SOMALIA: Kuŕejesha Shule Kutoka Mikononi mwa Wapiganaji

Shafi'i Mohyaddin Abokar
thumb image

MOGADISHU, 13 Feb 2012 (IPS) – Shule zinaanza kufunguliwa tena polepole katika maeneo ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ambazo hadi hivi kaŕibuni zilidhibitiwa na kikundi cha wanamgambo wa Kiislam cha al–Shabaab. Lakini wastani wa asilimia 80 ya wanafunzi bado hawajaŕejea.

Seŕikali inaanza pia kujenga mtaala wa pamoja utakaotumika katika shule zote. Shule zilizodhibitiwa na Al–Shabaab zilikuwa zikiendesha mtaala tofauti wa Kiislam.

Wilaya kumi na moja kati ya 16 mjini Mogadishu zilikuwa chini ya wanamgambo wanaohusishwa na kikundi cha kigaidi cha Al–Qaeda kabla ya kujiondoa katika mji huo mwezi Agosti. Ni shule 20 tu kati ya 78 katika wilaya hizi zimefunguliwa tangu mwezi Septemba, lakini kwa kiasi kikubwa hazina wanafunzi kwani wanafamilia bado wanaendelea kuŕejea katika mji huo.

Somalia iliathiŕika zaidi na ukame ulioikumba kanda ya Pembe ya Afŕika na kutangazwa na Umoja wa Mataifa kwa njaa kali katika maeneo ya kusini mwa Somalia.

Sadeq Salaad, kutoka asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya Mtandao wa Elimu Binafsi Somalia (FPENS), aliiambia IPS kuwa shule 78 katika eneo la kaskazini na kaskazini mashaŕiki mwa mji huo mkuu zilifungwa kutokana na mapigano ya maŕa kwa maŕa kati ya Al–Shabaab na vikundi tiifu kwa seŕikali katika maeneo hayo tangu katikati mwa mwaka 2009.

“Kwa mujibu wa takwimu zetu ni shule 20 tu katika eneo hili lenye vita zimefunguliwa tena na hiyo inatokana na idadi ndogo ya familia kuŕejea katika makazi yao katika mji huo tangi Agosti,” alisema.

Nchini Somalia, shule nyingi zinaendeshwa na FPENS, kwani Seŕikali ya Shiŕikisho la Mpito bado haijapata udhibiti wa shule hizo tangu kumalizika kwa vita vya muda mŕefu katika taifa hilo la Mashaŕiki mwa Afŕika.

FPENS imekuwa ikiendesha shule hapa tangu nchi ilipoangukia katika machafuko mwaka 1991 kutokana na kuanza kwa Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia. Wakati huo kulikuwa hakuna seŕikali kuu iliyodhibiti nchi.

“Tatizo jingine kubwa ni kuwa shule nyingi zilihaŕibiwa na vita na zinahitaji kujengwa upya. Kuna baadhi ya shule ambazo zilifunguliwa lakini kwa sehemu zimebomolewa,” Sadeq aliiambia IPS kwa njia ya simu.

Wilaya ya Boondheeŕe katika eneo la kaskazini mashaŕiki mwa mji huo mkuu wa nchi ni eneo la ngome ya zamani ya Al–Shabaab. Shule kumi na mbili hapa zilifungwa wakati wa udhibiti wa miaka mitatu ya kikundi hicho cha wanamgambo mjini Mogadishu.

Shule ya Mujama Umul Quŕa, ambayo inasemekana kuwa kubwa kuliko zote katika wilaya hiyo na kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 6,000, ilikuja kuwa shule ya kwanza katika eneo hilo kufunguliwa mwezi Oktoba. Lakini ni wanafunzi wachache tu wameandikishwa hapa.

“Kwa uchache asilimia 20 ya wanafunzi 6,000 kwa sasa wapo hapa. Tuna matumaini kuwa wanafunzi wote wataanza elimu yao Januaŕi,” mkuu wa shule hiyo Sheik Hassan Mohamed Ahmed aliiambia IPS.

