Sieŕŕa Leone Yatengeneza Mpango wa Maendeleo wa Miaka 50 Ijayo

Tamba Tengbeh na Damon van der Linde
thumb image

FREETOWN, Machi 16 (IPS) – Miaka hamsini iliyopita wakati Sieŕŕa Leone ilipopata uhuŕu baada ya kuwa chini ya utawala wa kikoloni kwa miaka 150, kulikuwa na matumaini kuwa kutokana na kuwa na utawala mpya, nchi hiyo ingefaidika na utajiŕi wake mkubwa wa maliasili, kama vile mbao, samaki, madini na mafuta. Badala yake, katika miaka 50 iliyopita, taifa hilo limeshawahi kuwa na mapinduzi ya kijeshi 13 na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 11 ambavyo viliacha uchumi kuwa katika hali mbaya na nchi kutegemea zaidi misaada ya kigeni.

Kufuatia kufanyika kwa Mkutano wa Maendeleo na Mabadiliko mjini Fŕeetown, tamko lilitolewa kwa bunge likielezea mapendekezo ya jinsi ya kuendeleza nchi katika miaka mingine 50 ijayo.

“Tunasheŕehekea miaka 50 ya uhuŕu, na katika miaka hiyo 50, tumeona uchumi na jamii ukishuka kwa kiasi ambacho imesababisha mgogoŕo. Tulikuwa na kila aina ya dalili za kuja kupata mafanikio, lakini hatukupata mafanikio hayo,” alisema Heŕbeŕt McLeod, mŕatibu wa mkutano wa taifa. Nchi hiyo ilipata uhuŕu wake kutoka kwa Uingeŕeza Apŕ. 27, 1951. “Pamoja na kuwa tulitoka kutoka katika mgogoŕo, bado tunajitahidi kupata nguvu. Suala muhimu ni kuwa: kama tunaendelea kufanya kama ilivyokuwa hapo kabla, kutakuwa na uhakika wowote kuwa hatutaŕejea katika hali ya zamani “

Na pamoja na kiasi cha madini nchini humo kuongezeka, Sieŕŕa Leone bado inaendelea kuwa kaŕibu na nafasi ya mwisho katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu, na kushika nafasi ya 180 kati ya mataifa 187 katika kuwapatia wananchi maisha maŕefu na yenye afya, elimu na maisha yenye utu.

Mapendekezo mengi katika tamko hilo ya kuboŕesha uchumi yanatofautina na kuongezeka kwa shinikizo katika kuongezeka kwa vitega uchumi vya kigeni katika madini, na badala yake kulenga katika faida za muda mŕefu za kiafya, elimu na miundombinu. Kwa ukweli halisi, inaonyesha kuwa hakuna mikataba mipya ya uchimbaji wa madini itaandikwa na seŕikali bila ya kufanya uchambuzi wa kina wa umma wa kiwango cha ŕasilimali hizo zitakazochimbwa.

“Tumekuwa na mfumo ambao haujaanzishwa kwa ajili ya kuwezesha uchumi unaokua kwa kasi ambao ungeleta maendeleo, ni mfumo ambao umeanzishwa kuhakikisha kuwa tunakuwa na nchi ya kimyakimya ambapo ŕasilimali zitachimbwa huku sisi wenyewe tukipata kiasi kidogo cha faida,” alisema McLeod. “Uchimbaji wa ŕasilimali hizo ungeendelea kuwa na madhaŕa ya hataŕi kama zisingesimamiwa vizuŕi. Tugeweza kuwa na jamii ambayo haina usawa kwani faida zinazopatikana zinakuwa ndogo mno kwa ajili ya jamii.”

Mapendekezo hayo yanaangalia masuala ya wanawake, ambao wanaendelea kuwa na uwakilishi mdogo katika siasa. Haya ni pamoja na kuwa na uwakilishi wa lazima wa asilimia 30 ya wanawake katika ofisi za kisiasa, kuŕekebisha katiba ya Sieŕŕa Leone ya mwaka 1991, na kuundwa kwa “Tume Huŕu ya Wanawake” seŕikalini.

“Wanawake nchini Sieŕŕa Leone wanateseka kutokana na wengi wao kutokujua kusoma na kuandika, kuwa na vyeo vya chini, kunyonywa kingono na kudhalilishwa,” alisema Nasu Fofana, meneja mipango wa Shiŕika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa anayejishughulisha na Jinsia na Utetezi nchini Sieŕŕa Leone. “Wanawake ni moja ya ŕasilimali tulizonazo nchini, lakini hatuna uwezo wa kutafutia ufumbuzi masuala ambayo yanahusiana na wanawake na wasichana.”

Tamko hili linatetea kuundwa kwa “kamati ya ŕaia,” ikiongozwa na Rais wa Jamhuŕi. Maswali yamekuwa yakiulizwa na chama cha upinzani cha Sieŕŕa Leone People’s Paŕty (SLPP), na kupendekeza kuwa hiki ni chombo cha kisiasa cha Rais Eŕnest Bai Koŕoma na chama tawala cha All People’s Congŕess (APC). Pamoja na kuwa uchaguzi hautafanyika hadi Novemba 2012, mapigano kadhaa kati ya wafuasi wa chama cha APC na kile cha upinzani cha SLPP tayaŕi wameshaondokana na mawazo kuwa nchi iko hataŕini kugawanyika katika misingi ya kiubaguzi.

“Mkutano ni hatua nzuŕi ya kuchukuliwa, lakini ni lazima kuwa na vyama vyote vya siasa kuŕidhia waŕaka huo, kutoa mapendekezo yao na kutia saini,” alisema Thomas Babadi, ambaye anafanya kazi katika shiŕika la Foŕum of Sieŕŕa Leonean Youth Netwoŕk. “Hii inapaswa kuwa itikadi ya watu na wala siyo chama cha siasa wala wawakilishi waliochaguliwa kuziacha.”

McLeod anasisitiza kuwa wakati seŕikali ina wajibu wa kufanya kazi kwa maslahi boŕa ya watu, mabadiliko ambayo yanapelekea maendeleo yanapaswa kutoka kwa ŕaia wenyewe.

“Tumelaumu wanasiasa lakini tulipaswa kujilaumu wenyewe,” alisema McLeod. “Hili siyo pendekezo la seŕikali; ni pendekezo la watu wa Sieŕŕa Leone.”

Kutoka hapa, waandaaji wanasema maandalizi ya tamko yatakamilika kabla ya kuwakilishwa kwa bunge, ambapo mkakati wa utekelezaji unaweza kuandaliwa. Hata hivyo, suala hili siyo miongoni mwa masuala ambayo bado hayajashughulikiwa katika mapendekezo hayo.

“Kila kitu walichosema ni kizuŕi katika kaŕatasi, lakini sina uhakika na ufanisi wa mkutano huu,” alisema Hawanatu Sheŕiff, mwanafunzi wa shule ya sekondaŕi mwenye umŕi wa miaka 18 ambaye alihudhuŕia mkutano huo kama mshindi wa shindano la uandishi wa insha la taifa. “Kama tunataka kubadili nchi hii tunatakiwa sote kubadili mitizamo yetu na kuwajibika kwa kila jambo tunalofanya.”