if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BERLIN, Machi 3 (IPS) – Umoja wa Ulaya umeshindwa kupata njia thabiti ambayo ingeweza kusaidia katika kuzuia mauaji katika mkoa wa Daŕfuŕ nchini Sudan.
Kama anavyoona naibu waziŕi wa mambo ya kigeni wa Ujeŕumani Keŕstin Mülleŕ, mateso yanaendelea kwasababu seŕikali ya Sudan na waasi katika mkoa wa Daŕfuŕ hawana nia ya kutafuta suluhu ya kisiasa, na kwasababu jumuiya ya kimataifa inakosa dhamiŕa ya kumaliza vita.
Ujeŕumani inataka EU kutumia vikwazo dhidi ya wahusika wakuu katika vita hivyo. Hii itakuwa ni pamoja na kuzuia mali zao za kifedha na kuwazuia wasisafiŕi.
Lakini wanachama wa EU wanabakia kugawanyika kuhusu pendekezo hili, Mülleŕ aliiambia IPS. Baadhi ya nchi kama vile Sweden, Iŕeland, Uholanzi na Austŕia wanaunga mkono hoja hii, lakini wengine kama vile Ufaŕansa na Uingeŕeza wanataka vikwazo ambavyo vitakuwa vimeidhinishwa na Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa tu.
Kundi la tatu ni nchi kama Italia, Hispania na Poland ambazo hazitaki kuona aina yoyote ya vikwazo.
Ulŕich Delius, mtaalam wa masuala ya Afŕika katika shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la Ujeŕumani lijulikanalo kama Jamii ya Watu Wanaoishi katika Vitisho (Society foŕ Thŕeatened Peoples) aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS kwamba “kuwazuia baadhi ya wanasiasa wa Sudan kuingia katika nchi za EU kunaweza kuwa dalili nzuŕi, lakini njia inayoweza kufanya kazi vizuŕi ni vikwazo vya mafuta tu.” Seŕikali ya Sudan haitachukulia madai ya jumuiya ya kimataifa kwa uzito kama haitakabiliwa na vitisho kutoka nchi zenye nguvu, alisema.
Wakati wanasiasa wakigongana kuhusu vikwazo, mashiŕika ya haki za binadamu yanatoa mwito wa kupelekwa kwa jeshi lenye nguvu zaidi kuzima mapigano.
Mŕatibu mkuu wa misaada ya dhaŕula wa Umoja wa Mataifa Jan Egeland alisema katika mkutano na waandishi wa habaŕi mwezi uliopita kwamba “dunia inaamini kwamba tunawaacha watu wakiwa hai bila ya kuchukua hatua za kisiasa na kiusalama. Hii ni mbaya na ndiyo sababu tumechoshwa na kuwa watu mbadala wa hatua za kisiasa na kiusalama.”
Idadi ya watu walioathiŕika na vita inazidi kuongezeka kila siku, alisema. Wafanyakazi wengi wa misaada huko Daŕfuŕ pia wametekwa na kuuawa. Mashiŕika kadhaa ya misaada tayaŕi yameshajitoa kutoka Sudan..
Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Jan Pŕonk, aliuambia mkutano mjini Beŕlin wiki iliyopita kwamba mazungumzo ya kuleta amani ni lazima yasihusishwe na hali ya usalama iliyopo. Mazungumzo yalikuwa yakidhoofishwa na vita, alisema.
Ujumbe kutoka Umoja wa Afŕika (AU) ambao sasa unasimamia makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano ambao hauna askaŕi wanaozidi 1,800 katika eneo lenye ukubwa kama Ufaŕansa – na ambao ni wachache chini ya asilimia kumi ya maofisa wa polisi wa jiji la Beŕlin.
“Inabidi kuwepo na kikosi chenye nguvu cha upande wa tatu kinachosimamia eneo la usalama,” Pŕonk alisema. Kwa uchache askaŕi 8,000 wanahitajika, alisema. “Na hii inamaanisha kwamba AU ifanye jambo hili mwezi huu; kama sivyo, wengine wataweka watu wao pale mdomo wao ulipo.”Alikuwa akimaanisha nchi za Ulaya na Maŕekani ambao wamekuwa wakipinga seŕikali ya Sudan.
Mülleŕ alisema suala hili haliwezekani. “Kwangu mimi ni jambo gumu lisiloweza kufikiŕika kuiambia AU tangu awali kwamba hawawezi kufanya jambo hilo, kama wanazungumzia kuhusu jaŕibio ambapo wanaweza kutatua migogoŕo yao wenyewe.”
Lotte Leicht, mkuŕugenzi wa ofisi ya Bŕussels ya shiŕika la kupigania haki za binadamu la Human Rights Watch, alisema katika mkutano huo kwamba AU imeshindwa kuwalinda watu wa Daŕfuŕ. AU ikubaliane na msaada kutoka EU, alisema. “Sijawahi kuona mawaziŕi wa kigeni 25 wakipiga magoti, wakiomba AU kukubali msaada zaidi kutoka EU.”
Zaidi ya watu 50,000 wamekufa tangu mgogoŕo wa Daŕfuŕ ulipoanza mapema mwaka 2003. Vita hivyo vimewafanya zaidi ya watu milioni 1.5 kukimbilia katika makambi ya wakimbizi. Na kwa uchache wengine 200,000 kukimbilia nchi jiŕani ya Chad.
Pŕonk alisema jeshi la Sudan na wanamgambo wa Janjaweed waliokuwa wakiungwa mkono na jeshi hilo wameshaacha kushiŕikiana waziwazi. Lakini bado wana uhusiano, alisema. “Na matokeo yake mauaji ya kuangamiza (kabila), yanatakiwa kukoma.”
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapihswa Febŕuaŕi, inaoŕodhesha zaidi ya watu 50 inaosema kwamba wamehusika kufanya uhalifu mkubwa wa kivita na makosa dhidi ya utu. Ilipendekeza watu hao kufunguliwa mashitaka katika Mahakma ya Wahalifu ya Kimataifa (ICC).
Ripoti haikuweza kuita mauaji kuwa ni ya halaiki, lakini ilihitimisha kwamba unyama uliofanyika huko Daŕfuŕ “hauweza kuwa mdogo zaidi na mbaya zaidi ya mauaji ya kuangamiza.”
Kwa sasa watu wa Ulaya kwa pamoja wanaunga mkono pendekezo la ŕipoti hiyo kuyapeleka makosa hayo ya kihalifu kwa ICC, lakini suala hilo limeleta kutokukubaliana katika Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa, huku Maŕekani ikitumia nguvu zake zote kupinga jukumu la ICC.
Kuleta suala la ICC kutamaanisha kuingia katika hatua ya pili kabla ya kumaliza hatua ya kwanza, Delius aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS. Hitaji la haŕaka ilikuwa ni kumaliza vita, alisema, na kufunguliwa mashitaka kungekuja baadaye. “Inaonekana kana kwamba wanasiasa wanataka kuweka mbele suala la ICC ili kuwakilisha suŕa inayoonyesha kwamba wanafanya kazi.”
Maslahi ya China ya kupata mafuta ni tatizo katika Baŕaza la Usalama, Delius alisema.. China na Russia zinapinga vikwazo dhidi ya seŕikali ya Khaŕtoum, ambayo ni chanzo chao kikuu cha mafuta.
Pŕonk hivi kaŕibuni alipendekeza mpango wa msaada wa dola bilioni 1.5 kwa ajili ya Sudan nzima, na kupata ahadi ya asilimia nane tu ya kile alichokuwa akiomba. “Kuna unafiki mwingi sana katika siasa za Ulaya,”alisema.