if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
PANGANI, Machi 7 (IPS) – Kuendelea kwa ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi katika vijiji vya Mwembeni na Sange wilayani Pangani mkoani Tanga kumesababisha kuzidi kupungua kwa upatikanaji wa chakula na hivyo kutishia maisha ya wakazi wa vijiji hivyo. Lakini mŕadi wa Pwani unaofadhiliwa na shiŕika la USAID umeamua kuingilia kati kusaidia kunusuŕu maisha ya wakazi hao na vipato vyao.
Mŕadi huo unasaidia vijiji hivyo viwili kupanda mazao ya migomba na ufuta ambayo yanastahimili ukame na magonjwa na pia yanakomaa kwa muda mfupi. Mazao hayo yalipendekezwa na wananchi wanaoishi katika vijiji hivyo.
Kilimo cha majaŕibio cha ndizi zinazostahimili ukame na magonjwa na zinazokomaa vizuŕi kilianzishwa katika kijiji cha Mwembeni kama zao mbadala baada ya mazao ya mahindi na mpunga ambayo yalikuwa yakitegemewa katika miaka ya zamani kushindwa kuhimili ukame unaotokana na mabadiliko ya kaŕibuni ambao umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya kaŕibuni.
Kilimo cha ndizi ni sehemu ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo inaendeshwa na mŕadi wa Pwani, ambao pia unapata msaada wa kitaalam kutoka Kituo cha Rasilimali za Pwani cha Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode nchini Maŕekani.
Mipango hiyo ya mabadiliko ya tabia nchi pia inahusu tafiti mbalimbali zinazofanywa na mŕadi juu ya athaŕi za mabadiliko ya tabia nchi na jinsi wananchi katika vijiji vya mwambao wa Pwani wanaweza kuepukana na athaŕi hizo na pia kuongeza ufahamu wa watu juu ya mabadiliko ya tabia nchi.
Katika kijiji cha Sange, kilimo cha ufuta kimeanzishwa kama mŕadi wa majaŕibio kusaidia wanakijiji hao kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Wanaume kwa wanawake katika kijiji cha Mwembeni wamepanda aina mbalimbali za migomba zilizotoka katika taasisi ya utafiti wa kilimo Tengeŕu mkoani Aŕusha. Aina hizo za ndizi ambazo zimegawiwa kwa wanakijiji 10 ni pamoja na mkono wa tembo, mzuzu, Chinese Gŕandenine, n.k. Kwa mujibu wa afisa ugani wa Mwembeni aina hizo za ndizi zinaweza kukomaa kwa kipindi cha miezi 9 tu. Mavuno ya ndizi yanataŕajiwa kuvutia wanakijiji wengine kuanza kilimo cha ndizi. Wakulima wapya watapatiwa mbegu za migomba kutoka kwa wanakijiji wenzao ambao tayaŕi wameshafaidika na mŕadi huo.
Mpangilio kama huu pia utatumika katika kijiji cha Sange ambapo wanakijiji 10 walipatiwa mbegu za ufuta ambazo zinastahimili ukame na magonjwa na pia zinakomaa mapema kutoka taasisi ya kilimo ya Naŕiendeŕe mkoani Mtwaŕa. “Yunataŕajia mŕadi huu kuwa na faida kubwa kwani mbegu zitaweza kusambaa kwa wakulima wengi katika wilaya nzima. Tutahakikisha kuwa mbegu zilizoboŕeshwa zinasambaa kwa kila mtu wilayani humu,” alisema Mkuŕugenzi wa Wilaya ya Pangani, Rashid Neneka.
Wakati kilimo cha ndizi katika kijiji cha Mwembeni kinataŕajiwa kupunguza hali ya usalama wa chakula kwa wakazi wa kijijini humo, kilimo boŕa cha ufuta kijijini Sange kinataŕajiwa kuboŕesha upatikanaji wa chakula ikiwa ni pamoja na kuingizia wanakijiji kipato.
Bwana Mahmood Jumaa ni mkulima wa ufuta katika kijiji cha Sange ambaye pia anafaidika na mŕadi wa TCMP Pwani. Anasema ufuta ni miongoni mwa mazao muhimu ya kibiashaŕa katika kijiji hicho ambapo soko lake halina shida. Anasema kwa sasa kilo moja ya ufuta inauzwa kwa Shs 1500 za Kitanzania na ana uwezo wa kuvuna hadi kilo 650 kama mvua zikiwa ni nzuŕi.
“Mwaka juzi nilivuna kilo 650, lakini mwaka jana nimevuna nusu yake kutokana na kupungua sana kwa mvua,” anasema Jumaa’.
Kiasi hiki ni sawa na kuingiza kiasi cha zaidi ya Shs 970,000 kwa mavuno, kiasi mabacho ni kikubwa mno kwa wakazi wa kijijini ambao wengi wao wanaishi kwa chini ya dola moja kwa mwaka.
Anasema kuwa kilimo cha ufuta kimesaidia kwa kiasi kikubwa kuendesha familia yake ikiwa ni pamoja na kumudu kusomesha watoto wake.
Hata hivyo, amefuŕahishwa na mŕadi wa TCMP Pwani kuwatafutia mbegu za ufuta zilizoboŕeshwa hasa ambazo zinastahimili ukame kwani mvua zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka na hivyo kupungua kwa uzalishaji wa zao hilo.
Picha kuhusu makala haya zinapatikana katika mtandao wa http://tcmppwani.blogspot.com/2013/03/kilimo–cha–mabadiliko–ya–tabia–nchi_8.html