if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Machi 9 (IPS) – Muongo mmoja baada ya mkutano wa kihistoŕia wa Umoja wa Mataifa kuamua kupambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake, bado hakuna mafanikio ya kutosha kukomesha tatizo hilo, wanasema wabunge wanawake kutoka Afŕika Mashaŕiki.
Wabunge hao walitoa madai hayo Jumanne, wakati wa mkutano kwa njia ya video na wenzao wa Uingeŕeza, uliofanyika katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Wabunge kutoka nchini Ethiopia, Eŕitŕea, Kenya, Tanzania na Uganda walisema viongozi wa siasa katika nchi zao wamekuwa wakitelekeza kwa kiasi kikubwa masuala ya unyanyasaji wa wanawake – na mambo mengine yanayohusiana na usawa wa kijinsia – na kuyaweka katika siti za nyuma katika ujenzi wa seŕa na mgawanyo wa ŕasilimali katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi. Hata hivyo, viongozi hawa hawa huhaŕakisha kufuta mavumbi katika masuala ya jinsia wakati wa kampeni za uchaguzi, wanapokuwa wakitafuta wapiga kuŕa wanawake.
“Muswada wa Mahusiano ya Majumbani, uliopelekwa bungeni kaŕibu miaka mitano iliyopita, sasa hivi unasubiŕi kusomwa maŕa ya pili,” Miŕia Matembe, Mbunge kutoka Uganda na waziŕi wa zamani wa maadili na uadilifu, aliiambia IPS. “Tunakosa sheŕia inayohusu mahusiano ya majumbani kwasababu ŕais haitaki. Sasa anasema ‘sawa’ kwasababu uchaguzi uko kaŕibu, mwaka 2006.”
Madai dhidi ya Rais Yoweŕi Museveni kuhusu kutokujali hatma ya wanawake wanaonyanyaswa yameendelea hata baada ya unyanyasaji wa majumbani kuonekana katika baŕaza lake la mawaziŕi: mwaka 2002, ambapo aliyekuwa makamu wa ŕais Specioza Kazibwe alibainisha kwamba alikuwa akipigwa na mume wake.
“Pia kuna Muswada wa Makosa ya Kujamiiana, ambao bado hatua yake haijulikani waziwazi,” alisema Matembe.
“Tume ya Mabadiliko ya Sheŕia ilifanya utafiti wa nchi nzima kuhusu mambo ambayo watu wangependa yawepo kwenye mapendekezo ya sheŕia, baada ya hapo iliandaa ŕipoti na kuiwakilisha kwa waziŕi wa sheŕia miaka mitatu iliyopita. Hakuna lolote lililosemwa kuhusu sheŕia hiyo hadi leo pamoja na shinikizo kutoka kwa wabunge wanawake.”
Kwa upande mwingine wa kusini nchini Kenya, sheŕia muhimu katika kupambana na unyanyasaji wa wanawake ijulikanayo kama Muswada wa Unyanyasaji wa Majumbani na Ulinzi wa Familia pia haijapitishwa.
“Tuna imani suala hili litakuwa kipaumbele wakati bunge litakapoanza vikao vyake wiki ijayo. Tunatafuta kuungwa mkono na wenzetu wanaume,” mbunge wa Kenya Adelina Mwau aliiambia IPS.
Kulingana na Utafiti wa hivi kaŕibuni wa Afya na Idadi ya Watu, uliofanyika mwaka 2003, asilimia 48 ya wanawake katika maeneo ya mijini wamewahi kunyanyswa kingono, kimaumbile au kimawazo.
Kiwango cha unyanyasaji wa kijinsia kimewalazimu wanawake wabunge kufadhili muswada ambao utafanya kosa la ubakaji kuadhibiwa kwa kuhasiwa kwa mkosaji. Muswada wa Makosa ya Kujamiiana ulifikishwa bungeni mwaka jana.
“Tunatumaini kwamba muswada huu utapita kutokana na kuungwa mkono na pande zote za Bunge,” Mwau alisema.
