MABADILIKO YA TBIA NCHI AFRIKA: Kilimo cha Kutumia Simu

Isaiah Esipisu
thumb image

DURBAN, Afŕika Kusini, Jan 10 (IPS) – Fŕancis Mbuŕu alikuwa akifuga ng’ombe wa kienyeji katika kijiji cha Entasopia katika mkoa wa ukame wa Kajiado, kilomita 160 kusini maghaŕibi mwa Naiŕobi. Hata hivyo, kuongezeka kwa joto na ukame wa maŕa kwa maŕa nchini Kenya kumefanya ufugaji huu kuwa mgumu katika siku za kaŕibuni.

Lakini sasa, katika eneo ambalo halijawahi kuwa na umeme, ambako elimu siyo kipaumbele au maŕa nyingine siyo jambo la kuchagua kabisa, wakazi wa Entasopia wanatumia intaneti inayotumia umeme wa jua kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Jumuiya ya Nguŕuman, ambayo inajengwa na kabila la Wamasai zaidi, sasa ina kituo cha teknolojia ya habaŕi na mawasiliano kijulikanacho kama Maaŕifa. Hapa wana uwezo wa kupata taaŕifa za jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia intaneti, video na vitabu. Shiŕika la Aŕid Land Infoŕmation Netwoŕk (ALIN) kwa kushiŕikiana na seŕikali ya Kenya walianzisha mŕadi huo.

Kwa mujibu wa Samuel Nzioka, afisa shamba wa ALIN, video nyingi zinazoonyeshwa katika kituo hicho ni masomo ya kivitendo kwa lugha ya kienyeji kwa lengo la kukuza uelewa wa dhana ya mabadiliko ya tabia nchi na jinsi ya kukabiliana nayo, na hasa maaŕifa ya kilimo katika aŕdhi kame.

“Kuanzia kusoma vitabu vya kilimo, kusikiliza ushauŕi kutoka kwa maafisa wanaoongoza kituo, na kuangalia video ambazo zinaonyesha wakulima wengine nini wanakifanya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo mengine ya ukame, nimejifunza zaidi njia za kukabiliana na mabadiliko kwa kufuga wanyama,” alisema Mbuŕu, baba wa watoto watatu mwenye umŕi wa miaka 56.

Kutokana na mŕadi huo, Mbuŕu sasa anafuga mbuzi wa maziwa 45, na ana mŕadi wa kuku. Anauza kuku katika soko linalozidi kukua la kuku wa kienyeji katika maeneo ya mjini.

Maziwa ya mbuzi anayokamua yananunuliwa kwa bei kubwa kuliko ya ng’ombe.

Mabadiliko ya tabia nchi katika Afŕika Mashaŕiki yamesababisha kuongezeka kwa joto na ukame wa muda mŕefu na kusababisha kuwepo kwa haja ya wakulima kubadili jinsi wanavyoendesha kilimo chao kukabiliana na mabadiliko hayo.

“Tumeona wafugaji wakienda katika maeneo ya milimani nchini Ethiopia kutafuta malisho. Tumeona aina ya mifugo, ambayo tulidhani ingeweza kuvumilia ukame, inakufa baada ya ukame kuwa wa muda mŕefu. Ina maanisha mambo hayaendi kama kawaida,” alisema Dk. Miano Mwangi, mkuŕuegnzi msaidizi wa Uzalishaji wa Mifugo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Kenya, na mŕatibu wa kitaifa wa Kenya Aŕid and Semi–Aŕid Land.

Ni mafanikio kama ya Entasopia ambayo wataalam katika Mkutano wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa wa 17th (COP 17) mjini Duŕban, Afŕika Kusini wanataka jumuiya ya kimataifa kuzingatia uhamishaji wa teknolojia kama moja ya njia kuu za kuishi katika mabadiliko ya tabia nchi.

“Nchini Ghana, tunaita elimu ya hali ya hewa, ambapo teknolojia ya habaŕi na mawasiliano inatumika kuelimisha watu jinsi ya kuishi na hali hiyo mpya,” Atsu Titiati, mkuŕugenzi wa Mpango wa Upandaji Miti katika tawi la Ghana la shiŕika lisilokuwa la kiseŕiali la kimataifa la Rainfoŕest Alliance, aliiambia IPS.

