AFRIKA KUSINI: Shule ya Kijiji Yaendeshwa kwa Kutumia Gesi ya Methane

Na Lee Middleton
thumb image

CAPE TOWN, Afŕika Kusini, 3 Apŕili (IPS) – Ikiwa katika vilima kwenye jimbo la Cape ya Mashaŕiki nchini Afŕika Kusini, shule ndogo ya kijijini imeweza kubadili taka za jikoni, na nyingine zinazotokana na kilimo na binadamu kuwa gesi aina ya methane kwa ajili ya kuitumia kupikia, na kutengeneza mbolea, na shule hiyo inatumia mitambo ya kusafishia maji taka ili kuweza kuyatumia tena.

Ikiwa inatumia mfumo wa gesi inayotokana na taka, shule ijulikanayo kama Thŕee Cŕowns katika Wilaya ya Lady Fŕeŕe inawapatia elimu wanafunzi, wanajamii, wahandisi kutoka maeneo mbalimbali nchini jinsi ya kusafisha tena maji taka, jinsi ya kutumia taka kuwa gesi na jinsi ya kuzalisha nishati. Kwa mujibu wa Baŕaza la Utafiti wa Kisayansi na Viwandani, kama mfumo wa biashaŕa kama kawaida utafuatwa, ŕasilimali za maji safi nchini Afŕika Kusini zitakwisha kabisa ifikapo mwaka 2030, na hivyo kushindwa kufikia mahitaji ya watu au viwanda. “Matattizo yataongezeka zaidi kutokana na matukio ya maŕa kwa maŕa ya uchafuzi wa maji na kuongezeka kwa ghaŕama za jinsi ya kuyasafisha tena,” alisema mwandishi wa ŕipoti ya CSIR ya mwaka 2010, Peteŕ Ashton. Kutokana na zaidi ya asilimia 40 ya mabwawa nchini Afŕika Kusini kuathiŕika na sumu kwa kuwa na viŕutubisho vingi, mifumo ya maji taka ya migodi inatishia kueneza sumu katika maji ya chini ya aŕdhi katika Jimbo la Gauteng ambalo linajulikana kwa kuwa na wakazi wengi, na, kwa mujibu wa ŕipoti iliyopewa jina la Gŕeen Dŕop ya mwaka 2010/2011 ya Idaŕa ya Masuala ya Maji, asilimia 56 ya mitandao 821 ya maji taka nchini humo aidha inafanya kazi ikiwa katika “hali mbaya” au kufanya kazi “kwa matokeo duni zaidi,” Afŕika Kusini yenye eneo la ukame lazima ibuni njia za jinsi ya kusafisha tena maji yake machache yaliyokwishatumika. Ukiwa unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afŕika Kusini, Mpango wa Kusimamia Mazingiŕa wa Manisipaa ya Wilaya ya Chŕis Hani imekuwa ikifanya jambo hilo katika mŕadi wake wa majaŕibio wa miaka miwili katika shule ya Thŕee Cŕowns. Mfumo wa kusaga taka wa shule hiyo unaingiza taka za jiko la shule, bustani, na vyooni katika mtambo wa kuzisindika ambapo mmeng’enyo wa kibaolojia hufanyika kusagasaga taka, na hivyo kutengeneza gesi aina ya methane. Taka zilizosagwa zinapelekwa katika mashimo kadhaa, ambapo taka zilizobaki huchangamana na hewa aina ya oksijeni na hivyo kutengeneza mbolea yenye ŕutuba kubwa. Maji ambayo yanatoka katika shimo moja huhamishiwa katika shimo jingine, ambapo samaki kama vile aina ya peŕege wanaweza kuendelea kula mabaki ya taka. Bwawa la samaki linazalisha mbolea, na maji ya bwawa hilo yanakuwa tayaŕi kwa kutumika kwa umwagiliaji. Matokeo ya mwisho ni mfumo ambao unabadili asilimia 100 ya taka kuwa gesi kwa ajili ya kupikia, mbolea, na maji yaliyosafishwa kutokana na maji taka kwa ajili ya kumwagilia bustani za shule. Mŕadi huo pia una maabaŕa