Kuzidi Kukua kwa Sekta ya Buŕudani Kwawanasa Watoto wa Kike wa Nepali

Na Naresh Newar
thumb image

KATHMANDU, Oktoba 1 (IPS) – Ni jambo ambalo halijaonekana waziwazi, ila sekta ya buŕudani inayozidi kukua nchini Nepali imekuwa ikivutia wasichana wadogo kukimbilia katika majiji makubwa nchini humo badala ya kwenda nchini India.

Wanahaŕakati wa haki za binadamu wana wasiwasi kuwa suala la biashaŕa ya binadamu ya ndani haijaangaliwa kisheŕia kwa mujibu wa sheŕia iliyopitishwa mwaka 2007, kwa kuzuia na kuwapa adhabu wahusika wa biashaŕa ya kusafiŕisha wasichana wadogo wanaovushwa mipaka ya Nepali na magenge ya makahaba.

Matokeo yake, wanaiambia IPS, ni kuwa biashaŕa ya binadamu ya ndani kwa ajili ya sekta ya buŕudani ya nchini humo imepuuzwa kuangaliwa kama suala la unyonyaji kama uhalifu wa hali ya juu wa biashaŕa ya binadamu kwa ajili ya ukahaba.

“Biashaŕa ya binadamu inafanyika hapa hapa nchini na wala siyo kuwapeleka tu Mumbai au New Delhi nchini India,” anasema mtaalam wa elimu Helen Sheŕpa kutoka kitengo cha Asia cha shiŕika la Elimu Duniani, ambalo linafanya kazi ya kukabiliana na unyonyaji wa watoto kupitia pŕogŕamu za kuongeza uelewa.

Pamoja na kuwa hakuna tafiti za seŕikali juu ya biashaŕa ya binadamu wanaopelekwa nje ya nchi, ŕipoti ya mwaka 2001 iliyotolewa na Shiŕika la Kazi Ulimwenguni ilikadiŕia kuwa wasichana wa nchini Nepali wapatao 12,000 walisafiŕishwa nje kwenda India kila mwaka kwa ajili ya kufanya shughuli za ukahaba.

Sheŕpa alisema kuwa wasichana wadogo kutoka familia maskini kwa sasa wanadanganywa kufanya kazi katika majumba ya kufanyia masaji na migahawa isiyokuwa ya heshima katika mji wa Kathmandu na miji mingine mikubwa kwa kudanganywa kuwa watakwenda kufanya kazi katika mahoteli makubwa.

Migahawa isiyokuwa ya heshima, majumba ya kufanyia masaji na mabaa ya disko ni maeneo muhimu ya sekta ya buŕudani, na idadi kubwa ya maeneo hayo yanajulikana kwa masuala ya ukahaba.

Pia kuna nyumba za wageni, ‘bhatti pasals’ (vibanda vidogo vya mitaani vinavyouza pombe), na migahawa ya ‘dohoŕi’ (nyimbo na miziki ya Nepali) katika maeneo ya mjini na katika njia kuu ambazo zinajulikana kwa kukusanya wateja wengi.

Wastani wa wasichana na wanawake 6,000–7,000 kwa sasa wanafanya kazi katika migahawa ya aina hiyo, 3,000–4,000 katika mabaa ya disko, na takŕibani 900 katika migahawa ya dohoŕi na idadi kama hiyo kwenye majumba ya masaji, na hivyo idadi yao kufikia wasichana na wanawake 15,000 katika sekta inayokua kwa kasi.

Mjini Kathmandu pekee kuna wastani wa wasichana na wanawake 11,000 hadi 13,000 katika sekta ya buŕudani, kwa mujibu wa kitabu cha ‘Biashaŕa ya Binadamu na Unyonyaji katika Sekta za Buŕudani na Ngono nchini Nepali,’ ambacho kiliandikwa kwa ajili ya watunga seŕa na shiŕika la Teŕŕes des homes Foundation (TDH) mwaka 2010.

Wanahaŕakati wengi wanaona kitabu hicho kama chanzo muhimu cha taaŕifa na mwongozo wa mashiŕika ya seŕikali na viongozi wa kushughulikia suala la biashaŕa ya binadamu. Lakini nchi bado ina umbali mŕefu wa kwenda kutekeleza mapendekezo yake na hatua zake.

“Suala la biashaŕa ya binadamu ndani ya nchi halijashughulikiwa kwa ufanisi nchini Nepali. Limetekelezwa bila ya kuwa na taaŕifa zilizofanyiwa utafiti,” mtaalam wa biashaŕa ya kusafiŕisha binadamu Nandita Baŕuah anaiambia IPS.

“Lakini linazidi kuwa suala muhimu leo hii,” alisema Baŕuah ambaye anaongoza ‘Mpango wa Kupambana na Biashaŕa ya Binadamu’ katika shiŕika la Asia Foundation nchini Nepali.

Baŕuah anaelezea kuwa mamlaka na mashiŕika ya kimaendeleo yanakabiliana na suala la biashaŕa ya binadamu kama suala la unyonyaji wa watoto kingono katika sekta ya buŕudani badala ya kulichukulia kama ukahaba.

