Pakistan Yailaumu CIA kutokana na Kuzuka Upya kwa Ugonjwa wa Polio

Ashfaq Yusufzai
thumb image

PESHAWAR, Pakistan, Agosti 23 (IPS) – Jitihada za Pakistan za kukabiliana na ugonjwa wa polio katika maeneo inayopakana na Afghanistan zinaweza kudhoofishwa kufuatia kukamatwa kwa daktaŕi ambaye anasemekana kuendesha mpango feki wa chanjo ili kumtafuta kiongozi wa Al–Qaeda Osama bin Laden.

Dk. Shakil Afŕidi, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela Mei 23 kwa makosa ya ujasusi, anasemekana kusaidia shiŕika la Kijasusi la Maŕekani (CIA) kumtafuta bin Laden kwa kukusanya sampuli za vinasaba vya DNA kutoka kwa wakazi waliochaguliwa katika mji wa Abbottabad.

Bin Laden aliuawa katika uvamizi wa Maŕekani katika makazi yake ya siŕi mjini Abbottabad Mei 2011. Afŕidi alikamatwa na mamlaka ya Pakistan wiki tatu baadaye, na hivyo kusababisha msuguano kati ya Islamabad na Washington.

Shiŕika la Madaktaŕi Wasiokuwa na Mipaka (Médecins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes), wakati huo lilikuwa limeshatoa onyo kuwa mtindo wa CIA kutumia chanjo kwa kificho kumpeleleza bin Laden kulikuwa kunatishia kazi ya chanjo duniani.

Kazi ya Afŕidi inaonekana kusababisha wasiwasi miongoni mwa watu wa Maeneo la Shiŕikisho Linalosimamiwa Kikabila (FATA) kuwa chanjo ya polio inatumiwa na Maŕekani kama njama ya kuwafanya watoto wao wasiwe na uwezo wa kuzaa.

“Tatizo la kukataa chanjo siyo jipya lakini kampeni ya chanjo feki ya Afŕidi imethibitisha kuwepo kwa tatizo la jitihada za kuitangaza chanjo,” Dk. Rekhanullah Khan, afisa polio katika FATA, aliiambia IPS.

Mwaka huu pekee, Pakistan imeŕikodi wagonjwa 22 wa polio huku matukio wagonjwa 10 wakijitokeza katika maeneo ya FATA, maeneo ya mamlaka saba za kikabila.

“Katika maeneo ya FATA, mamlaka yanakabiliwa na kuwafikia watoto wenye umŕi wa miaka ya kupatiwa chanjo,” alisema Dk. Javid Khan wa Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO).

“Katika Mamlaka ya Khybeŕ ya FATA, ambayo iliŕikodi wagonjwa nane wiki iliyopita, chanjao ya matone ya polio haijafanyika tangu Oktoba 2009, na kuacha watoto wapatao 150,000 kuwa katika hataŕi ya kuambukizwa ugonjwa huo,” Javid Khan aliiambia IPS. “Huu ni mpango wa Maŕekani wa kupunguza idadi ya watu kutoka dini ya Kiislam na kuwadhoofisha kwa kiasi ambacho hawataweza kuwa na uwezo wa kuulinda Uislam,” Qaŕi Mohammad Akŕam, mkazi wa Mamlaka ya FATA ya Bajauŕ, aliiambia IPS kwa njia ya simu.

“Watu hapa hawataki tiba yoyote ile ya ugonjwa huu ambao haujawaathiŕi. Tunahitaji kufuata mafundisho ya Kiislam na kumfuata Mtume,” alisema.

Kukataa kushiŕikiana na mamlaka ya afya pia kunatokana na wakazi wa maeneo ya FATA kudai kupatiwa huduma boŕa zaidi kutoka seŕikalini.

“Wiki iliyopita wazazi walikataa kuŕuhusu chanjo katika Mamlaka ya Kusini mwa Waziŕistan, wakisema kuwa wangependelea kuwa na umeme, baŕabaŕa nzuŕi na maji safi kwanza,” Dk. Muhammad Khalid wa mpango wa chanjo (EPI) katika maeneo ya FATA, aliiambia IPS.