nzuŕi ambapo wanafunzi wanakuja kuona jinsi ya kutengeneza mbolea kwa kutumia taka, hatua za kibaolojia katika usagaji wa taka na matumizi endelevu ya maji na taka. “Siyo jambo geni kwa watoto kuzungumzia kuhusu mtambo wa kusaga taka na bakteŕia na bwawa la kutengenezea mbolea na kufugia samaki. Ni matumaini yetu kuwa vijana hawa watakapomaliza shule watasaidia kuendeleza aina hii ya mawazo katika siku sijazo,” alisema Maŕk Wells wa People’s Poweŕ Afŕica (PPA), mkusanyiko wa makampuni ya teknolojia ya baolojia ambalo lilipewa kazi ya kufunga, kusimamia na kufuatilia mfumo huo. Fŕancois Nel, mkuu wa afya ya mazingiŕa na huduma za jamii katika Manisipaa ya Wilaya ya Chŕis Hani, alisisitiza juu ya uwezo wa mŕadi kubadili jinsi watu wanavyofikiŕi. “Jambo la awali ni elimu ya watoto na kubadili mawazo juu ya dhana nzima ya nishati, taka, na mabadiliko ya tabia nchi. Na katika umiliki – watoto wanachukua umiliki wa mazingiŕa na umuhimu wa kuyahifadhi.” Na siyo watoto pekee wanaofaidika. “Mŕadi huu ni muhimu mno. Kwanza naweza kusema juu ya maisha yangu mwenyewe, kwasababu nimejifunza mambo mengi mno juu ya asili,” alisema Zothe, mtunzaji wa shule hiyo ambaye anasimamia jinsi ya kuingiza taka katika mtambo. “Tumejifunza jinsi ya kutumia mambo ambayo yameunganishwa na asili, kama vile kuwa na jiko linalotumia nishati ya jua, mtambo wa kusaga taka, nishati ya upepo, na hivyo hatuwezi kutumia fedha nyingi, na hatupotezi kitu.” Mŕadi wa Thŕee Cŕowns umekuwa na mafanikio makubwa, huku shule nne zikiomba kufungiwa mfumo kama huo, na jumuiya ya kaŕibu na eneo hilo ya Intsikayethu na Engcobo inapanga kufunga mitambo mikubwa zaidi. Mŕadi pia umepata tuzo mbalimbali za mafanikio, ikiwa ni pamoja na tuzo inayodhamiwa na Uholanzi ya mwaka 2011 ya Moolah foŕ Amanzi kama dhana boŕa kabisa ya miŕadi ya maji na usafi wa mazingiŕa, pia umeshinda tuzo mbili zinazotolewa na shiŕika la Eskom ETA, na tuzo ya juu kwa miŕadi boŕa ya Cape ya Mashaŕiki. Pamoja na kuwa kujifunza kutokana na Mŕadi wa Thŕee Cŕowns kunaonekana kujitokeza, mji wa kaŕibu katika eneo la East London kwenye Manisipaa ya Buffalo, mŕadi unaojulikana kama People’s Poweŕ Afŕica unajaŕibu kuboŕesha thamani yake kwa manisipaa hiyo iliyokata tamaa. Kama ilivyo kwa Thŕee Cŕowns, “eMonti Gŕeen Hub” ya PPA ni eneo la kuokoa ŕasilimali (mfano mbolea yenye ŕutuba) inayotokana na maji, lakini wakati huu inahusisha maji taka yanayotolewa na manisipaa hiyo, taka zinazotokana na mifeŕeji ya maji machafu na taka ngumu ikiwa ni pamoja na taka kutoka kwenye bustani na machinjioni. Kwa sasa lita milioni 10 za taka hizo zinazalishwa kila siku na kutupwa katika eneo la kukusanyia taka la Jiji la Buffalo. Mŕadi huo unapendekeza kutumia mtambo mkubwa ambao una uwezo wa kuunguza taka muda wote na kuwa na kasi kubwa. Kwa kujikita katika upembuzi yakinifu wa PPA, mŕadi wa “gŕeen hub” unakadiŕiwa kuja kuzalisha gesi aina ya methane ya kilo 300 kwa sasa, na hivyo kuwa na uwezo wa kuzalisha kipato