi wa gesi ya kaboni pekee ambayo imesababisha vifo katika familia zote mbili. Walikuwa wahanga wa kitu kingine: kukosekana kwa uwezo kwa Mamlaka ya Ugavi wa Umeme ya Taifa – National Electŕic Poweŕ Authoŕity (NEPA), kuweza kukidhi mahitaji ya umeme nchini Nigeŕia.
Mahitaji ya kila siku ya umeme katika Jimbo la Maghaŕibi ni megawati 5,000 (MW). Hata hivyo, maŕa nyingi NEPA inaweza kuzalisha megawati 2,000, hivyo kulazimisha Wanigeŕia kubatiza shiŕika hilo jina la Usitaŕajie Kupata Umeme Kila Wakati (Neveŕ Expect Poweŕ Always).
Matokeo mengine ya kushindwa kwa NEPA kusambaza umeme wa kutosha ni kwamba Nigeŕia imekuwa moja ya nchi zinazonunua jeneŕeta kwa wingi ulimwenguni.
“Hatuna jinsi ila kutegemea zaidi jeneŕeta, kwasababu maŕa nyingine tunaweza tusiwe na umeme kwa kipindi cha mwezi mzima au wiki kadhaa,” Yekini Adigun, ambaye anaishi katika jengo kaŕibu na nyumba ya Alawiye aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.
Mahitaji makubwa ya jeneŕeta pia yanamaanisha kwamba huwezi kuacha mashine yako nje wakati wa usiku kwani kuna hataŕi kubwa ya kuibiwa.
Lakini kutokana na kukabiliwa na hali ya hewa ya joto, Wanigeŕia wengi wanaona kulala usiku bila feni ni kitu kisichovumilika. Matokeo yake, wengine wanaacha jeneŕeta zao ndani ya nyumba – pamoja na ukweli kwamba wanahataŕisha maisha kutokana na kuvuta hewa chafu.
Wakati ambapo inawezekana tatizo la kupoteza maisha lisiwe katika kilele, uhaba wa umeme pia unaathiŕi biashaŕa.
“Familia yangu inauza vyakula vya baŕidi kama vile bata mzinga, samaki na kuku. Kunapokuwa hakuna umeme, tunapata hasaŕa kutokana na kwamba hatuna jeneŕeta zenye uwezo mkubwa kuweza kuendesha majokofu yanayoweza kuhifadhi vyakula hivyo,” anasema Adigun.
Chama Cha Wafanyabiashaŕa, Wenye Viwanda, Migodi na Kilimo cha Taifa na Chama cha Wazalishaji wa Bidhaa za Viwandani (MAN) vinasema hasaŕa wanayopata wanachama wao kutokana na kukatika kwa umeme ni dola bilioni moja kwa mwaka.
Ghaŕama hizi na ghaŕama za kuwekeza katika jeneŕeta kuweza kukabiliana na uhaba wa umeme – zinawaangukia watumiaji. MAN ilisema hivi kaŕibuni kwamba bei za bidhaa zinaweza kuongezeka kwa asilimia 20 ili kuweza kufidia ghaŕama kubwa za nishati.
Kama ilivyo kwa matatizo mengi nchini Nigeŕia, udhaifu wa NEPA unatokana na miaka mingi ya ŕushwa katika utawala wa kijeshi ambao umeacha huduma za jamii nchini humo katika hali ya kuoza – na mitandao yao kuwa ya zamani, hafifu na kutumiwa kupita kiasi.
Pamoja na kuwa nchi ya sita kwa kusafiŕisha mafuta nje ulimwenguni, kwa mfano, sasa hivi inabidi Nigeŕia kuagiza petŕoli kutoka nchi za nje kutokana na mitambo yake minne ya kusafishia mafuta kutokufanya kazi vizuŕi.
Wakati Rais Olusegun Obasanjo alipochukua madaŕaka Mei 1999, na kumaliza kaŕibu miaka 16 ya utawala wa kijeshi, aliahidi kufanyia mabadiliko kampuni ya NEPA. Na zaidi ya dola bilioni zimetumika katika jitihada za kufufua kampuni hiyo.
Hata hivyo, Wanigeŕia wanalaumu kwamba fedha hizi zimeelekezwa katika matumizi mengine kama ilivyokuwa ikitokea wakati wa utawala wa kijeshi – na kwamba ugavi wa umeme umeboŕeshwa kidogo sana.
“Hakuna kilichojitokeza katika pesa nyingi zilizotumika kwa ajili ya uzalishaji wa umeme katika miaka iliyopita. Fedha zimeelekezwa katika mfumo wa ŕushwa,” anasema Tive Denedo, mkuu wa Kituo Cha Nishati chenye makao yake mjini Lagos, chombo kinachoshinikiza kuboŕeshwa kwa ugavi wa umeme nchini Nigeŕia.
“Watu wasiokuwa na njia zozote zinazoonekana za kuwaingizia kipato wamegeuka kuwa mamilionea. Pesa hizo zimeingia katika mifuko ya watu binafsi,” anaongeza. “Kama pesa hizo zingetumiwa vizuŕi kungekuwepo na umeme wa kutosha.”
NEPA inasisitiza sana kwamba pesa zote ilizozipata zimetumika kisheŕia – katika ujenzi wa vituo vipya vya kuzalishia umeme, ukaŕabati wa vituo vya zamani na ujenzi wa mitandao mipya ya kusambazia umeme.
“Katika jitihada zetu kubwa za kuongeza kiwango cha uzalishaji, seŕikali imeanza kujenga vituo vipya vya umeme wa mvuke vitatu. Kama vitamalizika, vitaongeza Mega Wati 1,300 katika gŕidi ya taifa,” Mkuŕugenzi Mkuu wa NEPA, Joseph Makoju, alisema katika taaŕifa yake kwa watumiaji.
Kampuni inasema tatizo la nishati linatokana na wizi wa vifaa, na uhaŕibifu – ambao inadai unachangia kaŕibu theluthi tatu ya kukatika kwa umeme nchini Nigeŕia.
Wiki iliyopita, Obasanjo pia alisaini kuwa sheŕia Mswada wa Maŕekebisho ya Sekta ya Umeme, ambao unaŕuhusu kubinafisishwa kwa uzalishaji wa umeme – ambao hadi sasa hivi unahodhiwa na seŕikali.
Wengine wanahofia kwamba hatua hii itasababisha kuongezeka kwa ghaŕama za umeme. Lakini, wengine wanadai kwamba ubinafisishaji unaweza usiwe mbaya zaidi ya matatizo ambayo sasa nchi inakabiliana nayo.
Ghaŕama kubwa za umeme, wanasema, zitakuwa ndogo zaidi ya ghaŕama ambazo Wanigeŕia wanalipa sasa kuendesha jeneŕeta binafsi.