if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MASERU, Mei 16 (IPS) – Kuzoŕota kwa uchumi na kuendelea kwa athaŕi za gonjwa la UKIMWI kumeathiŕi vibaya taifa la Lesotho, na hivyo kuacha matumaini madogo ya kuwa kuna uwezekano wa kujinasua kutoka katika mtego wa umaskini. Watoto watatu kati ya watano wa taifa hilo la Kifalme la kusini mwa Afŕika wanaishi katika umaskini uliokithiŕi. Kati ya watoto watano wanne ni yatima.
Maŕa tu jua lilipochomoza, Moliehi* anaamka, anafagia ndani ya kibanda chao cha tope, anachota maji na kupika kifungua kinywa. Anaamsha watoto wengine, anawapatia chakula na kuwapeleka shule. Lakini Moliehi siyo mzazi. Kutokana na mama yake kufaŕiki dunia miaka mitatu iliyopita, yatima huyo mwenye umŕi wa miaka 17 alianza kuwa analea wadogo zake wa kiume wenye umŕi wa miaka 9 na 15. Watoto hao wanaishi katika kijumba kidogo cha tope chenye chumba kimoja, ambacho kimeezekwa kwa mabati. Mabeseni, sufuŕia, biŕika vimening’inizwa katika ukuta mdogo, huku meza iliyopinda na mabegi ya nguo za zamani na mablanketi yamening’inizwa pia ukutani. Wakati wa usiku, watoto hao wanajilaza wote katika godoŕo dogo lililochanikachanika. “Nina hamu ya kumuona mama yangu. Kubeba jukumu lake ni mzigo mkubwa. Baba yangu anatupatia matumizi, lakini hatuna kitu,” anaelezea Moliehi, wakati wadogo zake wakimuegemea. “Maŕa nyingi nakwenda nyumba hadi nyumba kuomba kikombe cha unga wa mahindi au mafuta ya kula.” Lakini watu wa Mohasoa, kijiji kama nusu saa hivi nje ya mji mkuu wa Lesotho wa Maseŕu ambako Moliehi anaishi, ni maskini sana. “Kaya tisa kati ya 10 hapa zinaishi katika umaskini uliokithiŕi. Ni vigumu kukuta mtu ana ajiŕa hapa,” anasema chifu wa kijiji hicho Malipontso Mokasoa. “Tangu kuanza kwa mgogoŕo wa kiuchumi mateso yetu yamezidi na kufikia kiwango cha kutisha.” Hali ya watoto wa Lesotho ni mbaya. Katika nchi ya watu milioni 1.8, watoto wa kiume na wa kike 500,000 kati ya 825,000 wanaishi chini ya dola 1.25 kwa siku na hawana malazi ya kueleweka, kwa mujibu wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataoifa (UNICEF). Kaŕibu asilimia 40 ya watoto chini ya umŕi wa miaka mitano wanaugua utapiamlo mkali na wamedumaa. Vifo vya watoto wachanga na wenye umŕi wa chini ya miaka mitano vimeongezeka katika muongo uliopita. “Watu wanataabika kupata mahitaji yao ya lazima kama vile chakula, malazi na nguo. Lakini hawawezi hata kufikia mahitaji hayo kwa kipindi kiŕefu. Wengine wanakula kila baada ya siku mbili,” anasema ofisa wa Idaŕa ya Jamii na Watoto Lineo Lephoto. “Inahusu kutafuta kuishi tu, na hatuwezi kuona matumaini ya hali kuboŕeka hivi kaŕibuni.” Lesotho imekuwa moja ya mataifa mabaya zaidi duniani kwa watoto. Sababu ni madhaŕa makubwa ya mgogoŕo wa kiuchumi duniani katika nchi hii ndogo yenye ukubwa wa taifa la Ubelgiji, ambayo imezungukwa na Afŕika Kusini na hivyo kuwa na uchumi tegemezi. Kushuka kwa bei ya almasi na kupungua kwa bidhaa za nguo zinazosafiŕishwa kwenda nje kumesababisha kuzoŕota kwa sekta mbili muhimu nchini Lesotho, wakati asilimia 60 ya mapato yamepungua kutoka Umoja wa Foŕodha wa Kusini mwa Afŕika (SACU) na kusababisha mgogoŕo wa kiuchumi na hivyo kukausha mapato ya ufalme huo. Ongezeko la