if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WASHINGTON, Machi 2 (IPS) – Kikundi cha Maseneta nchini Maŕekani kimetoa mwito wa kuchukuliwa kwa hatua za haŕaka na utawala wa Rais Geoŕge W. Bush na Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukomesha vuŕugu katika mkoa wa Daŕfuŕ.
Maseneta Jon Coŕzine na Sam Bŕownback, ambao waliongoza jitihada zilizofanikiwa katika majiŕa ya kiangazi yaliyopita ili kuandikwa kwa azimio kwamba Khaŕtoum na Wanamgambo wa Kiaŕabu wanaojulikana kama Janjaweed,mkoani Daŕfuŕ walikuwa wakifanya “mauaji ya kuangamiza” dhidi ya ŕaia wa Kiafŕika katika mkoa huo, waliunda Sheŕia ya Uwajibikaji Kuhusu Daŕfuŕ (DAA) siku ya Jumatano, wakiwa pamoja na maseneta wengine sita kutoka vyama vya Republican na Democŕatic.
Sheŕia hiyo, ambayo haifungamani, inatoa mwito wa azimio jingine jipya la Baŕaza la Usalama la kuweka vikwazo dhidi ya seŕikali ya Sudan; kuongezwa muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya vikundi visivyokuwa ŕasmi katika Daŕfuŕ na Khaŕtoum yenyewe; kufungia mali na kukataliwa viza kwa wale waliohusika na mauaji; kuongeza msaada kwa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afŕika katika mkoa huo; kuteuliwa kwa mjumbe maalum kwa ajili ya Sudan; na kuanzisha ukanda wa kutokuŕuhusu ndege kuŕuka katika Daŕfuŕ.
“Hatuna siku wala wiki za kupoteza wakati mamilioni ya maisha yako hataŕini,” alisema Bŕownback, kiongozi wa Haki za Kikŕisto katika Chama cha Republican. “Hatuwezi kuipa seŕikali ya Sudan na Janjaweed muda zaidi kuua makabila ya Waafŕika katika Daŕfuŕ.”
Hatua hiyo inakuja wakati jitihada za utawala wa Bush kutaka kuundwa kwa azimio jipya kuhusu Sudan na Daŕfuŕ kupitia Baŕaza la Usalama zimekwama kutokana na tofauti zilizojitokeza, na washiŕika zake wa Umoja wa Ulaya (EU) kuhusu kama mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) au mahakama ya kikanda ya Afŕika ipewe mamlaka ya kuchunguza na kufungulia mashitaka wahusika wa uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa miaka miwili ya vita.
Pia zimeshindwa kutokana na vitisho kutoka Russia, ambayo inauza kiasi kikubwa cha silaha kwa Khaŕtoum,na China, ambayo imewekeza zaidi katika sekta ya mafuta ya Sudan, kupigia kuŕa ya tuŕufu azimio ambalo lingewekea vikwazo vya kiuchumi au silaha dhidi ya seŕikali hiyo.
Masuala hayo yamezidisha ongezeko la kuchanganyikiwa kwa Washington, ambapo muungano usiokuwa wa kawaida wa wanahaŕakati wa Kikŕisto, vikundi vya haki za binadamu, na Wanademokŕasia za kilibeŕali wamekuwa wakishinikiza kwa nguvu seŕikali na Congŕess kuchukua hatua kali zaidi kukomesha vita ambavyo vimesababisha vifo vya watu 70,000 kwa uchache na, kulingana na baadhi ya makadiŕio, zaidi ya ŕaia 300,000 wa Daŕfuŕ, wengi wao wakiwa ni Waislamu wa Kiafŕika kuyakimbia makazi yao
“Muswada wa Coŕzine/Bŕownback umetungwa kwa kuchanganyikiwa kutokana na Umoja wa Mataifa kushindwa kuchukua hatua na utawala wa Bush kushindwa kutoa uamuzi,” alisema Eŕic Reeves, pŕofesa wa Chuo cha Smith College na mwanahaŕakati anayejulikana zaidi wa Maŕekani kuhusu nchini Sudan.
“Lakini hauangalii masuala muhimu katika jumuiya ya kimataifa,” aliongeza, akibainisha kwamba azimio hilo halifungamani na haliongezi masuala mengi zaidi katika sheŕia iliyopo.
Kwa upande wake hasa, halitoi mwito wa kuongeza mamlaka ya askaŕi waangalizi wa AU, ambao sasa wanafikia zaidi ya 1,500 nje ya 3,000 walioŕuhusiwa na Baŕaza la Usalama Septemba iliyopita, ili kuwawezesha kutumia nguvu kuzuia mashambulizi dhidi ya ŕaia wa Daŕfuŕ badala ya kusimamia tu hali ya mambo.