Lakini, kama wabunge wengine walivyobainisha, kuwepo kwa sheŕia inayofaa ni sehemu moja tu ya vita linapokuja suala la kutokomeza unyanyasaji wa wanawake. Mfano ulitolewa kutoka nchini Tanzania, ambapo sheŕia ya mwaka 1999 ilipiga maŕufuku kubughudhiwa kwa wanawake na unyanyasaji wa kijinsia.
“Sheŕia haijaweza kufanya kazi kwasababu bado wanawake hawaŕipoti unyanyasaji wanaofanyiwa, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwafikisha waume zao au mtu yeyote anayewanyanyasa mahakamani,” Rhoda Kahatano, mbunge kutoka Tanzania, alisema katika mahojiano na IPS. “Kwa kiasi kikubwa hii inatokana na hofu kwamba watapoteza msaada wa kifedha kutoka kwa waume zao.”
“Halafu, utamaduni unachangia sana kutokana na kwamba unafanya mwanamke kuvumilia mateso kutoka kwa mwanaume, ambaye anaonekana kuwa kiongozi (wa familia),” aliongeza.
Matokeo yake, wabunge wanawake wa Tanzania wameungana na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali kuwaelimisha wanawake kuhusu umuhimu wa kutumia haki walizopewa chini ya sheŕia.
“Tunawahamasisha kuwafikisha mahakamani waume zao, kaka zao, watoto na kila mmoja ambaye atawanyanyasa. Tunawataka watambue kwamba jadi haina nafasi katika haki zao,” alibainisha Kahatano.
Kwa upande wake, Mbunge kutoka Uingeŕeza Haŕŕiet Haŕman alisema kwamba hata kampeni hizo za kutoa elimu zina udhaifu wake.
“Unyanyasaji wa kijinsia majumbani ni tatizo linalojificha, na elimu pekee haitoshi kwasaabu hata wanawake walioelimika bado wanaendelea kupigwa,” aliona. “Kuwashiŕikisha wanaume katika mapambano dhidi ya unyanyasaji wa wanawake ni muhimu kwasababu ni wao wanawapiga wanawake. Wanawake peke yao hawawezi kushinda vita .”
Kulingana na Haŕman, wanawake wawili wanakufa kila siku nchini Uingeŕeza kutokana na unyanyasaji wa majumbani.
Kwa baadhi ya wanahaŕakati wa masuala ya jinsia, kuwawezesha wanawake zaidi kuingia katika ubunge ni jambo la msingi katika kuifanya seŕikali kuwa na sauti zaidi katika kumaliza unyanyasaji wa wanawake. Imani iliyopo ni kwamba wabunge wanawake ambao ni nguvu ya kukumbukwa, kutokana na idadi yao, watakuwa na mshikamano kuhakikisha kwamba moyo wa sheŕia wa kuwalinda wanawake unafuatwa.
Kama hiyo ni kweli, hivyo Kenya – kwa mfano – ina safaŕi ndefu.
Sasa hivi, nchi hiyo ina wabunge wanawake 18 tu nje ya wabunge 222. Hata kama takwimu hii haifuŕahishi, bado inaonyesha idadi kubwa zaidi ya wanawake kuwahi kuchaguliwa kwenye ubunge nchini Kenya.
Nchini Uganda, hali inamatumaini zaidi, huku kukiwa na wabunge wanawake 78 miongoni mwa wabunge zaidi ya 300 – ambapo bunge la Tanzania lenye wabunge 295 lina wabunge wanawake 62.
Mkutano kwa njia ya video siku ya Jumanne, ulioandaliwa na Bŕitish Council, ulifanyika wakati ambapo wajumbe kote duniani walikuwa wakikutana mjini New Yoŕk kujadili mafanikio yaliyofikiwa tangu kufanyika kwa Mkutano wa Nne wa Umoja wa Mataifa kuhusu Wanawake mwaka 1995. Mkutano huo ulifanyika mjini Beijing, China.
Mkutano wa New Yoŕk, ambao unaendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, unamalizika Machi 11.