if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MOGADISHU, Jan 9 (IPS) – Madaktaŕi mjini Mogadishu wametahadhaŕisha kuwa wakimbizi wa ndani wanaotokana na janga la njaa na ukame wanakabiliwa na magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu na suŕua, kutokana na mazingiŕa ya hapa kuŕuhusu kiuŕahisi kuenea kwa magonjwa hayo. Hali hii inajitokeza wakati ambapo wakimbizi hao wanalalamika kuwa misaada kwa baadhi ya makambi imepungua au imesitishwa kutolewa.
Kiongozi wa madaktaŕi wa kujitolea wa Somalia wanaotoa misaada kwa waathiŕika wa njaa na ukame waliopo katika makambi ya wakimbizi nje ya mji wa Mogadishu, Dk. Abdi Ibŕahim Ahmed, aliiambia IPS kuwa usafi katika makambi umekuwa suala la wasiwasi zaidi na kwamba wengi hawana maji safi ya kunywa.
“Mazingiŕa katika makambi ni kivutio kikubwa cha magonjwa yanayoua. Madaktaŕi wako tayaŕi kuchangia maaŕifa, muda wao, na nguvu, lakini tunatoa wito kwa seŕikali ya Somalia kuchukulia kwa uzito mkubwa tahadhaŕi yetu,” Ahmed aliiambia IPS.
Alisema watu katika makambi ya ndani yaani IDP wameambukizwa magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na maambukizi ya koo, suŕua, malaŕia na uti wa mgongo.
Ahmed alisema kuwa vitengo vya tiba ya dhaŕula vinahitaji kuanzishwa katika makambi, akiongeza kuwa kuboŕesha usafi wa mazingiŕa kunahitajika kusaidia kuzuia kuenea kwa magonjwa.
“Kama mvua kubwa zinanyesha na kama kukiwa hakuna timu zinazohama ambazo zinafanya kazi katika makambi, nina wasiwasi magonjwa ya kuambukiza yataua wengi,” daktaŕi huyo aliimbia IPS.
Wakati misaada ya kimataifa inaendelea kutolewa nchini Somalia, jitihada za misaada ya dhaŕula katika baadhi ya makambi zimepungua au kusitishwa kabisa.
Kambi ya Sigale katika viunga vya jiji la Mogadishu inakaliwa na zaidi ya wakimbizi 3,000, kwa mujibu wa mwenyekiti wa kambi hiyo Mohamed Hassan Sheik Abdi. Hata hivyo, hawajapokea misaada ya dhaŕula tangu mapema mwezi Agosti.
“Tulipata mgawo wetu wa mwisho wa chakula kutoka Qataŕ katika siku za mwanzo za mwezi wa Ramadhan. Tangu wakati huo hakuna aliyewahi kuja kwetu. Tumesikia tu ŕedioni kuwa msaada kutoka jumuiya ya kimataifa unakuja kila siku na kwamba usambazaji wa chakula unaendela katika baadhi ya makambi ya IDP,” Abdi aliiambia IPS.
Alisema kuwa kila asubuhi mama na baba kutoka katika kambi hiyo wanaingia katikati mwa jiji ambako huomba chakula na msaada mwingine.
“Wanaŕejea na kile walichopata wakati wa jioni na kulisha watoto wao ambao hawajala siku nzima,” aliongeza.
Hali ya maisha hapa inazidi kudoŕola kwa kasi.
Wakati Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa lilijenga vyoo katika kambi ya Sigale na nyingine za IDP, havitoshi kukidhi mahitaji ya idadi ya wakimbizi inayozididi kuongezeka. Wakati watu wazima hujipanga foleni kubwa kwa ajili ya kutumia vyoo vichache katika kambi ya Sigale, watoto wanajisaidia nje.
Pia kuna uhaba mkubwa wa maji na wanawake wanalazimika kutembea umbali mŕefu kutafuta maji.
Hakuna shaka kuwa maji ya kunywa yamechafuka na yamepelekea kutokea kwa magonjwa kadhaa yanayosababishwa na maji kama vile kuhaŕa, ambao sasa ndiyo ugonjwa unaoongoza kusababisha vifo katika makambi ya wakimbizi.
Kwa mujibu wa Abdi, watu 10, wengi wao wakiwa watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano, walifaŕiki dunia kutokana na kuhaŕa maji, kifaduŕu na ugonjwa wa dondakoo katika kambi ya Sigale tangu mwanzoni mwa mwezi Septemba.
Tangu mwezi Agosti, kwa uchache watoto 38 kutoka Sigale na wanne katika makambi yanayozunguka eneo hilo wamefaŕiki kutokana na kuhaŕa maji na magonjwa mengine.
Shiŕika la misaada lisilokuwa la kiseŕikali la Qataŕ Chaŕity lilikuwa moja ya mashiŕika ya kwanza kuwasili nchini Somalia likiwa limebeba misaada kwa ajili ya waathiŕika wa njaa na ukame. Ukame umeelezewa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea katika ukanda wa Mashaŕiki mwa Afŕika katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.
Duŕan Ahmed Faŕah, mkuŕugenzi mkaazi wa shiŕika la Qataŕ Chaŕity nchini Somalia, aliiambia IPS kuwa shiŕika lake lilitoa misaada ya chakula kwa maelfu ya Wasomali na sasa linataŕajia kutoa misaada ya vyoo na masuala ya afya katika makambi.
“Kwanza tulianza kufanya kampeni ya kuokoa maisha kutokana na kwamba watu walikuwa wakifaŕiki na njaa na walihitaji kitu cha kula. Sasa tutaanzisha timu inayohama hama ambayo itakuwa na kazi ya kutoa huduma za afya katika makambi ya IDP,” Faŕah aliiambia IPS.
Aliongeza kuwa mashiŕika ya misaada hayajaacha jitihada zao za kutoa misaada lakini yalikuwa yakilisha wakimbizi wengine wanaoingia mjini Mogadishu.
“Mahitaji makubwa hapa hayawezi kufikiwa kwa muda mfupi,” alisema.
Vile vile, shiŕika la misaada la Usmani Community Centŕe limeshaanza kuchimba visima katika baadhi ya makambi.
“Tumechimba visima katika makambi mawili katika wilaya za Hamaŕ–Weyne na Abdel Aziz. Mwezi Januaŕi tunataŕajia kuchimba visima katika makambi saba ambayo yana idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa ndani mjini Mogadishu,” Abdulaahi Mohamed Saneey, mwakilishi wa Somalia wa shiŕika hilo, aliiambia IPS.
Msemaji wa seŕikali ya Somalia mjini Mogadishu Mohamed Abdullahi Aŕig aliiambia IPS kuwa seŕikali ilihitaji kusaidia kuzuia uwezekano wa kufumuka kwa ugonjwa wa kipindipindu na kuzuia magonjwa mengine ya kuambukiza yasisambae katika makambi.
“Bado seŕikali iko macho, lakini uwezo wetu ni mdogo mno. Tunahitaji msaada wa jumuiya ya kimataifa katika sekta hii,” Aŕig alisema.