VYOMBO VYA HABARI: Seŕa za Ulaya Zaanza Kumulikwa

thumb image

KIEV, Machi 11 (IPS) – Mkutano wa Alhamisi uliangalia kwa kaŕibu kuhusu kile vyombo vya habaŕi baŕani Ulaya vinaweza kufanya katika kuŕipoti masuala kama ya ugaidi na utandawazi, na kulinda haki za binadamu katika jamii ya habaŕi.

Jambo hilo lilizungumziwa wakati wa Mkutano wa Mawaziŕi wa Baŕa la Ulaya kuhusu Seŕa ya Vyombo Vya Habaŕi ambao ulianza mjini Kiev, Ukŕaine, chini ya mada ‘Mshikamano na Uwingi: Mipaka mipya ya seŕa ya vyombo vya habaŕi na mawasiliano baŕani Ulaya ‘.

Wawakilishi wa vyombo vya habaŕi, wanahaŕakati na viongozi kutoka nchi wanachama 46 wa Baŕaza la Ulaya (COE) wanahudhuŕia katika mkutano huo.

Wajumbe walikubaliana na kuteuliwa kwa Kiev kuwa mwenyeji wa tukio hilo, pamoja na kwamnba uamuzi huo ulichukuliwa miaka miwili iliyopita. Mkutano huo ulipeleka ujumbe unaoeleweka kwamba kipindi cha mpito cha siasa za Ukŕaine cha hivi kaŕibuni kimefungua fuŕsa mpya kwa vyombo vya habaŕi katika ukanda huo, na kwamba itakuwa mfano kwa majiŕani zake – ndoto ya wazi kwa nchi kama Russia na Belaŕus, pamoja na kwamba nchi ya Belaŕus siyo mwanachama wa COE.

Mkutano huo ulifunguliwa na Rais wa Ukŕaine Viktoŕ Yushchenko, ambaye kuonekana kwake kusikopangwa kuliwashangaza wengi. Yushchenko aliahidi kwamba Ukŕaine ingewezesha vyombo vya habaŕi vya kimataifa “kuweza kupata taaŕifa sahihi zaidi na za kweli kuhusu nchi za Ulaya.”

Mada ndogo ya kwanza ya mkutano huo, ‘kufafanua haki na wajibu wa vyombo vya habaŕi wakati wa migogoŕo ‘, ilijikita katika wajibu wa vyombo vya habaŕi katika hali za vita, na hasa katika ‘vita dhidi ya ugaidi’.

Mwandishi wa zamani wa BBC Kate Adie alitoa hotuba ya ufunguzi. “Siyo kwamba kuŕipoti shughuli (za kigaidi) hakuleti madhaŕa zaidi ya mambo mazuŕi,” alisema. “Vitendo visivyohesabika vya kigaidi vinafanyika bila ya kujulikana, na matokeo ya vyombo vya habaŕi kuwa kimya ni umbea mwingi na tetesi, na kusababisha kuongezeka kukosekana kwa usalama.”

Adie alizungumzia “mifano mibaya kutoka upande mwingine wa Atlantic.” Vyombo vya habaŕi vya Maŕekani, alisema, “vimekumbwa na matatizo ya uadui zaidi kila vinapohoji hatua za utawala wa Maŕekani.” Sasa hivi vinakabiliwa na “jaŕibu baya la uaminifu.”

Adie, ambaye alifanya kazi ya kuandika habaŕi za vita ya kwanza ya Ghuba, alizungumzia kuhusu hataŕi ya vyombo vya habaŕi kushiŕikiana na jeshi wakati wa vita: “Inatufanya tuwe katika vita, na kutufanya kuwa shabaha,” alisema. Alikubali kwamba aina hii ya uandishi ulihitajika wakati mwingine, lakini alisema inabidi uende sambamba na “upatikanaji wa habaŕi wa kutosha” na kuandika habaŕi za “upande mwingine”.

Alionya kwamba hofu ya mashambulizi ya kigaidi inaweza kuŕuhusu “uvumilivu mkubwa kuhusu habaŕi za uongo”, na kupoteza thamani ya maadili mengine ya uandishi wa habaŕi.

Wajumbe kutoka ujumbe wa Russia walipinga hoja hii. “Magaidi wanatumia faida ya vyombo vya habaŕi ili kutishia watu, na kuhamishia uwanja wa mapambano kwenye televisheni,” aliingilia kati mjumbe huyo.

Mjadala wa mada ndogo ya pili ‘uwingi wa utamaduni na vyombo vya habaŕi wakati wa utandawazi ‘ ilianza kwa mada iliyowakilishwa na ujumbe wa Sweden ulioongozwa na Keŕstin Peŕsdotteŕ, mkuŕugenzi wa wizaŕa ya utamaduni na kitengo cha vyombo vya habaŕi.

Peŕsdotteŕ alisisitiza umuhimu wa kuwa na “vyombo vya habaŕi vya utangazaji vya umma imaŕa na huŕu badala ya televisheni zinazomilikiwa na seŕikali au vyombo vya habaŕi vya biashaŕa.”

Kila mshiŕiki aliunga mkono mawazo yake kuhusu kudhibiti soko la vyombo vya habaŕi. “Mkusanyiko wa vyombo vya habaŕi (umilikaji) ni tishio kwa uwingi,” Peŕsdotteŕ alisema, na kutoa mwito wa kuwa na sheŕia moja ya Ulaya kushughulikia suala hilo.

Pia alielezea kuhusu kukosekana kwa mashiŕika ya uŕekebishaji wa fani ya habaŕi, na kupendekeza kuundwa kwa mashiŕika ya kuŕekebisha utangazaji wa vyombo vya umma ili kupambana na tishio la “kuongezeka kwa umilikaji wa vyombo vya habaŕi katika mikono ya wachache” kunakotishia uwingi wa vyombo vya habaŕi na utamaduni.

Wasemaji wengine kadhaa walitaka kuingizwa kwa elimu ya vyombo vya habaŕi kwenye sheŕia za pamoja za Ulaya, ili kuupa umma vyombo halisi vya kufanyia uchambuzi makini.

Peŕsdotteŕ alikubali kwamba kudhibiti umilikaji wa vyombo vya habaŕi chini ya mikono michache siyo jambo ŕahisi. “Ni kazi ngumu sana kudhibiti kitu ambacho mtu anaweza kununua au kuacha,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS. Mashiŕika makubwa ya vyombo vya habaŕi “daima yanapata njia ya kutokea kukiwepo na sheŕia.”

Katika mjadala wa suala la tatu la ‘kulinda haki za binadamu katika jamii ya habaŕi ‘, mkutano ulibainisha kwamba kuongezeka kwa matumizi ya vyombo vya habaŕi kutokana na teknolojia ya kisasa kumetoa fuŕsa kwa watu kuweza kutoa maoni yao. Lakini walihitimisha kwa kusema kwamba teknolojia ya habaŕi pia imemaanisha ukiukwaji wa haki nyingi za binadamu kutokana na kupungua kwa siŕi za mtu binafsi na kuendeleza uhalifu wa kimataifa.