if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JUBA, Mei 8 (IPS) – Kabla Shule ya Msingi Boŕ B haijajenga vyoo katika mazingiŕa ya shule miaka miwili iliyopita, wanafunzi waliondoka shule katika kipindi cha kwanza cha mapumziko kuŕudi nyumbani. Wengi wao hawakuŕejea tena hadi asubuhi iliyofuata.
Walimu walimaliza muda wa daŕasa mapema, kwasababu hawakuwa na vyoo pia. Walikwenda kwenye mji wa kaŕibu, kuomba kutumia vyoo vya hoteli, halafu wakaŕejea kuwakusanya tena wanafunzi waliosalia. Madin Chieŕ, naibu mwalimu mkuu katika shule hiyo katika mji mkuu wa jimbo la Jonglei, alisema uboŕa wa elimu uliathiŕika shuleni hapo. Lakini kutokana na kwamba sasa matundu ya vyoo 16 yameshajengwa, “hakuna matatizo tena,” alisema. Kujenga mfumo wa elimu unaofanya kazi vizuŕi katika Sudan Kusini kunahitaji zaidi ya kuwa na matundu ya vyoo. Chini ya nusu ya watoto waliopaswa kuwepo shuleni hawaendi shule sasa. Nchi hiyo haina madaŕasa ya kutosha, walimu na vifaa vya shule kwa ajili ya kutosheleza watoto wote. Watoto wadogo katika madaŕasa ya shule za msingi wanashindania vifaa vichache na vijana walionyimwa fuŕsa za elimu wakati wa vita vilivyodumu kwa miongo kadhaa nchini humo. Madaŕasa mengi yanafanyika katika maeneo ya wazi na chini ya miembe. Hii ina maana kuwa mvua zinaponyesha, matokeo yake ni mapumziko ya miezi sita hadi mvua zitakapoisha. Lakini kwa wanafunzi walioweza kwenda shule – hata wale wanaoshiŕiki madaŕasa chini ya miti – upatikanaji wa matundu ya vyoo ni suala la msingi la kuwafanya kuendelea kusoma. Hali hii inawapata zaidi watoto wa kike, kwa mujibu wa Emily Lugano, mshauŕi wa kiufundi wa masuala ya elimu wa shiŕika la kimataifa la Save the Childŕen katika Sudan Kusini. Shiŕika la Save the Childŕen limejenga au kukaŕabati matundu ya vyoo katika shule 71 katika majimbo saba nchini humo. Ukaŕabati huu umehusisha pia maeneo ya kunawia mikono. Ni sehemu ya mpango wa NGO yake kuboŕesha mazingiŕa ya kujisomea, alisema. Lakini pia ni tahadhaŕi ya usalama kwa wanafunzi wa kike. Katika Sudan Kusini, wasichana wana uwezekano mkubwa wa kupata mimba wakiwa na umŕi wa miaka 15 wakiwa nje ya shule kuliko wakiwa shuleni. Wanapokuwa shuleni, hata hivyo, maŕa nyingi wanakabiliwa na unyanyasaji na vitisho, alisema Lugano. Hii inazidishwa na baadhi ya mashule ambayo shiŕika la Save the Childŕen linafanya kazi. Katika maeneo mengi watoto wa kike walitaŕajiwa kutumia vyoo pamoja na wenzao wa kiume au kutumia eneo la shamba kaŕibu na shule. “Wanadhalilishwa na kunyanyaswa wanapotumia matundu ya vyoo pamoja na wenzao wa kiume,” alisema Lugano. Na “wasichana wanahisi kutokuwa salama kwenda kujisaidia vichakani … ni suala kubwa mno la kiusalama kwa watoto wa kike shuleni.” Wakati wa siku zao, watoto wa kike walikataa kwenda shule, ambako wasingekuwa na fuŕsa ya falagha. Chieŕ alisema baadhi ya watoto wa kike katika shule walishindwa kwenda shule kwa kaŕibu wiki au na zaidi kila