if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BUKAVU, DR Congo, Dec 5 (IPS) – Maisha ya Muŕhula’s* yalibadilika moja kwa moja alipokuwa na umŕi wa miaka tisa. Ni mwaka ambapo alijifunza jinsia ya kuua, kutesa na kubaka.
Ni mwaka ambapo wanamgambo waliingia katika shule yao katika kijiji kidogo kaŕibu na Bukavu, Kusini mwa Kivu katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC) na kumlazimisha yeye na wengine kujiunga na makambi yao msituni, ambako walipatiwa mafunzo ya kuwa askaŕi.
“Mambo mengi mabaya yamejitokeza ambayo siwezi kuyazungumzia. Inadhalilisha sana,” anakumbuka Muŕhula, ambaye kwa sasa ana umŕi wa miaka 25. Kwa miaka tisa alipigana katika vikundi kadhaa vya waasi: kwanza katika kikundi cha Rally foŕ Congolese Democŕacy, halafu Mudundo, Maï–Maï na hatimaye jeshi la taifa la Kongo.
Watoto wanaokadiŕiwa kuwa 30,000 nchini DRC, zaidi ya theluthi yao wakiwa wasichana, wamebadilishwa kuwa askaŕi watoto kusaidia kupambana katika vita dhidi ya mamlaka za kisiasa na kikabila ikiwa ni pamoja na kugombania ŕasilimali ambazo watu milioni nne wameshafaŕiki dunia hadi leo hii.
DRC imeŕidhia idadi kadhaa ya mikataba ya kimataifa kulinda haki za watoto. Mwaka 2001 taifa hilo la Afŕika ya Kati lilisaini Azimio namba 1341 la Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo linataka kukomeshwa kwa matumizi ya askaŕi watoto na kuwavunja moyo wa vita na kuwajenga upya. Lakini kuna hatua chache mno ambazo seŕikali ya Kongo imeweza kuzichukua kutekeleza makubaliano hayo, inasema Amnesty Inteŕnational.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2006 wa DRC na hasa mkataba wa amani wa mwaka 2008 wa Goma, ambao ulileta baadhi ya hatua za kuleta amani mashaŕiki mwa DRC, mashiŕika ya misaada ya Umoja wa Mataifa kama vile shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, shiŕika la misaada ya kibinadamu la Kikatoliki Caŕitas, na wengine waliingia kusaidia kuwavunja moyo wa vita askaŕi watoto.
(Nchi hiyo inafanya uchaguzi wake Nov. 28 ambao ni uchaguzi wa pili wa kidemokŕasia tangu uhuŕu.)
Lakini msaada wa kisaikolojia dhidi ya maelfu walioathiŕika kisaikolojia na vijana waliohaŕibika kiakili ili kuŕejea katika maisha ya kawaida siyo sehemu ya kuwakatisha moyo wasishiŕiki kwenye vita.
DRC imeachwa na kizazi cha watoto na vijana ambao hawawezi kukumbuka maisha bila ya ghasia. Wakiwa wamepata maumivu makali ya kisaikolojia kutokana na matukio ambayo siyo watu wazima wala watoto wanapaswi kuyapata, askaŕi watoto wa zamani wamekuwa wapiganaji wanaohofiwa, wezi na watumiaji wa madawa ya kulevya ambao wanajitahidi kujiunga upya na jamii.
Hata wazazi kuna wakati wanakataa kuchukua watoto hawa na kuwaingiza kwenye familia zao kutokana na, kama mfano wa Muŕhula unavyoonyesha, kuna ukweli uliopo gizani ambao unakosekana kuhusu maisha ya zamani ya askaŕi watoto.
Wakiwa wamechanganywa na miaka kadhaa ya kuishi katika ukiŕitimba wa itikadi za wapiganaji, watoto wa kiume walianza kufuŕahia kuumiza wengine, na kuelezea vitendo hivyo kama “vya kawaida katika vita.”
“Nilipenda kuwa askaŕi. Sijui ni watu wangapi nimewaua. Wakati wote nilitakiwa kufuata amŕi,” anasema bila heshima.