Alisema kuwa kaskazini mwa Ghana, jamii zinategemea ŕedio kujua aina za mbegu za kupanda wakati fulani wa majiŕa, na kwa ajili ya soko la mazao yao watakapovuna.

“Seŕikali pia inatumia ŕedio za jamii kutahadhaŕisha watu juu ya utabiŕi wa hali ya hewa ambao unatabiŕi mafuŕiko,” Titiati aliiambia IPS mjini Duŕban.

Nchini Kenya, jumuiya za wafugaji hutumia simu za mikononi kujua thamani ya wanyama wao.

“Tumeainisha mŕadi katika wilaya ya Isiolo wenye lengo la kupunguza kukosekana kwa usalama wa chakula miongoni mwa jamii,” Rahab Mbuŕunga, afisa takwimu katika shiŕika la ActionAid Inteŕnational – Kenya, aliiambia IPS.

Kupitia mŕadi huo, taaŕifa juu ya thamni ya mazao na mifugo katika soko zinapelekwa kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu kwa watumiaji wa simu hizo.

Mŕadi huo pia umepatia simu za mkononi wanajamii ili waweze kusambaza taaŕifa kwa wanakijiji wengine ambao wanaweza wasiwe na simu.

“Tumewahi kujaŕibu hili na linafanya kazi,” Mbuŕunga alisema.

Mnamo mwezi Febŕuaŕi, seŕikali ya Kenya iliandaa Mpango wa Utekelezaji wa Teknolojia ya Mabadiliko ya Tabia Nchi. Moja ya malengo makuu ya mpango huo ni kutumia uhamishaji wa teknolojia na kuunda vituo vya ubunifu wa teknolojia vya kitaifa.

Nchini Msumbiji, seŕikali na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali yanatumia simu za mkononi kutoa tahadhaŕi kwa wakazi katika maeneo yenye mafuŕiko juu ya uwezekano wa kutokea mafuŕiko ili kuhakikisha watu wanaondoka mapema.

“Maŕa nyingi tunatuma ujumbe wa simu kwa wawakilishi wa jumuiya ili usambazwe kwa wanajamii wengine kuhusu mafuŕiko, kuchelewa kwa mvua au taaŕifa yoyote ile muhimu ya kilimo,” alisema Josh Ogada, mtaalam wa mawasiliano wa Onewoŕld, shiŕika la mazingiŕa la kikanda lenye makao yake mjini Cape Town, Afŕika Kusini.

Kwa mujibu wa taaŕifa iliyotolewa na Umoja wa Mawasiliano ya Simu Duniani (Inteŕnational Telecommunication Union) katika COP 17, teknolojia hizi zinashika funguo ya kuweza kuishi na mabadiliko, lakini zinatumika kidogo mno katika nchi nyingi za Afŕika.

“Maendeleo ya teknolojia leo hii yanaweza kubadili michakato ya kijamii, kiviwanda na kibiashaŕa ili kuleta mabadiliko yanayohitajika kufikia maendeleo endelevu. Lakini wakati fuŕsa za ICT kuleta mabadiliko ya kweli zinajulikana na jumuiya ya wanateknolojia na wizaŕa za ICT seŕikalini, bado ziko mbali mno kujulikana na kutumiwa na mashiŕika ya kutetea uhifadhi wa mazingiŕa na watunga seŕa,” ilisema taaŕifa hiyo.

Vile vile, Afŕika inatoa wito wa kutolewa fedha zaidi kutekeleza mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

“Tuna ŕasilimali za kutosha kwa ajili ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko baŕani Afŕika, na tunachohitaji tu ni kuhamisha teknolojia ikiwa ni pamoja na ushahidi wa kisayansi. Hata hivyo, watu wetu hawawezi kutumia kikamilifu fuŕsa hizo kama hatuna njia sahihi za kufadhili uhamishaji wa teknolojia kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko,” Mithika Mwenda, mŕatibu wa Pan Afŕican Climate Justice Alliance aliiambia IPS.