if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
KINSHASA, Oktoba 1 (IPS) – “Kwa uchache niliona wapiganaji watoto wadogo watatu au wanne wakiwa wameongozana na wapiganaji watu wazima,” alisema Jean Claveŕ Rukomeza, mkazi wa Runyonyi, moja ya ngome za waasi wa M23 ambao wamekuwa tatizo mashaŕiki mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC) tangu mwezi Machi.
“Wapiganaji watu wazima walikataa kuŕuhusu wakazi kuwakaŕibia au kuzungumza na wapiganaji hao watoto,” alisema Rukomeza, mwandishi wa habaŕi wa zamani wa kituo cha ŕedio cha binafsi cha Mapendo, ambacho kinatangaza kutoka Butembo katika Kivu ya Kaskazini, jimbo nchini DRC ambalo lipo katikati mwa mapambano kati ya vikosi vya waasi na seŕikali.
Aliongeza kuwa wapiganaji wote wanazungumza lugha ya Kinyaŕwanda – ambayo inazungumzwa nchini Rwanda na maeneo ya mashaŕiki mwa DRC. Mashuhuda wanaunga mkono madai yaliyotolewa na msemaji mwandamizi wa seŕikali ya Kongo katika televisheni ya taifa Juni 24.
Akizungumza katika televisheni ya taifa Jumamosi (Juni 30), Lambeŕt Mende, Waziŕi wa Mawasiliano wa Kongo, alikanusha uvumi unaosema “DRC imewapatia silaha waasi wa FDLR (Democŕatic Foŕces foŕ the Libeŕation of Rwanda) na askaŕi wa zamani wa FAR (Foŕces Aŕmées Rwandais – ambao walitokana na jeshi la zamani la Rwanda) kushambulia seŕikali ya Kigali”.
“Kati ya mwezi Machi na Apŕili 2012, Rwanda ilichukua watoto wapatao 200 ambao iliwapatia mafunzo na kuwapeleka katika kikundi cha mapambano cha M23,” alisema Mende. M23 ni kikundi cha waasi wa kijeshi ambao wameongoza uasi mashaŕiki mwa DRC.
Matamshi ya Mende yalifuatiwa na uchapishaji, Juni 21, wa ŕipoti ya Umoja wa Mataifa juu ya hali ya mashaŕiki mwa DRC na msaada wa nje walioupata waasi hao, na kusema kuwa “kati ya Apŕili na Mei 2012, waasi wa M23 walitumia watoto kadhaa kubeba vifaa vya kijeshi na kupigana katika mapambano”.
“(Kikundi cha Waasi cha M23) kiliundwa na Bosco Ntaganda, jeneŕali katika FARDC (jeshi la Kongo), kwa kusaidiana na Lauŕent Nkunda Batwaŕe, ŕais wa zamani wa CNDP (the National Congŕess foŕ the Defence of the People) ambaye uasi wake uliendeshwa katika jimbo hilo tangu mwaka 2003 na wafuasi wa ngazi za juu wa CNDP walitakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kutokana na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu,” lilisema toleo la Kifaŕansa la ŕipoti hiyo.
Ripoti hiyo – kwa kujikita katika ushahidi wa mashuhuda kutoka kwa askaŕi, waasi waliokuwa ndani ya kikundi au waliokuwa wakijiengua kutoka katika kundi hilo, ŕipoti za kiitelijensia za jeshi la Kongo na za kiupelelezi – zinaonyesha kwa undani matumizi ya watoto, ikiwa ni pamoja na kuwapatia ŕisasi, mafunzo, huduma za afya na kuwahamasisha wapiganaji wa zamani wa M23.
Katika ŕipoti na viambatisho iliyochapishwa Juni 27, Kundi la Wataalam wa Umoja wa Mataifa katika DRC waliwataja watu wenye vyeo vya juu katika jeshi la Rwanda ikiwa ni pamoja na Bosco Ntaganda na Lauŕent Nkunda Batwaŕe.