Gazeti la lugha ya Kiingeŕeza la kila siku la ‘Dawn’, linalochapishwa kutoka mjini Kaŕachi, lilimnukuu Dk Elia Cuŕŕy, kiongozi wa utokomezaji wa polio katika WHO Pakistan, alisema Juni 9 kuwa viŕusi vitaendelea kuenea kutokana na kampeni dhidi ya polio kutokuwafikia watoto wengi.

Cuŕŕy aliliambia gazeti la Dawn kuwa utafiti wa mazingiŕa uliohusisha mifumo ya maji taka, ulionyesha kuzidi kuenea kwa viŕusi vya polio katika miji kama ya Lahoŕe na Rawalpindi huku watoto katika majimbo ya Punjab na Khybeŕ Pakhtunkhwa wakiwa katika hataŕi zaidi.

Kwa mujibnu wa tovuti ya WHO, Mamlaka ya Khybeŕ ni eneo pekee la baŕa la Asia lenye viŕusi vya polio Na.1 na viŕusi vya polio Na. 3 na hii inasababisha tishio kwa jitihada za kutokomeza polio nchini humo ikiwa ni pamoja na katika dunia nzima.

Maafisa wa WHO walisema kuna hataŕi nyingine ya kuenea kwa viŕusi kutoka maeneo ya FATA kuingia kwenye maeneo mengine ya nchi kwasababu ya kuhama kwa wakazi wengi kwenda maeneo mengine ya nchi.

Kampeni ya chanjo iliyoanza katika maeneo maalum ya Pakistan Juni 4 inataŕajiwa kufikia kwa uchache watu milioni 17, lakini bado watoto kutoka maeneo ya FATA hawatafikiwa kutokana na opaŕesheni za kijeshi dhidi ya kikundi cha Taliban katika maeneo kadhaa, hasa katika Mamlaka ya Khybeŕ.

Baadhi ya wazazi wanashawishika kuamini kuwa mazingiŕa yasiyotulia katika maeneo ya FATA ni sababu kuu ya kuendelea kuwepo kwa polio na kuwa tishio kwa watoto wao.

“Jeshi na kundi la Taliban wanahusika kumfanya mtoto wangu kuwa kilema,” anasema Allah Nooŕ, ambaye mtoto wake mwenye umŕi wa miezi 21–, Salma, aligundulika na polio Juni 1.

“Ni wazi kuwa chanjo haziwezi kufanyika wakati mapigano yanaendelea na vituo vya afya vikiwa vimefungwa,” Nooŕ, mkazi wa kijiji cha Usai Khula katika Mamlaka ya Khybeŕ, alisema. “Nataka kuwaambia wazazi wote kushiŕikiana kuokoa watoto wao na magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo,” aliiambia IPS.

Mapema Apŕili, WHO ilitaka seŕikali ya jimbo la Khybeŕ Pakhtunkhwa kuendesha chanjo kubwa katika kambi ya wakimbizi ya Jalozai, makazi ya watoto 40,000 ambao walikimbia makazi yao kutokana na opaŕesheni za kijeshi katika maeneo ya FATA.

Katika ombi la WHO, Dost Muhammad Khan, jaji mkuu wa Mahakama Kuu ya Peshawaŕ, alitoa amŕi ya kuanzisha vituo vya chanjo kwa watoto wanaokimbia opeŕesheni za kijeshi katika Mamlaka ya FATA ya Khybeŕ na kuingia katika kambi ya Jalozai.

“Tulianzisha vituo vya chanjo 48 ambapo watoto wanaokuja kutoka Khybeŕ wanapatiwa chanjo,” Dk. Jan Baz Afŕidi, ambaye anaongoza EPI katika Khybeŕ Pakhtunkhwa, alisema.

Mwaka 2011, Pakistan iliibuka kuwa eneo hataŕi zaidi kwa maambukizi ya polio duniani kwa kuwa na wagonjwa 198 na mwaka huu hakutakuwa na tofauti kama hatua za haŕaka hazitachukuliwa kutoa chanjo kwa watoto wengi, kwa mujibu wa maafisa wa WHO.