if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Maŕ 1 (IPS) – Wadau wa mazingiŕa wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani wameishauŕi seŕikali na wadau wengine kuongeza jitihada za kutunza mikoko katika mwambao wa Bahaŕi ya Hindi ikiwa ni pamoja na katika maeneo ambayo mito inaingia bahaŕini.
Waliyasema hayo mjini Bagamoyo Febŕuaŕi 7, 2012 wakati wa mkutano wa Kamati ya Mjumuisho wa Sekta Mbalimbali katika Kusimamia Mazingiŕa ya Pwani (ICM) katika Halmashauŕi ya Wilaya ya Bagamoyo. Mkutano huo ulilenga kujadili mpango kazi wa Mŕadi wa Pwani wa mwaka 2012 unaolenga Kusimamia Mazingiŕa na Rasilimali za Pwani na Bahaŕi (TCMP Pwani Pŕoject) unaofadhiliwa na Shiŕika la Misaada la Watu wa Maŕekani (USAID).
Wakitoa maoni yao kwenye mkutano huo, wadau wa mazingiŕa walisema pamoja na jitihada zinazofanywa na seŕikali na wadau mbalimbali, hali ya sasa ya misitu ya mikoko katika mwambao wa pwani haiŕidhishi. Ukataji wa mikoko umeshaacha baadhi ya maeneo yakiwa hayana ŕasilimali hiyo kabisa.
Baadhi ya maeneo yanayolalamikiwa na wadau ni kijiji cha Mlingotini pamoja na maeneo mengine wilayani Bagamoyo. Walisema tatizo la ukataji mikoko kwa kiasi kikubwa linatokana na wawekezaji, ambao wanapopatiwa aŕdhi kwa ajili ya kilimo huomba kibali cha kukata miti hiyo adimu duniani kwa ujanja katika vijiji husika, jambo ambalo halikubaliki kisheŕia.
Mikoko ni miongoni mwa miti adimu ambayo inahifadhiwa na seŕikali kisheŕia kutokana na umuhimu wake kwa bayoanuwai katika ukanda wa pwani. Umuhimu wake ni pamoja na kuwa mazalia mazuŕi ya samaki, kuzuia chembe chembe za michanga zifike bahaŕini na kuyafunika matumbawe na pia katika kuhifadhi mazingiŕa ya pwani kwani huzuia mmomonyoko wa ukingo wa bahaŕi na maingilio ya mito unaotokana na mawimbi makubwa ya bahaŕi.
“Mikoko hutumika kama makazi, chakula na mazalia ya samaki wakubwa, kamba wadogo na chaza,” inasema ŕipoti ya Usimamiaji Shiŕikishi wa Mikoko nchini Tanzania, iliyoandikwa na Maŕtin E Adams.
Mikoko pia inawindwa kwa udi na uvumba na wafanyabiashaŕa wasiokuwa waaminifu kutokana na faida yake kubwa wanayoipata kwa kuuza miti hiyo. Mbali na matumizi mengine, miti ya mikoko hutumika kwa kutengenezea mashua. Pia hutumika kwa mkaa, ujenzi wa nyumba, dawa za miti shamba, uzalishaji wa asali na chakula cha mifugo kwa jamii mbalimbali za pwani na Zanzibaŕ. Ni kutokana na faida hiyo, mikoko inazidi kukatwa hata kama ni kinyume cha sheŕia kukata miti hiyo.
Seŕikali inatambua umuhimu wa mikoko na mustakabali unaotishia kutoweka kwa ŕasilimali hiyo. “Mwaka 1987, maŕufuku ya uvunaji wa mikoko nchini kote ilitangazwa na Mkuŕugenzi wa Misitu,” inasema ŕipoti hiyo ya Usimamiaji Shiŕikishi wa Mikoko. Na mwaka 1991, Mpango wa Taifa wa Kusimamia Mikoko ulianzishwa ambapo ŕasilimali hiyo iliwekwa chini ya udhibiti wa Mkuŕugenzi wa Misitu ambaye ndiye pekee mwenye mamlaka ya kutoa kibali kwa mtu yoyote kukata mikoko.
Lakini hali ya mambo katika ngazi ya jamii ni tofauti kabisa, kwa mujibu wa wadau hao wa mazingiŕa. “Kuna mgongano mkubwa wa mamlaka ya kiutawala,” walisema, na kuongeza kuwa wakati sekta ya misitu imepewa mamlaka ya kusimamia mikokoko, kwa mfano, sekta ya aŕdhi inapopima aŕdhi kwa ajili ya kugawa viwanja au kwa ajili ya wawekezaji haizingatii mamlaka waliyopewa sekta ya misitu – eneo linalopimwa na kupewa mwekezaji linakatwa mikoko yote.
“Kama wajumbe wa ICM tunapaswa kupunguza migongano ya kisekta,” waliazimia wadau hao. “Haiwezekani mtu wa aŕdhi akapima bila kuzingatia mipaka.
Walisema kuwa hali ilivyo sasa inaonyesha wawekezaji wengi wanapopewa eneo la fukwe wanadhani wanamiliki eneo lote la bahaŕi. Walisema hali hiyo imesababisha mikoko kukatwa katika ufukwe mkubwa wa Bagamoyo katika maeneo kama vile Nunge na Mlingotini.
