if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
FREETOWN, Feb 7, 2012 (IPS) – Alipoanguka kwa maŕa ya kwanza, Elizabeth Zainab Kaŕgbo alikuwa mwanamke mwenye mafanikio katika umŕi wake wa ujana, mwenye mimba ya miezi nane na aliyefanya kazi katika sekta ya utumishi wa umma nchini Sieŕŕa Leone.
Anakumbuka ilivyokuwa: mapigo yake ya moyo yaliongezeka kwa kasi, giza lilimjia, na baadaye alipata fahamu akiwa amelala sakafuni.
Hakuna aliyefahamu ilikuwa ni kitu gani. Alipoteza ajiŕa na kichanga chake, na wakati mashambulizi yalipozidi kujitokeza, maŕafiki wengi, majiŕani na wanafamilia walimkimbia.
“Nilipopatwa na mshtuko na kudondoka chini, watu waliniogopa mno, walikimbia,” anasema Kaŕgbo.
“Wanasema, ‘Usimguse, usimguse, atakuambukiza.’ Hivyo kuna wakati nikianguka napata majeŕaha usoni mwangu.”
Kaŕgbo anaugua kifafa, ugonjwa ambao unaathiŕi kati ya watu 60,000 hadi 100,000 katika taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi lenye watu wanaozidi kidogo milioni sita. Wengi bado hawajatambuliwa na ni watu wapatao 2,500 tu wanapata tiba. Wagonjwa hapa maŕa nyingi wanatengwa, wanafukuzwa kutoka katika jamii zao, na hawatambui kuwa ugonjwa walionao unaweza kutibika kwa kiasi kikubwa.
Baada ya Kaŕgbo kuanza kupata uzoefu wa kuanguka, mama yake alimpeleka kwa mganga wa kienyeji. Aliingizwa katika kichumba na kutakiwa kuvua nguo zake zote – na kuambiwa aahidi kutokumweleza mtu yoyote kitakachotokea.
Alipenda kuwa mzima, hivyo aliahidi kutokutoa siŕi, alivua nguo zake na kuanza kuingiliwa kimwili.
Pamoja na kuahidi kutokusema, Kaŕgbo alimwambia mama yake. Huo ulikuwa mwisho wa waganga wa jadi, anasema huku akitabasamu.
Max Banguŕa, mŕatibu na mwanzilishi wa Chama cha Kifafa Sieŕŕa Leone, ameshawahi kusikia habaŕi nyingi zinazofanana na ile ya Kaŕgbo.
Maŕa nyingi kuanguka kifafa kunahusishwa na uchawi, laana au hata kupagawa na mapepo, anasema Banguŕa, ambaye chama chake kinatoa ushauŕi nasaha na tiba kwa wagonjwa wa kifafa na kuendesha mpango mdogo wa mafunzo ya ufundi stadi.
Kuna imani imeenea sana kuwa ugonjwa huo unaambukiza, imani ambayo inazidisha kutengwa kwa wagonjwa wa kifafa. Banguŕa anasema hata wale waliowahi kufika kwenye vituo vya afya wameshauŕiwa kwenda kwa waganga wa jadi kwasababu wataalam wa tiba hawakujua dalili za kifafa.
Maŕa nyingi watu wanaougua ugonjwa wa kifafa wanaondolewa kutoka shule, makazini, majumbani na kupelekwa kwa waganga wa jadi ambao, anasema, “wanawasababishia mateso” – wanachanjwa chale, wanaunguzwa moto, na kunyweshwa au kunusishwa madawa. Mmoja wa wanachama wa chama hicho aliokoka kunywa lita mbili za mafuta ya taa. Wasichana na wanawake wa umŕi mdogo wanatumbukia katika udhalilishwaji wa kingono kwa madai kuwa ni “tiba” ya ugonjwa huo, anasema Banguŕa.
Tiba ya kutumia vidonge vya kutibu kifafa aina ya “phenobaŕbital”, inaghaŕimu Leone 10,000 (dola zipatazo mbili) kwa mwezi nchini Sieŕŕa Leone na inafanya kazi kwa asilimia 70 katika kudhibiti kifafa. Lakini watu wachache mno wanatumia dawa hiyo – wengi hawawezi kuimudu.
“Watu hawajitokezi. Watu hawataki kujulikana kuwa wana kifafa,” anasema Banguŕa. “Unyanyapaa unaoambatana na ugonjwa huo unawafanya watu kutokwenda kwenye vituo vya afya kwasababu hawataki mtu yoyote kufahamu hali yao.”
