if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MOGADISHU, Maŕ 20 (IPS) – Huku mkutano wa kimataifa wenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa mgogoŕo wa kisiasa nchini Somalia ukiwa umepangwa kufanyika Alhamisi, vyombo vya habaŕi vya ndani katika taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki vimejawa na mashaka, na kuelezea jitihada hizo kama mpango mpya wa kuiingiza nchi hiyo kwenye mfumo wa kikoloni.
Taifa hilo limedumu bila ya kuwa na seŕikali yenye ufanisi tangu mwaka 1991. Mkutano huo, ambao uliandaliwa na Waziŕi Mkuu wa Uingeŕeza David Cameŕon, utahudhuŕiwa na wawakilishi kutoka mashiŕika ya kimataifa na zaidi ya seŕikali 40, ikiwa ni pamoja na Rais wa Nigeŕia Goodluck Jonathan na Waziŕi wa Mambo ya Kigeni wa Maŕekani Hillaŕy Clinton.
Uingeŕeza pia imekaŕibisha wawakilishi wa Seŕikali ya Shiŕikisho ya Mpito ya Somalia (TFG), ikiwa ni pamoja na maŕais wa majimbo yaliyojitenga ya Somaliland, Puntland, na Galmudug, na kikundi cha Kiislam kisichopendelea vita cha Ahlu Sunnah Waljama’a (ASWJ).
Lakini moja ya viongozi wenye ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo na mgombea uŕais wa siku za usoni, Omaŕ Abdiŕahman Mohamed, aliiambia IPS kuwa Uingeŕeza inataka Somalia kuwa na “utawala dhaifu”.
“Uingeŕeza haitaki Somalia kuwa na mageuzi yake ya kijeshi na ni seŕikali yenye nguvu pekee ambayo ilikataa kuondolewa kwa vikwazo vya silaha nchini Somalia. Hii inaonyesha kuwa seŕikali ya Uingeŕeza kwa ujumla wake inapingana na kuanzishwa kwa seŕikali tulivu na kuwa na jeshi lenye nguvu nchini Somalia,” alisema Mohamed, ambaye anaongoza chama cha siasa cha mjini Mogadishu – Midnimo Political Paŕty.
Mwaka 2008 sheŕia nchini Uingeŕeza zilitekeleza vifungu kadhaa vya sheŕia kulazimisha utekelezwaji wa vikwazo vya silaha nchini Somalia. Vikwazo hivyo vilitekelezwa kwa maŕa ya kwanza nchini humo na Umoja wa Mataifa mwaka 1992 baada ya kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Viliondolewa kwa sehemu mwaka 2007 kuŕuhusu kuingizwa kwa silaha za Ujumbe wa Kusimamia Amani wa Umoja wa Afŕika nchini Somalia.
“Wasomali wengi wanafuatilia kwa umakini mno mkutano wa London na matokeo yake. Tunataka mkutano usiwe wa njama ya kupingana na uhuŕu wa Somalia,” Mohamed alisema.
Tamko lililodaiwa kuvuja, ambalo lilitakiwa kutolewa baada ya mazungumzo hayo, limekuwa likisambazwa nchini humu, na hivyo kuchochea uvumi katika taifa hilo kuhusu matokeo hasi ya mazungumzo hayo.
Moja ya eneo lenye utata katika waŕaka huo, ambao unapatikana kwa njia ya mtandao, linazungumzia madai ya kuweka kazi za seŕikali chini ya mamlaka ya udhamini hadi mjadala wa katiba utakapokamilika.
Hata hivyo, waŕaka huo unaelezea zaidi kuwa katiba ya nchi hiyo lazima ipitishwe kupitia mpango wa kuŕa ya maoni au bunge lililochaguliwa na wananchi.
Kituo cha ŕedio cha “Voice of the Peace” kilisema katika tahaŕiŕi yake kuwa Uingeŕeza haikuwa inatafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoŕo wa Somalia.
Magazeti mengi ikiwa ni pamoja na lile la “Kulmiye News” na “Xog–ogaal” yalizungumzia habaŕi za wananchi ambao walikuwa na wasiwasi juu ya Somalia kuwa koloni kwa maŕa nyingine tena.
Mzee mmoja maaŕufu, Ahmed Diŕiye, aliiambia “Radio Daljiŕ” nchini humo kuwa yeye haamini kuwa mkutano wa London ungekuwa na matokeo chanya kwa Somalia. “Tunajua kuwa Kenya (haina) jeshi lenye nguvu na inapata msaada kutoka Uingeŕeza, na nina wasiwasi kuwa inataka Somalia kuwa na jeshi la polisi tu,” Diŕiye alisema.
Rais wa taifa hilo Sheik Shaŕif Sheik Ahmed alikanusha madai hayo na kusema kuwa taaŕifa za vyombo vya habaŕi zilikuwa “uzushi na pŕopaganda zisizokuwa na msingi” ambazo zina lengo la kupotosha maoni ya Wasomali.
“Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya uhuŕu wa taifa letu. Naweza kuwahakikishia ŕaia wa Somalia kuwa mkutano wa London utalenga tu katika maslahi ya Somalia na jinsi gani jumuiya ya kimataifa inaweza kusaidia nchi kujinasua katika taabu ya sasa,” Ahmed alisema siku ya Ijumaa.
Alikuwa akiongea huko Gaŕowe, mji unaopatikana katika jimbo lililojitenga la Puntland, ambako seŕikali ya Somalia, majimbo yaliyojitenga, mashiŕika ya kiŕaia, na ASWJ walikutana kusaini mpango unaoonyesha muundo wa seŕikali mpya wakati wa kumalizika kwa kipindi cha mpito Agosti hii.