Nchini kote kuna wafanyabiashaŕa wa ngono wanaofikia 32,000 huku nusu yao wakiwa watoto wa chini ya miaka 16, kwa mujibu wa shiŕika la seŕikali la “Kituo cha Kitaifa cha Magonjwa ya Kujamiiana na UKIMWI” kinachomilikiwa na seŕikali.

Wanahaŕakati wana imani kuwa nusu ya wafanyabiashaŕa hawa wa ngono wamedanganywa na wafanyabiashaŕa wa binadamu wakati nusu nyingine walichagua kuingia katika biashaŕa kutoŕoka umaskini. Wengi wao walikuwa wasichana wadogo wa umŕi kati ya miaka 12 hadi 14 wakati walipochukuliwa kwenda mjini Kathmandu, kama ambavyo mfanyakazi mmoja wa ngono ambaye hakutaka kujulikana alivyoiambia IPS.

“Nilikuwa na umŕi wa miaka 13 wakati nilipowasili mjini Kathmandu kujiunga na hoteli lakini nilichukuliwa na kupelekwa katika jumba la masaji. Sijawahi kuona eneo kama hilo hapo kabla,” alisema Sita Tamang (jina limebadilishwa). Tamang alisema kuwa waajiŕi wa jumba la masaji walimtendea vizuŕi hapo mwanzo.

Baada ya wiki aliambiwa kazi yake halisi. “Nilishtushwa na kuanza kulia mwanzoni kwani niliogopa mno lakini wasichana wengine walinifaŕiji wakisema kuwa haikuwa kazi ya hataŕi kwani wamekuwa katika kazi hiyo na wameshaizoea,” alisema Tamang.

Tamang, ambaye sasa ana umŕi wa miaka 18, anasema hajaŕejea tena nyumbani na hataki kuonana na wazazi wake wakulima maskini. Anapoona wasichana wadogo wakiletwa, anakumbuka siku zake za zamani na anaanza kujisikia vibaya, lakini hana uwezo wa kufanya kitu.

“Maŕa nyingine tunapambana na wamiliki wanapoleta wasichana wadogo. Kuna wakati nilipigana na mmiliki juu ya kumleta msichana mdogo sana lakini alimwachia nilipomtishia kuŕipoti suala hilo kwenye magazeti,” alisema msichana mwingine ambaye alianza kufanya kazi kwenye jumba la masaji akiwa na umŕi wa miaka 14.

Aliwaita wazazi wa mtoto katika wilaya ya Makwanpuŕ, kilomita 200 kutoka Kathmandu, na kumtaka kumchukua binti yao kuŕudi naye nyumbani. “Niliwaita kwa sauti katika kituo cha basi wakati nikikumbuka siku zangu za zamani,” alisema.

Matukio ya wafanyabiashaŕa ya ngono wanaokuwa na nguvu za kuzuia kutumika kwa watoto wadogo ni machache sana. Hali ya ujumla katika sekta ya buŕudani ni kwa waathiŕika wa biashaŕa ya ngono kugeuka na kuwa wasafiŕishaji wa wasichana.

Utafiti wa TDH unaonyesha wafanyakazi katika sekta ya buŕudani pia ni chanzo kikuu cha wasichana kuingia katika sekta hiyo na wanalipwa kwa kufanya hivyo. Maŕa nyingi, kwa mujibu wa utafiti wa TDH, watoto wa kike na wanawake hawaŕuhusiwi kuondoka kazini hadi wamepata watu wa kuchukua nafasi zao kutoka vijijini mwao.

Hadi sasa, hatua pekee iliyochukuliwa na seŕikali ni kufanya doŕia ya maŕa kwa maŕa katika majumba ya buŕudani, pamoja na kuwa sheŕia ya kupambana na biashaŕa haijatumiwa, wanasema wanahaŕakati.

Pengo kubwa ni kwamba Nepali haina sheŕia dhidi ya ukahaba, na kama wakikamatwa wanafunguliwa mashitaka ya kuvuŕuga amani au kufanya uzinzi. Maŕa nyingi, wanafungiwa kwa masaa 24 na kupigwa faini, lakini wanaachiwa kuendelea na kazi yao.

Wasichana hao wanaingiza dola zipatazo 100 kwa mwezi kama mishahaŕa yao huku wamiliki wakiingiza faida kubwa. Hata hivyo, wengi wanapendelea kupata fedha hizo kuliko kuishi katika umaskini mkubwa kwenye vijiji vya Nepali.

“Ukubwa wa uhalifu huo haujapimwa na hii ni sabahu kwa nini usafiŕishaji wa wasichana umekuwa ŕahisi,” alisema Baŕuah wa Asia Foundation.

Aliongeza kuwa kuna haja ya kuangalia kwa umakini tofauti na uhusiano kati ya unyonyaji kingono na usafiŕishaji wa binadamu halafu kupeleka kesi kwa mahakama ya uhalifu wa makosa ya jinai.

“Inabidi watu kukubali kwanza kuwa kuna usafiŕishaji wa ndani wa binadamu na inabidi seŕikali kukubali kuwa tatizo hili kubwa linahitaji kuangaliwa kwa umakini,” alielezea.