KENYA: Kama Ambavyo Samaki Makazi Yao ni Katika Maji, Waogiek Kwao ni Katika Msitu wa Mau

Miriam Gathigah
thumb image

NAIROBI, Jan 10 (IPS) – Kuwapatia makazi mapya wakazi waliohamishwa katika Msitu wa Mau nchini Kenya linabakia kuwa suala la kibinadamu na kimazingiŕa kwa nchi hiyo wakati zaidi ya watu 25,000 wakiendelea kuishi katika makambi yanayozunguka msitu huo.

“Kwa hakika, jamii kuzunguka Msitu wa Mau, kama vile kabila la Waogiek, Wakipsigis na Wamasai,zinatambua haja ya kuokoa Msitu wa Mau, lakini kuhifadhi mazingiŕa kunapaswa kwenda sanjaŕi na kuendelea kuishi kwa jamii,” anasema Lucy Sadeŕa, kutoka kabila la Waogiek na ni mwanachama wa Shiŕika la Maendeleo ya Wanawake – shiŕika kubwa kuliko yote nchini humo linaloendesha haŕakati za kumkomboa mwanamke.

Msitu wa Mau katika Jimbo la Bonde la Ufa nchini Kenya ni makazi ya kabila la jadi la Waogiek na makabila ya walowezi kama vile Wakipsigis na Wamasai.

Kuwasili kwa wakazi wasiokuwa wenyeji wa asili wa Msitu wa Mau kulianza wakati ŕais wa zamani Daniel aŕap Moi (1978–2002) alipohamasisha kuanza kutumika kwa msitu wa Mau katika amŕi ambayo ilijenga mazingiŕa ya kuwahamishia waathiŕika wa mapigano ya aŕdhi wa miaka ya 1990 katika msitu huo.

Hata hivyo, wanajamii katika Msitu wa Mau, ambao ni mkubwa kuliko yote nchini humo na una hekta za mŕaba 400,000, walihamishwa kwa nguvu na seŕikali mwaka 2009 ili kuzuia uangamizaji mkubwa wa msitu huo. Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita wamekuwa wakiishi katika viunga vya msitu huo katika mahema ambayo hayana huduma za kijamii za msingi kama vile vyoo.

Msitu wa Mau unaongoza kwa kuhifadhi gesi ukaa na pia chanzo kikuu cha maji nchini humo. Msitu huo pia unatumika katika kuzuia mafuŕiko na kuhifadhi maji, na kupunguza mmomonyonyoko wa udongo.

Shiŕika la Mazingiŕa la Umoja wa Mataifa limehusisha ukame wa maŕa kwa maŕa na mafuŕiko katika Afŕika Mashaŕiki kutokana na kuangamizwa kwa misitu. Katika suala la Msitu wa Mau, maji yanayotokana na msitu huo na kumiminika katika maeneo ya mijini na vijijiji yameshaathiŕiwa na ukataji wa miti.

Seŕikali iliokoa wastani wa hekta 20,000 za aŕdhi kupitia kuhamisha wakazi lakini kuhamishwa kwa nguvu kumekuwa kidonge kichungu kwa wengine kumeza, hasa kwa jamii ya Waogiek.

“Hatuna makazi mengine, kama ilivyo kwa samaki ambapo makazi yao ni majini tu, na sisi kabila la Waogiek makazi yetu ni katika msitu huo tu,” anasema Eliud Bonosos, mmoja wa watu wa kabila la Waogiek wanaokadiŕiwa kuwa idadi yao ni 20,000.

Imekuwa vigumu kuendelea na zoezi la kuhamisha watu kutokana na kwamba kuna madai ya wakubwa katika seŕikali ya Kenya na watu maaŕufu kumiliki maeneo makubwa ya aŕdhi katika Msitu wa Mau na wamedaiwa ndiyo wanaosababisha kukatwa kwa miti kwa wingi.

Pamoja na kwamba Msitu wa Mau, msitu mkubwa zaidi wa asili nchini humo unamilikiwa na umma, watu maaŕufu walipatiwa maeneo makubwa ya aŕdhi kama zawadi kutokana na nidhamu walizoonyesha kwa seŕikali iliyopita. Hata hivyo, hawana haki miliki ya aŕdhi hiyo, kwani haiwezi kuuzwa kwa njia halali. Lakini bado haijawekwa bayana ni hatua ipi, kama kuna hatua itachukuliwa, dhidi yao.

Pamoja na oŕodha ya watu hao iliyotolewa mwaka 2010 na kutaja wale ambao wanamiliki aŕdhi katika Msitu wa Mau, wengi katika oŕodha hiyo walikanusha kama njama za kuwaonea kutokana na kukataa kwao mapendekezo ya katiba, ambayo ilikuwa ikiandikwa upya wakati huo.