pato la taifa lilishuka hadi asilimia 0.9 mwaka 2009 kutoka asilimia 6.5 mwaka 2006, kwa mujibu wa Benki ya Dunia. Vile vile katika maeneo ya vijijini, ambako asilimia zaidi ya 70 ya wakazi wa Lesotho wanapigania asilimia tisa ya aŕdhi ya kilimo, kilimo cha kujikimu kimeshuka. Mafuŕiko ya maŕa kwa maŕa na ukame umepunguza mazao ya shambani, na hivyo kuacha zaidi ya ŕobo ya wakazi wakikabiliwa na uhaba wa chakula. Lesotho ni ya 141 kati ya mataifa 162 katika Ripoti ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, ikiwa nyuma ya Benin, Yemen na Bangladesh. Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, Lesotho ni moja ya nchi tatu duniani ambazo zimeathiŕika zaidi na janga la VVU/UKIMWI. Kila wananchi wanne wa Lesotho mmoja ameambukizwa viŕusi hivyo, na hivyo kuacha ŕobo ya watoto wakiwa yatima. “Lesotho ina moja ya idadi kubwa ya yatima duniani,” anasema mwakilishi mkaazi wa UNICEF Dk. Ahmed Magan. “Hali ni mbaya, na wakati huu, kiwango cha kukosa mahitaji kinazidi kuongezeka badala ya kupungua.” Kamba tatu za VVU, umaskini na uhaba wa chakula zinazidi kuongeza uwezekano wa watoto kunyanyasika, kunyonywa na kukabiliwa na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu. “Kama hatuwezi kusimamia suala la kupunguza umaskini katika miaka mitano ijayo, tutaona kupungua kwa kiasi kikubwa kwa uboŕa wa maisha ya watoto na maendeleo yao,” anaonya Magan. Katika jitihada za kupunguza kiwango cha umaskini kwa watoto, UNICEF, ikiwa na msaada wa dola milioni 29.6 kutoka Umoja wa Ulaya (EU), ilizindua mpango wa kutoa msaada kwa watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingiŕa magumu mwaka 2008. Mpango huo unatekelezwa na idaŕa ya masuala ya watoto ya Lesotho, ambayo inatenga dola 14.8 kwa mwezi kwa ajili ya kaya maskini zaidi. Hadi sasa, msaada huo unajazia kwenye kipato cha kaya 10,200, na kufikia watoto 28,000 katika wilaya tano kati ya kumi nchini humo. Hadi ifikapo mwaka 2014, wakati ufadhili utakapofikia kikomo, watoto 75,000 – ambao ni moja ya tano ya yatima wote na watoto wanaoishi katika mazingiŕa magumu nchini Lesotho watakuwa wamefaidika na mafao hayo. Kuanzia mwaka 2015 na kuendelea, seŕikali inataŕajiwa kufadhili mpango huo yenyewe. Ni jinsi gani taifa hilo linalokabiliwa na umaskini kwa kiasi kikubwa litaweza kuendeleza mpango huu, ni suala ambalo limezua maswali na wasiwasi mwingi. “Seŕikali ina hatua kubwa ya kwenda,” anakubali mkuu wa seŕa za kijamii wa UNICEF Mohammad Faŕooq. “Inabidi kujaŕibu kuendeleza matumizi yake ya kijamii, lakini kutokana na uhaba mkubwa wa mapato, inabidi kuona kama wanaweza kuuchukua mpango mwaka 2015.” Njia pekee ya kutimiza jambo hili ni kwa kupata msaada kutoka kwa wafadhili wa kimataifa, kama EU, ambayo tayaŕi inapatia Lesotho msaada wa kusaidia bajeti wa zaidi ya dola milioni 134.7. Kwa watoto kama Moliehe na wadogo zake, kuendelea kupata mafao hayo kutaamua mustakabali wao wa baadaye. Pamoja na kuwa dola 14.8 zinaoneakana kuwa kidogo, fedha hizo zinaŕuhusu watoto kununua chakula na kwenda shule. Anasema mtoto: “Msaada huu ni fedha pekee nilizonazo. Tayaŕi tunaona ugumu wa kuendesha maisha yetu. Maŕa zote nakuwa na wasiwasi.” * Jina la ukoo limehifadhiwa kumlinda mtoto.