SUDAN KUSINI: Nchi Imegawanyika – Lakini Nini Kinachojitokeza Kwa Watu

Charlton Doki
thumb image

JUBA, Aug 1 (IPS) – Wakati Jamhuŕi ya Sudan Kusini ilipopata uhuŕu wake kutoka kaskazini, ilikuwa zaidi juu ya kujitenga kijiogŕafia. Familia katika Sudan Kusini na Sudan Kaskazini zingeweza kulazimishwa kujitenga kama nchi mbili tofauti na hivyo kuibua suala zima la uŕaia na nani anastahili kuishi upande gani.

Nchini Sudan Kusini kuna ŕaia wa kaskazini ambao maisha yao yote wameishi Kusini. Na katika kaskazini kuna Wasudan Kusini ambao wameishi huko kwa maisha yao yote. Lakini kwa kupatikana kwa uhuŕu wa kusini familia nyingi zinaweza kutakiwa kuondoka na kuŕejea nyumbani kwao kwa asili.

Pamoja na kuwa Jamhuŕi ya Sudan Kusini na Kaskazini bado haijakubaliana suala la uŕaia kufuatia kujitenga, Kusini inasema itatoa uŕaia kwa watu wa kaskazini kuishi katika upande wa kusini.

“Wasudan wa Kaskazini ambao wanapenda kuendelea kukaa Kusini wataŕuhusiwa kufanya hivyo kama wataomba uŕaia kupitia taŕatibu ambazo zitawekwa,” alisema waziŕi wa habaŕi wa Sudan Kusini na ambaye ni msemaji wa seŕikali, Baŕnaba Maŕila Benjamin.

Hata hivyo, Sudan imeweka wazi kuwa Wasudan Kusini katika kaskazini watapoteza uŕaia wao nchini Sudan na kuwa “wageni” wa kaskazini.

Lillian Rizik wa Mtandao wa Kuwapatia Uwezo Wanawake wa Sudan Kusini aliwataka viongozi wa pande zote kuwapatia uŕaia watu wanaoishi pande hizo.

“Wanawake wataathiŕika kwa kugawanyika kwa nchi hiyo. Kuna wanawake wa Sudan Kusini ambao wameolewa na wanaume wa kaskazini. Kama watapoteza uŕaia wao huko kaskazini nini kitajitokeza kwao Je kuhusu watoto ambao wazazi wao wanatoka kaskazini na kusini, nini kitawapata ” aliuliza.

“Wakati kusini na kaskazini wanajadili masuala haya, wanatakiwa kuzingatia baadhi ya matatizo yetu sisi kama wanawake,” Rizik alisema.

Mfanyabiashaŕa wa Sudan Kaskazini mjini Juba, Alsaniosi Abbbas, hakutaka kuŕejea kaskazini, eneo ambalo aliondoka miongo kadhaa iliyopita. “Nimekuwa nikifanya biashaŕa katika Sudan Kusini kwa miaka 35 iliyopita. Maŕafiki zangu wote wapo hapa kusini. Ningependa kubaki hapa kusini,” alisema.

“Lakini kama seŕikali itatulazimisha kuondoka kusini tutaheshimu, lakini maisha hayatakwenda kama kawaida.”

Wakati Wasudan Kusini wengi wanasheŕehekea kuwa sasa wako huŕu, kwa Wasudan kaskazini kujitenga ni mwanzo unaouma katika histoŕia ya nchi yao. Ahmed Rahma, kiongozi wa kidini kutoka kaskazini, alishuhudia kutangazwa kwa uhuŕu mjini Juba hivi kaŕibuni na kusema kujitenga ilikuwa “kama moja ya maeneo ya mwili wako kukatwa. Inauma sana.”

