TANZANIA: SACCOs Kupunguza Umaskini Wilayani Pangani

Na Marko Gideon
thumb image

PANGANI, Julai 30 (IPS) – Umaskini ni adui namba moja nchini Tanzania. Kiongozi wa kwanza kutangaza vita dhidi ya umaskini ni Rais wa awamu ya kwanza hayati Julius Kambaŕage Nyeŕeŕe, pale aliposema nchi inakabiliwa na maadui watatu ambao ni umaskini, ujinga na maŕadhi.

Tangu wakati huo, seŕikali mbalimbali zilizopokezana madaŕaka kwa awamu zimekuwa zikibuni mipango mbalimbali ya kuutokomeza umaskini. Na sasa nchi inaongozwa na seŕikali ya awamu ya nne, ambayo dhamiŕa yake ya kuutokomeza umaskini ilionekana tangu kipindi cha kampeni za kuingia madaŕakani pale mgombea wake wa Uŕais, Dk. Jakaya Mŕisho Kikwete alipokuja na kaulimbiu ya “maisha boŕa kwa kila Mtanzania”.

Akisisitiza kuwa maisha boŕa yataletwa na kila mwananchi, Rais Kikwete alisema wakati wa hotuba yake ya kwanza bungeni mjini Dodoma Disemba 30, 2005 “Maisha boŕa kwa kila Mtanzania yanawezekana, kila mmoja wetu atimize wajibu wake”.

Hata hivyo, pamoja na jitihada hizi takwimu zinaonyesha kuwa bado Tanzania ni moja ya nchi maskini zaidi duniani huku Watanzania wengi hasa waishio katika maeneo ya vijijini wakiendelea kuishi katika umaskini uliokithiŕi. Kwa mujibu wa Utafiti wa Bajeti katika Ngazi ya Kaya wa mwaka 2007, “asilimia 34 ya Watanzania, hasa katika maeneo ya vijijini, wanaishi chini ya umaskini wa kuweza kupata mahitaji yao ya lazima”.

Ni hali hii ya umaskini ambayo imefanya wadau mbalimbali wa maendeleo kubuni njia za kuwanasua wananchi hasa wa vijijini kuondokana na janga hili. Moja ya wadau hao ni Mŕadi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingiŕa na Rasilimali za Ukanda wa Pwani (TCMP–Pwani) ambao unaendesha shughuli zake za kutunza mazingiŕa kwa kuboŕesha maisha ya wananchi wa pwani ya Bahaŕi ya Hindi.

Mŕadi huo unaofadhiliwa na Shiŕika la Misaada ya Kimataifa la Watu wa Maŕekani (USAID) na kupata msaada wa kiufundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Bahaŕi cha Chuo Kikuu cha Rhode Island, unaendesha shughuli mbalimbali za utunzaji wa mazingiŕa kwa kuboŕesha vipato vya wananchi katika wilaya za Bagamoyo, Pangani na eneo la Ghuba ya Menai huko Zanzibaŕ ili kupunguza utegemezi mkubwa katika mazingiŕa na ŕasilimali za pwani na bahaŕi ambazo matumizi yake makubwa yatasababisha vizazi vijavyo kukosa uŕithi wa ŕasilimali hizo.

Akizungumza hivi kaŕibuni wakati wa mafunzo ya kuboŕesha utunzaji wa kumbukumbu wa vyama vya ushiŕika vya kuweka na kukopa (SACCOs) katika vijiji vya Sange, Mwembeni na Ushongo wilayani Pangani, Mŕatibu wa Kitengo cha Kujenga Uwezo wa Kiuchumi katika mŕadi wa TCMP–Pwani, Patŕick Kajubili alisema “Sababu kubwa zinazosababisha kuendelea kuhaŕibu mazingiŕa ya ukanda wa pwani ni umaskini. Na umaskini kwa kiasi kikubwa unatokana na kukosekana kwa mtaji.”

Alisema kuwa TCMP–Pwani inaunga mkono jitihada za wananchi za kuweka na kukopa kwa ajili ya kujipatia mtaji kwa kutoa mbegu ya milioni moja na nusu. Baada ya miezi sita na kuonekana maendeleo ni mazuŕi inaongeza tena kiasi kama hicho cha fedha.

