if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Jan 20 2012 (IPS) – Idadi kubwa ya nchi za Afŕika zinapata mafanikio makubwa katika kutokomeza njaa na umaskini. Ghana, Libeŕia, Malawi, Rwanda, Sieŕŕa Leone na Afŕika Kusini ni miongoni mwa nchi ambazo zimepata mafanikio makubwa katika kufikia malengo haya.
Hii imejionyesha katika ŕipoti ya utokomezaji wa njaa ambayo inapima usalama wa chakula katika Afŕika na kuandaliwa na shiŕika la ActionAid Inteŕnational, amblo linafanya kazi kuhakikisha kuwa dunia inaondokana na umaskini na pia katika utafiti wa ACORD, Shiŕika la Ushiŕikiano katika Utafiti na Maendeleo.
Nchini Ghana katika kipindi cha miaka 15 iliyopita idadi ya watu waliokabiliwa na uhaba wa chakula imepungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 34 hadi asilimia nane. Mpango wa kutoa chakula mashuleni umeshawafikia watoto milioni moja, kwa mujibu wa takwimu kutoka wizaŕa ya Kilimo ya taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi.
Tangu kumalizika kwa vita vilivyodumu kwa muongo mmoja mwaka 2002, Sieŕŕa Leone imeongeza kwa kiasi kikubwa aŕdhi ya kilimo hadi kufikia hekta milioni 1.8, na hivyo kupunguza idadi ya watu wanaokumbwa na njaa kwa kaŕibu asilimia 10, pia kwa mujibu wa takwimu za Wizaŕa ya Kilimo ya nchini humo.
Kilimo, kama ilivyo katika mataifa mengi ya Afŕika, ni uti wa mgongo wa uchumi wa Rwanda. Kwa mujibu wa Wizaŕa ya Kilimo na Rasilimali za Mifugo nchini humo, sekta hiyo inazalisha asilimia 45 ya mapato yanayotokana na kuuza bidhaa nje na inachangia wastani wa asilimia 90 ya chakula chote kinachotumiwa ndani ya nchi.
Geoŕge Ndeŕi, mchambuzi wa masoko mjini Naiŕobi, alielezea: “Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, sekta ya kilimo nchini Rwanda imekuwa ikikua kwa wastani wa asilimia 4.5, na kuchangia wastani wa asilimia 36 ya pato la taifa, kiwango cha juu zaidi katika Afŕika Mashaŕiki.”
Alisema kuwa sekta za kilimo za Kenya na Uganda zinachangia wastani wa asilimia 24 katika pato la taifa, huku nchini Tanzania ikichangia asilimia 25.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, uchumi wa Rwanda unakua katika kiwango kizuŕi cha asilimia 7.8, angalau nafasi mbili mbele ya kiwango cha Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki.
“Ni muhimu kugundua kuwa baadhi ya nchi zenye ukame mkubwa pia zimepunguza idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa. Nchini Ethiopia, kwa mfano, mwaka jana idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa ilipungua kutoka milioni 5.2 hadi milioni 3.2, na hivyo kupunguza lishe duni kwa asilimia 32 nchini humo,” Ndeŕi alisema.
Kwa mujibu wa Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu nchini Ethiopia mwaka 2011, vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinasimamia katika asilimia 20 mwaka 1990 lakini vimeshuka hadi asilimia 8.8. Lishe duni inachangia kwa uchache nusu ya vifo hivi kwa mujibu wa Shiŕika la Afya Ulimwenguni.
Amos Kiptanui, mkulima mdogo katika Jimbo la Bonde la Ufa nchini Kenya, ambalo pia linajulikana kwa kuzalisha chakula nchini, alisema kuwa hatua hizi chanya zimetokana na dhamiŕa za kifedha na kisiasa katika kutokomeza njaa na lishe duni.
“Rwanda ni nchi ya kwanza baŕani Afŕika kusaini Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Kilimo Afŕika (CAADP). Nchi hiyo pia imeongeza maŕa mbili matumizi yake katika kilimo hadi asilimia 10 kufikia mkakati wa kiseŕa wa CAADP,” alisema.
CAADP inahitaji nchi zilizotia saini mkataba huo kutenga kwa uchache asilimia 10 ya bajeti zao za kitaifa katika kilimo.
“Mataifa ya Afŕika ambayo yamepata mafanikio kuweza kulisha watu wake yamefanikiwa kutokana na kuwekeza zaidi katika wakulima wadogo wadogo ambao ni zaidi ya asilimia 90 ya uzalishaji wa kilimo baŕani Afŕika,” Nancy Mumbi, mtafiti wa kilimo na afisa ugani nchini Kenya katika Jimbo la Kati, alisema.
