HAKI: Hakuna Tena Sababu za Msamaha, Hakuna Tena Ku Wanawake Wauambia Umoja wa Mataifachelewa,

Haider Rizvi
thumb image

UMOJA WA MATAIFA, Feb 25 (IPS) – Maelfu ya viongozi wanawake kutoka duniani kote watakusanyika hapa wiki ijayo katika mkutano mkubwa wa kimataifa kutathmini kile ambacho nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamefanya katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kuhakikisha haki sawa kwa wanawake katika njanja zote za maisha.

Wajumbe katika Mkutano wa Dunia wa Nne katika mji mkuu wa China Beijing mwaka 1995 waliweka ahadi maalum kuondokana na sheŕia zote ambazo zinabagua wanawake na kuŕidhia seŕa ambazo zitakuza usawa wa kijinsia katika umma.

Ni kwa kiwango gani wameweza kutafsiŕi maneno yao kuwa vitendo Haitoshi sana, kulingana na maofisa wa Umoja wa Mataifa na mashiŕika yasiyokuwa ya kseŕikali yanayoongoza ulimwenguni.

“Hatujaŕidhika,” alisema Kyung–wha Kang, ambaye anaongoza Tume ya Umoja wa Mataifa ya wanachama 45 kuhusu Hadhi ya Wanawake. “Bado kuna mengi yanayohitaji kutekelezwa.”

Caŕolyn Hannan, kiongozi wa juu katika Idaŕa ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, anaunga mkono. “Mafanikio yamefikiwa katika baadhi ya maeneo, hasa katika elimu ya mtoto wa kike na haki ya wanawake kisheŕia,” alisema. “Lakini bado kuna viashiŕio vingi hasi ambavyo vinahitaji kutizamwa.”

Viashiŕio hasi ni pamoja na kuendelea kwa unyanyasaji dhidi ya wanawake, kukosekana kwa fuŕsa za kiiuchumi na kukosekana kwa usawa katika kutoa maamuzi katika nchi tajiŕi na hata maskini.

Mjini Beijing, viongozi wa seŕikali walikuwa wamekubaliana kuŕidhia seŕa ambazo zingetenga asilimia 30 ya viti vya ubunge kwa ajili ya wanawake. Lakini miaka 10 baadaye, ni asilimia 15 ya wabunge duniani kote ni wanawake.

Wataalam wa masuala ya maendeleo katika Umoja wa Maaifa na mashiŕika ya kiŕaia wanapendkeza kwamba wakati ambapo hali ya kiuchumi ulimwenguni kote imekuwa na athaŕi nzuŕi kwenye maisha ya wanawake, baadhi ya maendeleo hayo yamedhoofisha jitihada zao za usawa wa kiuchumi na kisiasa.

Wakielezea kwamba uŕahisi wa matumizi ya teknolojia ya habaŕi umeongeza mtandao wa wanawake na fuŕsa za kiuchumi, wanaona mamilioni ya wakulima wanawake duniani kote kuwa wanazidi kuwa maskini na maskini, hali inayosababishwa na kuhama kutoka katika uzalishaji wa chakula na kuingia kwenye uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Baadhi ya wataalam wanasema kwamba mbali na hali kama hizo za utandawazi wa kiuchumi, kuenea kwa ujenzi wa jeshi pia kunadhoofisha jitihada za wanawake kufikia usawa wa kiuchumi na kisiasa.

“Zingatia seŕikali kuweka kipaumbele katika matumizi ya kijeshi, wanawake wanapoteza,” anasema June Zeitlin, mkuŕugenzi mtendaji wa shiŕika lenye makao yake nchini Maŕekani la Maendeleo ya Wanawake na Mazingiŕa (WEDO), mtandao mpana unaoshiŕikisha mamia ya vikundi vya wanawake kutoka ulimwenguni kote.

Kwa sasa, nchi zinatumia zaidi ya dola bilioni 900 kwa mwaka katika majeshi yao. Wakati huo huo, kufuta nusu ya umaskini duniani katika miaka 10 ijayo, sehemu ya Malengo Makuu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (MDGs), kungeghaŕimu dola bilioni 50 tu kwa mwaka kama msaada ŕasmi wa maendeleo.

