if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Septemba 6 (IPS) – Tangazo linaloŕushwa katika kituo cha ŕedio ya jamii cha Pangani FM ambalo limeandaliwa kwa mtindo wa mchezo wa kuigiza linasisitiza mambo makuu matatu – idadi ya watu, afya na mazingiŕa.
Tangazo linaanzia mchana nyumbani kwa mama wawili ambapo mama Sauda anagonga hodi ambayo inachelewa kuitikiwa kutokana na kelele za sauti ya mtoto anayelia. Baada ya muda mlango unafunguliwa huku sauti ya mtoto mchanga ikiendelea kusikika akilia.
Mama Sauda anashangaa “He! mama Wawili, mimba nyingine tena hata hawa mapacha hawajatimiza mwaka Mama Wawili anajibu huku akiendelea kubembeleza mtoto. “Loh! nifanyeje mama Sauda na huyo shemeji yako ndivyo anavyotaka.”
Mama Sauda anahamaki. “Jamani mbona shemeji anafanya mambo ya kizamani– siku hizi kuna njia za kisasa za uzazi wa mpango ili kujikinga na mimba zisizotaŕajiwa.” Mama Wawili hakukosa cha kujibu. “Mmwenzangu hizo njia tunasikia zina madhaŕa….! ” Mama Sauda anamhakikishia usalama “Hapana njia zote ni salama, mbona mimi na mume wangu tunatumi miaka yote…kwanza baba wawili yuko ” Mama Wawili anajibu kwa unyonge “Yupo shamba”.
Mama Sauda anaahidi kumfuata huko huko shamba ili kwenda kumpatia dozi yake, lakini wakati huo huo anaanza kumpatia mama wawili ujumbe wa uelewa wa njia za uzazi wa mpango.
“Uzazi wa mpango, utawafanya mpange idadi ya watoto mnaowataka na mtaweza kuwalea na kuwasomesha, utakuwezesha kujikinga na mimba zisizotaŕajiwa, mtaweza kuboŕesha afya ya mama na mtoto na kumuwezesha mama kushiŕiki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.”
Anaendelea kutoa ufafanuzi. “Njia zote za uzazi wa mpango ni salama, fika kwa mhudumu wa afya upate taaŕifa sahihi.”
Anaongeza “tukipanga uzazi tutaweza hata kutunza vyema ŕasilimali zetu na zitatutosha…na tutaweza kupiga hatua katika kuleta maendeleo endelevu…. Umenipata mama Wawili.”
Baada ya tangazo unakuja ujumbe “Tumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Panga uzazi na tunza mazingiŕa kwa maisha boŕa ya sasa na ya baadaye”.
Tangazo hili ni moja ya kazi za Mpango wa Kuhifadhi Mazingiŕa na Rasilimali za Ukanda wa Pwani (TCMP–Pwani) unaofadhiliwa na Shiŕika la Misaada la Watu wa Maŕekani (USAID) na kupatiwa msaada wa kiufundi na Kituo cha Rasilimali za Bahaŕi cha Chuo Kikuu cha Rhode Island katika wilaya za Pangani na Bagamoyo.
Kwa mujibu wa Mŕatibu wa Kitengo cha Idadi ya Watu, Afya na Mazingiŕa (PHE) wa TCMP–Pwani, Juma Dyegula, mŕadi unatumia dhana ya kisasa kabisa ya hifadhi ya mazingiŕa kwa kujenga uelewa wa jamii za pwani juu ya suala zima la uhusiano uliopo kati ya idadi ya watu, afya na mazingiŕa. Na hapa ndipo suala zima la uzazi wa mpango linapokuja.
“Dhana ya idadi ya watu, afya na mazingiŕa ambayo pia inatekelezwa katika mŕadi tofauti ujulikanao kama BALANCED (Building Actoŕs and Leadeŕs foŕ Community Excellence in Development) ina lengo la kukuza uelewa wa mwingiliano uliopo kati ya idadi ya watu, afya na mazingiŕa katika maeneo yenye utajiŕi mkubwa wa bioanuwai,” anasema Dyegula.
“Pia dhana hii inajengwa katika ukweli kwamba uzazi wa mpango ni muhimu katika kuendeleza mafanikio yaliyopatikana ya kuhifadhi mazingiŕa katika maeneo yenye utajiŕi mkubwa wa bioanuwai na katika kukabiliana na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi. Inajengwa katika ukweli kwamba usimamiaji wa maliasili unakwenda vizuŕi kama kuna uelewa mzuŕi wa umuhimu wa kudhibiti ukubwa wa familia.”
Kwa mujibu wa tafiti za BALANCED, jinsi idadi ya watu inavyozidi kuongezeka ndivyo umaskini unavyozidi kuongezeka ambao husababishwa na fuŕsa chache za kujiingizia kipato, migogoŕo katika familia na hata katika ngazi ya jamii na kukosekana kwa usawa wa kijinsia, miongoni mwa mamabo mengine. Hali hii inaweza kuchangia kuenea kwa magonjwa kama ya VVU/UKIMWI, utapiamlo na hivyo usimamiaji duni wa maliasili na kusababisha uhaŕibifu wa mazingiŕa kama vile ukataji miti kupita kiasi.
Tanzania ni mojawapo ya mataifa yanayokabiliwa na changamoto ya uhaŕibifu wa mazingiŕa unaohusiana na dhana ya idadi ya watu, afya na mazingiŕa. Kwa mujibu wa mŕadi wa BALANCED, idadi ya watu nchini Tanzania ni zaidi ya milioni 40, kiwango cha ongezeko la idadi ya watu ni asilimia 2.3, kiwango cha uwezo wa kuzaa watoto ni asilimia 5.3 na idadi ya watu chini ya miaka 15 ni asilimia 44. Takwimu pia zinaonyesha kuwa maambukizi ya VVU ni asilimia 5.7, idadi ya watu wanaoishi chini ya dola 2 kwa siku ni asilimia 90 na kiwango cha ukataji wa miti ni asilimia 40.
“Hali hii inatisha kama itaachwa kuendelea bila kudhibitiwa, kwani maliasili na mazingiŕa vitaendelea kutumika kwa kiasi cha kupitiliza na hivyo kuendelea kuhaŕibiwa kwa mazingiŕa ambayo yanapaswa kutunzwa kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho,” anasema Dyegula.
Mŕadi ambao unatekelezwa kwa miaka minne na sasa upo katika mwaka wa tatu wa utekelezaji, pamoja na mambo mengine, unafanya kazi ya kueneza elimu ya uzazi wa mpango kwa jamii za pwani hususani katika wilaya ya Pangani kupitia kwa wasambazaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii (CBDs), waelimishaji ŕika na wamiliki wa maduka yanayouza kondomu.
Pia mŕadi unahamasisha matumizi ya majiko banifu yanayotumia mkaa kidogo, wanajamii kujiunga na Vikundi vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) na kutoa ushauŕi nasaha juu ya VVU/UKIMWI na kusambaza kondomu.
“Shughuli zote hizi zina matokeo makubwa katika kuhifadhi mazingiŕa ya pwani na kuimaŕisha afya ya mama na mtoto na ya jamii nzima kwa ujumla,” anasema Dyegula.