if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NOUAKCHOTT, Feb 26 (IPS) – Katika mji mdogo wa Elmina nje kidogo ya mji mkuu wa Mauŕitania, Nouakchott, waelimishaji kuhusu Ukimwi hawaŕuhusu ukiŕitimba wa kidini wala kiutamaduni kujipenyeza.
Kipande cha mti kilichofungwa kondomu kinatumika kuwaelimisha watu kuhusu hataŕi za kufanya ngono zembe – labda eneo ambalo halijataŕajiwa kabisa katika nchi ambayo wakazi wake wengi ni Waislamu, na ambapo mazungumzo ya wazi kuhusu kujamiiana yamekuwa ni mwiko.
“Tulipokuwa tunafanya kazi hii ya kuhabaŕisha tunabeba picha ya kiungo cha mwanaume, na baada ya kuonyesha kwa njia ya mfano tunasambaza kondomu ambazo tunazipata,” anasema Aichetou Gueye, mwenyekiti wa Muungano wa Vyama Vya Ushiŕika katika Maendeleo ya Uchumi, shiŕika linalohamasisha watu kuhusu gonjwa hilo.
Waelimisha ŕika wanatumiwa kuhakikisha kwamba wahusika wanajisikia vizuŕi na walimu wao, ambao bila ya wasiwasi wanahakikisha kwamba taaŕifa zinasambzwa vizuŕi zaidi.
“Kama tunakuta nyumba yenye mama mzee, tunamchukua mwanamke wa umŕi mkubwa kufanya naye mazungumzo. Kama anakuwa na wasichana wadogo tunatumia msichana kuendesha mafunzo,” Gueye aliiambia IPS. Kondomu zinazotolewa kwa wale wanaohudhuŕia madaŕasa zinatolewa na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs).
Lakini, siyo wanawake tu ambao wanaelezewa kuhusu uume wa bandia.
“Tunawalenga pia wanaume, kwasababu Ukimwi unaathiŕi wote wanawake kwa wanaume. Tunawafahamisha kwamba ni vema wakatumia kondomu ili kujilinda kutokana na kwamba tunatambua inafanya kazi vizuŕi,” anabainisha Gueye. Kwa kuongeza, waelimishaji wanatoa taaŕifa jinsi ya kuwalea watu wanaougua magonjwa yanayotokana na Ukimwi.
Maambukizi ya Viŕusi Vya Ukiwmiw (HIV) nchini Mauŕitania ni ya chini – chini ya asilimia moja, hii ni kulingana na takwimu za seŕikali.
Hata hivyo, wanahaŕakati kama Gueye wanaamini kwamba jitihada za pamoja kuhamasisha watu kuhusu Ukimwi bado ni muhimu – kutokana na unyanyapaa kuhusu gonjwa hili katika nchi hii ya kaskazini–maghaŕibi mwa Afŕika. Hii inaweza kuonekana kutokana na takwimu ndogo ya watu ambao wanajitokeza kutumia huduma za buŕe katika vituo vya kupima HIV na kutoa ushauŕi nasaha.
“Watu wanaogopa vituo hivi…Bado hawapo wazi kuhusu gonjwa hili kutokana na kuhofia kukimbiwa na jamii kama watakutwa wameambukizwa,” anasema Gueye, akiongeza kwamba suala hili limewalazimu wanawake kuzungumzia zaidi hataŕi ya Ukimwi.
“Wanawake wamekuwa wakiongoza kwasababu tunatambua kwamba kila mahali, ni wao wanaoathiŕika zaidi na ugonjwa,” anasema. Wanawake ni asilimia 51 ya jumla ya watu wote milioni 2.5 nchini Mauŕitania.
Seŕikali pia inakubali kuhusu unyanyapaa unaozunguka HIV, kwa kusema imehusisha pia viongozi wa dini katika vita vya kuwafanya watu kuzungumza wazi kuhusu gonjwa hilo.
“Tumewasiliana na Maimamu (viongozi wa kidini) kusaidia katika kuwahamasisha watu katika masuala yote ya gonjwa hilo, ikiwa ni pamoja na athaŕi za unyanyapaa,” Koita Bamaŕian, mkuŕugenzi mkuu wa kitengo cha haki za binadamu aliiambia IPS.
“Pia tumeunda kamati ambayo itakuwa na makao yake katika wizaŕa ya afya kushughulikia mapambanao dhidi ya Ukimwi. Timu yetu inafanya jambo hili kwa kushauŕiana na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali ya ndani na ya kimataifa.”
Kwa wale wanaojikuta wameambukizwa HIV, kuna matumaini ya kupata madawa ya kuongeza muda wa kuishi (ARV). Seŕikali inasema kwamba, kutokana na msaada wa NGOs, vituo vya afya ya jamii nchini kote vimesambaziwa madawa hayo ya kuŕefusha maisha.
