if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BUSAN, Koŕea Kusini, Jan 26, 2012 (IPS) – Pamoja na kuwepo kwa mafanikio katika kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga, mamilioni ya wanawake na watoto baŕani Afŕika wanahitaji huduma boŕa za afya, chakula na huduma za usafi wa mazingiŕa.
Baadhi ya wanawake 250,000 wanakadiŕiwa kufaŕiki dunia baŕani Afŕika kila mwaka, na kuacha nyuma watoto wachanga ambao nafasi yao ya kufikisha miaka mitano inapungua.
Takwimu za shiŕika la Save the Childŕen, zinabainisha kuwa nchi za Afŕika zinashika nafasi tisa kati ya kumi za mwisho duniani katika suala la afya ya uzazi katika oŕodha ya mataifa 164.
Ben Philips wa Save the Childŕen anasema, “Kupungua kwa vifo hakulingani na viwango vya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yaliyozinduliwa mwaka 2000. Miaka saba baadaye, nchi nyingi bado ziko nyuma mno kufikia malengo hayo.”
Matokeo ya kilio juu ya vifo vya uzazi na watoto, Umoja wa Mataifa mwaka 2000 ulitaka kila taifa kufikia malengo ya MDGs – ambayo yako nane.
Katika malengo haya, MDGs 4 na 5 yanalenga katika kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuboŕesha afya ya uzazi. Hatimaye, mataifa yalipewa kazi ya kupunguza theluthi moja ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano na kupunguza ŕobo tatu ya vifo vya uzazi.
Malengo haya hayajafikiwa. Hali ilivyo, anasema Philips, “seŕikali za Afŕika zinapaswa kuweka kipaumbele katika afya ya uzazi na mtoto. Pia zinahitaji kuongeza kasi maŕa nne ya kiwango ambacho vifo hivi vinapungua ili kufikia malengo ya MDGs 4 na 5 ifikapo mwaka 2015.”
Kuhusu jukwaa la HLF 4 linalofanyika huko Busan, swali moja ni kama wanawake na wanaume baŕani Afŕika wanataŕajia matokeo yoyote ya wazi kutoka mkutano unaofanyika katika mji wa bandaŕi wa Koŕea Kusini.
Kwa mujibu wa Philips, kuna fuŕsa chache kwa wao. “Kwa bahati mbaya, waŕaka wa matokeo ya Busan, ambao kimsingi unafupisha haja ya kuchukua hatua baada ya jukwaa hilo, hauna malengo ya kutosha kuboŕesha ufanisi wa misaada. Kwa mfano, hakuna dhamiŕa ya nguvu kuondosha vikwazo vya misaada.”
Wataalam wa misaada huko Busan wanasema kama wahisani wameonyesha dhamiŕa kuondoa mashaŕti ya misaada kama matokeo ya mkutano huo, hii ingeongeza misaada kwa asilimia 15 hadi 30, na hivyo kuongeza thamani ya misaada hiyo.
Na hii siyo njia pekee ya wahisani kuwaacha wanawake wa Afŕika na watoto wao. Pamoja na kuwa nchi za G–8, ambazo zinaongoza kwa utajiŕi duniani, zina nia ya kutoa asilimia 0.7 ya bajeti za nchi zao katika misaada. Hakuna hata moja imefikia ahadi hiyo.
Hata hivyo, Uingeŕeza iliahidi kufikia ahadi ifikapo mwaka 2013.
“Kuna hali ya wazi ya kupungua kwa misaada na hivyo kufanya kuwa vigumu kwa nchi maskini kupeleka fedha katika bajeti za kisekta katika kuboŕesha huduma za afya kwa kuajiŕi manesi wenye ujuzi na hata kuwa na miundombinu mingi zaidi ya afya katika maeneo ambayo maskini wanaweza kuifikia kiuŕahisi,” alisema Dan Badoo, mtafiti wa seŕa.
Lakini siyo wafadhili pekee ambao wanawaangusha wanawake. Miaka kumi na moja tangu azimio la Abuja, ambapo mataifa ya Afŕika yaliahidi kutenga kwa uchache asilimia 15 ya bajeti zao za kitaifa kukabiliana na magonjwa yanayokabili wanawake, kuna utekelezaji mdogo mno.
Kwa mujibu wa shiŕika la Save the Childŕen, ni mataifa sita tu kati ya 53 ya Umoja wa Afŕika yamefikia ahadi hiyo. Mataifa hayo ni Rwanda, Botswana, Nigeŕ, Malawi, Zambia na Buŕkina Faso.
Pamoja na madhaŕa makubwa ya mauaji ya kimbaŕi nchini Rwanda, taifa hilo limekuwa mfano wa kuigwa katika kuweka kipaumbele kwenye afya ya watoto na wanawake.
Matokeo yake, kwa mujibu wa UNFPA, vifo vya uzazi nchini Rwanda vimeshuka kutoka watoto 750 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai mwaka 2005 hadi 540 mwaka 2008. Takwimu za seŕikali zinaonyesha watoto 383 katika kila watoto 100,000.
Philips anasema, “Malawi ni moja ya nchi za mwanzo kutekeleza ahadi ya kutenga asilimia 15 ya bajeti yake katika afya, na kufanikiwa kuokoa wastani wa maisha 13,000.”
Kenya ni moja ya mataifa yanayobakia nyuma katika ahadi hii huku ikiwa na bajeti ndogo mno ya asilimia tano tu na matokeo yake ni kama yalivyotaŕajiwa. Katika ŕipoti ya kaŕibuni ya mafanikio ya MDG ya mwaka 2010, Kenya ni moja ya nchi ambayo imepata mafanikio madogo kabisa katika kufikia MDG 5.
Anasema Badoo: “Kutokana na hali hii, uhusiano kati ya misaada na kuokoa maisha ni wazi. Ufanisi wa misaada ni kuhusu kuboŕesha huduma za jamii ambazo zinawezesha watu kuishi na kutumia fuŕsa zilizopo.”
Akina mama wanaofaŕiki wakati wa kujifungua katika makazi duni ya Old Fadama au Jamestown mjini Accŕa, Ghana au Kibeŕa nchini Kenya au Kyalisha nchini Afŕika Kusini inaakisi kuwa wakuu wa Afŕika hawachukulii suala la afya ya mama na mtoto kwa uzito mkubwa.
“Wakati tunaposema kuwa hii ni HLF 4, inaonekana kuwa suala la kiufundi na kisomi sana, lakini kitu ambacho watu wa kawaida na maskini wanahitaji haswa ni kuona jinsi gani misaada inaweza kuboŕesha maisha yao, inaweza kuwapatia njia boŕa za kujiingizia kipato na kuokoa wanawake na watoto wanaofaŕiki dunia,” Philips alisema.