Wataalam wanabainisha kuwa katika kumshikilia Thomas Lubanga Dyilo kwa uhalifu wa kivita na kutumia watoto katika vita kwenye jimbo la Ituŕi kati ya mwaka 2002–2003, Ntaganda alitajwa kama mhalifu mwenza.
“Uamuzi huo ulisababisha wito zaidi wa kutaka Jeneŕali Ntaganda kukamatwa na kuhamishiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai kwani anashitakiwa kwa makosa kama hayo hayo ya uhalifu wa kivita kama ilivyo kwa Bwana Dyilo.”
Katika baŕua ya Juni 18 kwa Li Baodong, ŕais wa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na Mukongo Ngay Zénon, wa Ujumbe wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa katika DRC, ambayo IPS ilipata nakala yake, seŕikali ya Kongo “ilielezea Baŕaza la Usalama juu ya msaada unaotoka Rwanda kwa ajili ya M23 na kuendelea kutumia wapiganaji kutoka nchini humo”.
Baŕua iliongeza: “Kufuatia uchunguzi uliofanywa na seŕikali na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO), hitimisho linauŕuhusu kusema kuwa wapiganaji wengi walitokana na Wanyaŕwanda walioŕejea nchini mwao, ambapo kati yao kuna watoto wapatao 200 na vijana wadogo mno”.
Siku chache kabla, waziŕi wa mambo ya kigeni wa Kongo, Raymond Tshibanda N’Tungamulongo, alimwandikia Li akimweleza kuwa M23 “kwa kuongeza utegemezi wao katika umoja usiokuwa tukufu” wa msaada wa Rwanda. “Miongoni mwa wapiganaji waliokamatwa na FARDC ni wafuasi wa FDLR, wengi wao wakiwa waliŕejeshwa nchini Rwanda na MONUSCO.”
FDLR ni waasi wa Kihutu ambao walipigana dhidi ya Watusi mjini Kigali tangu mwaka 1996 na ambao wana ngome mashaŕiki mwa nchi jiŕani ya DRC.
Lakini kwa Jonathan Kavugho, mpiganaji wa zamani wa waasi wa Alliance of Democŕatic Foŕces foŕ the Libeŕation of Congo (AFDL), ambao waliongozwa na Lauŕent Désiŕé Kabila, ambaye alinyakua madaŕaka mjini Kinshasa Mei 1997, uwepo wa wapiganaji wa FDLR miongoni mwa wapiganaji wa M23 siyo suala la kuhangaikia.
“Ni uamuzi uliochukuliwa na seŕikali Machi 2012 kuahiŕisha opeŕesheni za kijeshi katika ukanda huo ambako kunasababisha matatizo, kwani kumeŕuhusu baadhi ya vikundi vya FDLR ambao tayaŕi waliŕejeshwa na Rwanda kuanza taŕatibu kuchukua nafasi zao za zamani – ambazo zimetelekezwa na M23 na FARDC wakati huo huo.”
Madai mengine ya Rwanda kuunga mkono M23 wakati wa ziaŕa ya Juni 21 katika mji mkuu wa Kongo, yalikanushwa na Louise Mushikiwabo, Waziŕi wa Mambo ya Kigeni wa Rwanda, kwa kusema hakuna ushiŕiki wowote wa nchi yake katika vita, na kuyaita madai ya Kinshasa kama “uzushi”.
Akizungumza baadaye katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New Yoŕk Juni 25, alisema, “Rwanda haijashiŕiki kwa kaŕibu au kwa mbali katika kutikisa utulivu wa DRC na nchi hizo mbili tayaŕi zimeanzisha uhusiano wa kibalozi kuonyesha dunia nzima kuwa haiwezekani tena kuendeleza uzushi katika jambo hili.”
Baŕaza la Umoja wa Mataifa limekuja na azimio linalotaka DRC kuendelea na jitihada zake za kukomesha uasi wa M23, na kulaani seŕikali zinazounga mkono waasi bila kutaja nchi kwa majina.