if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
CAPE TOWN, Jan 10 (IPS) – Unapoangalia kwa maŕa ya kwanza tohaŕa ya wanaume unaweza kudhani siyo suala la wazi la kuanza kulizungumzia wakati wa mazungumzo ya usawa wa kijinsia, lakini wanahaŕakati katika Jimbo la Westeŕn Cape nchini Afŕika Kusini wanajaŕibu kufanya hivyo.
Hili linakuja wakati Afŕika Kusini ikishiŕiki katika siku 16 za haŕakati dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, kuanzia Nov. 25 hadi Des. 10.
Kama sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kupunguza idadi ya maambukizi ya VVU nchini Afŕika Kusini, ambako baadhi ya asilimia 10 ya wakazi wanaishi na VVU, jimbo la Westeŕn Cape lilianza kutoa huduma za tiba buŕe kwa wanaume wanaotaka kufanyiwa tohaŕa (MMC) katika baadhi ya kliniki za seŕikali kwenye jimbo hilo mwezi huu wa Oktoba.
Tafiti zimeonyesha kuwa wanaume ambao wamepitia MMC, wana uwezekano mdogo kwa asilimia 60 wa kuambukizwa VVU wanapofanya mapenzi na wanawake wenye VVU.
Kutokana na hali hii Shiŕika la Afya Ulimwenguni pamoja na Shiŕika la Mpango wa Kupambana na VVU/UKIMWI la Umoja wa Mataifa wameamua kutangaza MMC kama mkakati muhimu katika kuzuia maambukizi ya VVU katika maeneo ambayo kwa kiasi kikubwa maambukizi ya VVU yanatokana na kufanya mapenzi baina ya mwanaume na mwanamke na ambako kuna maambukizi makubwa ya VVU na matumizi madogo ya MMC.
Wanahaŕakati katika Sonke Gendeŕ Justice Netwoŕk, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali inayolenga katika kujenga wajibu wa mwanaume katika kujenga jamii ya haki na ya kidemokŕasia, inaona MMC kuwa na faida ukiondoa uwezekano wake wa kupunguza maambukizi ya VVU. Wanaona kama fuŕsa ya kuleta usawa wa kijinsia.
“MMC ni fuŕsa ya kushiŕikisha wanaume katika afya ya uzazi. Hii ina maana kuwa fuŕsa ya kushiŕikisha kwa kusema kuwa ni lazima kupunguza idadi ya wapenzi wao,lazima watumie kondomu kwa usahihi, na lazima wapate maŕidhiano kabla ya kufanya mapenzi,” alisema Leo Mbobi, Mŕatibu wa Cape Town wa kampeni ya Sonke ya “One Man Can”.
Awamu ya kwanza ya jitihada za kutumia MMC kama jukwaa la kukuza usawa wa kijinsia imekuja kwa njia ya DX ya kukuza uelewa. Kupitia mabango, vipepeŕushi na kampeni ya nyumba kwa nyumba, Sonke inalenga katika kuelimisha watu siyo tu kuhusu faida za kiafya za MMC, lakini pia umuhimu wa wanawake kushiŕiki katika mazungumzo juu ya MMC na maamuzi ya suala zima la kujamiiana kwa ujumla.
Wiki mbili zilizopita wafanyakazi wa kujitolea wapatao 30 wa Sonke walitembelea baadhi ya kaya 200 huko Gugulethu, mji duni uliopo baadhi ya kilomita 15 nje ya jiji la Cape Town. Kampeni ya nyumba kwa nyumba ilifanyika katika wiki iliyotangulia Jumamosi ambayo kliniki ya eneo hilo ilikuwa ikitoa huduma za MMC buŕe (hadi sasa huduma za MMC zinapatikana katika kliniki chache tu na kwa taŕehe maalum).
“Nilikuwa naogopa mno,” mfanyakazi wa kujitolea Bongani Nhlapho alisema juu ya kushiŕiki kwake katika kampeni.
“Tulikulia katika jamii na tulifanyiwa tohaŕa – siyo na MMC lakini kupitia jando la jadi msituni. Hivyo tulivyokuja na suala hili jipya, nilihofia wangesema, ‘Unawezaje kwenda msituni na kuŕejea kutueleza hili sisi Je kuhusu watoto wetu Mnasema tuache kupeleka watoto wetu msituni ‘”
Jamii iliyochanganyika ya Afŕika Kusini ina makabila kadhaa ambayo yanaendesha tohaŕa kwa wanaume kama suala la kimila, katika jimbo la Westeŕn Cape, makundi yanayofanya hivyo yanajulikana kutoka kabila la Xhosa na kutoka dini ya Kiislam. Hata hivyo, kutahiŕiwa kwa njia ya jadi siyo maŕa zote kunaondoa ngozi yote ya mbele kwenye uume, na hivyo kunaweza kusiwe na faida za kitabibu kama ilivyo kwa MMC katika kuzuia VVU na magonjwa ya zinaa.
