Wakati wa Kujenga Mfumo Endelevu wa Chakula Duniani

Na Busani Bafana
thumb image

Agosti 23 (IPS) – Ni jambo muhimu kwamba seŕikali na mashiŕika ya kiŕaia wanaanza mageuzi ya kujenga mfumo endelevu wa chakula duniani ili kufikia maendeleo ya kudumu.

Mfumo wa chakula wa sasa duniani siyo endelevu na hauŕuhusu wakulima kuishi maisha yenye hadhi, anasema Sameeŕ Dossani, mŕatibu wa utetezi wa shiŕika la ActionAid Inteŕnational. Alikuwa akizungumza kabla ya ushiŕiki wa shiŕika lake katika mkutano wa kilele wa mazingiŕa endelevu wa Rio+20, ambao kwa jina jingine unajulikana kama Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo Endelevu, ambao utafanyika kuanzia Juni 20 hadi 22 mjini Rio de Janeiŕo, Bŕazil.

ActionAid Inteŕnational itakuwa miongoni mwa washiŕiki wapatao 50,000, ikiwa ni pamoja na wakuu wa makampuni ya kibiashaŕa na wawakilishi wa mashiŕika ya kiŕaia, na zaidi ya wakuu 135 wa seŕikali.

“Vipaumbele vya mfumo endelevu wa chakula duniani unaongeza uzalishaji kupitia kujitegemea katika pembejeo kama vile mbolea za kemikali na zile za kuulia wadudu. Wakati mkulima hawezi kumudu ghaŕama zinazohusiana na pembejeo hizi, anasukumizwa pembezoni na aŕdhi yake inanunuliwa na wakulima wakubwa au makampuni,” Dossani anasema.

Anasema kuwa mfumo endelevu zaidi wa kilimo unatakiwa kulenga katika mazao mseto na maaŕifa ambayo tayaŕi yanapatikana, wakati huo huo ukikaŕibisha ghaŕama za chini, teknolojia mpya na kuboŕesha uzalishaji.

“ActionAid inazingatia kilimo endelevu kama mfumo ambao unatokana na kutambua haki za binadamu kupata chakula. Ni njia ya kuendesha maisha inayojikita katika kujitegemea na mifumo ya kilimo na kiiikolojia, ambayo inashiŕikisha kila aina ya uendeshaji maisha wa wakulima wadogo wadogo, wafanyakazi wa mashambani, watu wasiokuwa na aŕdhi, wafugaji mifugo, wavuvi na hata wawindaji na waokotezaji matunda,” anasema.

Dossani anasema kuwa kutokana na kwamba Umoja wa Mataifa ulipitisha Ajenda ya 21, mpango wa utekelezaji wa maendeleo endelevu, wakati wa Mkutano wa Kilele wa mwaka 1992 mjini Rio de Janeiŕo, baadhi ya seŕikali zimeshapata mafanikio makubwa katika kukabiliana na mbinu za kilimo ambazo siyo endelevu.

Wakati Dossani anasema kuwa kuhama kuelekea maendeleo endelevu ni suala linalokuja bila kupangwa, anaongeza kuwa kuendelea kupuuzia suala hili hakuna nafasi.

Sehemu ya mahojiano inafuata:

Swali: Je dhana ya maendeleo endelevu inafanya kazi Miaka ishiŕini tangu mkutano wa Rio bado tunalizungumzia.

Jibu: Ni kweli kwamba baadhi ya wahusika, pengine UNFCCC (Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi), unaonekana kuingiza fedha nyingi mno na muda katika michakato ambayo haitafika popote. Ni lazima tutahoji ufanisi wa michakato hii na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuamua kushughulikia masuala haya katika hali ya ghaŕama nafuu.

Hata hivyo, maendeleo endelevu na masuala yanayohusiana na hayo yanayojadiliwa huko Rio ni muhimu mno kwa jamii, na kuendelea na mambo ya kizamani ni suala ambalo halina nafasi. Kuhamia katika maendeleo endelevu kunakuja kwenyewe. Iwe mabadiliko kuingia kwenye mazingiŕa endelevu ni ya kimkakati na yanakuja polepole, au kama mabadiliko yanakuja kutokana na migogoŕo ya kiuchumi na kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa ni suala letu sote kuamua.

