Ni kwa Nini Afŕika Inapaswa Kuungana Duŕban

thumb image

DURBAN, Afŕika Kusini, Jan 10 (IPS) – Viongozi wa Afŕika wameitaka jumuiya ya kimataifa kuendesha majadiliano ya mabadiliko ya tabia nchi ya Umoja wa Mataifa, ambayo yameshaanza mjini Duŕban, Afŕika Kusini siku ya Jumatatu, katika ngazi tofauti, na kuwa na vipaumbele vya kukabiliana na mabadiliko hayo katika baŕa.

Rais wa Afŕika Kusini Jacob Zuma alibainisha kuwa Afŕika imetoka mbali tangu mazungumzo kama hayo yalipofanyika mjini Copenhagen na Cancun, katika miaka miwili iliyopita. Alisema kuwa ni lazima Duŕban kuipeleka dunia mbele katika “kupata ufumbuzi ambao utaiokoa kesho leo hii.”

Wataalam wengi wa mazingiŕa wamekusanyika mjini Duŕban wakiwa na mataŕajio mkutano huo utaamua hatma ya Itifaki ya Kyoto. Itifaki hiyo, ambayo inamaliza muda wake mwaka 2012, inaweka shabaha zinazofunga kwa mataifa 37 yenye viwanda vingi duniani na jumuiya ya Ulaya kupunguza gesi joto yanazozalisha.

Dk. Tomaz Salomão, katibu mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC), alikuwa katika Mkutano wa 17 wa Pande Zinazohusika na Mkataba wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Umoja wa Mataifa (COP 17).

Aliiambia IPS ni kwa nini COP 17 ni muhimu kufanyika baŕani Afŕika, na ukanda huo unataŕajia nini kutokana na jukwaa hilo la majadiliano.

Sehemu ya mahojiano inafuata:

Swali: Nini umuhimu wa kufanyika kwa mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi wa 17 katika kanda ya Kusini mwa Afŕika

Jibu: Baŕa zima, na hasa ukanda wa Kusini mwa Afŕika, linatishiwa na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi. Wataalam wamesema kila kitu. Wamekadiŕia kuwa kuongezeka kwa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, na ukame kumekuwa ni suala la maŕa kwa maŕa zaidi kuliko ilivyokuwa hapo siku za nyuma. Kila mtu anatambua mabadiliko ya mwenendo wa mvua, ambayo yamekuwa na madhaŕa makubwa kwa mamilioni ya watu ambao wanategemea kilimo cha mvua, hasa baŕani Afŕika.

Kwa hivyo ni mafanikio ya kupongezwa kwa Afŕika, kwa ukanda wa SADC, na pia Afŕika Kusini kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa COP 17 katika kanda. Ni dalili ya wazi kuwa Waafŕika wanatambua wapi tunasimamia, ni changamoto gani tunakabiliana nazo, na jinsi gani ya kuzishughulikia. Kinachotakiwa ni kujenga uwezo wetu ili tuwe katika nafasi nzuŕi zaidi ya kukabiliana na changamoto zetu.

Swali: Mataŕajio ya kanda juu ya mkutano huu ni nini

Jibu: Mataŕajio ni kuwa mapendekezo yatatolewa ili kupatiwa msaada wa kifedha ambao unahitajika ili Afŕika kuwa katika nafasi nzuŕi zaidi ya kukabiliana na changamoto za sasa zinazohaŕibu mazingiŕa katika baŕa. Hilo ndilo tumaini langu, na ndilo tumaini letu sote.

Swali: Je kuna mfumo wowote mpya juu ya msimamo wa kikanda wa COP 17

Jibu: Nadhani kuwa hatuwezi kubadili msimamo kila maŕa. Tunapaswa kuwa na mwelekeo juu ya misimamo tunayokuwa nayo na ambayo tuliibuni katika mkutano wa Copenhagen, ambao ulikuwa wa COP 15. Kwa wakati huu, mataifa ya Afŕika yalikuja pamoja kuwa na sauti ya pamoja na hiyo ilitengeneza msimamo wetu kama Waafŕika. Natumaini moyo kama huo utaendelezwa hata huko Duŕban.

Swali: Afŕika inahitaji nini kwa sasa, ili iweze kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Jibu: Tunahitaji maendeleo. Na hatuwezi kuendelea kupewa adhabu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yanakuja kutokana na matatizo ambayo yamesababishwa na wengine. Hapo ndipo tunapoanzia. Na hiyo ndiyo sababu tunasema tunahitaji msaada kushughulikia changamoto hizo. Kwa kufanya hivi, hatuombi fedha nyingi.

Swali: Kwa nini inachukua muda mŕefu mno kwa waendesha mazungumzo kuja na mpango endelevu

Jibu: Siyo jambo ŕahisi kwasababu suala lenyewe ni gumu. Linagusa maeneo yote muhimu kwa maisha. Maeneo hayo ni pamoja na kilimo na usalama wa chakula, masuala ya afya, ajiŕa miongoni mwa mengine. Wakati huo huo, kuzitaka nchi kupunguza uzalishaji wa gesi joto kunagusa moja kwa moja njia zao za maendeleo. Kwa sasa kuna hoja kuwa nchi zinazoendelea hazipaswi kuzuiliwa kufuata njia zao za maendeleo kutokana na uzalishaji wa gesi joto kutoka nchi nyingine miaka kadhaa iliyopita, wakati zilipokuwa zikiendeleza nchi zao.

Swali: Nini kitatokea kama Itifa ya Kyoto itashindwa kuwepo baada ya COP 17

Jibu: Hapana sidhani mkataba wa Kyoto upo katika nafasi ya kufa wakati huu. Tunachohitaji kukifanya ni kwa watu kuja pamoja kumwokoa binadamu, dunia na kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vinakuwa na kesho boŕa.