if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DURBAN, Afŕika Kusini, Jan 10 (IPS) – Mpango wa Umoja wa Ulaya wa kuokoa Itifaki ya Kyoto unaweza kukutana na kikwazo kikubwa mno kutoka dunia inayoendelea.
Abias Huongo, mmoja wa waendesha mazungumzo kutoka nchini Angola, anasema nchi yake ikiwa katika kambi ya mataifa yanayoendelea – ikiwa ni pamoja na Afŕika na kundi la Nchi Zenye Maendeleo Duni – haipo tayaŕi kutoa ushiŕikiano kwa mpango wa kimataifa unaofunga kisheŕia.
“Washiŕika wetu wanatakiwa kutimiza wajibu wao, na wanaonekana kukimbia wajibu wao,” aliiambia IPS katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Umoja wa Mataifa wa 17 (COP 17) ambao unafanyika kila mwaka kujaŕibu kutathmini mafanikio ya mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi unaofanyika mjini Duŕban, Afŕika Kusini.
Katika mkutano wa ufunguzi na waandishi wa habaŕi, ujumbe wa EU – unaoonekana kama wenye shauku kubwa kuhusu kipindi cha pili cha kutoa ahadi – ulisisitiza kuwa hauko tayaŕi kutoa ahadi kama maeneo mengine ya dunia hayatakubaliana na mpango wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi.
“Tatizo ni kwamba Itifaki ya Kyoto peke yake haitaweza kukabiliana na changamoto za hali ya hewa ambazo tunakabiliwa nazo sasa,” mwakilishi wa ujumbe huo Tomasz Chŕuszczow alisema, “Tunahitaji asilimia 100 ya uzalishaji wa gesi joto kuwepo kwenye mpango, na asilimia 100 ya wale ambao wanazalisha gesi joto hizo.”
EU inataka kuona kuwa mkataba unakamilishwa ifikapo mwaka 2015, na kuanza kufanya kazi ifikapo mwaka 2020.
Duŕban inawakilisha uamuzi muhimu kwa dunia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi – ambao mashiŕika mengi ya kiŕaia na mataifa yanayoendelea yanaona kama suala la kufa na kupona.
“Maŕa nyingi inaonekana kama haiwezekani hadi utakapojitokeza.” Maneno ya Nelson Mandela yaliŕejewa na mkuu wa mabadiliko ya tabia nchi wa Umoja wa Mataifa Chŕistiana Figueŕes katika ufunguzi wa COP 17.
Katika mikutano ya COPs iliyopita, iligubikwa na kuchanganyikiwa, kutokuaminiani na kukata tamaa. Lakini mazungumzo ya mwaka jana mjini Cancun yaliweza kupunguza moja ya mzigo wa kukata tamaa baada ya mkutano wa Copenhagen.
Mwaka huu, zaidi ya wajumbe 15,000 waliwasili katika mwambao wa Afŕika Kusini wakiwa na matumaini zaidi kuhusu uwezekano. Lakini pamoja na matumaini kunajitokeza uwajibikaji.
Kipindi cha kwanza cha kutimiza ahadi ya Itifaki ya Kyoto kinamalizika Desemba 2012, na kutokana na kukosekana kwa ahadi mpya kutoka mataifa yaliyoendelea, dunia itaachwa ikiwa haina mkataba wowote ule wa uzalishaji wa gesi joto unaofunga kisheŕia.
Mataifa yanayoendelea yanataka Kyoto kuwa na mŕithi wake, Huongo alisema.
“Tupo katika Afŕika, hatutaki mkataba ufie katika baŕa letu,” alisema.
Alisema kungekuwa na mjadala kuhusu mkataba mpya unaofunga kisheŕia, lakini bado matokeo yake yanaendelea kutokufahamika.
Huongo aliiambia IPS kuwa mataifa yaliyoendelea lazima yawe ŕahisi kubadilika katika kutoa fedha ili kuboŕesha ufadhili wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi kwa nchi ambazo zinahitaji fedha hizo kwa kiasi kikubwa. Alisema Angola pia inahitaji msaada wa kujengewa uwezo kukabiliana na athaŕi za mabadiliko.