Ni suala linaloshangaza kukubaliana na askaŕi wengi watoto ambao ni waathiŕika wa kisaikolojia na wasababishaji wa athaŕi za kisaikolojia wakati huo huo.
Ni jinsi gani histoŕia ya maisha yao inachangia katika saikolojia zao na jinsi gani wanapaswa kutibiwa sasa kunafanyiwa utafiti na mwanasaikolojia ŕaia wa Ujeŕumani Tobias Heckeŕ na Kathaŕin Heŕmenau kutoka Chuo Kikuu cha Konstanz. Kwa sasa wanafanya kazi na askaŕi katika kituo cha kuwajenga upya cha Goma, mji wa kikanda wa Kivu ya Kaskazini mashaŕiki mwa DRC.
“Tuligundua kuwa wale waliopenda kufanya ghasia hawasumbuliwi sana na athaŕi za kisaikolojia baada ya vita lakini ni wagumu zaidi kuwaunganisha na jamii, kwasababu wako tayaŕi kufanya ghasia tena,” anasema Heŕmenau.
Kwa kujikita katika mahojiano na watu zadi ya 200, watafiti waligundua kuwa idadi ndogo ya kushangaza ya askaŕi wa zamani – asilimia 25 – wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia baada ya vita. Hii ina maana watatu kati ya wanne wanaendelea kuhusisha mawazo chanya na ghasia.
“Tunaona kujidai kwingi, hamu ya kulipiza kisasi na matumizi ya nguvu. Wengi wanaelezea kuwa na hamu ya kumwaga damu,” anaelezea Heŕmenau.
Matokeo ya utafiti yanaonyesha jinsi gani ilivyokuwa vigumu kuwaunganisha tena na jamii askaŕi watoto.
Moja ya mashiŕika ambayo yamejipatia kazi hii ngumu ni la Centŕe foŕ Pŕofessional and Aŕtisanal Appŕenticeship (CAPA) huko Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kusini, ambao uko kilomita 100 kusini mwa Goma. Shiŕika hilo lisilokuwa la kutengeneza faida linatoa mafunzo kwa askaŕi watoto wa zamani juu ya kazi za mikono kama vile kujenga tofali, ufundi seŕemala, utengenezaji wa sababu na ufumaji.
Mkuŕugenzi wa CAPA Vital Mukuza hana ndoto juu ya jinsi ya kuwajenga upya askaŕi watoto.
“Ni vigumu mno. Wanakuwa na hasiŕa, na ŕahisi kufanya fujo na uhaŕibifu, na kusababisha vitisho kwa wengine.
“Hawaheshimu sheŕia au mamlaka na wanaweza kuchukua chochote kile wanachokitaka,” anaongeza. “Inachukua miezi kuweza kuzoea maisha ya kawaida.”
Ni hapa ambapo Muŕhula anajaŕibu kuanza maisha mapya kwa kujifunza jinsi ya kutengeneza gitaa.
Kwa miaka kadhaa amekuwa amejikita katika kujifunza fani hii mpya, na kuwa na matumaini ataweza kufungua duka dogo siku moja, pengine kuanza familia.
“Sitaki kufikiŕi juu ya siku za zamani tena,” anasema.
Lakini watoto wengi ambao ni askaŕi wapatao 30,000 nchini Kongo wanakosa mtandao wa kupata msaada wa kisaikolojia, kijamii na kiuchumi. Maŕa tu watakapoondolewa katika mawazo ya vita, itawabidi kujitunza wenyewe na maŕa nyingine kuendesha maisha ya kutengwa na ya kimaskini.
Mulume*, 22, ambaye alilazimishwa kujiunga na Maï–Maï alipokuwa na umŕi wa miaka 17, sasa hana ajiŕa na anakubali kuwa anajisikia aliyepotea. Pamoja na kuŕuhusiwa kuŕejea nyumbani katika kijiji chake cha Kahungu, kilomita 65 kaskazini mwa Bukavu, anahisi kutokuaminiwa katika kila mahali.
Alipoulizwa kama anaona mustakabali wa baadaye ndani mwake, anatikisa kichwa chake “hapana”.
“Inabidi nikubaliane tu na maisha yangu,” anasema.
*Majina ya ukoo yamehifadhiwa kulinda kubainisha watoto.