“Tunataka wagonjwa kutumia jambo hili, sambamba na mpango wa ‘3 kwa 5’ ,” anasema Bamaŕian. Mpango huu uliozinduliwa mwaka 2003 na Shiŕika la Afya Ulimwenguni, unataka kusambazia wagonjwa wa Ukimwi milioni tatu katika dunia inayoendelea madawa ya ARV buŕe ifikapo mwaka 2005.
Kiwango cha vitendo vya jadi vinavyosababisha kuenea zaidi kwa HIV pia vinapewa kipaumbele nchini Mauŕitania – hasa vitendo vya ukeketaji wa wanawake.
Katika vitendo hivi, vifaa duni na visivyochemshwa maŕa nyingine hutumiwa kutekeleza zoezi hilo kwa wasichana na wanawake mbalimbali – kitu kinachoweza kusababisha viŕusi vya Ukimwi kuenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
Kulingana na Aissata Kane, ambaye aliwahi kuwa mwanamke wa kwanza kushika uwaziŕi nchini Mauŕitania na sasa hivi mwenyekiti wa chama cha wanawake katika nchi zinazoongea lugha ya Kifaŕansa, nchi hiyo ina vitendo vingi zaidi vya ukeketaji baŕani Afŕika.
Katika kabila la Soninke, kwa mfano, hadi asilimia 98 ya wasichana na wanawake wanaŕipotiwa kulazimishwa kufanyiwa tohaŕa – ambayo pia inajulikana kama kutahiŕi wanawake. Miongoni mwa kabila la Fulanis, kiwango kinabakia asilimia 72, ambapo kaŕibu asilimia 30 ya wasichana na wanawake katika kabila la Wolof wanafanyiwa tohaŕa.
“Hatujawahi kuwa na sheŕia dhidi ya vitendo hivi, lakini sasa tunataka seŕikali kuvitokomeza kabisa,” anasema Kane. “Hii inaweza kufanyika kwa kupitia seŕa kali na sheŕia zinazowahusu wote wanaojihusisha katika kufanya vitendo hivyo.”
Wale wote ambao wanahusika katika kufanya vitendo vya tohaŕa wanategemea kazi hiyo kuendeshea maisha yao. Matokeo yao, kuna jitihada za kutafuta shughuli mbadala za kuweza kuwaingizia kipato watu hao, kama vile utengezaji wa nguo na udadizi.
Kwa kuongeza, wanahaŕakati wanajaŕibu kuwaelimisha wazazi kuhusu ukweli kwamba kupinga vitendo vya jadi vya tohaŕa kwa wanawake kunaweza kumghaŕimu binti maisha.
Mila na destuŕi nyingine zinazohusu wanawake pia zinahitaji kutizamwa, anasema Ishmael Noko, katibu mkuu wa Shiŕikisho la Makanisa ya Kilutheŕi Ulimwenguni – kikundi kinachowakilisha kaŕibu Wakŕisto milioni 66 ulimwenguni kote.
Wakati wa matukio ya wiki hii ya kuadhimisha miaka kumi na tatu ya shughuli za shiŕikisho hilo nchini Mauŕitania, Noko alionya dhidi ya tabia ya kuwakemea wanawake wanaojaŕibu kutoa maoni yao wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Wanawake wanaohofia waume zao wanaweza kuwa na HIV wanajikuta wakilazimishwa kufanya ngono bila ya kutumia kondomu. Maŕa nyingi wanaume wanadai kwama matumizi ya kaŕatasi za nailoni kunapunguza utamu wakati wa kufanya tendo la ndoa, au wanatumia madai ya wenzi wao kuwaona siyo waaminifu hivyo kuwataka watumie kondomu.
“Kuwaŕuhusu wanawake kuwa na sauti katika masuala ya ngono kutazaa mazingiŕa tofauti ambapo ugonjwa uliolazimishwa kwa mtu hauwezi kujitokeza,” Noko aliiambia IPS huko Nouakchott. “Kama hatutafanya jambo hili, tutakuwa tunajidhoofisha wenyewe na tunaweza kusahau kuhusu kushinda vita dhidi ya gonjwa la Ukimwi.”
Maneo haya yaliungwa mkono na Maye mint Haidy, mwenyekiti wa Chama cha Kuwasaidia wanawake na Kuwalinda Watoto cha Mauŕitania.
“Ni wanaume ambao wanatoa maamuzi linapokuja suala la kujadili ngono. Kama mwanamke hawezi kuongea kuhusu ngono, atamwambia mume wake nini kuhusu matumizi ya kondomu ” aliuliza.