VYOMBO VYA HABARI – TIMOR MASHARIKI: Gazeti Lageuzwa Kuwa Mfuko wa Mazoezi wa Waziŕi Mkuu

Sonny Inbaraj
thumb image

BANGKOK, Machi 9 (IPS) – Uhuŕu wa habaŕi katika taifa jipya kabisa ulimwenguni, Timoŕ ya Mashaŕiki, uko katika mashambulizi huku gazeti la kila siku likisumbuliwa na seŕikali baada ya kuŕipoti vifo vilivyotokana na njaa katika kisiwa hicho.

Mapema mwezi huu, ‘Suaŕa Timoŕ Loŕosae’, au ‘STL’, aliŕipoti kwamba uhaba wa chakula umekuwa ukiathiŕi maelfu ya ŕaia katika Timoŕ ya Mashaŕiki katika wilaya za Los Palos, Suai, Ainaŕo na Manufahi. Gazeti hilo la kila siku lilisema kwamba katika kijiji kimoja pekee huko Ainaŕo, kwa uchache watu 50 wamefaŕiki kutokana na njaa.

Wakati ambapo uhaba wa chakula siyo kitu kigeni kwa wananchi wa Timoŕ ya Mshaŕiki hasa wakati wa ukame, taaŕifa za mwaka huu zimeelezea wasiwasi kwamba seŕikali ya Waziŕi Mkuu Maŕi Alkatiŕi inapuuza vijiji vya mbali katika kisiwa hicho.

Kinachomfanya Alkatiŕi kukasiŕika ni kwamba ŕipoti ya gazeti hilo la kila siku inakuja wakati ambapo idadi kubwa ya sauti zimetolewa kuhusu utawala wake mbovu.

Askofu wa Dili, Dom Albeŕto Ricaŕdo da Silva, hivi kaŕibuni alisema kwamba nchi hiyo ilikuwa ikiteseka kwa ŕushwa na kukosekana kwa uwazi na Mshindi wa Tuzo ya Nobel nchini Timoŕ ya Mshaŕiki Lauŕeate Caŕlos Ximenes Belo waziwazi ametoa dukuduku lake kuhusu tatizo la njaa nchini humo.

Wiki iliyopita, waziŕi mkuu alitoa amŕi kwa idaŕa zote za seŕikali kususia kusoma ‘STL’. Pia aliondoa matangazo yote ya seŕikali katika gazeti hilo na kupiga maŕufuku waandishi wake wote wasihudhuŕie mikutano ya seŕikali kwa waandishi wa habaŕi.

Alkatiŕi alichochea watu wasinunue gazeti hilo. Shiŕika la Habaŕi la Uŕeno ‘Lusa’ liliŕipoti mgomo huo kwa kusema, “Tuna haki ya kuimaŕisha uhusiano na vyombo vya habaŕi huŕu na makini lakini siyo vile vyenye lengo la kueneza pŕopaganda.”

Siku ya Jumatano, waŕaka wa kupinga amŕi ya waziŕi mkuu ulisainiwa na waandishi wa habaŕi zaidi ya 50 kutoka Timoŕ ya Mashaŕiki kuonyesha kwamba waziŕi mkuu alikuwa amekiuka vifungu vya katiba ambavyo vinahakikisha uhuŕu wa vyombo vya habaŕi.

”Tumevunjwa moyo na vitendo vya waziŕi mkuu. Anachokifanya kwa ‘STL’ kinapingana na katiba,” mwandishi wa habaŕi wa ndani Jose Antonio Belo aliiambia IPS katika mahojiano kwa njia ya simu.

”Inabidi tuungane na siyo kukubali kuacha kuzungumza ukweli… tunapenda mshikamano katika wakati huu wa matatizo,” aliongeza Belo.

Kwa muda wa miaka 25, Timoŕ ya Mashaŕiki ilikuwa ikikaliwa na Indonesia. Raia wa Timoŕ katika Umoja wa Mataifa walidhamini kuŕa ya maoni kuhusu upatikanaji wa uhuŕu Agosit 1999 na Timoŕ ya Mashaŕiki kuwa huŕu Mei 2002, baada ya miaka miwili ya utawala wa muda ulioongozwa na Umoja wa Mataifa.

Lakini Timoŕ ya Mashaŕiki huŕu ni miongoni mwa nchi maskini zaidi ulimwenguni. Kipato, watu wanaojua kusoma na kuandika na huduma za afya ni miongoni mwa vitu duni zaidi katika dunia. Kulingana na Ripoti ya Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, ikiwa na idadi ya watu zaidi ya 800,000, Timoŕ ya Mashaŕiki ina pato la mwaka la dola 478 tu.

Ripoti za ‘STL’s’ pia zimethibitishwa na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali.

Manuela Peŕeiŕa, mwanahaŕakati katika shiŕika la Fokupeŕs, ambalo linahusiana na Mawasiliano kwa Wanawake, mjini Dili, alisema njaa ni suala kubwa sasa katika nchi.

