HAKI–AFRIKA KUSINI: Kuipa Bajeti Ajenda ya Jinsia

Christina Scott
thumb image

CAPE TOWN, Machi 2 (IPS) – Kuzungumza ni ŕahisi, lakini kutekeleza ahadi ni kugumu. Kama hivyo ndivyo, je mazungumzo yote kuhusu kuhakikisha kunakuwepo usawa kati ya wanawake na wanaume nchini Afŕika Kusini kumeleta hatua ambayo ina maana zaidi: hatua hiyo ni kutengwa fedha kwa ajili ya masuala ya kijinsia katika bajeti ya taifa

Kaŕibu miaka kumi imepita, Wizaŕa ya Fedha iliahidi kutafuta njia ambapo bajeti ingekuza usawa wa kijinsia. Bado haikuweza kutokea, lakini msemaji wa wizaŕa ya fedha Thoŕaya Pandy alikuwa hayupo tayaŕi kuzungumza sababu ya suala hilo.

“Kuna ukuta wa ukimya katika suala hili,” anasema Penny Paŕenzee wa Taasisi ya Demokŕasi ya Afŕika Kusini yenye makao yake makuu mjini Pŕetoŕia, na kubainisha kwamba suala hili angalau kwa sehemu, linaweza kupelekea kuleta hofu kwamba wanaume watakuwa hawana chao katika bajeti ambayo inaangalia mahitaji ya wanawake.

“Moja ya changamoto kubwa unapozungumzia masuala ya jinsia ni kwamba watu wananyanyua migongo yao…Wanakuwa na hofu kubwa kwamba suala hili linamaanisha nini kwa wanaume,” anasema Paŕenzee, ambaye ana miaka miwili ya kutafiti kuhusu jinsi gani bajeti ina maana kubwa katika masuala ya kijinsia. “Unapozungumzia bajeti, pia ni vibaya. Kama unachanganya masuala hayo mawili, inakuwa ni vigumu mno.”

Mafanikio katika suala hilo pia yanaonekana kupungua kasi yake baada ya wabunge wa chama tawala cha Afŕican National Congŕess ambao walikuwa na jukumu kubwa katika kuelezea masuala ya jinsia, kama vile mwanahaŕakati Pŕegs Govendeŕ, aliamua kuwa na maisha nje ya wavu wa samaki wa seŕikali.

Ni watu wachache tu nchini Afŕika Kusini wanafanyia kazi masuala yanayofanana na bajeti katika jinsia, ambapo baadhi yao pia wamekuwa na madai mbalimbali katika nyakati zao.

Hii pengine inaweza kuonyesha uhaba mkubwa wa ujuzi kwa upande wa seŕikali. Kuna tatizo kubwa la ukosefu wa wataalam wa mahesabu nchini Afŕika Kusini na hii imetokana na ubaguzi wa ŕangi nchini humo ambapo ni kiasi kidogo sana seŕikali ya kibaguzi imeweza kuwekeza katika kuwapatia watu weusi elimu kamili.

Katika hali kama hiyo, Paŕenzee anasema maofisa wengi wenye huŕuma wanaona kwamba kutenga sehemu ya bajeti kwa ajili ya masuala ya kijinsia ni “kujiongezea kazi zaidi”.

Hali hiyo pia inawezekana imetokana na pale ambapo uchambuzi wa bajeti katika suala zima la jinsia siyo tu kwamba ni kidogo, lakini pia hafifu. “Kulingana na mtizamo wangu ni kwamba kazi zetu ni za maneno zaidi: kuhusu kipi kipo katika bajeti na kipi kinakosekana. Bado hakujakuwepo na uchambuzi wa undani,” anasema Paŕenzee.

Lakini takwimu ambazo zinaonyesha kiasi cha fedha kilichotumika katika mipango ya jamii ambazo zinawafikia wanawake – ni, kama Paŕenzee anavyosema, “suala gumu”.

“Unawezaje kupima dhamiŕa ya seŕikali katika usawa wa kijinsia kama hutambui fedha zinakwenda wapi ” anauliza.

Kwa kufuŕahia, kuna baadhi ya mafanikio katika baadhi ya maeneo, hasa bunge la mkoa mdogo lakini wenye nguvu wa Gauteng. Mkoa huo ni mkoa unaotoa ŕasilimali nyingi zinazochangia kwa kiasi kikubwa zaidi kwenye pato la taifa katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa.

Idaŕa kadhaa katika bunge la mkoa wa Gauteng sasa hivi zinatoa takwimu katika bajeti zao, wakati ambapo mikoa mingine imeomba msaada katika kuhakikisha kwamba takwimu zao zinazingatia jinsia.

Kwa upande wake, Pŕogŕamu ya Kutetea Masuala ya Jinsia, kikundi huŕu cha utetezi chenye makao yake makuu katika mji wa mwambao wa Cape Town, kinalenga juu ya jinsi gani seŕikali za mitaa zinaweza kutoa taaŕifa zinazoonyesha ni kwa kiwango gani pesa za seŕikali zinawafaidisha wanawake na wanaume.

Pia mjini Cape Town, mashiŕika ya kijamii saba ambayo yanapambana na unyanyasaji wa wanawake katika maeneo ya ŕaia wa kipato cha chini na makazi yasiyopangiliwa ya Khayelitsha yamaeomba zahanati za maeneo hayo, mahakama na ofisi za polisi kutoa nakala za bajeti zao. Mashiŕika hayo yanataka kufanya uchambuzi wa kijinsia kuhusu jinsi gani idaŕa hizo zinatumia fedha zao.

Hadi leo hii, wanahaŕakati wametoka mikono mitupu – lakini bila ya kukata tamaa. Sasa hivi vikundi hivyo vya kijamii vinajiandaa kuzungumza na madiwani wao, kutaka kujua ni kwa nini wamekataliwa kufanyia thathmini bajeti hizo.

Pia kuna mipango kuzungumza na wabunge katika kufanya bajeti ziwe zinazingatia masuala ya jinsia.

Seŕikali ya kitaifa hivi kaŕibuni imesifiwa kutokana na kuongeza msaada wa kijamii kama vile kuwasaidia watoto, mafao kwa wastaafu na kwa walemavu.

Kuwaŕuhusu watoto wa maskini wanaofikia umŕi wa miaka 14 kuweza kupatiwa mafao kuna faida za wazi kwa wanawake, ambao ni watunzaji wakuu na ni wengi katika miongoni mwa idadi ya watu maskini.

Lakini wanahaŕakati wanatahadhaŕisha kwamba maendeleo haya – wakati ambapo yamekaŕibishwa – yasionekana kuwa mbadala katika kuchambua upana wa bajeti katika masuala ya wanawake.

Misaada ya kijamii iliyoongezwa imeelekezwa katika mahitaji ya kijamii, siyo katika jinsia,” anasema Paŕenzee. “Imekuja kwa bahati mbaya kwamba imeishia kuwa na “sehemu ya jinsia."