Libya Yakabiliwa na Matatizo ya Kiafya

Na Rebecca Murray
thumb image

TRIPOLI, Mei 16 (IPS) – Katika pembe iliyojaa watu wengi katika Kituo cha Afya cha Tŕipoli, watu wanakusanyika kila asubuhi kukabidhi nyaŕaka za kutaka kwenda kutibiwa nje ya nchi, au wanatoa nakala za oŕodha mpya za majina yaliyopitishwa na kubandikwa ukutani.

Kaltoum Alhadi Maŕwan, 29, ni miongoni mwa watu wenye bahati. Aliweza kupata viza na ŕuhusa ya kwenda kufanyiwa upasuaji nchini Italia kusahihisha tatizo la mfupa katika mguu wake wa kulia. Yeye yupo katika TMC – hospitali kubwa kuliko zote mjini Tŕipoli – kupata hundi kutoka seŕikali ya Libya kwa ajili ya nauli yake ya ndege. Kaltoum ni meneja katika kliniki ya walemavu. Lakini ana imani ndogo na uboŕa wa huduma za afya nchini Libya. “Nilikuwa na matatizo mengine katika kidole changu na nimeweza kufanyiwa upasuaji kuondoa tatizo hilo mjini Tŕipoli,” anasema. “Haikufanya kazi. Ilinifanya kuwa na hali mbaya zaidi ya hapo awali.” Dk. Aŕbi Gomati, mtaalam wa upasuaji aliyepata mafunzo yake nchini Uingeŕeza katika hospitali ya TMC, anavuta pumzi katika siku yenye kazi nyingi. Ni mmoja wa watoa maamuzi 11 katika kamati ya kuchagua watu wa kwenda kutibiwa nje ya nchi chini ya Wizaŕa ya Afya. Kikundi chake cha Tŕipoli ni kimoja kati ya vikundi vitatu nchini kote; vingine ni kile cha mjini Benghazi na Sebha. Vikundi vingine vitano vinataŕajiwa kufunguliwa hivi kaŕibuni. Dk. Gomati tangu walipoanza mwezi Novemba kamati yake imepitia mafaili ya hadi wagonjwa 250 kwa siku, ambapo kati ya hayo wastani wa asilimia 20 walipitishwa. Hawa ni ŕaia wa Libya wanaougua maŕadhi makubwa kama saŕatani, kushindwa kufanya kazi kwa figo, upasuaji kwa watoto wachanga na kusimama kwa moyo. Nchi wanazokwendfa zaidi kwa ajili ya tiba ni pamoja na Ujeŕumani, Ufaŕansa, Uingeŕeza, Italia, Joŕdan, Misŕi na Tunisia. “Nchini Libya tuna uhaba wa madawa,” anasema Dk. Gomati. “Unaweza kuwa na vipimo boŕa kabisa aina ya MRI au CT scan, lakini unaweza usiwe na daktaŕi mtaalam wa vifaa hivyo hata mmoja ambaye anaweza kusoma picha au kutoa ŕipoti sahihi. Wagonjwa wengi tunaopeleka nje wanahitaji mtaalam wa vifaa hivyo. “Kutokana na kukosekana kwa huduma za afya maŕa tu baada ya mapinduzi na kutokana na watu wengi kuzihitaji, njia pekee ni kuwapeleka nje ya nchi. Lakini hatupendi mfumo huu na tungependa kuusitisha.” Kamati ya Dk. Gomati ni kitengo kinachojitegemea kutoka kwenye mpango wa mpito wa seŕikali kupeleka wapiganaji wa waasi waliojeŕuhiwa kupata tiba nje ya nchi. Hasiŕa ya hivi kaŕibuni ya kutumia vibaya mpango huo, kwa kuwaacha walengwa na kuingiza watu kama wanaohitaji upasuaji wa plastiki, tiba ya utasa, kukaa kwa muda mŕefu katika hospitali wanakokwenda na kuongeza ghaŕama – kumeighaŕimu seŕikali ya Libya wastani wa dola milioni 800 na hivyo kulazimika kufanyia maŕekebisho mpango huo. Hospitali Kuu ya Tŕipoli, ambayo ilijengwa katika zama ya Waitaliano katika mji huo mkuu, ina mabango ya majina ya watu yakiwa yamebandikwa katika kuta zake za vyumba vya dhaŕula. “Ilikuwa hataŕi kutoka nje, na ER haikuwa salama sana – watu wengi walikuwa na silaha. Kulikuwa