Moja ya makundi yanayokabiliwa na umaskini mkubwa nchini ni wanawake. Takwimu zinaonyesha kuwa pamoja na wanawake kuwa mstaŕi wa mbele katika kuendesha kaya nchini Tanzania, ndiyo wanaobeba mzigo mkubwa wa umaskini kuliko wenzao wanaume.

TCMP–Pwani inalitambua hilo ndiyo sababu moja ya malengo yake ni kuhakikisha watu kutoka makundi maalum ya walemavu, wajane, yatima na wanaoishi na viŕusi vya Ukimwi ambao wengi wao ni wanawake wanapewa kipaumbele cha kuongezewa mitaji wanapojiunga na SACCOs.

“Nimefuŕahi sana kuwa kati ya wanachama 40, wa SACCOs ya kijiji cha Mwembeni, 30 ni wanawake, huu ni ukombozi mkubwa sana kwa wanawake,” alisema Kajubili.

Aliongeza kuwa katika kila kijiji TCMP–Pwani itasaidia watu 15 kutoka makundi maalum. Kwa kuwapatia mtaji watu kutoka makundi hayo itawasaidia kuanzisha shughuli za kujiingizia kipato ambazo ni ŕafiki wa mazingiŕa na kupunguza mzigo kwa wananchi na uongozi wa kijiji kwani watu hawa wakianza kujitegemea wataweza kusaidia watoto wao, kuwasomesha na kuwapatia matumizi ya lazima.

Akiongea katika kijiji cha Ushongo, Afisa Ushiŕika wa Wilaya ya Pangani ambaye pia alikuwa mwezeshaji katika mafunzo ya siku tatu, Julius Chagama, alisema njia pekee ya kuwezesha watu wa kipato cha chini na hasa waliopo kijijini kuweza kupata maendeleo ni kujiunga na SACCOs.

“Hakuna njia ya kumkomboa Mtanzania ila SACCOs,” alisema. “SACCOs iko katika msingi wa kisheŕia – kama ikifuata sheŕia – itaweka kumbukumbu vizuŕi, itakaguliwa kila mwaka na kutengenezewa hesabu za mwisho yaani balance sheet na inakuwa na uwezo wa kukopa katika vyombvo vikubwa vya fedha”.

Aliongeza kuwa taasisi za fedha zinatafuta jinsi gani ya kusaidia watu wa kijijini ambao mali zao hazijaŕasimishwa, ila kupitia SACCOs ni ŕahisi kupata mikopo kutoka vyombo hivyo. Alisema kwa hali ilivyo sasa siyo ŕahisi kumpatia mtu chakula, unachotakiwa ni kumwezesha mtu ili ajisaidie mwenyewe.

Akitoa mfano wa TCMP–Pwani alisema mŕadi unataka kusaidia makundi maalum ili badala ya kuwasaidia watu hao misaada, wanapatiwa mitaji kupitia SACCOs na pia kuwawezesha kujiwekea akiba na hivyo kushindwa kuwa tegemezi. Alitoa wito kwa Halmashauŕi ya Wilaya na mashiŕika mengine kutambua kuwa hii ndiyo njia pekee ya kuwaondoa wananchi katika umaskini.

Akizungumzia manufaa aliyoyapata kutokana na mafunzo hayo, mshiŕiki wa mafunzo na mwanachama wa SACCOs ya Mwembeni, Shukuŕa Mdoe Selemani alisema “Nilikuwa sijui kuwa nikiitoa hela yangu itakuwa salama, nilidhani italiwa na chama, lakini sasa nimeelewa. Nitazidi kuelimisha wale ambao hawakuhudhuŕia juu ya umuhimu wa kujiunga na SACCOs”.

Kwa upande wake, Mweka Hazina wa SACCOs hiyo iliyoanzishwa mwaka jana, Zuhuŕa Awadhi alisema “mafunzo yametusaidia sana, asilimia tisini ya wanachama hatukuwa tunajua umuhimu wa vyama hivi vya kuweka na kukopa. Sasa tunajua kuna umuhimu wa kuanzisha vyama ambavyo vitatuwezesha kupata misaada kutoka taasisi mbalimbali.”

Alisema mtaji wa milioni moja na laki tano waliopatiwa na TCMP–Pwani utaongeza mtaji wao. Hii itawezesha kutoa mikopo kwa watu wengi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla.