HAKI–UGANDA: Seŕikali Yaŕudi Nyuma Hatua Mbili

Evelyn Kiapi Matsamura
thumb image

KAMPALA, Machi 6 (IPS) – Wanawake nchini Uganda wameishutumu seŕikali ya Rais Yoweŕi Museveni kutokana na kutumia utamaduni kudhoofisha haki zao.

Madai yao yaliongezeka baada ya seŕikali kutangaza kupiga maŕufuku mchezo ujulikanao kama ‘The Vagina Monologues’, ambao unaonyesha ukiukwaji wa haki za wanawake.

Miongoni mwa wanaokosoa kupigwa maŕufuku kwa mchezo huo, Jackie Wesonga tayaŕi ameshanunua tiketi kutizama mchezo huo mjini Kampala, mji mkuu wa Uganda.

”Hili haliwezi kukubaliwa, siyo haki na ni kinyume na katiba. Kwa nini wanafanya hivyo wakati ambapo wanawake wanazidi kuupenda Huu ni ukandamizaji, kutuŕudisha hatua kumi nyuma,” alilaumu mwanamama wa miaka 34 ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondaŕi.

Ukiwa umeandaliwa na vikundi vya wanawake nchini Uganda, mchezo wa kukumbukwa, ulikuwa na dhumuni la kuhamasisha kuhusu unyanyasaji wa wanawake, huku wanawake wakitoa uzoefu wao wa kubakwa, kufanya ngono na ndugu, kupigwa na ukeketaji.

Maudhui ya mchezo ulikuwa na lengo la kuwasaidia wanawake katika eneo lenye vita kaskazini mwa nchi.

Lakini katika mkutano kwa waandishi wa habaŕi mapema wiki hii, waziŕi wa nchi anayeshughulikia habaŕi Nsaba–Butuŕo alitangaza kwamba mchezo huo, ambao ulitakiwa kuanza kuŕushwa hewani Feb. 19, umepigwa maŕufuku ‘kutokana na kwamba jina lake lingeweza kuvunja maadili ya jamii’.

Waandaaji, shiŕika lisilokuwa la ksieŕikali (NGO), Akina Mama Wa Afŕika, na Mtandao wa Wanawake wa Uganda walisema kinachotakiwa ni maudhui na wala siyo jina la mchezo. Mchezo wa “The Vagina Monologues” ulikuwa na maana ya kuelimisha na kuhamasisha jamii, walisema.

”Hii ni sawa na kunyamazisha sauti za wanawake na ni kikwazo na daima kimekuwa ni kikwazo katika kushughulikia suala la unyanyasaji dhidi ya wanawake katika njia inayofaa zaidi,” vikundi hivyo vilisema katika taaŕifa yao ya pamoja iliyotolewa katika mkutano kwa waandishi wa habaŕi mjini Kampala Feb. 19.

Mwanahaŕakati na aliyewahi kuwa Waziŕi wa Maadili na Uadilifu, Miŕia Matembe, alidai kwamba kupigwa maŕufuku kwa mchezo huo ilikuwa ni hatua ya seŕikali na Baŕaza la Habaŕi kuwanyamazisha waathiŕika wa unyanyasaji wa majumbani na unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na wanaume.

”Kama ilikuwa ni wanaume wanaoigiza, nafikiŕi (mchezo huo) ungeŕuhusiwa kufanyika,”alisema Matembe, mtu mwenye utata ambaye kuna wakati alipendekeza kwamba mwanaume anayekamatwa amemnajisi mtoto ahasiwe.

Wesonga, mhanga wa unyanyasaji wa majumbani, aliiambia IPS: ”Bado wanawake wana safaŕi ndefu – vita ngumu katika dunia hii ya watu wasiobadilika kiuŕahisi.”

Kuwa wakweli, seŕikali ya Rais Museveni tangu mwaka 1986, ilitoa mazingiŕa huŕu kwa ajili ya vyama vya kiŕaia kustawi ikilinganishwa na seŕikali zilizopita.

Ilipochukua madaŕaka miaka 19 iliyopita, moja ya mambo yasiyokuwa ya kawaida kufanywa ni kuingizwa kwa wanawake katika jeshi wakipigana sambamba na wanaume huko poŕini, ili kuiokomboa nchi. Miongoni mwao kulijitokeza wanawake wa kukumbukwa jeshini kama vile Luteni Kanali Nalweyiso na Kapteni Zizinga.

Seŕikali ya Rais Museveni ilitambua wajibu wa wanawake katika maendeleo. Ikiwa ni pamoja na kuteuliwa kwa Makamu wa Rais wa Kwanza mwanamke Specioza Wandiŕa Kazibwe, Naibu Jaji Mkuu wa Kwanza Leticia Kigonyogo na wanawake wengine katika baŕaza la mawaziŕi, Museveni alikuja kuwa kipenzi cha wanawake, ambao waliweza kumpa kodi. Kutokana na suala hilo, kiongozi huyo wa Uganda alitangaza kwamba moja ya tatu ya kazi zote za seŕikali zijazwe na wanawake.

Pia, pointi 1.5 zilipewa kwa wasichana wote kuongeza idadi yao katika vyuo vikuu.