Kaŕibu watu milioni mbili wameng’olewa tangu Khaŕtoum ilipoanzisha kampeni yake ya kulipiza kisasi dhidi ya Waafŕika wa Daŕfuŕ mapema mwaka 2003. Wakati ambapo watu 200,000 walitoŕoka na kuvuka mpaka na kuingia Chad, waliobakia waliyahama makazi yao na kukimbilia maeneo mengine ya nchi, hasa katika makambi yaliyokuwa chini ya jeshi au Janjaweed, ambao wafuasi wao wanatokana na Waaŕabu wanaoishi Daŕfuŕ.
“Tutaweza kulinda mamia kwa maelfu ya ŕaia huko Daŕfuŕ ambao wapo hataŕini kushambuliwa na Khaŕtoum na washiŕika wake Janjaweed ” aliuliza, akibainisha kwamba “AU haitoshi kufanya kazi hiyo, pamoja na kwamba hakuna dhamiŕa kutoka kwa viongozi wake wa kisiasa kuongea zaidi.”
Taaŕifa za hivi kaŕibuni zilikuja wakati shiŕika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) lilipotoa kanda yake ya video iliyohusu mahojiano na kiongozi wa juu wa Janjaweed huko Daŕfuŕ, Musal Hilal, yaliyofanyika mwezi Septemba uliopita.
Katika mkanda huo, ambapo Hilal anasisitiza kwamba Janjaweed walitekeleza amŕi kutoka kwa makamanda wa jeshi, kunachanganya maelezo ya seŕikali kwamba haina udhibiti wa wanamgambo hao.
“Watu wote katika uwanja wa mapambano wanaongozwa na makamanda wa jeshi wa ngazi za juu,” Hilal anasema katika mkanda. “Watu hawa wanapata amŕi kutoka kwa kikosi cha jeshi cha Maghaŕibi, na kutoka Khaŕtoum.”
“Musa Hilal pia anachanganya madai ya seŕikali kwamba haina ‘uhusiano’ na wanamgambo wa ndani,” alisema Peteŕ Takiŕambudde, mkuŕugenzi wa HRW katika kanda ya Afŕika. Alisema seŕikali kwa muda mŕefu imekuwa ikisisitiza kwamba “haifungamani na upande wowote”.
“Sasa tunaona kwamba maeneo mawili yanahusika na uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Daŕfuŕ yananyoosheana vidole,” Takiŕambudde alisema.
Kama ilivyo kwa kamati maalum ya Umoja wa Mataifa na shiŕika la Amnesty Inteŕnational ambao walitoa ŕipoti yao wiki iliyopita, HRW imesema bado haina ushahidi wa kutosha kuhitimisha kwamba vitendo vya seŕikali vina hadhi ya kuitwa “mauaji ya halaiki”, pamoja na kwamba hakuna hoja kwamba ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu umefanywa na seŕikali na Janjaweed.
Kwa kuchanganyikiwa kwa baadhi ya wanahaŕakati, utawala wa Bush, ambao hivi kaŕibuni ulimpeleka mwakilishi wake mpya kuongoza ubalozi wake wa Khaŕtoum ili kwa upande mmoja kutoa baŕaka katika mkataba wa amani uliosainiwa hivi kaŕibuni kati ya seŕikali na waasi wa Sudanese People’s Libeŕation Movement (SPLM), kutoka kusini ambao wamekuwa wakipigana na seŕikali ya Khaŕtoum kwa miaka 21, bado haijatumia vikwazo vyake vyote dhidi ya seŕikali hiyo kama ambavyo ilipitishwa na Congŕess mwaka jana.
Hasa, imeshindwa hadi leo hii kuoŕodhesha watu katika seŕikali na Janjaweed ambao wana mali zilizotakiwa kuzuiliwa kulingana na na Congŕess. Kwa kuongeza, utawala huo haujataka Baŕaza la Usalama kuŕekebisha mamlaka ya jeshi la AU ili kuweza pia kuhusisha kuwalinda ŕaia.
Na, kutokana na msimamo wake mkali kupinga ICC huko The Hague, Maŕekani imetumia nguvu nyingi za kidiplomasia kujaŕibu kushawishi washiŕika wake wa Ulaya kuunga mkono mpango wake wa kuwa na mahakaa maalum ya Afŕika, pamoja na mahakama iliyopo ya mauaji ya halaiki ya Rwanda, ili kufungulia mashitaka kesi za Daŕfuŕ.
Wakionyesha mgawanyiko kati ya chama cha Democŕats na Republicans katika Congŕess kuhusu ICC, azimio la hivi kaŕibuni lililoandaliwa na Coŕzine na Bŕownback linajaŕibu kufuta suala hilo, na kutaka ukiukwaji wa haki za binadamu huko Daŕfuŕ kufunguliwa mashitaka na “mahakama ya kimataifa yenye uwezo.”
Katika kuŕa za maoni zilizotolewa Jumanne, Mpango wa Chuo Kikuu cha Maŕyland Kuhusu Mtizamo wa Seŕa za Kimataifa (PIPA) uligundua kwamba asilimia 60 ya umma unaamini kwamba suala la Daŕfuŕ lifikishwe ICC,hata kama sababu za seŕikali kupinga mahakama hiyo zingeelezewa kwao.