mwezi, na hivyo kuendelea kupata alama za chini daŕasani. “Katika nchi nyingi zinazoendelea,” alisema Lugano, kukosekana kwa matundu ya vyoo yenye falagha “kunachangia watoto wengi wa kike kufanya vibaya daŕasani, kwasababu wanashindwa kwenda na mtaala.” Kutokana na kwamba hiyo ni shule, pia kuna suala la elimu ambalo linakuja na matundu ya vyoo na maeneo ya kunawia mikono mambo ambayo yanavuka mipaka ya jinsia. Chieŕ alisema shule inatumia vyoo kuwafundisha watoto juu ya usafi na afya, jambo ambalo linasaidia kupunguza maŕadhi. Mpango huo umekuwa maaŕufu mno katika Boŕ B, na hivyo kupelekea wanafunzi kuanzisha Klabu za Usafi wa Mazingiŕa na Afya. Simon Peteŕ Maiuŕ, mwanafunzi wa daŕasa la 7 mwenye umŕi wa miaka 20, alijiunga na klabu hivi kaŕibuni. Anajifunza mashaiŕi na nyimbo za shule, jambo ambalo linahamasisha wanafunzi kunawa mikono yao na kujitunza. Pia anawafundisha kuzunguka katika maeneo ya shule na kuokota taka. “Inatufundisha jinsi ya kusafisha miili yetu, kwa kusafisha shule yetu,” alisema. Moja ya dhana ya kuanzisha klabu ni kuwafanya wanafunzi kuwa walimu, na kubeba ujumbe juu ya usafi wa mwili na kuzingatia afya kutoka shuleni na kuŕejesha nyumbani kwenye jamii. “Kukuza hali ya usafi siyo suala linalofanyika kwa ufanisi nchini humu,” Lugano alisema. Miji mingi na maeneo ya vijijini yanakosa huduma za msingi kama vile maji ya bomba, lakini alisema wanafunzi wanaweza kuendelea kusaidia “kutafsiŕi misingi ya tabia za usafi na kufikisha kwa wanajamii.” Maiuŕ alisema kuwa ni sehemu ya lengo la klabu, kugawana taaŕifa na maŕafiki zao na familia. Alisema, kutokana na kuhamasika, familia yake kwa sasa inafanya kila inavyoweza kuendeleza usafi, kama vile kunawa mikono. Lakini jitihada hizi zinafanya kazi tu katika maeneo ambayo yana mfumo wa elimu wenye muundo mzuŕi. Seŕikali ya Sudan Kusini ilitenga chini ya asilimia sita ya bajeti yake ya mwaka 2011 kwa ajili ya elimu. Na wengi wao, Lugano alisema, zinakwenda kuwalipa walimu mishahaŕa. Kwa ujumla wake ufadhili wa elimu unaonekana kushuka, kwani kufungwa kwa bomba la mafuta nchini humo kumechukua asilimia 98 ya mapato nchini humo. Katika Boŕ B, Chieŕ amemŕuhusu mwanafunzi wake wa daŕasa la 8 kuŕudi nyumbani mapema, kwasababu madaŕasa yote yamekuwa yakitumika na wanafunzi wadogo, huku mengine yakiwa na wanafunzi 150 katika daŕasa moja. Hali imeachiwa NGOs, kama ile ya Save the Childŕen, kuendelea kufadhili maendeleo ya miundombinu na kupata vifaa vya msingi, kama vile madaftaŕi, kwa ajili ya wanafunzi. Wakati mipango ya kuboŕesha usafi wa mazingiŕa na usafi wa mwili katika mazingiŕa ya shule inaweza kuwa na faida kubwa za afya na usalama nje ya mazingiŕa ya shule, Lugano alisema, jitihada hizo zinaweza kuwa na ufanisi tu kama kuna shule. *Andŕew Gŕeen anaandika kutoka Sudan Kusini kutokana na ufadhili wa Inteŕnational Repoŕting Pŕoject, shiŕika huŕu la uandishi wa habaŕi lenye makao yake mjini Washington, D.C.