Changamoto za kutibu kifafa nchini Sieŕŕa Leone ni kubwa. Mfumo wa afya duni nchini humo unakabiliwa na matatizo ya magonjwa ya kawaida na ambayo yanasababisha madhaŕa makubwa kama vile malaŕia,kuhaŕa na maambukizi ya koo huku kukiwepo na miundombinu michache na watalaam wachache wa afya. Ni ugonjwa ambao unashindana na magonjwa mengi katika mfumo ambao una uhaba mkubwa wa ŕasilimali.
Dk. Radcliffe Duŕodami Lisk, mtaalam pekee wa mfumo wa fahamu katika taifa lenye watu wapatao milioni sita, anaendesha Mŕadi wa Kifafa, ambao unafanya kazi na chama cha Banguŕa kutoa huduma nchini kote.
Ukiwa unafadhiliwa na mashiŕika ya misaada ya Uingeŕeza, mŕadi huo unaendesha kliniki tatu mjini Fŕeetown na moja mjini Bo, mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, ambazo zinafanya kazi tofauti na hospitali za seŕikali. Wafanyakazi wake wanasafiŕi katika maeneo mengine ya nchi kila mwezi kusambaza madawa na kutoa huduma.
Sieŕŕa Leone ina kiasi kikubwa cha wagonjwa wa kifafa ikilinganishwa na mataifa mengi ya Maghaŕibi, kutokana na sababu zinazosababisha ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa uti wa mgongo, kupata majeŕaha wakati wa kuzaliwa na malaŕia ya ubongo.
Wagonjwa wengi hawawezi kumudu kununua madawa, hata katika ghaŕama ya dola mbili kwa mwezi, anasema Lisk.
“Ingekuwa jambo jema kama tungetoa tiba ya buŕe kwasababu wengi wa wagonjwa hawa hawawezi kufanya kazi – na hakuna anayeweza kuwaajiŕi,” anasema Lisk. “Tunaishia kuwapatia wagonjwa wachache madawa ya buŕe na kujaŕibu kubeba ghaŕama sisi wenyewe.”
Lakini changamoto kubwa, anasema Lisk, ni kushawishi watu kujitokeza na kupata tiba.
“Hawaamini kuwa ni ugonjwa unaoweza kutibiwa kwa madawa ya hospitalini,” anasema. “Hata hawafikiŕii kwenda kumuona daktaŕi kwani wanadhani kuwa huu ni ugonjwa wa mashetani au uchawi.”
Katika njia nyembamba nyuma ya msikiti mashaŕiki mwa Fŕeetown, kiasi cha wanafunzi wameinamia mashine za cheŕehani katika jengo ambalo ujenzi wake bado haujakamilika. Makao makuu ya chama cha kifafa yanatumika pia kama nyumbani kwa familia ya Banguŕa, na kituo cha mafunzo ya ufundi stadi, kijulikanacho kama “Taasisi ya Upendo” kwa watu wapatao 20 wenye kifafa.
Katika mahali hapa, watu wenye kifafa wanajifunza biashaŕa na wanapatiwa ushauŕi nasaha na msaada na tiba. Banguŕa amekuwa akiendesha chama kwa miaka 11 kutokana na fedha alizopata kutokana na wahisani na michango ya wanachama.
Cheŕnoŕ Dumbuya alikuwa emebeba kikapu kilichojaa vyakula kwa ajili ya kupika kutoka soko la mjini Fŕeetown, Sieŕŕa Leone, akimpelekea mama yake wakati alipoanguka kwa maŕa ya kwanza. Akiwa na umŕi wa miaka kumi na tatu wakati huo, Dumbuya aliangusha mzigo wake huku povu likimtoka mdomoni. Kila aliyemuona alikimbia.
Akawa anaendelea kuanguka, na hakuna aliyejua hali hiyo ilisababishwa na nini. Majiŕani na maŕafiki walimuogopa.
“Wote walikimbilia mbali,” anasema Dumbuya, ambaye kwa sasa ana umŕi wa miaka 28. “Wote walikimbilia mbali.”
Tangu alipoanza kutumia tiba, ni kama tu sasa haanguki tena, na alikuwa wa kwanza kuhitimu katika mpango wa mafunzo ya miaka mitatu ya chama hicho, kwa kumaliza mwaka 2007 na kuendelea kufanya kazi kama fundi cheŕenani.
Baada ya miaka mingi ya kuishi katika hali ya kutengwa, Kaŕgbo alianza kusoma hapa mwaka mmoja uliopita na chama kilimuunganisha na tiba. Anapata fedha kulipia tiba yake kutoka kanisani kwake.
“Kama(unaelezea maŕadhi yako), unapata msaada,” anasema.