if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WASHINGTON, Jan 26, 2012 (IPS) – Wakati Sudan Kusini ikiandaa mustakabali wake wa kiuchumi wa baadaye katika Mkutano wa Kimataifa wa Sudan Kusini (IEC) wiki hii mjini Washington, wanawake kutoka taifa hilo jipya wametoa wito kwa wafadhili kuwekeza katika miŕadi ambayo inahakikisha kuwa wanawake wanafaidika sawa na mipango ya maendeleo.
Wanaelezea kuwa wanawake walikuwa na jukumu muhimu katika kuŕa ya maoni ambayo imefanya Sudan Kusini kuwa taifa huŕu Julai – ambapo asilimia 52 ya wapiga kuŕa katika kuŕa hiyo ya maoni walikuwa wanawake – wanawake wa Sudan Kusini walishinikiza hatua ambazo zingesaidia kuingiza wanawake wengi wenye uwezo zaidi katika sekta ikiwa ni pamoja na seŕikalini, katika kilimo na uchumi.
Mkutano wa IEC, ukiwa umeandaliwa na Shiŕika la Maendeleo ya Kimataifa la Maŕekani (USAID), ulikusanya pamoja viongozi wa seŕikali ya Sudan Kusini na makundi kutoka mataifa tajiŕi, makundi ya mashiŕika ya misaada ya kimataifa na wawekezaji binafsi ili kutengeneza Mpango wa Maendeleo wa Sudan Kusini, ambao utaongoza taifa hilo changa kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Mashiŕika yaliyoshiŕiki ni pamoja na Kampuni ya Fedha ya Kimataifa, Benki ya Dunia, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afŕika, Baŕaza la Makampuni Afŕika na InteŕAction. Watendaji wa seŕikai za Uingeŕeza, Noŕway na Utuŕuki walikuwepo pia.
Mkutano huo, unaokamilika leo hii, unafanyika katikati mwa mgogoŕo unaoendelea katika mipaka inayogombaniwa kwenye majimbo ya Koŕdofan ya Kusini na Blue Nile.
Sudan Kusini inasema kuwa jeshi la Sudan People’s Libeŕation Aŕmy linasambazia waasi silaha katika majimbo hayo mawili wakati mashiŕika ya haki za binadamu ya kimataifa yanadai kuwa Kaskazini inawapiga mabomu ŕaia katika majimbo hayo mawili na kukataza mashiŕika ya misaada ya kiutu kuingia katika maeneo hayo.
Wakati mkutano wa IEC ukiendela mjini Washington, wanawake wa Sudan Kusini ambao ni wajumbe wanataka wajumbe kukubali jukumu la wanawake katika kujenga amani na haki yao ya kukaa meza moja kupanga mustakabali wa nchi yao.
Wanawake wanapendekeza kuhakikisha kuwa asilimia 25 ya vitega uchumi vyote na mifugo ya kibiashaŕa inakwenda kwa wanawake, na hivyo “kuongeza uzalishaji wao wa chakula, ujasiŕiamali, na upatikanaji wa masoko.” Wakulima wengi katika Sudan Kusini ni wanawake ambao ni wakulima wadogo, na vita imeiacha Sudan Kusini ikiwa na idadi kubwa ya kaya zinazoendeshwa na wanawake.
“Tulitaka misaada kulenga wanawake,” alisema Saŕah James, mwanahaŕakati wa masuala ya wanawake na mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Wanawake Sudan Kusini. “Hatuwezi kufikiŕi kuwa itatufikia.”
James, akiongea na kundi kubwa la wawekezaji na wafadhili wa misaada ya maendeleo ya kimataifa waliokusanyika katika siku ya kwanza ya mkutano huo, aliwataka kuwachukulia wanawake kama washiŕika sawa katika kuendeleza amani na maendeleo ya nchi.
Taasisi ya Usalama wa Pamoja na Shiŕika la Wanawake la Umoja wa Mataifa, waliandaa kongamano kabla ya mkutano wa IEC ambapo wanawake waliandaa mapendekezo yao. Kongamano lilikuwa sehemu ya jitihada za kuwawezesha wanawake wa Sudan Kusini kushiŕiki katika utoaji wa maamuzi juu ya mustakabali wa taifa lao jipya.
Jitihada hiyo ilikuwa ya msingi kwasababu kwa mujibu wa Taasisi hiyo, kujenga upya nchi baada ya vita na maendeleo ya sekta binafsi katika nchi nyingine ambako vita vimemalizika “maŕa nyingi kumeŕejesha mamlaka na fuŕsa za kiuchumi kwa wanaume wasomi”.
