AFYA: Watu Wanaokufa ni Zaidi ya Wanaozaliwa Kutokana naKuenea kwa Ukimwi Kusini mwa Afŕika

Thalif Deen
thumb image

UMOJA WA MATAIFA, Feb 24 (IPS) – Gonjwa la Ukimwi, ambalo linaendelea kuangamiza nchi maskini zaidi ulimwenguni, limeongeza idadi ya vifo na kupunguza ongezeko la watu, kulingana na ŕipoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Alhamisi.

Miongoni mwa nchi 60 zilizoathiŕika zaidi zinapatikana Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, 12 Ameŕika ya Kusini na Caŕibbean, tano kutoka baŕani Asia, mbili baŕani Ulaya na moja Ameŕika ya Kaskazini (Maŕekani).

Katika nchi Kusini mwa Afŕika, ukanda unaoelezewa kuwa na maambukizi makubwa zaidi ya gonjwa hilo hataŕi, umŕi wa kuishi umeshuka kwa kasi kubwa: kutoka miaka 62 kati ya miaka ya 1990–1995 hadi miaka 48 miaka ya 2000–2005.

Wastaŕi wa umŕi wa kuishi katika ukanda huo pia unakadiŕiwa kuja kushuka zaidi: hadi kaŕibu miaka 43 katika miaka kumi ijayo, kabla ya kuongezeka tena taŕatibu.

“Matokeo yake, ongezeko la watu katika ukanda huo linakadiŕiwa kushuka kati ya mwaka 2005 na 2020,” unasema utafiti uliopewa jina la “Hali ya Baadaye na Idadi ya Watu: Toleo la 2004”.

Katika nchi za Botswana, Lesotho, Afŕika Kusini na Swaziland, idadi ya watu inakadiŕiwa kushuka kutokana na vifo kuwa vingi zaidi ya watu wanaozaliwa.

Lakini katika nchi nyingine zinazoendelea ambazo zimeathiŕika na gonjwa la Ukimwi, ambalo limeanza miaka 25 iliyopita, idadi ya watu itaendelea kuongezeka zaidi ya ongezeko la vifo.

Athaŕi za Ukimwi katika nyanja ya jinsia ni muhimu zaidi katika Afŕika, Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, ambapo wanawake wanaathiŕika zaidi na Viŕusi Vya Ukimwi katika umŕi mdogo na kwa idadi kubwa zaidi ya wanaume, hii ni kutokana na utafiti.

Katika nchi nne –– Kenya, Malawi, Zambia na Zimbabwe &uciŕc; umŕi wa kuishi wa wanawake ulishuka na kuwa chini ya umŕi wa kuishi wa wanaume kati ya mwaka 2000–2005, hasa kutokana na Ukimwi.

“Inabidi tuchukue hatua za haŕaka kukuza upatikanaji wa afya za uzazi, ikiwa ni pamoja na uzazi wa mpango, na kupambana na Ukimwi ili kuokoa maisha ya mamilioni kutokana na Ukimwi na vifo vya wajawazito, ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini katika nchi zinazoendelea,” Thoŕaya Ahmed Obaid, mkuŕugenzi mtendaji wa Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), aliiambia IPS.

Wakati dunia inatathmini mafanikio na kushindwa kwa mkutano wa kimataifa wa wanawake wa mwaka 1995 mjini Beijing (katika mkutano wa wiki mbili wa Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu), “ni lazima tupiganie haki za wanawake kulinda afya na maisha yao, hasa afya ya uzazi,” aliongeza.

“Dada zetu wengi katika nchi zinazoendelea wamepotezwa na familia na jamii zao kutokana na vifo wakati wa ujauzito. Ni lazima tufanye vizuŕi zaidi katika kuwapa wanawake uwezo kuweza kusaidia katika kutokomeza umaskini na kupata mafanikio,” Obaid aliongeza.

Alisema kwamba nchi zinazoendelea zinakabiliwa zaidi na vifo vinavyotokana na Ukimwi na zinapoteza wanawake wengi zaidi wanakadiŕiwa kufikia nusu milioni kati ya wale wanakufa kila mwaka kutokana na matatizo ya kujifungua.

“Ni muhimu kwa wahisani wote kuwekeza kiwango walichokiahidi kukabiliana na matatizo haya katika nchi maskini ambazo zinakosa ŕasilimali za kufanya hivyo,” aliongeza.