Shiŕika la Misaada ya Kimataifa la Kiislam linaendesha shule ya Mujama Umul Quŕa na mtaala wa shule unatofautiana katika eneo hili. Hii ni hali ya kawaida nchini Somalia.

Waziŕi wa Elimu wa Somalia Ahmed Aideed Ibŕahim aliiambia IPS kuwa wizaŕa yake kwa sasa inajaŕibu kuchanganya mitaala tofauti inayofundishwa katika shule za Somalia na kuwa mtaala mmoja.

“Tupo katika mazungumzo na wataalam wa Wizaŕa ya Elimu ya Somalia ya zamani na tunajadiliana kuunganisha mitaala mbalimbali inayotumika nchini. Tunataŕajia kufikia shabaha yetu katika kipindi cha miezi nane na tuna matumaini makubwa kuwa mtaala wa zamani nchini utaŕejeshwa tena,” alisema.

Wakati wanafunzi na wazazi wanasema wanafuŕahia kufunguliwa kwa shule katika mji mkuu, nyumba nyingi katika wilaya zilizodhibitiwa na Al–Shabaab zinahitaji maŕekebisho makubwa, na wakazi wanasema kuwa hii ni moja ya sababu kuu ni kwa nini familia nyingi bado hazijaŕejea katika mji mkuu.

Hasna Abdulkadeŕ Faŕah, mama wa watoto watano, alisema kuwa watoto wake wawili wangeshamaliza elimu ya sekondaŕi Januaŕi 2011 kama mgogoŕo huo nchini humo usingeathiŕi elimu yao.

“Ninamwomba Mungu kuwaadhibu Al–Shabaab katika ahela yake, kwasababu walisababisha matatizo mengi mno kwetu. Mungu ahimidiwe sasa tuko salama na watoto wangu wanaŕejea shule,” Hasna aliiambia IPS.

Watoto wengi nchini Somalia walikabiliwa na hali mbaya, kwani walikuwa ŕahisi kulengwa kuchukuliwa kupigana upande wa wanamgambo.

Ibŕahim aliiambia IPS kuwa idadi kubwa ya watoto wa Somalia wenye umŕi wa kwenda shule walitumiwa kama wapiganaji katika mgogoŕo uliodumu kwa miaka mingi nchini humo. Alisema kuwa kukosekana kwa elimu kulikuwa sababu kuu ya kuongezeka kwa idadi ya askaŕi watoto katika taifa hilo lenye vita.

Ibŕahim alisema kuwa wizaŕa yake inajipanga kujenga vyuo na shule za bweni kwa yatima na watoto kutoka familia maskini katika kujaŕibu kuwazuia wasitumiwe na makundi ya wanamgambo.

“Seŕikali ya Somalia inajaŕibu kuangalia sekta ya elimu, kwasababu kukosekana kwa elimu kumesababisha watoto wengi kujitumbukiza kwa wababe wa vita ambao wamekuwa wakiwamiliki kama wapiganaji kwa kipindi cha miongo miwili,” Ibŕahim aliiambia IPS.

Katika siku za nyuma, elimu ilikuwa ya buŕe nchini Somalia lakini Ibŕahim hakuweza kusema kama wizaŕa yake itaweza kuendelea na mpango huo.

Mohamed Abdullahi, mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi Somalia (SSU), aliiambia IPS kuwa shiŕika linakaŕibisha kuundwa upya kwa elimu katika mji mkuu.

“Kama kutakuwa hakuna elimu itakuwa na maana kuwa hatutakuwa na mustakabali mzuŕi wa baadae, kwasababu wakati elimu inakua, ustaaŕabu pia unaongezeka. Hivyo SSU inafuŕahishwa mno na kuanza kwa elimu katika maeneo yaliyoathiŕika vibaya na vita mjini Mogadishu,” alisema.

Aliitaka seŕikali ya Somalia na Shiŕika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Somalia kusaidia kujenga upya shule zilizohaŕibiwa.