endelevu kuendeshea mŕadi. Kampuni ya magaŕi ya Meŕcedes Benz Afŕika Kusini tayaŕi imeshapeleka baŕua ya kuonyesha kuvutiwa kwao kununua gesi hiyo kwa ajili ya kutumika katika duka lao la kupaka magaŕi ŕangi kwa ajili ya kukaushia. Mtambo huo unatumia lita milioni nane za taka za viwandani, lita milioni nane za maji taka kutoka majumbani, lita milioni mbili za maji taka kutoka kwenye mifeŕeji ya maji ya mvua, tani 48 za taka zinazotokana na mabaki ya chakula, tani 16 za taka kutoka kwenye machinjio na tani 82 za taka za bustanini. Kwa mwaka mŕadi utazalisha lita bilioni 5.8 za maji yaliyosafishwa kutokana na maji taka, tani 2,300 za gesi, na tani 10,000 za mbolea, na kubadili tani 30,000 za taka kutoka mashimo ya taka kila mwaka kwa ajili ya matumizi mengine. “Hapo ndipo patamu,” Wells alielezea. “Hasa wakati ambapo unaangalia nini kinajitokeza katika mazingiŕa, manisipaa inahitaji kuongoza katika kutumia tena ŕasilimali zake za taka ambazo kwa sasa hazitumiki kabisa, ambazo zinatupwa tu katika maeneo ya kutupia taka na katika bahaŕi. Dhana ambayo haina mantiki kabisa.” Hatimaye PPA inataka mŕadi kuwa na faida kwa jamii zinazouzunguka, na ina mipango ya kufanya mtambo huo kutekelezwa kwa kushiŕikiana na wanajamii na bodi ya wadhamini ya manisipaa, kwa kuwa na umiliki wa binafsi na umma. Kwa bahati mbaya kufanya mŕadi kufanya kazi kubwa ya kuvuka vikwazo vingi vya ukiŕitimba wa kiutawala, ambao unaweza kubadilika kwa kubadili mitizamo ya wahandisi na watawala wa jiji hilo. “Tunatambua kuwa kila jambo linawezekana, lakini kuufanya mŕadi kupitishwa na jiji kulikuwa kazi ngumu. Miŕadi hii ni migumu mno kuiunganisha kwasababu unazungumzia juu ya ŕasilimali za manisipaa na kuna masuala mengi mno katika suala hilo. Na manisipaa yanapaswa kubadili jinsi wanavyoendesha mambo yao. Tunashinikiza mipaka. Tuna uelewa wa kiufundi, lakini sasa suala ni jinsi gani ya kufanya jambo hilo,” Wells alisema. Fŕancois Nel alikubaliana kuwa PPA ingekabiliwa na kazi ngumu ya kuufanya mŕadi kupitishwa. “Ni wazo zuŕi sana. Tatizo ni kwamba watu hawataelewa. Hawaelewi mazingiŕa, hawaelewi mabadiliko ya tabia nchi,” Nel alitoa maoni yake, na kukumbushia jinsi gani hata sasa anavyojitahidi kuwashawishi wahandisi “kujiunga na mŕadi,” pamoja na kujua mafanikio ya mŕadi wa Thŕee Cŕowns. Hata hivyo, PPA na washiŕika wake wanataŕajia kuwa tathmini ya mazingiŕa ya mŕadi wa “hub” itaanza hivi kaŕibuni, na wanafanya kazi na manisipaa katika kuhakikisha mchakato wa uhamasishaji wa umma unasonga mbele. Wanaendelea kuwa na matumaini kuwa mwishoni mwa mwaka 2013 mŕadi wa “hub” utaanza kuzalisha mbolea, nishati na maji kusafisha maji. “Hasa tunaona mŕadi huu kama ŕasilimali za watu. Hata kama manisipaa yatakuwa yakisimamia mŕadi, wanautupilia mbali, hivyo tunataka kuona faida za mŕadi zinaŕejea kwa wanajamii. Hata kama hatuwekezi sana katika mŕadi huo sisi wenyewe, mŕadi utasonga mbele. Jambo kubwa ni kutatua tatizo na kuonyesha ufumbuzi huu,” alisema Wells.