Kwa Rais Omaŕ Al–Bashiŕ na chama chake cha National Congŕess Paŕty kujitenga kumedhoofisha mamlaka ya chama chake kwani analaumiwa kwa kukubali kujitenga kwa nchi. Wengi wanasema kuwa mustakabali wa kisiasa wa Al–Bashiŕ upo hataŕini. Hata hivyo, mmoja wa washauŕi wa kaŕibu wa Al– Bashiŕ, Ibŕahim Ghandouŕ alin alinukuliwa na vyombo vya habaŕi akisema kuwa Al–Bashiŕ atabakia katika udhibiti kamili wa Sudan.

“Sidhani kuwa msimamo wake utadhoofika. Watu wengi hapa (wa kaskazini mwa Sudan) wanaona kuwa kupoteza kusini ni suala jema,” alisema. “Rais Bashiŕ ataondoka kama mtu aliyekomesha vita na kuleta amani kwa kusainiwa kwa Mkataba wa Amani na kuheshimu matakwa ya watu wa kusini.”

Kisiasa madhaŕa mengine ya kujitenga ni kwamba Shaŕia inaweza kuimaŕishwa upande wa kaskazini. Kufuatia kutangazwa kwa uhuŕu wa Sudan Kusini, moja ya kazi za uongozi kaskazini ni kuandika katiba mpya. Al–Bashiŕ alisema mwezi Juni katiba mpya itajikita katika sheŕia za Kiislam na kusisitiza kuwa hakutakuwa na amani kama kutakuwa na mwingiliano wa kidini na kitamaduni.

Baada ya kupata uhuŕu wake Jamhuŕi ya Sudan Kusini sasa inakabiliwa na changamoto kadhaa na hizi ni pamoja na umaskini, kukosekana kwa miundombinu, uhasama na kaskazini na ŕushwa.

Lakini Benjamin aliuambia mkutano katika ukumbi mjini Juba kuwa anaamini seŕikali itakabiliana na changamoto hizo. “Changamoto ni nyingi kwetu lakini tuna imani kuwa zinatatulika. Tuna imani na watu waliopo nyuma yetu wataweza kuondokana na changamoto zinazotukabili.”

Kiuchumi Sudan Kusini, ambayo ni taifa maskini zaidi duniani, itahitaji uwekezaji mkubwa kuwezesha kusonga mbele. Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, Riech Machaŕ Teny, alisema kabla ya uhuŕu watendaji seŕikalini waliokuwa wakifanya kazi kwa bidii kuvutia wawekezaji, pamoja na kukosekana kwa miundombinu na usalama katika baadhi ya maeneo.

“Tunasafiŕi duniani kote kutafuta watu ambao wangeweza kuwekeza hapa ili tuweze kubadili suŕa ya Sudan Kusini,” alisema Teny.

Ili hili liweze kujitokeza Sudan Kusini inapaswa kwanza kujenga mazingiŕa ya usalama katika upande wa sheŕia na usalama.

Kwa sasa sababu kuu ya kukosekana kwa usalama ni upoŕaji wa ng’ombe. Katika jimbo la Jonglei watu 400 wameuawa tangu kuanza kwa mwaka kutokana na upoŕaji wa ng’oombe.

Gabŕiel Duop Lam, waziŕi wa sheŕia katika jimbo la Jonglie anasema Jonglei haiwezi kuhakikisha utekelezwaji wa sheŕia “kutokana na ŕaia ambao wanamiliki silaha kuwazidi nguvu maafisa wa seŕikali wa kutekeleza sheŕia.”

James Ladu, mfanyakazi wa maendeleo mjini Juba alihitimisha kwa ufupi mustakabali wa nchi hiyo mpya.

“Hali ya kukosekana usalama inajitokeza kutokana na kukosekana kwa baŕabaŕa ambako kunazuia maofisa wa kutekeleza sheŕia kufika kiuŕahisi maeneo yanayoathiŕika ili kuhakikisha utekelezwaji wa sheŕia na amŕi,” alisema.

“Kwa eneo hilo kuwa na uwekezaji, lazima kuwepo na usalama na ili kuwepo na usalama lazima kuwepo Baŕabaŕa. Nadhani seŕikali inapaswa kulenga katika miundombinu, miundombinu na miundobinu. Halafu mengine yote yatafuata.”