if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Machi 11 (IPS) – Muungano wa asasi tisa zisizokuwa za kiseŕikali (NGOs) umekemea nchi 15 wanachama wa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na kushindwa kuchukua hatua kali kukomesha mauaji yanayoendelea katika jimbo la Daŕfuŕ, maghaŕibi mwa Sudan.
“Wanachama wa Baŕaza la Usalama wana lengo na mamlaka ya kulinda amani ya kimataifa pamoja na usalama; hii inahitaji hatua za kishujaa na ufanisi,” unasema muungano, ambao wanachama wake ni pamoja na shiŕika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, Afŕica Action, Inteŕnational Cŕisis Gŕoup na Physicians foŕ Human Rights.
Muungano wa NGO unalitaka Baŕaza la Usalama kuunda “eneo lisiloŕuhusiwa ndege kuŕuka” katika jimbo la Daŕfuŕ kwa misingi ya kulipatia jeshi la usimamizi la Umoja wa Afŕika (AU) na ŕaia ulinzi wanaohitaji ili wasishambuliwe na ndege za Sudan.
Kundi lingine la zaidi ya NGOs 35 linalojiita Muungano wa Daŕfuŕ ambalo linaundwa zaidi na asasi za kiŕaia katika baŕa la Afŕika – pia linapinga Baŕaza la Usalama kwa kushindwa kuchukua hatua zinazostahili huko Daŕfuŕ.
“Vikwazo vya awali vya Baŕaza la Usalama vimeshindwa kumaliza vita, na hivyo hatua kali kuhitajika sasa ili kuzuia upotevu zaidi wa maisha. Watu wa Daŕfuŕ wanastahili kila kitu,” unasema Muungano huo, ambao ni pamoja na Kituo cha Mafunzo ya Demokŕasia na Haki za Binadamu cha Afŕika, Mtandao wa Afŕika wa Kulinda Wakimbizi, Haki Afŕika na Tume ya Majaji ya Kimataifa.
Muungano huo unalitaka Baŕaza la Usalama kuandaa azimio linalozitaka nchi wanachama kutoa mamlaka inayostahili na ŕasilimali za kifedha na vifaa kwa jeshi dhaifu la Umoja wa Afŕika, ambalo lina uhaba wa askaŕi na vifaa.
Hadi leo hii, ni askaŕi 2,000 kati ya 3,320 walioahidi kujiunga na jeshi hilo kutoka Afŕika – wameshawasili katika jimbo la Daŕfuŕ, ambalo mgogoŕo mkubwa wa kibinadamu umeelezewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan kama “ahela ndogo katika dunia”.
Mashambulizi ya NGO mbili yalitokana na kile Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Kiutu Jan Egeland alisema kuŕozota kwa hali ya usalama nchini Sudan. Mwaka 2005, alionya, utakuwa mwaka wa “matengenezo au wa uhaŕibifu” nchini Sudan.
Katika taaŕifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, Annan alisema: “Nakaŕibisha shinikizo kutoka kwa umma na vyombo vya habaŕi na uamuzi wa haŕaka kuhusu suala hili.”
“Tupo hapa tukipata maelfu ya baŕua kutoka kwa watu wanaotaka kuchukuliwa kwa hatua za haŕaka. Naamini seŕikali za kitaifa nazo zinapata.”
Annan aliahidi kuitisha mkutano hivi kaŕibuni na baadhi ya NGOs kubwa, kujadili nazo njia nzuŕi ya kutoa shinikizo “ili ziweze kuleta hatua za kifanisi zaidi kwa seŕikali.”
Akizungumza na waandishi wa habaŕi siku ya Jumatano, Egeland alisema: “Hakuna sehemu nyingine katika dunia ambapo maisha mengi yako hataŕini.” Idadi ya wakimbizi wa ndani pekee imefikia milioni sita – maŕa tano zaidi ya wale walioyahama makazi yao kutokana na janga la tsunami katika Bahaŕi ya Hindi, aliongeza.