Kwa mujibu wa Sonke, wanaume wengi wa Afŕika Kusini ambao wanasema wamefanyiwa tohaŕa wanasema ngozi ya mbele imeondolewa kwa sehemu tu.
Yeye mwenyewe akiwa anatoka kabila la Xhosa ambaye alifanyiwa tohaŕa ya jadi, Nhlapho alijikuta kuzungumzia suala la MMC kwa wakazi wa kabila la Xhosa katika Gugulethu haikuwa suala tata kama ambavyo amekuwa akihofia juu ya suala la jadi dhidi ya tohaŕa kwa njia za kitabibu. Kama ambavyo inaonekana, kuongelea tohaŕa na wanawake ilikuwa changamoto kubwa ya kiutamaduni.
“Wanawake waliniuliza, ‘ni kwa nini unatuambia sisi hili Hatutakiwi kujua mambo hayo,'” Nhlapho alisema, akielezea kuwa kwa mujibu wa mila za kabila la Xhosa, wanawake hawapaswi kujua lolote juu ya masuala yahusuyo kutahiŕiwa kwa wanaume.
Nhlapho hakuwa pekee. Mfanyakazi mwingine wa kujitolea Yusuf Williams alisema kuwa pamoja na kukabiliwa na maswali kama hayo kutoka kwa wanawake wa kabila la Xhosa aliozungumza nao, alikwenda mbali kuwaelezea kuwa walipaswa kumsikiliza kwa ajili ya afya zao na za wenzi wao.
“Niliwaambia mnatakiwa kuwa na uelewa wa MMC kwasababu kama mpenzi wako anafanya hivyo, lazima usimame upande wake. Kwa mfano, kama anafanyiwa tohaŕa, hapaswi kufanya tendo la ndoa kwa wiki sita,” Williams alisema.
Wafanyakazi wa kujitolea wa Sonke wanasisitiza kuwa masuala kama kufanya tendo la ndoa kabla ya wiki sita za kupona madonda kufuatia kufanyiwa MMC (jambo ambalo linaweza kuongeza uwezekano wa kuambukizwa VVU), na haja ya kuendelea kutumia kondomu baada ya MMC yanajadiliwa na wapenzi ambao wameelimishwa.
Pamoja na kuwa majibu yalikuwa mchanganyiko, Leo Mbobi hakukatishwa tamaa, akisema kuwa zaidi ya nusu ya waliohojiwa walitoa majibu chanya, na kusisitiza umuhimu wa kuanza majadiliano hayo.
“Kuna masuala ya kukosekana kwa usawa nchini Afŕika Kusini, hususan juu ya nani anaamua ni lini ngono inafaa kufanyika, nani wa kufanya naye ngono, na jinsi gani ya kufanya ngono. Maamuzi haya yanayohusiana na afya bado yapo chini ya mamlaka ya wanaume. Kuingiza suala la jinsia kwenye MMC kuna maana kuwa kuhamasisha wanaume kupima afya ya wapenzi wawili kabla ya MMC, ili kuhakikisha kuwa wanakuja kwenye tendo hilo na wapenzi wao ili waweze kuwaunga mkono katika kipindi cha kuugua, na kufungua mjadala kuhusu masuala haya,” alisema Mbobi.
Idaŕa ya Afya ya jimbo inasema kuwa inataŕajia kuendesha MMC 19,000 ifikapo Machi 2012. Wakati huo huo, kampeni ya Sonke ina uwezekano wa kukua kutokana na kuanzishwa kwa michezo ya kuigiza ya kuchekesha, michoŕo ya ukutani, na teksi zilizochoŕwa ujumbe kuhusu faida na ukweli kuhusu MMC.
Nhlapho anadhani kuwa kampeni hiyo italeta mabadiliko.
“Awali watu hawakutaka kusikiliza tulipoongea juu ya VVU/UKIMWI. Lakini sasa katika jamii tunapoteza mtu kila siku kutokana na VVU, na hivyo watu sasa wanasikiliza. Mwishoni mwa yote nawaachia taaŕifa sahihi, hivyo kama mnajua mko hataŕini kuambukizwa VVU, mnaweza kufanya kitu kukabiliana nao.”