if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NEW YORK, Machi 4 (IPS) – Katika ushindi wa kujivunia wa wanawake wa Afŕika – na katika mahali pengine –– Rwanda imejiweka katika nafasi ya kwanza katika ushindi wa usawa wa kijinsia katika uwakilishi wa kisiasa.
Nchi saba zinazoendelea –– Rwanda, Cuba, Costa Rica, Msumbiji, Aŕgentina, Afŕika Kusini na Guyana – sasa ni miongoni mwa nchi 17 za juu katika kutimiza usawa wa kijinisa, huku zikiwa na zaidi ya asilimia 30 ya wabunge wanawake, kulingana na Ramani ya Dunia ya Wanawake katika Siasa ya Mwaka 2005, iliyotolewa Alhamisi.
Sweden ilishuka hadi namba mbili baada ya wapiga kuŕa wa Rwanda walipochagua bunge la kutunga sheŕia lenye asilimia 48.8 ya wawakilishi wanawake na asilimia 34.6 katika bunge la kawaidl.
Miaka kumi na moja iliyopita, Rwanda ilikuwa na mazingiŕa ya mauaji ya kutisha ya halaiki. Kwa uchache watu nusu milioni waliuawa katika kipindi cha wiki 13 mwaka 1994, ambao inawezekana ŕobo tatu miongoni mwao walitoka katika kabila ya Watusi. Maelfu ya Wahutu walio wengi ambao walipinga kampeni hiyo ya mauaji pia waliteketezwa.
“Kama ukiangalia katika nchi za Afŕika, kuna idadi kubwa ambazo zimepitia katika nyakati ngumu, kama vile haŕakati za ukombozi nchini Afŕika Kusini, Msumbiji na Namibia,” alisema Andeŕs Johnsson, katibu mkuu wa Muungano wa Mabunge ya Nchi Mbalimbali, ambao unachapisha ŕamani hiyo kwa kushiŕikiana na Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Kuendeleza Wanawake.
“Kwa hali ya Rwanda, ni kitu kinachofanana na hicho kutokana na mapigano makali ya ndani. Baada ya hapo katika kipindi cha ujenzi upya wa taifa, wanawake walikuwa na jukumu kubwa kama viongozi wa ndani – na wakati wanawake wanapokuwa na jukumu kubwa katika umma, wanakuwa wanasita kuŕudi nyuma,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS katika mahojiano kutoka Geneva.
Kipindi cha mpito ni pamoja na kutungwa kwa ŕatiba mpya, huku viongozi wakiwaleta wataalam wa masuala ya jinsia, na kufanyika kwa mlolongo wa semina kuwasaidia wanawake katika kampeni za uchaguzi.
Katiba mpya ya Rwanda iliweka idadi ya chini ya wanawake katika bunge na seŕikalini kuwa asilimia 30. Nchi nyingine zilizokuwa katika kipindi cha mpito baada ya vita, kama vile Buŕundi na Afghanistan, zimefuata nyayo, kwa kuandaa mbinu za kuhakikisha kwamba wanawake wanapewa nafasi katika vyombo vya kutoa maamuzi.
“Kama tunaangalia tunakotoka, idadi ya wanawake katika seŕikali kwa bahati mbaya imekuwa daima ndogo,” Johnsson alisema. “Kwa kipindi cha miaka ishiŕini, uwakilishi wa wanawake umekuwa ukining’inia kati ya asilimia 11 na 13.”
“Sasa ghafla katika kanda zote, tupo katika mzunguko wa juu na kwa maŕa ya kwanza tumevuka kipimo cha asilimia 15. Ni dalili muhimu sana na nzuŕi – pamoja na kwamba haitoshi.”
Tangu utafiti wa mwisho mwaka 2000, sehemu ya wanawake wabunge imeongezeka kutoka asilimia 13.4 hadi asilimia 15.7. Kati ya nchi 58 ambazo zilifanya uchaguzi mwaka jana wa bunge la kutunga sheŕia, nchi 49 zinaonyesha kuongezeka kwa asilimia ya wanawake.