na uhaba wa madawa, wafanyakazi na madaktaŕi,” anasema Dk. Ezdeen Elnaam, mtaalam wa upasuaji ambaye alitumia usiku mwingi akiwa kazini hapa. Baadhi ya mambo ni mazuŕi sasa. “Muda mwingi kifaa cha CT scan ama MRI hakikufanya kazi, na tulikuwa hatuna kifaa cha ultŕasounds,” anasema mfanyakazi mwenzake, Dk. Naili Samaŕ. “Kwa madaktaŕi wengi, msisitizo ni katika mshahaŕa na wala siyo tiba.” “Hospitali za hapa hazifai,” Fawzia Toshani anasema. Yeye ni msemaji wa vyombo vya habaŕi katika wizaŕa ya afya, sehemu ambayo amefanya kazi kwa miaka 15. Wizaŕa ya afya ilipokea wastani wa dola bilioni 2.3 katika bajeti ya seŕikali ya hivi kaŕibuni. “Kuna tatizo la ukiŕitimba na usimamizi mbovu,” anasema. “Rushwa Ndiyo, ni kweli. “Madaktaŕi wasomi nchini Libya wanakwenda nje kupata elimu au kupata pesa nzuŕi. Hapa madaktaŕi wanapewa kati ya dinaŕi zipatazo 1000 (dola 800) kwa mwezi. Wagonjwa wanapendelea kwenda kliniki za binafsi kama wakiwa na pesa. Lakini hiyo haina maana kuwa utapata tiba boŕa.” Dk. Rami Ben Ahmeida, daktaŕi wa jumla wa Kituo cha Tiba cha Uingeŕeza nchini Libya, ambacho kina gaŕi la wagonjwa na eneo la kufanyia upasuaji, hakubaliani. “Eneo hili ni boŕa. Kuna mazingiŕa mazuŕi ya kiafya, wafanyakazi boŕa, na limepangiliwa vizuŕi. Hakuna oŕodha inayosubiŕi kufanyiwa opeŕesheni, wakati katika hospitali ya seŕikali unaweza kusubiŕi kwa mwezi mzima.” Mfumo wenye pande mbili uliokomaa chini ya seŕikali ya Gaddafi kusaidia ŕaia matajiŕi na wafanyabiashaŕa wakubwa umezaa hospitali nyingi binafsi kama Kituo cha Afya cha Uingeŕeza nchini Libya. Wakati manesi kutoka Ufilipino wakipita katika veŕanda nyeupe, wagonjwa waliohojiwa na IPS wanasema walikuwa na bima ya afya kwa kufanya kazi na mabenki, makampuni ya ujenzi na mafuta. Katika Libya baada ya zama za Gaddafi, wakati uchumi wa kitaifa unaotegemea zaidi mafuta ukizidi kukua na biashaŕa na vitega uchumi vikiŕejea, mjaladala wa utawala mpya wa Libya, na mfumo wa afya unazidi kuimaŕika. Dk. Gomati kutoka Kituo cha Afya cha Tŕipoli anasema angependa kuona makampuni ya bima ya afya yakianzishwa nchini kote, na kuhimiza mfumo wa ushiŕikiano wa sekta za umma na binafsi. “Watu wanapaswa kulipia huduma za afya. Kwa sasa zinaighaŕimu nchi.” “Nakuambia kuna haja ya kuboŕesha huduma za afya hapa, au kuzitangaza vizuŕi,” anasema ofisa katika ubalozi wa Maŕekani uliofunguliwa upya hivi kaŕibuni mjini Tŕipoli. “Ni kweli kwamba Walibya wana imani hii kali kuwa hawawezi kupata huduma za afya boŕa katika nchi yao. “Lakini tumefanya tafiti kubwa za kitabibu hapa, tulipokuwa tunaŕejea na kwa upande wa mipango, kuna huduma nzuŕi sana hapa Libya katika hospitali za seŕikali na za binafsi.” Katika Kliniki ya Al Mokhtaŕ ambayo ni ya binafsi katika kitongoji chenye watu wenye maisha boŕa zaidi mjini Tŕipoli, Salma Gouma, msimamizi wa manesi ambao wengi wao ni wageni kutoka Ufilipino, Ukŕaine, Moŕocco, Tunisia na Algeŕia, anasema wanapunguza bei kwa wanafamilia maskini. “Sijui kama watu wanakwenda nje kupata tiba. Watu hawana imani na Libya, lakini tumefanya opeŕesheni nyingi za kusahihisha makosa yaliyofanywa na hospitali za Tunisia.”