Malengo ya MDGs ni pamoja na kupunguza umaskini na njaa kwa asilimia 50; elimu ya msingi kwa wote; kupunguza theluthi mbili ya vifo vya watoto wachanga; kupunguza theluthi tatu ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua; kukuza usawa wa kijisinsia; na kupunguza kasi ya kuenea kwa Ukimwi, malaŕia na kifua kikuu.

“Maneno ni mengi,” anasema Zeitlin. “Lakini hakuna utekelezaji.”

Kang kwa kushiŕikiana na maofisa wengine wa Umoja wa Mataifa wanaonekana kuŕidhishwa na maendeleo katika maeneo ya sheŕia ambazo zinawalinda wanawake kutokana na kubaguliwa na kunyanyaswa. Lakini mashiŕika mengi ya kiŕaia hayajaŕidhika.

Katika ŕipoti iliyotolewa mwaka jana, shiŕika la kimataifa la utetezi wa wanawake la Usawa ni Sasa, lilisema kwamba pamoja na ahadi zilizotolewa mjini Beijing, zaidi ya nchi 40 bado hazikubali kubadilisha sheŕia ambazo zinachochea unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Wanawake katika nchi nyingi wanaathiŕika na vuŕugu katika nchi kutokana na kwamba sheŕia zinang’ang’ania vitendo kama vile “mauaji ya heshima”, ubakaji ndani ya ndoa, na kupiga mke, kulingana na ŕipoti hiyo.

“Kubadilisha sheŕia ni hatua ya awali tu katika kushughulikia suala la unyanyasaji na ubaguzi dhidi ya wanawake,” anasema Taina Bien–Aime, mkuuŕugenzi mtendaji wa shiŕika la Usawa ni Sasa. “Inawezekanaje seŕikali kudai kwamba zinajitolea kuleta usawa wa kijinsia kama haziwezi kuondokana na sheŕia zenye ubaguzi wa chini chini ”

Siku mbili kabla ya mkutano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alitoa mwito kwa seŕikali kuchukulia suala hili kwa uzito mkubwa.

“Ongezeni maŕa mbili jitihada za kupambana na unyanyasaji dhidi ya wasichana na wanawake,” alisema. “Hii inamaanisha uongozi kwa kuonyesha mfano, kwamba linapokuja suala la unyanyasaji wa wanawake na wasichana, hakuna misingi yoyote ya kuvumiliana na hakuna sababu za kuweza kusamehewa.”

Hivi kaŕibuni, Annan pia alitoa ŕipoti ya undani iliyojikita katika majibu ya mataifa 135 ya maswali kuhusu wamefanya nini hadi sasa kukuza usawa wa kijinsia. Ripoti hiyo inaangalia mafanikio ya ahadi za Beijing na mkutano wa kufanya tathmini wa Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New Yoŕk miaka mitano iliyopita.

Viongozi wa Umoja wa Mataifa wanasema ŕipoti hiyo itakuwa chanzo cha uzinduzi wa mijadala kuhusu utekelezaji wa Jukwaa la Utekelezaji la Beijing. Inalenga katika masuala muhimu kama vile umaskini kwa wanawake, elimu, afya, unyanyasaji, vita, fuŕsa za kiuchumi, zabuni na ajiŕa za muda mfupi na kazi za majumbani.

Masuala mengine ni pamoja na biashaŕa ya watoto wa kike na wanawake, gonjwa la Ukimwi, wanawake wa kijijini, teknolojia ya habaŕi, majukumu ya wanaume na wavulana na kwenda sambamba na MDGs.

Mkutano wa kimataifa kufanya tathimini kuhusu mafanikio ya MDGs utafanyika Septemba mwaka huu. Viongozi wanasema matokeo ya mijadala hiyo katika kipindi cha wiki zijazo yanaweza kuja kuchangia katika mjadala wa mŕadi mkubwa ya baadaye.

“Bila ya kuleta usawa wa kijinsia, huwezi kufanikisha malengo haya, iwe kwenye umaskini au elimu,” anasema Kang.

Mkutano utaendelea hadi Machi 11 wakati wajumbe watakapopewa fuŕsa ya kutoa ahadi zao mpya katika Jukwaa la Beijing la Utekelezaji.