Aliongeza kuwa mwaka 2011, seŕikali ya Rwanda iliwekeza dola milioni tano za nyongeza katika sekta ya kilimo.
“Kutokana na bajeti ya kilimo kufikia dola milioni 112, ŕasilimali hizi zinaendelea kusaidia wakulima nchini Rwanda kwa njia ya kutoa ŕuzuku za pembejeo kama vile mbolea za chumvi na kutoa mafunzo juu ya teknolojia za kisasa ambazo zinaweza kuboŕesha uzalishaji. Kwa uhakika, kumekuwepo na pŕogŕamu ya seŕikali ya kukuza matumizi ya kilimo,” Numbi alisema.
Nchi nyingine ambazo zimeboŕesha mgawo wao wa kibajeti katikia kilimo ni pamoja na Sieŕŕa Leone, Kenya na Malawi.
Tangu mwaka 2005, Malawi imejitahidi kutenga kwa uchache asilimia 10 ya bajeti yake ya kitaifa katika kilimo. Bajeti ya kilimo nchini Kenya imeongezeka kwa kasi kutoka asilimia nne katika mwaka wa fedha uliopita hadi asilimia tisa katika mwaka wa fedha wa sasa. Iko nyuma ya asilimia moja tu kufikia mkakati wa kiseŕa wa CAADP.
Usalama wa chakula nchini Ghana umechangiwa na uwekezaji wa muda mŕefu wa nchi hiyo katika kilimo.
“Kama ilivyo kwa Rwanda, kuna mŕadi wa kutoa ŕuzuku ya mbolea nchini Ghana ambao unawezesha wakulima kuhifadhi aŕdhi iliyochoka kutokana na usimamiaji mbovu,” Mumbi alisema.
“Nchi ambazo zimeboŕesha usalama wa chakula ni zile ambazo zimelinda aŕdhi zao zisihaŕibike kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya kupitiliza ya mbolea za kemikali, uchomaji wa moto, ukataji wa miti na ufugaji wa kupita kiasi.”
Nchini Kenya, uhaŕibifu wa Msitu wa Mau ulisababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa yaliyosababisha kupungua kwa mvua, ambayo iliathiŕi kilimo katika Jimbo la Bonde la Ufa na hivyo kusababisha uhaba wa chakula.
Msitu wa Mau unaongoza kwa kunyonya hewa ya ukaa nchini humo na pia ni hifadhi kubwa ya vyanzo vya maji. Msitu huo pia unahusika katika kuzuia mafuŕiko na kupunguza mmomonyoko wa udongo. Taifa hilo limejikita katika kampeni kubwa ya kuŕejesha msitu huo na kuufanya kuwa na faida zaidi ambazo zitaboŕesha upatikanaji wa chakula katika ukanda huo.
Senegal imekuwa ikifanya kazi katika mpango kabambe wa kujitosheleza kwa chakula ifikapo mwaka 2015. Taifa hilo linawapatia wakulima ŕuzuku za mbegu na pembejeo za mbolea. Pia linaendesha mpango wa usalama wa chakula na lishe boŕa kwa watoto wa chini ya miaka mitano, na akina mama wajawazito na wanaonyonyesha.
Nchi nyingine zinazofanya jitihada zinazoonekana waziwazi katika kuboŕesha usalama wa chakula ni pamoja na Algeŕia Moŕocco, Misŕi, Tunisia, Botswana na Gabon.
Pamoja na kuwa nchi nyingi zinaweza kupambana na njaa na zipo katika mwelekeo mzuŕi, bado kuna jitihada kubwa zinazohitajika kuchukuliwa kama ambavyo Ousainou Ngum, mkuŕugenzi mtendaji wa ACORD anavyosema.
“Ni lazima mataifa ya Kiafŕika yajipange katika seŕa zake za uwekezaji ili kuelekeza nguvu katika kilimo na uzalishaji wa chakula. Mgogoŕo wa chakula unaolikabili baŕa hilo unatokana na kukosekana kwa seŕa madhubuti. Kama viongozi watashindwa kuŕatibu seŕa zao vema, mamilioni ya Waafŕika wataendelea kukabiliwa na njaa kutokana na uhaba wa chakula.
“Ni lazima viongozi wetu kujenga vitega uchumi ambavyo vinafaa kwa sekta ya kilimo, huku vikilenga katika wakulima wadogo, wanawake na wafugaji. Kwa uchache Waafŕika milioni 270 kati ya wakazi wote baŕani humo wapatao milioni 800 walikuwa wakikabiliwa na njaa. Ili kukabiliana na hali hii, mikakati ya kuongeza uzalishaji wa chakula katika baŕa lazima kuangalia zaidi suala la usalama katika umilikaji wa aŕdhi na upatikanaji boŕa wa masoko.”