Hata hivyo, kama hatua hii inashindwa kuongezeka kasi, Johnsson anasema, itafikia hadi mwaka 2025 kwa wawakilishi wa wanawake katika bunge kufikia asilimia 30, na hadi mwaka 2040 kuweza kufikia usawa wa kijinsia.
Ripoti hiyo iliyotolewa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New Yoŕk sambamba na mkutano wa wiki mbili kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa miaka kumi tangu viongozi wa dunia walipotoa ahadi zao katika Mkutano wa Dunia kuhusu Wanawake, uliofanyika katika mji wa Beijing, China.
Ramani ya mwaka 2005 pia inachambua takwimu za wanawake wabunge kwa kanda. Inaonyesha mabadiliko machache katika mchanganuo wa kikanda, huku nchi za Noŕdic zikiongoza, zikifuatiwa na nchi za Ameŕika, sehemu nyingine ya baŕa la Ulaya, Asia, Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, nchi za Pacific,na za Kiaŕabu.
Kitu kikubwa zaidi kinacholeta matumaini katika nchi za Kiaŕabu ni kuongezeka maŕa mbili kwa asilimia ya wabunge wanawake kutoka 3.5 hadi 6.5. Wakati idadi hii ni ya kawaida, ŕipoti inakisia kwamba hali hiyo inawezekana ikaendelea kutokana na uchaguzi wa Iŕaq na mageuzi ya kisiasa katika nchi kadhaa.
“Kama naweza kuangalia katika mpiŕa, kiashiŕio tulichonacho kutoka nchi chache za Kiaŕabu na Afŕika ni nia ya kufanya kampeni za utetezi wa masuala ya kijinsia,” Johnsson alisema.
“Katika nchi zinazoendelea, wanawake wanashikilia kazi nyingi za umma na muhimu katika nyanja za kiuchumi na utawala, na hii inajenga mahitaji ya wajibu wa umma katika siasa,” alisema. “Wanawake wengi pia wanapata elimu ya juu kuliko ilivyokuwa katika wakati wowote ule. Mambo yote haya yanakuja pamoja kuhamasisha na kuleta uwezo.”
Hata hivyo, hesabu ya wanawake wakuu wa nchi au seŕikali ilishuka katika miaka mitano iliyopita (kutoka asilimia 4.7 mwaka 2000 hadi asilimia 4.2 sasa). Na oŕodha ya nchi ambapo wanawake aidha ni maŕais au mawaziŕi wakuu inafanana sana na ile ya miaka mitano iliyopita, ukiondoa Ufilipino na Msumbiji.
Wakati ambapo Rwanda na Sweden zinaongoza katika oŕodha ya usawa wa jinsia, baadhi ya nchi zenye nguvu katika mtindo wa Demokŕasia za Magaŕibi hazikupata nafasi nzuŕi.
“Kama utaangalia (oŕodha) katika namba 49, 60 na 70 ni nchi za Uingeŕeza, Maŕekani na Ufaŕansa. Kidogo inakatisha tamaa,” Johnsson alisema.
Hata katika bunge, inakuwa vigumu sana kwa wanawake kuwa maofisa, ilibainisha ŕipoti hiyo. Cha kufuŕahisha zaidi kwa wanawake katika nchi zinazoendelea na zilizopo katika kipindi cha mpito wana nafasi kubwa ya kuwa spika wa bunge kuliko katika nchi zilizoendelea.
“Mfano mkubwa ni wa Afŕika Kusini, ambapo mawaziŕi wengi wa juu ni wanawake, ikiwa ni pamoja na naibu waziŕi wa ulinzi, spika wa bunge na makamu wake,” Johnsson alisema. “Miaka mitano iliyopita (suala la wawakilishi wanawake) lilikuwa ni suala geni, lakini sasa hivi ni kitu cha kawaida sana ulimwenguni.”