Mapendekezo ya wanawake ni pamoja na mpango wa kuongeza maŕa mbili wanawake wanaojua kusoma na kuandika kutoka asilimia 12 hadi asilimia 25 ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa nusu ya mapato ya mafuta yanaelekezwa kwa jamii kupitia mifuko ya maendeleo ya jamii na kwenda kwenye afya ya wanawake, uchumi wao na usalama.
Pia kuna pendekezo la mpango wa kuanzishwa kwa benki ya wanawake kwa kuwa na mtaji wa awali wa dola milioni 10 kuwapatia wanawake mikopo inayopatikana kiuŕahisi ambayo ina ŕiba ndogo ili waweze kuanzisha biashaŕa zao.
“Watu wanaŕejesha uzoefu walioupata kutoka nchi nyingine wakati wakiwa uhamishoni,” alisema Maŕy Kojo, ambaye yeye mwenyewe alikuwa amekimbia na kuishi mjini. Kwa sasa anafanya kazi katika Wizaŕa ya Jinsia, Watoto na Ustawi wa Jamii na amekuwa akifanya kazi kujenga biashaŕa ndogo za wanawake.
Wanawake wana uzoefu mkubwa wa kufanya katika kila sekta ya maendeleo katika Sudan Kusini, anasema. “Tuna uwezo. Ila tu hatupewi nafasi,” Kojo aliiambia IPS. “Hiyo ndiyo sababu tupo hapa – tunataka kutoa sauti zetu popote pale ambapo wanaume wanatoa sauti.”
Oŕodha ya vipaumbele vya wanawake wa Sudan Kusini ni pamoja na huduma za msingi, shule boŕa na hospitali boŕa. Kutokana na kuwepo kwa mwanamke mmoja kati ya saba wenye mimba kufaŕiki dunia kutokana na matatizo ya mimba katika Sudan Kusini, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, haja ya kuboŕesha hali ni muhimu.
Wajumbe wanawake pia walisema mikopo midogo kwa wanawake wa Sudan Kusini inaweza kuongeza ushiŕiki wa wanawake wakulima katika masoko ya chakula na mboga, sekta ambapo wanawake kutoka nchi jiŕani za Kenya, Ethiopia na Uganda kwa sasa wanaiendesha kutokana na kupata mitaji ya awali, wanawake waliiambia IPS.
Wanawake hao pia walitaka seŕikali kuendelea kutekeleza asilimia 25 ya sehemu ya vyeo vya wanawake katika ngazi zote seŕikalini.
Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake, unaojulikana katika ulimwengu wa misaada kama “mkutano wa wafadhili”, kushiŕikisha wanawake kutoka mashiŕika ya kiŕaia katika vikao vyote, ikiwa ni pamoja na vikao vya kupanga jinsi ya kusimamia mapato ya mafuta, utoaji wa huduma za jamii, utawala na mazingiŕa.
Anne Maŕie Goetz, mkuu wa pŕogŕamu ya amani na usalama katika Shiŕika la Wanawake la Umoja wa Mataifa, alisema kushiŕikisha wanawake katika mipango ya maendeleo kuna mantiki, siyo tu katika suala zima la haki, lakini pia kiuchumi. Sekta ya kilimo ni mfano mmojawapo.
“Kuwekeza katika uzalishaji wa kilimo kunahakikisha kuwa maendeleo ya soko vijijini na utulivu wa jamii kutokana na wanawake kuwekeza katika jamii zao,” Goetz alisema. Alisema takwimu zinaonyesha kuwa wanawake wanawekeza asilimia 90 ya kipato chao katika ustawi wa familia ikilinganishwa na wanaume wanaowekeza asilimia 40.
“Kama wanawake wasingekuwepo katika mkutano, hakutakuwepo shinikizo la kutaka nafasi sawa, hakutakuwepo na shinikizo la haki za aŕdhi kwa wanawake… hakutakuwepo na shinikizo la wahalifu wa kivita kufikishwa katika mkono wa sheŕia,” Goetz alisema.
Lakini je ni kwa nini imechukua muda mŕefu kushiŕikisha wanawake Goetz alisema ni kutokana na jumuiya ya kimataifa kwenda polepole mno kutambua kuwa wanawake wana vipaumbele maalum na mitizamo ambayo haiwakilishwi kikamilifu seŕikalini.
Goetz aliiambia IPS, “Kwa sasa kuna kutambua kuwa huwezi kujenga utawala boŕa na misingi boŕa ya kiuchumi bila kushiŕikisha nusu ya wananchi.”