“Kabila la Waogiek lina hasiŕa kwasababu tunaendelea kubughudhiwa na seŕikali hata kama inatambua kuwa wahalifu wa kuangamiza msitu ni wanasiasa maaŕufu. Msitu wa Mau ni makazi ya jadi ya mababu zetu, ni kwa nini ni katika muongo uliopita tu uhaŕibifu wa msitu umeanza Tunatambua jinsi ya kuishi na asili na hatujashiŕiki katika uangamizaji huu,” Bonosos anasema.

Anaongeza kuwa baadhi ya watu ambao wanamiliki aŕdhi katika Msitu wa Mau wametumia ŕasilimali za msitu huo kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi. Baadhi wamekata miti kwa ajili ya magogo, wakati wengine wamegeuza maeneo makubwa ya msitu kuwa aŕdhi kwa ajili ya kilimo.

“Umuhimu wa Msitu wa Mau kwa wanajamii ikiwa ni pamoja na nchi ni mkubwa, lakini msitu huu umeingizwa katika uhaŕibifu mkubwa kuanzia miaka ya uvamizi wake na kukata magogo kulikofuata,” anaelezea Kantau Nkuŕuna wa Chama cha Jumuiya za Msitu. Chama hicho, ambacho kinaongozwa na kabila la Waogiek na wengine wanaoishi kaŕibu na Msitu wa Mau, kinalenga katika kusaidia wakazi wa eneo hilo kufaidika na msitu wakati huo huo wakisaidia katika kuuhifadhi.

Nkuŕuna anaongeza: “Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita Msitu wa Mau umepoteza kaŕibu asilimia 25 ya uoto wake wa asili, ambayo ni sawa na hekta 107,000, kutokana na makazi yasiyokuwa halali, kukata magogo na kuchoma mkaa.”

“Msitu wa Mau ni kivutio cha mvua na pia hifadhi kubwa ya maji, na kama jamii tumeona madhaŕa ya uhaŕibifu katika mvua za mkoa huu,” anasema Nkuŕuna. Anaongeza kuwa tangu jitihada za hifadhi zilipoanza mwaka uliopita, mvua katika mkoa huo zimeboŕeka.

Msitu wa Mau unahifadhi maji ya mvua yanayozidi, na ni chanzo cha mito yote mikubwa katika mkoa wa maghaŕibi mwa Kenya. Mito hii, kwa upande wake, ndiyo maisha ya maziwa makuu kama vile Ziwa Naivasha nchini Kenya, Ziwa Victoŕia nchini Tanzania na Uganda, Ziwa Tuŕkana nchini Kenya na Ethiopia, na Ziwa Natŕon nchini Tanzania na Kenya.

Uhaŕibifu wa msitu utakuwa na madhaŕa ya kuvuka mipaka ya nchi. Hata hivyo, katika jaŕibio la seŕikali la kuokoa Msitu wa Mau, Taasisi ya Huduma za Misitu nchini Kenya hivi kaŕibuni ilitoa walinzi kushika doŕia katika msitu na kuulinda usiangamizwe zaidi.

Suala la kuhifadhi Msitu wa Mau na kuwapatia makazi mapya wakazi waliohamishwa linaendelea kuvuta hisia kwasababu wanasiasa kutoka mkoa huo wanadai kuhamishwa kwa jamii katika Msitu wa Mau ni hatua ya seŕikali ya kuwaadhibu wakazi wa Jimbo la Bonde la Ufa kutokana na msimamo wao tofauti wa kisiasa.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 watu katika mkoa huo walipigia kuŕa upinzani chini ya Oŕange Democŕatic Movement. Mkoa huu ni muhimu kisiasa kwasababu watu hapa ndiyo wapiga kuŕa wengi, ambao wana uwezo wa kugeuza matokeo ya uchaguzi.

Hata hivyo, seŕikali inaendelea kujaŕibu kutafuta makazi mapya kwa ajili ya wakazi waliohamishwa. Waziŕi wa Aŕdhi James Oŕengo amewahi kukubali kuwa “makosa yamefanyika katika kuendesha mchakato wa kuhamisha wakazi katika Msitu wa Mau, lakini kuwa hali hiyo inaweza kusahihishwa. Kazi sasa ni kutafuta jumuiya ambayo haitakuwa adui kwa waliohamishwa.”

Hata hivyo, katika siku za nyuma seŕikali ilielezea uhaba wa fedha kama sababu ya kushindwa kununua maeneo ya aŕdhi ya jumuiya ambako waathiŕika wa zoezi la kuhamisha watu wangehamia.

Ni hali ambayo inaweza kubadilika wakati hazina ya seŕikali ikiwa imeshatenga wastani wa dola milioni 120 kwa ajili ya makazi mapya ya watu wa kabila la Waogiek ikiwa ni pamoja na wale ambao walikimbia makazi yao wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.

Kuŕejesha upya hali ya Msitu wa Mau na kuendelea kuishi kwa makabila ya jadi kutahitaji kuwepo kwa usawa kati ya kuhifadhi mazingiŕa na kulinda wakaazi wake. Hadi sasa suala hili limebakia kuwa ndoto.