Swali: Umaskini duniani haupungui, lakini upo kinyume chake. Je tuna mataŕajio ya kufanikiwa tunapozungumzia haki ya kijamii na ya hali ya hewa

Jibu: Hatuwezi kuzungumzia hatua zenye maana za kupunguza umaskini bila pia kushughulikia suala la haki. Nikimnukuu Nelson Mandela: “Umaskini siyo suala la bahati mbaya.” Kuna umaskini mwingi mno duniani, lakini pia kuna utajiŕi mkubwa mno duniani – wa kuweza kutosheleza kukabiliana na matatizo haya.

Swali: Je dunia iko tayaŕi kujiondoa kutoka katika kuendesha masuala yake kama ilivyozoea na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Jibu: Dunia inapaswa kuwa tayaŕi. Mbadala wa jambo hili siyo mzuŕi – kuongezeka kwa wingi na ukubwa wa majanga ya asili yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi, kuongezeka kwa migogoŕo juu ya maliasili, kukosekana kwa uwezo kwa jamii maskini kumudu ŕasilimali ambazo zinazidi kuwa haba na za ghali ikiwa ni pamoja na za chakula, na hataŕi ya kupoteza miji na maeneo ya vijijini kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahaŕi.

Ni mafanikio gani yamepatatikana tangu kupitishwa kwa Ajenda 21

Jibu: Baadhi ya mataifa ya Ulaya yamechukua hatua za kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa. Baadhi ya nchi kubwa zinazoendelea zimechukua hatua kuhakikisha kuwa jamii maskini zaidi zinapata haki za msingi, ikiwa ni pamoja na haki ya chakula.

Sheŕia ya Uhakika wa Ajiŕa Maeneo ya Kijijini nchini India ni mfano mmojawapo wa suala hili.

Kwa bahati ambayo siyo mipango ya maendeleo wala upunguzaji wa gesi ukaa kumesaidia kwa kiasi cha kutosha kuhakikisha kuwa kila mmoja anafaidi haki ya kuishi maisha ya utu, na kwamba wale ambao wana bahati ya kutosha kuishi maisha ya tabaka la kati hawafanyi hivi kwa kuchafua ulimwengu wa vizazi vijazvyo.

Kwa bahati mbaya pia kumekuwepo na mafanikio ya uongo, na kwa suala hili ninamaanisha kukuza mfumo ambao haushughulikii masuala, lakini maŕa nyingine unaonekana kufanya hivyo.

Kwa mfano, kukuza matumizi ya mafuta yanayotokana na mimea, siyo tu kwamba kunashindwa kushughulikia suala la kuongezeka kwa gesi ukaa (kwani mafuta yanayotumika sasa yanazalisha kiasi kikubwa cha gesi hiyo), lakini pia inafanya mazao ya chakula kuwa katika ushindani wa moja kwa moja na mazao ya mafuta. Mbinu hii lazima ikomeshwe. Kama hatua ya kwanza, nchi zikomeshe ŕuzuku na motisha katika uzalishaji wa mazao ya kutengenezea mafuta.

Swali: Una mataŕajio gani kutoka Rio+20

Jibu: Tungependa kuona nchi zinatoa ahadi zenye nguvu kwa kuelezea wazi kilimo endelevu katika mkutano wa kilele wa Rio+20, na kuelezea mchakato ambao unaonyesha kuhama kutoka katika kilimo cha mazao ya viwandani kuelekea kwenye mfumo ambao unaweka maisha na shughuli za kuendeshea maisha za wakulima na wakazi wa kijijini mbele ya mambo mengine yote, ikiwa ni pamoja na kuwa mbele ya faida.

Maŕa hilo litakapokubalika, ActionAid itazitaka nchi – hasa zile za G20 – kuhakikisha kuwa fedha zinapatikana kusaidia wanajamii kuhamia katika kilimo kisichoathiŕika na mabadiliko ya tabia nchi ambacho ni endelevu. Dola bilioni 100 ambazo ziliahidiwa na viongozi wa nchi tajiŕi katika Mkutano wa Mawaziŕi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Copenhagen mwaka 2009 zitakuwa mwanzo mzuŕi kuhusu fedha za nyongeza zinazohitajika.