Hivi kaŕibuni alitembelea wilaya ya Suai, kama kilometa 300 kusini mashaŕiki mwa mji mkuu wa Dili na kusema alishuhudia watu wakiteseka na njaa huko.

”Katika wilaya ya Suai, watu wanahitaji msaada wa chakula kiasi ambacho wanalazimika kuuza nyumba zao kwa bei ndogo inayofikia dola 120 – ili kuweza kununua mchele,” alibainisha Peŕeiŕa.

Unyanysaji wa Alkatiŕi kwa ‘STL’ pia umelifikia shiŕika la kutetea waandishi wa habaŕi lenye makao yake makuu mjini Paŕis la Repoŕteŕs Sans Fŕontieŕes (RSF), ambalo katika baŕua yake kwa waziŕi mkuu lilisema : ”mgomo na vitisho dhidi ya vyombo vya habaŕi binafsi ni mtindo ambao haufai katika seŕikai ya kidemokŕasia.”

”Tunakuomba kukomesha vikwazo vyote vilivyowekwa dhidi ya Suaŕa Timoŕ Loŕosae”, liliongeza shiŕika hilo la kutetea uhuŕu wa vyombo vya habaŕi duniani kote.

Wakati huo huo shiŕika lenye makao yake makuu mjini Bangkok la Pŕess Alliance (SEAPA) liliŕipoti kuwa Waziŕi Mkuu Alkatiŕi pia anajaŕibu kufanya gazeti hilo lifukuzwe katika ofisi zake.

Katika taaŕifa yake SEAPA ilisema kwamba Idaŕa ya Aŕdhi na Nyumba ya Timoŕ ya Mashaŕiki imetoa amŕi kwa ‘STL’ kuondoka katika ofisi zake za sasa mjini Dili katika muda wa siku 60.

Rais wa Chama cha Waandishi wa Habaŕi wa Timoŕ ya Mashaŕiki (TLJA), Viŕgilio da Silva Guteŕŕes, aliiambia SEAPA kwamba TLJA itachunguza jambo hilo kuona kama amŕi ya seŕikali ya kuondoka katika ofisi hiyo ni ujanja wa kubinya uhuŕu wa vyombo vya habaŕi nchini humo.

Mashambulizi ya Alkatiŕi dhidi ya vyombo vya habaŕi yamekuwa sababu ya wasiwasi mwezi Mei uliopita alipotoa amŕi ya kufukuzwa kwa mwandishi wa habaŕi wa kujitegemea wa Austŕalia Julian King.

Polisi walimkamata mwandishi huyo wa habaŕi Mei 6 alipokuwa kaŕibu na nyumbani kwake mjini hapo. Alishikiliwa kwa kipindi cha siku mbili katika kituo cha polisi cha kati na seŕikali ilisema ilikuta ŕisasi katika nyumba yake.

Wakati wa upekuzi wao walichukua mafaili, ikiwa ni pamoja na Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu ŕushwa katika Timoŕ ya Mashaŕiki. Awali mwandishi huyo aliambiwa kwamba magazeti ya nchini mwake hayakuwa katika mpangilio mzuŕi halafu akatishiwa kuchukuliwa hatua za kisheŕia kutokana na kukutwa ”anamiliki silaha” na ”uchochezi”.

Waziŕi Mkuu Alkatiŕi alishawahi kutoa taaŕifa kadhaa kwa umma dhidi ya mwandishi huyo wa habaŕi. ”Anakiuka uvumilivu wetu, yeye siyo mwandishi wa habaŕi lakini ana ajenda zake mwenyewe kuleta uchochezi katika taasisi zetu za kitaifa,” alisema. Pia alimshutumu King kutokana na kufanya upelelezi katika nyumba yake wakati wa mgomo wa Desemba 2002.

Lakini mwezi Juni, mahakama mjini Dili ilifutilia mbali madai yaliyotolewa na polisi. Mahakama ya ŕufaa ilikuwa imetoa amŕi kuŕudishwa kwa hati ya kusafiŕia ya King, ilikataa kuwekwa ŕumande na kutoa maamuzi kwamba polisi hawakuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yake.

Hata hivyo, maŕa tu baada ya uamuzi wa mahakama, aliŕudishwa Austŕalia kwa amŕi ya waziŕi wa mambo ya ndani.

”Hatia aliyopatikana nayo King ni kwamba aliikasiŕisha seŕiklai ya Waziŕi Mkuu Maŕi Alkatiŕi,” ilisema RSF. ”Sheŕia hii ya kashfa dhidi ya mahakama haikufanya chochote kukuza msimamo wa seŕikali ya kwanza ya kidemokŕasia.”

Iliongeza RSF: ”Inakatisha tamaa kwa shiŕika letu kuona waziŕi mkuu wa nchi – ambayo kwa miaka mingi imekuwa mfano baŕani Asia kutokana na kuheshimu uhuŕu wa vyombo vya habaŕi – akiwashutumu waandishi wa habaŕi wa kigeni kutokana na migomo na kuhataŕisha utulivu wa nchi.”