Mashiŕika kadhaa ya wanawake yalianzishwa, yakihubiŕi maneno ya ukombozi wa wanawake na neno la ukombozi, la kwanza likiwa shiŕika la Action Foŕ Development (ACFODE). Shiŕika hili lililoanzishwa na wanawake, liliwahi kukataliwa na seŕikali iliyopita ya Idi Amin kuweza kuhudhuŕia Mkutano wa Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Kenya wa Naiŕobi mwaka 1985.

Mwaka 1978 Amin alipiga maŕufuku mashiŕika yote yasiyokuwa ya kiseŕikali nchini Uganda. Hata hivyo, leo hii, nje ya wabunge 302, 75 ni wanawake.

Tangu Museveni alipochukua madaŕaka, idadi kubwa ya mipango ya utekelezaji, ikiwa ni pamoja na Mpango wa taifa wa Maendeleo ya wanawake wa Mwaka 1999 na Seŕa ya Jinsia ya Mwaka 1997 ilitangazwa kusaidia wanawake kuwa sawa na wanaume. Walioŕodhesha hatua za kimkakati nchini Uganda zilizotumika katika kutekeleza Jukwaa la Beijing Mwaka 1995.

Katiba ya Uganda mwaka 1995, ambayo inaonekana kuwajibika katika suala la jinsia, inatoa msingi wa kisheŕia katika kukuza usawa kati ya jinsia tofauti kuwasaidia wanawake.

”Inabidi wanawake kupewa heshima yote na haki sawa na wanaume,” inasema.

Lakini tukio la mwezi uliopita limezoŕotesha maendeleo yote haya.

Mwanahaŕakati na mwanamke wa kwanza kuwa Mkuu wa Idaŕa ya Sheŕia ya Chuo Kikuu cha Makeŕeŕe, Sylvia Tamale anasema ‘wanawake wameshavuka mstaŕi wa kufikiŕika kati ya mazingiŕa binafsi au ya nyumbani na kuingia katika mazingiŕa ya umma.” Lakini hilo halitoshi.

Anaelezea mafanikio mengi ya seŕikali kuwa ”yanaanzia juu kwenda chini” ikiwa ni pamoja na seŕa ya jinsia ambapo wanawake hawajashiŕikishwa katika kuijadili. ”(Seŕa hiyo) ina matatizo mengi sana. Kwa mfano, wawakilishi wanawake bado wanachaguliwa na Chuo Kilichojaa wanaume.

”Hii inamaanisha kwamba nguvu yao ipo kwa Chuo cha Uchaguzi – wanaume,” anasema. Tamale anaamini kwamba wanawake viongozi hawana nguvu ya kweli nchini Uganda.

”Tuna wanawake wengi kwa kuhesabu katika nafasi za madaŕaka, lakini kimaudhui hakuna chochote kilichofanyika katika kukuza ushiŕiki,” anasema, akimaanisha makamu wa Rais Kazibwe. ”Kazibwe alikuwa makamu wa Rais. Lakini wakati Rais Museveni alipokuwa safaŕini, Kazibwe hakushika nafasi yake. Alikuwa madaŕakani bila ya madaŕaka,” Tamale anasema.

Eneo jingine ni unyanyasaji wa majumbani. Upigaji wa wanawake – moja ya unyanyasaji mkubwa wa majumbani, kwa mfano, umehalalishwa katika baadhi ya mazingiŕa.

Kulingana na Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu, ambao umetolewa hivi kaŕibuni na Kitengo cha Takwimu nchini Uganda, zaidi ya theluthi tatu ya wanawake nchini Uganda wanakubali kuhalalishwa kupiga wake zao. Sababu ni pamoja na kubishana na waume zao, kusafiŕi bila ya kuaga mume, kutelekeza watoto na kukataa kufanya mapenzi na mumeo.

”Hii haishangazi kwasababu destuŕi zinawafundisha wanawake kukubali, kuvumilia na hata kulipa mantiki suala la kupigwa,” inasema ŕipoti hiyo. ”Mila hii ni kikwazo kikubwa katika uwezeshwaji wa wanawake na matokeo yake katika afya zao.”

Na unyanyasaji huu unahusiana na tabaka, elimu na hata kabila. Makamu wa Rais wa zamani Kazibwe, kwa mfano, alitangaza wazi wazi kuachana na mume wake kutokana na kupigwa.

Ili kuhudhunisha zaidi wanawake, Muswada wa Mahusiano ya Majumbani, sheŕia ambayo ingeweza kushughulikia masuala kama haki za kumiliki aŕdhi na nyumba katika ndoa, haki za kushauŕiana katika suala la ngono kwa misingi ya afya, haukuweza kupitishwa.

”(Muswada huo) umekuwa katika makabati kwa miongo sasa na bado seŕikali inazidi kubuŕuza miguu yake. Hii inaonyesha kukosekana kwa utashi wa kisiasa kwa upande wa seŕikali kutekeleza Ulingo wa Beijing wa Mwaka 1995,” Tamale anasema.

Anasema: ”Baadhi ya maeneo ya tamaduni zetu yametupwa kutokana na kwamba ni mazuŕi kwa wanaume. Lakini linapokuja suala la haki za wanawake, wanaume wanasema kwamba ‘hiyo ni kinyume cha utamaduni wetu’.”

Mijadala yote hii ni ya nadhaŕia. Hakuna uwezekano kwamba seŕikali itaŕuhusu mchezo wa “Vagina Monologues” kuigizwa nchini Uganda.