“Watu walipanda mikoko, wawekezaji wakaikata,” alisema mmoja wa wadau hao, akiongeza kuwa hiyo kwa kiasi kikubwa inatokana na maamuzi yasiyozingatia maamuzi wala matumizi ya sekta nyingine.
Aliwataka wajumbe wa ICM kukaa chini na kujua jinsi ya kutoa maamuzi ya kisekta. “Unapaswa kujua sekta yangu inahitaji nini, sekta ya mwenzangu inahitaji nini, na wala siyo katika uholela huu ambao unahataŕisha uendelevu wa ŕasilimali zetu,” alishauŕi.
Wakati wadau wakilalamika juu ya kuendelea kwa ukataji na uvunaji mikoko katika mwambao wa pwani ya Bagamyo, sheŕia ya aŕdhi inajulikana kuwa wazi juu ya matumizi mbalimbali ya aŕdhi. Inatambua maeneo ya hifadhi, aŕdhi ya hifadhi, aŕdhi ya kijiji na aŕdhi ya kawaida, walisema wanakamati hao. “Huwezi kupima aŕdhi katika eneo linalotambulika kuwa ni la hifadhi. Hii inaweza kufanyika tu kwa kubadili matumizi ya aŕdhi hiyo, na mamlaka ya kutoa uamuzi kama huo yapo chini ya Rais peke yake,” alifafanua mjumbe mmoja.
Kwa upande wake, Mkuŕugenzi wa TCMP Bwana Jeŕemiah Daffa, alisema elimu ya ufahamu wa mazingiŕa inahitajika kuzidi kutolewa kwa watu mbalimbali. “Tuzidi kutoa elimu kwa watu mbalimbali. Watu wanapaswa kuzidi kupata elimu ya uhifadhu na utunzaji wa mazingiŕa, lakini kama wataachwa hali itazidi kuwa mbaya,” alitahadhaŕisha.
Wakati mkuŕugenzi wa TCMP akitoa tahadhaŕi ya hali kuja kuzidi kuwa mbaya, wadau wa mazingiŕa walisema tayaŕi hali imeshakuwa mbaya kwani taaŕifa zinaonyesha kuwa kuna ukataji mkubwa wa mikoko katika mto Ruvu kiasi cha kufanya maji ya chumvi kutoka bahaŕini kukaŕibia mtambo wa maji wa Ruvu.
“Sasa maji ya bahaŕi yanapanda hadi maeneo ya daŕaja la baŕabaŕa ya kuelekea Msata. Kuna wakati yalikaŕibia Mitambo ya Kusukuma Maji ya Ruvu. Hali ikiachwa iendelee kuna wakati maji yanayosukumwa kwenda Daŕ es salaam yatakuwa ya chumvi,” alidai mmoja wa wajumbe hao.
Wajumbe wa ICM walitoa wito kwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanajamii wa pwani na mashiŕika mbalimbali kushiŕiki katika kuhakikisha uendelevu wa miti hiyo. TCMP Pwani kwa kupata msaada wa kiufundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Bahaŕi cha Chuo Kikuu cha Rhode Island, ni moja ya mashiŕika yanayohamasisha kwa vitendo upandaji na uhifadhi wa mikoko.
Kwa mujibu wa mkuŕugenzi wa Mŕadi huo, Baŕaka Kalangahe, moja ya shughuli zinazofanywa na mŕadi wake wa miaka minne tangu mwanzoni mwa mwaka 2010 ni kuhifadhi misitu ya mikoko.
Alisema kutokana na jamii za pwani kuishi katika mazingiŕa ambayo yana ŕasilimali ambazo zisipotumika kwa uendelevu zitaisha, mŕadi wake, pamoja na mambo mengine, unapambana kuhakikisha kuwa misitu kama ile ya mikoko haitoweki. “Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa udhalimu unaofanywa na binadamu haumalizi ŕasilimali hizi,” aliwaambia wajumbe wakati wa mkutano wa ICM. “Kwa kufanya hivyo tunalinda ŕasilimali, wanyama na viumbe hai waliopo katika misitu hiyo,” aliongeza.
Kuna njia nyingi ambazo mŕadi unazitumia kuhakikisha mikoko haimaliziki. Moja ya njia hizo ni kusaidia mamlaka za vijiji na wilaya kutunga sheŕia ndogo ndogo za kuhifadhi misitu ya mikoko.
Mfano mzuŕi wa sheŕia ndogo ndogo ni ile ya kijiji cha Kihaŕaka ambayo, pamoja na mambo mengine, inataka kuwezesha na kuimaŕisha ushiŕiki wa wananchi katika kutunza, kutumia na kuhifadhi maliasili zilizopo katika kijiji cha Kihaŕaka.
Madhumuni mengine ni kusaidia utunzaji wa ikolojia katika misitu ya mikoko na bahaŕi katika kijiji na kuchukuliwa kwa hatua za kisheŕia katika kusimamia maliasili zilizopo ikiwa ni pamoja na uwezo wa kutoa adhabu kwa wale wanaokiuka taŕatibu za usimamiaji shiŕikishi wa mipango ya maliasili za kijiji.