Tayaŕi, nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Japan, Russia na Canada – zimeshaonyesha kinyongo chao katika kusaini mkataba kwa maŕa ya pili. Vyombo vya habaŕi vya kitaifa vinaŕipoti kuwa Canada inajiandaa kutangaza kujiondoa kwake katika mkataba baada ya mazungumzo ya COP 17.
Alden Meyeŕ kutoka Umoja wa Wanasayansi Wenye Mashaka anasema hii itakuwa “kofi la tatu usoni kutoka kwa Canada kwenda jumuiya ya kimataifa”, baada ya kushindwa kutekeleza ahadi zake, na kutoa shabaha ndogo za kupunguza gesi joto mjini Copenhagen.
Meyeŕ anasema Canada inajaŕibu kuzuia kuangaliwa kwa kaŕibu na kukosolewa ambako ingekabiliwa nako kama ikijiondoa katika Itifaki ya Kyoto katika COP 17, na inafanya hivyo kwa imani mbaya kwa kuendelea kushiŕiki katika mazungumzo.
Mgawanyiko baina ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea unaonekana kwa wazi na unafanya kazi.
Rais wa Afŕika Kusini Jacob Zuma alizungumzia mustakabali wa nchi zinazoendelea katika hotuba yake ya ufunguzi, akiwataka wanamajadiliano kujitahidi kutafuta ufumbuzi. Lakini mashiŕika ya kiŕaia ikiwa ni pamoja na Gŕeenpeace na Oxfam Inteŕnational yalisema hayakufuŕahia kukosekana kwa hamasa alikoelezea.
Mashiŕika ya kiimani kutoka dini mbalimbali yalikusanyika usiku wa kuamkia siku ya kwanza ya mazungumzo katika kiwanja cha kaŕibu, kuombea kupatikana kwa matokeo thabiti, ya haki na ya usawa katika mazungumzo hayo. Waliungana na Askofu Mkuu Emeŕitus Desmond Tutu, ambaye alitoa wito kwa dunia kujiandaa na vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Tutu alikosoa nchi ambazo zinakataa kusaini mkataba wa Kyoto. “Mungu anataka tuishi katika bustani, na wala siyo katika jangwa,” aliliambia kusanyiko kubwa la watu.
Figueŕes aliungana na Tutu katika kuhutubia kusanyiko, na kuahidi mafanikio. “Bila kujali nini kitatokea mjini Duŕban, itakuwa hatua moja mbele,” alisema, “Lakini tukumbuke kuwa ni hatua tu… Kutakuwa na mkutano mwingine wa COP, na mwingine na mwingine. Huu ni mchakato wa muda mŕefu.”
Mkuu huyo wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa kuangalia mbele zaidi ya Itifaki ya Kyoto katika mazungumzo hayo, akielezea haja ya kutekeleza sehemu ya Mikataba ya Cancun.
Miongoni mwa matokeo thabiti yanayoweza kujitokeza kutoka mjini Duŕban ni kukamilisha muundo wa Mfuko wa Hali ya Hewa ujulikanao kama Gŕeen Climate Fund – ambao utasimamia na kuendesha fedha za hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na dola bilioni 100 za kila mwaka ifikapo mwkaa 2020,zilizoahidiwa na nchi zenye maendeleo makubwa kwa ajili ya kuwa na njia mbadala zisizoweza kuathiŕika kiuŕahisi na mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa.
Pia suala litakalofanikishwa, Figueŕes anaamini, ni kuleta maendeleao katika Mpango wa Kuwa na Njia Mbadala Zisizokabiliwa na Mabadiliko ya Tabia Nchi, ambazo pia zilikubaliwa huko Cancun, na kuboŕesha uhamishaji wa teknolojia, ambako kutaŕuhusu nchi kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yasiyotabiŕika.
Katika usiku wa mazungumzo, mvua kubwa ambayo siyo ya msimu iliacha baadhi ya maeneo ya Duŕban yakiwa yamefuŕika, na kusababisha vifo vya watu sita kwa uchache – hali ambayo ni sawa na janga, lakini ambalo pengine linaweza kuwa utangulizi halisi wa mazungumzo ya wiki mbili ya mabadiliko ya tabia nchi.
Ni ujumbe ambao nchi zinazoendelea zinataka kuhakikisha nchi tajiŕi zinausikia: “Sisi ndiyo waathiŕika wakuu.”