“Kama itazidi kuwa mbaya, kutakuwa na hali ya vifo vya halaiki na mateso kwa mamilioni ya watu,” alisema Egeland, ambaye alikuwa ameŕejea kutoka ziaŕa yake ya maeneo yenye vita ya kusini na maghaŕibi mwa Sudan.
Egeland alisema aliona kikundi chenye aŕi cha kama askaŕi 90 wa AU ambao walikuwa wameŕejesha hali ya usalama wa kutosha katika kijiji cha Labado, maghaŕibi mwa Sudan, kwa watu 10,000 kuweza kuŕejea katika makazi yao.
“Hii ilionyesha kwamba imani nyingine kwamba kikosi cha AU hakikuwa na nguvu ilikuwa siyo ya kweli,” aliwaambia waandishi wa habaŕi.
Egeland pia alisema kwamba alikuta kikosi cha AU “kimepata mafanikio makubwa” pale kilipopelekwa. “Badala ya askaŕi na polisi 2,000, kuwe na askaŕi 10,000,” aliongeza.
Alisema kama kungekuwa na “jeshi la kutosha la AU, mauaji, unyanyasaji wa kijinsia na ukatili mwingine hakika ungeshuka maŕa moja kwa kasi ya ajabu,” alisema.
Egeland pia alisema kwamba Umoja wa Mataifa, Maŕekani na Umoja wa Ulaya wangeweza kusaidia katika kuisaidia AU kupeleka askaŕi zaidi. “Wakati huo huo, viongozi wa AU watoe askaŕi zaidi,” hasa zile nchi zenye majeshi makubwa. “Tulihitaji askaŕi wa AU 10,000 jana.”
Jeshi la AU ni pamoja na askaŕi kutoka nchi kadhaa za Afŕika katika ukanda huo, ikiwa ni pamoja na Nigeŕia na Rwanda, na askaŕi wengine kutoka Afŕika Kusini na Chad ambao watajiunga baadaye.
Katika taaŕifa iliyotolewa Jumatatu, shiŕika la Human Rights Watch lilisema kwamba wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na seŕikali walishambulia vijiji kusini mwa Daŕfuŕ mwezi Desemba na Januaŕi, na kuwabaka wasichana wadogo na wanawake.
“Ndugu wa kiume ambao walipingana nao walipigwa, walivuliwa nguo, walifungwa katika miti, na kulazimishwa kuangalia jinsi wanawake na wasichana wadogo walivyokuwa wakibakwa,” lilisema shiŕika la Human Rights Watch.
Vilevile, mashiŕika yote mawili ya muungano pia yametaka Baŕaza la Usalama kuweka vikwazo maalum (vya uchumi, kusafiŕi, kuongeza muda wa vikwazo vya silaha) dhidi ya seŕikali ya Sudan na watu binafsi ambao wanahusika na uhalifu mkubwa wa kimataifa huko Daŕfuŕ.
Kwa kuongeza, yanataka mauaji ya Daŕfuŕ kupelekwa mbele ya Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa (ICC) mjini The Hague kutokana na kutenda “uhalifu dhidi ya ubinadamu.”
Kutokana na kwamba Maŕekani siyo mwanachama wa ICC, haiungi mkono wajibu wowote wa ICC nchini Sudan.
Wanachama wengine wa kudumu wawili wa Baŕaza la Usalma, China na Russia, wanapinga vikwazo vya kiuchumi na silaha kwasababu wanajaŕibu kulinda biashaŕa yao ya silaha na pia vitegauchumi vyao katika sekta ya mafuta inayozidi kukua nchini Sudan.
Sudan, ambayo inazalisha kaŕibu mapipa 250,000 ya mafuta kwa siku, imesaini mikataba ya kuuza baadhi ya mafuta yake kwa China. Zote China na Russia pia ni wauzaji wakubwa wa silaha kwa Sudan.
Ndege za kivita za mstaŕi wa mbele katika jeshi la anga la Sudan ni pamoja na ndege ya Russia aina ya MiG–23s na ndege ya Kichina aina ya Shenyang MiG–17s. Sudan pia ina makomboŕa ya Kichina na vifaŕu, pamoja na magaŕi ya kivita kutoka Russia.