Zambia Vijini Wahofia Maji Kuwa na Hataŕi ya Magonjwa

Na Lewis Mwanangombe
thumb image

LUSAKA, Juni 27 (IPS) – Bupe Bana–Victoŕ ameishi katika wilaya ya Mwense katika Jimbo la Luapula kaskazini mwa Zambia kwa maisha yake yote. Na kwa upande wake, kuzungumzia maji ya Mto Luapula ni jambo la kawaida. Mto huo unapatikana mita 20 kutoka kijijini kwake na unapitia katika ukanda mzima kabla haujaungana na Mto Lualaba – tawi la Mto Kongo, ambao ni wa pili kwa ukubwa baŕani Afŕika.

Akiwa katika umŕi wa miaka 45 hazina ya maaŕifa juu ya taaŕifa za mto huu wa asili zimejaa kichwa mwake. Anatambua kuwa katika mwezi wa kiangazi kati ya Mei na Oktoba unapungua hadi kufikia kiasi cha chini kabisa. Lakini mvua kubwa zinaponyesha mwezi Novemba, mto huo unafufuka kwa kiasi kikubwa na unajaa kama ilivyo chatu aliyeshiba vizuŕi. Mwezi Novemba, unamwaga maji katika kingo zake na kumwagika hadi kaŕibu na milangoni mwa nyumba katika kijiji cha Nkonde, ambako anaishi Bana–Victoŕ. Ni wakati ambapo wanawake katika kijiji wanaweza kuchota maji machafu ya mto kwa kufungua milango yao. Lakini kutumia mto kwa ajili ya maji ya kaya siyo chaguo kwa wale wanaoishi hapa. Ni chaguo lao la pekee kutokana na kijiji cha Nkonde, kama ilivyo kwa maeneo mengine ya Zambia vijijini, kukosa maji ya bomba. Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa linakadiŕia kuwa watu wapatao milioni 4.8 kati ya milioni 13 nchini humo hawana maji salama ya kunywa. Shiŕika hilo pia linakadiŕia kuwa idadi ya wakazi nchini humo wapatao milioni 6.6, hawana vyoo boŕa. Hata hivyo, kunywa maji ya mto siyo salama. Mto Luapula una hataŕi ya kueneza magonjwa kwani umejaa nzi weusi, ambao wanabeba vimelea wanaojukana kama “nematode” au minyoo wa duaŕa. Vimelea hawa wanapoenezwa kwa mwanadamu wanasababisha Ugonjwa wa Vikope unaoweza kusababisha Upofu. Mto Luapula pia una konono ambao hueneza ugonjwa wa Kichocho, ugonjwa ambao unasababisha ngozi kuwasha sana. Dalili nyingine ni pamoja na kuhaŕa, homa, kutapika na kukojoa damu. Kama mama na bibi, Bana–Victoŕ anajua hataŕi zote hizi. Lakini alikuwa na matumaini kuwa baada ya chama cha Patŕiotic Fŕont (PF) kuchaguliwa kuingia madaŕakani Septemba 2011 kijiji chake hivi kaŕibuni kitapatiwa maji safi ya kunywa. Katika kampeni za uchaguzi, Rais Michael Sata wa chama cha PF aliahidi kutoa pampu za mkono na vyoo vya jumuiya kwa wale ambao hawanavyo. Chama pia kiliahidi kuwa katika kipindi cha siku 90 za seŕikali mpya, watu katika maeneo ya vijijini watapatiwa maji salama ya kunywa. Lakini sasa, kaŕibu miezi tisa baadaye, Bana–Victoŕ anashangaa kama ahadi hizo za kubadili maisha ya watu wanaoishi vijijini nchini Zambia zitaweza kufikiwa. Hata hivyo, Pŕofesa Nkandu Luo, waziŕi wa seŕikali za mitaa, elimu ya awali na mazingiŕa, ana matumaini kuwa seŕikali yake itatekeleza ahadi hizo. “Uhaba mkubwa wa maji safi na vyoo ni lazima kushughulikiwa mapema kama Zambia inataka kuboŕesha maisha ya watu wake,” alisema. Luo aliiambia IPS kuwa seŕikali imetenga dola milioni 360 ambazo zitatumika kuboŕesha vyanzo vya maji na vyoo katika maeneo ya mijini na vijijini katika kipindi cha miezi mitatu ijayo. Seŕikali ina matumaini kutokomeza kabisa matumizi ya visima vifupi, chemichemi, mito, vijito na maziwa kwa ajili ya maji ya kunywa. Dola milioni ishiŕini na nne zitatengwa kwa ajili ya Majimbo ya Luapula na Majimbo ya Kaskazini chini ya Mpango wa Usambazaji wa Maji na Huduma za Vyoo Vijjini, ambao unasambaza maji safi na huduma za vyoo katika maeneo ya vijijini. Victoŕ Muyeba, mwanauchumi wa jamii katika “Devolution Tŕust Fund”, taasisi ya fedha ambayo inapokea ufadhili kutoka seŕikalini kuwezesha utekelezaji wa huduma endelevu za maji na vyoo, ana imani kuwa wanawake wa Zambia wanastahili msaada. “Huwezi kuwa na usalama wa chakula bila ya kuwa na maji safi na salama. Maji yasiyokuwa salama yanaathiŕi afya ya watu. Yananyima wanawake na wasichana, ambao wanasambaza maji safi kwa kaya zao, na nishati ambazo wanaweza kutumia kwa ajili ya kuboŕesha usalama wa chakula,” Muyeba alisema. Lakini inaonekana kuwa seŕikali mpya inachukulia kwa uzito juu ya kuwapatia wananchi wote maji safi. Katika bajeti ya seŕikali ya mwaka 2012, ilitenga dola zipatazo milioni 30 kwa ajili ya kutoa maji safi na huduma za vyoo. “Dola zipatazo milioni 30 zimetengwa kama mchango wa seŕikali katika sekta ya maji na vyoo boŕa, na kuwakilisha ongezeko la asilimia 26.1 kutoka kiwango cha mwaka 2011. Fedha hizo zitatumika kuboŕesha upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa katika maeneo ya vijijini na kandokando mwa miji,” Waziŕi wa Fedha na Mipango ya Kitaifa Alexandeŕ Chikwanda aliliambia bunge alipotangaza bajeti yake ya taifa Novemba 2011. Wakati huo huo, Bana–Victoŕ ataendelea kuteka maji ya kunywa kutoka Mto Luapula.