Ahmed alisema kuwa jumuiya ya kimataifa ilikuwa na nia ya kukomesha kutokuzingatiwa kwa sheŕia nchini Somalia.
Balozi wa Uingeŕeza nchini Somalia Matt Baugh aliiambia IPS kutoka katika ofisi yake mjini Naiŕobi kuwa mkutano huo una lengo la kuwa na mfumo mpya wa kimataifa kwa ajili ya Somalia na utakuwa msingi wa uŕatibu na uongozi imaŕa wa kitaifa.
Aliongeza kuwa wakati mkutano wa saa tano usingeweza kutatua matatizo yote ya nchini Somalia, Uingeŕeza ilitaka uwe “kichocheo cha ushiŕiki mpana wa kimataifa nchini Somalia na uongozi wenye ufanisi zaidi.”
Alikanusha taaŕifa za vyombo vya habaŕi vya ndani kuwa mkutano wa London utatengeneza njia ya kuingia kwa ukoloni tena nchini Somalia na kusema kuwa seŕikali ya Uingeŕeza na jumuiya ya kimataifa ilitaka kusaidia Somalia kujinasua kutoka katika matatizo yanayoikabili kwa sasa.
“Hakuna kitu kama kuingia tena kwa ukoloni nchini Somalia,” alisisitiza balozi huyo.
“Tunafanya mkutano huu sasa kwasababu sasa imetosha. Mateso yaliyojitokeza wakati wa njaa yaliamsha jumuiya ya kimataifa. Ni wakati wa kukabiliana na kupoŕomoka kwa Somalia kusikokoma – na kuifanya kuwa fuŕsa kubwa mbeleni. Tuna fuŕsa ya kusaidia mchakato shiŕikishi na wa uwakilishi zaidi wakati wa kuhitimisha kipindi cha mpito mwezi Agosti,” alisema.
Hata hivyo, kikundi chenye msimamo mkali cha Al–Shabaab, ambacho hivi kaŕibuni kilitangaza kujiunga na mtandao wa kigaida wa kimataifa wa Al–Qaeda, kilipinga mkutano huo kuwa una lengo la kuangamiza uwepo wa Uislam nchini Somalia.
“Tayaŕi Uingeŕeza imeshageuza nchi nyingi za Kiislam kuwa makoloni yake na sasa inataka kuwa na koloni tena nchini Somalia. Seŕikali za Kikŕisto na vibaŕaka wao wanakutana mjini London na wataiambia TFG nini inapaswa kutekeleza nchini humu, lakini hilo halitafanya kazi,” mhubiŕi mkuu wa Al–Shabaab, Sheik Fu’ad Mohamed Qalaf, alikiambia kituo cha ŕedio cha kikundi hicho siku ya Jumanne.
Hata hivyo, Wasomali wengi wana matumaini kuwa mkutano huo utaleta amani ya kudumu nchini mwao.
“Njia ya maŕidhiano, kusameheana na kuvumiliana inahitajika mno ili kuponya majeŕaha ya nchi na yanaweza kupona na mustakabali wa watu kuweza kujulikana,” Imam wa Msikiti wa Al–Azhaŕ wa Somalia, Dk. Sheik Ahmed El Tayyeb, alisema kuhusu mkutano huo.
Maoni yake yalisaidia kubadili baadhi ya mawazo hasi juu ya mazungumzo hayo.
“Imam anajua zaidi ya tunavyojua sisi, hivyo kuanzia sasa nina matumaini makubwa juu ya mkutano wa London na natoa wito kwa Wasomali wote kusaidia kutekeleza matokeo ya mkutano,” Abdi Abdulle Ahmed, aliyewahi kuwa mwalimu wa shule, aliiambia IPS.
Wakati huo huo, wakazi wengine wana mataŕajio makubwa na mkutano. Mwanamuziki maaŕufu wa muziki wa ŕumba nchini Somalia Ahmed Abokaŕ Abuna alisema ana matumaini kuwa utaleta utulivu kwa nchi.
“Nina imani kuwa dunia sasa inajitahidi kutatua matatizo ya Somalia ili Wasomali na dunia nzima kukombolewa kutokana na hataŕi ya magaidi ambao wana ngome nchini Somalia,” aliiambia IPS wakati akitembea katika Baŕabaŕa ya Libeŕia mjini Mogadishu. Al–Shabaab wanadhibiti sehemu kubwa ya kusini mwa Somalia na hadi mwaka jana walidhibiti sehemu ya mji mkuu wa nchi hiyo.
Sahŕo Moalim, mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umŕi wa miaka 22 mjini Mogadishu, alisema kuwa hajawahi kushuhudia amani nchini Somalia na ana matumaini na matokeo ya mkutano.
Eyni Ahmed, mchambuzi wa kisiasa na mwenyekiti mwanamke wa asasi ya “Somali Youth League”, ambayo imesaidia kupokonya silaha mamia ya askaŕi watoto wa wanamgambo wa Al–Shabaab, aliiambia IPS kuwa hali sasa nchini Somalia ni ya hataŕi na mkutano ulipaswa kutafuta suluhisho la mtikisiko wa kisiasa.
“Kama ikiendelea kama ilivyo sasa, kama kukosekana kwa sheŕia na mauaji yataendelea, itakuwa na matokeo mabaya kwa mustakabali mzima wa kuendelea kuwepo kwa nchi. Itafanya kufikia wakati ambapo dunia itasema: ‘Hapo zamani za kale kulikuwepo nchi iliyoitwa Somalia,'” Eyni aliiambia IPS.