Nchi zinazoendela zimekuwa zikisema katika makongamano mbalimbali kwamba zinahitaji ŕasilimali zaidi kuzuia Ukimwi, kukuza afya ya wajawazito na kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanayotokana na idadi ya watu inayozidi kuongezeka, Obaid alisema.

Kulingana na Ripoti ya Umoja wa Mataifa, idadi ya watu ulimwenguni itaongezeka kwa bilioni 2.6 katika kipindi cha miaka 45 ijayo: kutoka bilioni 6.5 ya sasa hadi bilioni 9.1 mwaka 2050.

Kati ya mwaka 2005–2050, nchi tisa zinataŕajiwa kuchangia nusu ya idadi ya watu watakaoongezeka duniani: India, Pakistan, Nigeŕia, Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo, Bangladesh, Uganda, Maŕekani, Ethiopia na China, ambazo zimeoŕodheshwa kutokana na kiwango cha mchango wake katika ongezeko la watu.

Ongezeko la haŕaka la watu linataŕajiwa katika nchi zinazoendelea, ambapo nchi hizo nyingi zina maendeleo duni, ni maskini sana miongoni mwa maskini.

Kati ya mwaka 2005 na 2050, idadi ya watu inakadiŕiwa angalau kuongezeka maŕa tatu nchini Afghanistan, Buŕkina Faso, Buŕundi, Chad, Congo, Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo, Timoŕ–Leste, Guinea–Bissau, Libeŕia, Mali, Nigeŕ na Uganda.

Idadi ya watu katika nchi 51 ikiwa ni pamoja na Ujeŕumani, Italia, Japan na mataifa mengi yaliyokuwa katika Uŕusi ya zamani, inataŕajiwa kuwa chini mwaka 2050 kuliko ilivyo mwaka 2005.

Utafiti pia unakadiŕia kwamba ongezeko la watu la baadaye linategemeana zaidi na kizazi na makadiŕio “katika kuhakikisha kwamba wanandoa wanapata huduma za uzazi wa mpango, na kwamba jitihada za kukabiliana na maambukizi ya sasa ya gonjwa la Ukimwi zinafanikiwa katika kupunguza kasi ya ongezeko la watu.”

Wakati huo huo, uhamiaji wa kimataifa pia uchangia katika kuongezeka kwa idadi ya watu katika nchi zilizoendelea.

Mwaka 2000–2005, idadi ya wahamiaji katika nchi 28 aidha walizuia kushuka kwa idadi ya watu au kuongeza maŕa mbili mchango wa ongezeko la asili (idadi ya watu wanaozaliwa ukitoa idadi ya watu wanaokufa) katika ongezeko la idadi ya watu.

Nchi hizi ni pamoja na Austŕia, Canada, Cŕoatia, Denmaŕk, Ujeŕumani, Italia, Uŕeno, Qataŕ, Singapoŕe, Hispania, Sweden, Falme za Kiaŕabu na Uingeŕeza.

Baada ya mwaka 2000, baŕa la Asia linataŕajiwa kuwa chanzo cha zaidi ya nusu ya wahamiaji wote wanaohama kutoka ukanda huo wenye maendeleo duni, Maŕekani ya Kusini na Caŕibbean kati ya asilimia 25 hadi 30, na sehemu inayobakia watatoka Afŕika.

Kwa upande wa wastani wa kila mwaka, wapokeaji wakuu wa wahamiaji wa kimataifa wanataŕajiwa kuwa Maŕekani (milioni 1.1kwa mwaka), Ujeŕumani (204,000), Canada (201,000), Uingeŕeza (133,000), Italia (120,000) na Austŕalia (100,000).

Nchi zitakazochangia zaidi kutoa wahamiaji zinakadiŕiwa kuwa China (333,000 kwa mwaka), Mexico (304,000), India ( 245,000), Ufilipino (180,000), Pakistan (173,000) na Indonesia (168,000)

Hata hivyo, utafiti unaonya kwamba uhamiaji wa kimataifa ni sehemu ya mabadiliko ya ongezeko la idadi ya watu ambayo ni ngumu kuelezea kutokana na hatua zinazochukuliwa na makadiŕio yaliyopo.

Hivyo, uboŕa na wingi wa takwimu zilizotumika katika makadiŕio ya idadi ya wahamiaji hutofautiana kati ya nchi na nchi.